Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16

UKWELI KUHUSU SABATO


Sabato ni kielelezo cha uumbaji wa Mungu


KWELI 100 KUHUSU SABATO YA BIBLIA

è Kwanini unapaswa kutunza sabato?
è Ni nani unayeabudiwa kaatika siku ya sabato?
è Nani aliiianzisha?
è Ilianzishwa lini na kwaajili ya nani?
è Ni siku gani ambayo ni sabato?
è Wengi hutunza siku ya kwanza ya juma au jumapili je wanamamlaka gani kimaandiko?
è Baadhi hutunza siku ya saba au jumamosi Je wana mamlaka gani ya kimaandiko kwa hilo?
è Je ibaada ya jumapili ilianza lini, ni nani aliyeianzisha, biblia husemaje kuhusu kuadhimisha siku ya jumapili kama siku ya Ibada?
è Hapa kuna ukweli kuhusu siku hizo zote, kama inavyoelezewa wazi na neno la Mungu.

ZIFUATAZO NI KWELI 100 ZA BIBLIA KUHUSU SABATO.
1)Baada ya kuumba dunia kwa siku sita, Mungu akapumzika siku ya saba. Mwanzo 2:1,3.
2)Jambo hili lilitia muhuri siku hiyo kama Siku ya Mungu ya mapumziko , au siku ya sabato , kama sabato imaanishavyo pumziko. Mtu azaliwapo siku fulani, siku hiyo huwa siku yake ya kuzaliwa (birthday). Kwahiyo Mungu alipopumzika katika siku ya saba, siku hiyo ikawa kumbukumbu ya kuzaliwa/ kuumbwa kwa dunia na vyote vilivyomo au siku ya sabato.
3)Kwahiyo siku ya saba lazima iwe siku yua sabato ya Mungu. Waweza kubadilisha birthday yako  kutoka siku ambayo ulizaliwa mpaka siku ambayo  hukuzaliwa? Hapana, pia huwezi kubadili siku ya Mungu ya pumziko ikawa siku ambayo mungu hakupumzika. Kwahiyo siku ya saba bado ni sabato ya Mungu.
4)Mungu aliibariki Siku ya Sabato (Mwanzo 2:3.)
5)Mungu aliitakasa Siku ya Sabato. (Kutoka 20:11.)
6)Aliifanya kuwa Siku ya Sabato katika Bustani ya Edeni. (Mwanzo 2:1-3)
7)Ilianzishwa kabla ya anguko, kwahiyo haikuwa kivuli kwa maana vivuli (vielelezo) vilianzishwa baada ya anguko. Kwasababu hiyo haijakomeshwa kwasababu ni kumbukumbu ya uumbaji wa mungu.
8)Mungu alisema ilifanyika kwaajili ya Mwanadam (Marko 2:27.) Hii humaanisha kwa wanadamu wote, kama vile neno mwanadamu hapa halina kikomo; kwahiyo ni kwaajili ya myahudi na mmataifa.
9)Ni kumbukumbu ya uumbaji . (Kutoka 20:11; 31:17.)Kila tupumzikapo siku ya sabato, kama Mungu alivyopumzika tunaadhimisha (sherekea) uumbaji.
10)Ilikabidhiwa kwa Adamu, Baba wa jamii ya wanadam. (Marko 2:27; Mwanzo 2:1-3.)
11)Kwahiyo kupitia kwake, kama Muwakilishi wetu, ni kwa mataifa yote. (Matendo 17:26.)
12)Si siku ya Waayahudi kwani ilianzishwa miaka 2,3000 kabla ya kuwepo Wayahudi.
13)Kamwe Biblia hahiiti sabato ya Wayahudi, lakini mara zote “sabato ya Bwana Mungu  wako.” Wanadamu wanapaswa kujihadhari na kuikanyaga sabato ya Mungu
14)Kielelezo cha sabato kama siku ya saba ya wiki , kinawekwa katika kiipindi cha wazee wa imani. (Mwanzo 2:1-3; 10:10,12: 29:27, 28 n.k)
15)Ilikuwa ni sehemu ya Sheria ya Mungu kabla ya Sinai. (Kutoka 16:4, 27-29.)
16)Kisha Mungu akaiwake kama kiini (Moyo) cha sheria yake ya maadili. (Kutoka 20:1-17.) Kwanini aliiweka pale kama haikuwa sawa na amri nyingine tisa ambazo hazibadiliki. Yesu alipoangikwa msalabani hakufuta amri kumi ,ndo maana uzinzi, wizi n.k bado ni dhambi, iweje uvunjaji wa sabato isiwe dhambi?
17)Siku ya saba ya Sabato iliamriwa kwa sauti ya Mungu aliye hai. (Kumbukumbu La Torati 4:12,13.)
18)Kisha Mungu akaandika amri hiyo kwa vidole vyake mwenyewe. (Kutoka 31:18.)
19)Akaitia muhuri katika jiwe lisilofutika, ikiashiria kwamba inaasili ya kutokuharibika. ( Kumbukumbu La Torati 5:22.)
20)Ilitunzwa katika sanduku lilioko Patakatifu Pa Patakatifu. ( Kumbukumbu La Torati 10:1-5.)
21)Mungu alikataza kufanya kazi siku ya sabato, hata katika nyakati ngumu zenye kazi nyingi.(Kutoka 34:21.)
22)Mungu aliwaadhibu wana wa Israeli jangwani kwasababu waliihalifu Sabato.(Ezakieli 20:12,13.)
23)Sabato ni ishara ya Mungu wa kweli, ambaye kupitia hiyo tunamtofautisha na miungu wa uongo. ( Ezekieli 20:20.), Wana wa israeli walipokuwa wakitoka Misri Sabato iliwatofautisha na waabudu miungu, hii inatokana na ukweli kwamba Amri ya nne Kutoka 20:8-...ndiyo amri pekee imtambulishayo Mungu kama muumbaji.
24)Mungu aliahidi kwamba Yerusalemu ingedumu milele endapo wayahudi wangeitunza sabato.(Yeremia 17:24,25.)
25)Mungu aliwaacha (Israeli) utumwani babeli kwasababu waliivunja Sabato. (Nehemia 13:18)
26)Aliiangamiza Yerusalemu kwa kuivunja Sabato.(Yeremia 17:27.)
27)Mungu ameahidi mibaraka maalumu kwa wamataifa na wote watakaoitunza Sabato.(Isaya 56:6,7.)
28)Hii ipo katika unabii , ambayo kwa ujumla inahusu ukristo. (Isaya 56.)
29)Mungu ameahidi kuwabariki wote waitunzao sabato. (isaya 56:2.)
30)Mungu anatuhitaji sisi tuiite siku takatifu ya heshima. (Isaya 58:13.) Iweni na tahadhari ninyi mnaoiita “Sabato ya zamani ya Wayahudi”, “nira ya utumwa.”
31)Baada ya Sabato takatifu kukanyagwa chini “vizazi vingi” itarejeshwa tena katika siku za mwisho. (Isaya 58:12,13.)Hapa Sabato inaelezewa kama mojawapo ya matengenezo ya ibada ya kweli katika siku za mwisho.
32)Manabii wote watakatifu waliitunza Sabato.
33)Mwana wa Adam (Yesu Kristo) alipokuja, aliitunza Sabato maisha yake yote. (Luka 4:16; Yohana 15:10.) Kwa  kufanya hivyo alifuata kielelezo cha Baba yake cha uumbaji. Je hatuwezi kuwa salama zaidi kwa kufuata kuelelezo cha Baba na  Mwana?
34)Siku ya Sabato ni siku ya Bwana ( Ufunuo 1:10,Marko 2:28, Isaya 58:13; Kutoka 20:10.)
35)Yesu Kristo ni bwana wa sabato (marko 2:28.), hii inamaanisha kuipenda na kuitunza, kama mume ni Bwana wa mke , kwa kumpenda Yesu ambaye ni Mume na kichwa ca kanisa(Waefeso 5:22-27) , tunamtii kwa kuitunza sabato ambayo ni agizo lake (si ombi) kwetu .
36)Yesu aliifunua Sabato kama taasisi ya neema iliyoundwa kwa kumtakia mema mwanadam. (Marko 2:23-28.)
37)Yesu Badala ya kuihalifu sabato , kwa umakini mkubwa alifundisha namna ya kuitunza.(Mathayo 12:1-8,Marko 3:1-5,Luka 14:1-5.),Mafarisayo walifanya sabato kuwa ngumu kwa kuzuia hata shughuli njema zisifanyike,Yesu akasema shughuli njema yaani za kuokoa uhai kama vile kutibu wagonjwa, kumpikia mwenye njaa ni halali kuzifanya Siku ya Sabato (Mmat 12:12.)
38)Yesu aliwafundisha wanafunzi wake wasifanye kitu Siku ya Sabato kilicho kinyume na sheria. (Mathayo 12:12.)
39)Yesu aliwasisitiza wanafunzi wake kwamba waombe baada ya kunyakuliwa kwake hata siku watakapokimbia maangamizi ya Yerusalemu, isiwe sabato maana wangeihalifu.(Mathayo 24:20.)Hili linadhiirisha kwamba hata Yesu alijua kwamba atakapo kufa, atakapo fufuka na kunyakuliwa sabato haitasitishwa.
40)Wanawake walioambatana na Yesu kwa umakini waliitunza sabato baada ya kifo cha Yesu.(Lika 23:56.)
41)  Miaka thelathini, baada ya Yesu kunyakuliwa , Roho Mtakatifu kupitia Paulo anaitaja kama “Siku ya Sabato,” (Matendo ya Mitume 13:14.)
42)Paulo, Mtume kwa watu wa mataifa, “aliita Siku ya Sabato” katika mwaka 45.A.D ( Matendo ya Mitume 13:14) Je Paulo hakujua? Au tuwaamini walimu wa sikuhizi wasemao iligongomelewa msalabani yaani iliishia kipindi Yesu aliponyakuliwa Mbinguni?
43)Luka, mwanahistoria wa Kikristo aliyevuviwa, akiandika miaka ya 62 A.D anaiita “Siku ya Ssabato.”(Matendo 15:21.)
44)Waongofu wa mataifa waliita Sabato. (Matendo ya Mitume 13:42.)
45)Katika baraza kubwa la Wakristo mwaka 49 A.D mbele ya mitume na maelfu ya wanafunzi , Yakobo anaiita “Siku ya Sabato.” ( Matendo ya Mitume 15:21)
46)Ilikuwa ni desturi kufanya maombi kufanya kusanyiko la maombi siku hiyo.( Matendo ya Mitume 16:13.)
47)Pauo  alisoma maandiko matakatifu katika kusanyiko takatifu katika Siku ya Sabato. ( Matendo ya Mitume 17:2,3.)
48)Ilikuwa ni desturi ya Paulo kuhubiri Siku ya Sabato.( Matendo ya Mitume 17:2,3.)
49)Kitabu cha Matendo ya Mitume kinatoa rekodi ya Paulo kufanya mikutano ya ibada 84, katika siku ya sabato.( Matendo ya Mitume 13:14,44; 16:13 ; 17:2 ; 18:4,11.)
50)Hapakuwa na ugomvi wowote kati ya Wayahudi na Wakristo juu ya Sabato.Huu ni uthibitisho kwamba wakristo waliitunza sabato ileile iliyotunzwa na Wayahudi.
51)Wakristo walipomshtaki Paulo, kamwe hawakumshtaki kwa suala la kutunza Sabato. Kwanini hawakumshtaki kama si kwasabau walikuwa wakiitunza?
52)  Lakini Paulo mweyewe alikiri kwamba aliitunza sheria. (Matendo 25:8.) Je hili lawezaje kuwa sahihi kama Paulo hakuitinza Sabato?
53)Sabato hutajwa katika aganojipya mara hamsini na nane,, na marazote kwa heshima ikibeba jina lile lile ililokuwanalo katrika Agano la Kale kama “Siku ya Sabato.”,na matendo ya kupumzika,ibada na matendo mema.Mathayo 10,Marko 11,Luka 18, Yohana 10 na Matendo  ya Mitume 9.
54)Katika agano jipya hakuna neno lionyeshalo kuwa Sabato ilisitishwa, kuondolewa, kubadilishwa , au kitu chochote cha aina hiyo.
55)Mungu kamwe hajaruhusu mwanadamu yoyote kufanya kazi katika siku hiyo, ndugu msomaji ni kwa mamlaka ya nani unaitumia siku ya sabato kwa kazi za kawaida?
56)Katika Biblia Hakuna Mkristo katika agano jipya, eidha kabla au baada ya kunyakuliwa kwa Yesu, ambaye alifanya kazi za kawaida Siku ya saba ya Sabato.Kwanini wakristo wa leo hufanya tofauti na Wakristo wa kwenye Biblia?
57)Hakuna rekodi kwamba Mungu ameondoa Mbaraka na Utakaso wa Siku ya Sabato.
58)Kama vile Sabato ilivyotunzwa Edeni kabla ya Dhambi (Anguko), vivyohivyo itatunzwa mbinguni baada ya dhambi kuangamizwa.(Isaya 66:22,23.)
59)Sabato ya Siku ya Saba ilikuwa na nafasi muhimu katika amri kumi za Mungu, kama ilivyotoka katika kinywa cha Mungu, na kuandikwa kwa kidole chake mwenyewe juu ya jiwe pale Sinai (tazama Kutoka 20.) Yesu alipoanza kazi alisema kwa uwazi kabisa Hakuja kuitangua Torati (sheria). “Msidhani ya kwamba nalikuja kuitangua torati, au manabii.” (Mathayo 5:17.)
60)Yesu aliwakemea vikali Mafarisayo  kwamba ni wanafiki wakiigiza kama walimpenda Mungu, na bado wakati huohuo wliihalifu sheria moja kati ya Amri kumi za Mungu kwa kufuata mapokeo yao. Uutunzaji wa jumapili kama siku ya Ibada ni mapokeo ya wanadam.


KWELI AROBAINI ZA BIBLIA KUHUSU SIKU YA KWANZA YA JUMA.

61)Kitu cha kwanza kurekodiwa katika Biblia ni kazi iliyofanyika siku ya kwanza ya juma.(Mwanzo 1:1-5.) Muumbaji mwenyewe alifanya hili.Kama Mungu aliiumba dunia siku ya jumapili,je yaweza kuwa dhambi kwa sisi kufanya kazi siku ya jumapili?
62)Mungu huwaamuru wanadamu wafanye kazi siku ya kwanza ya juma.( Kutoka 20:8-11.) Je ni dhambi kumtii Mungu?
63)Hakuna Mzee wa imani aliyeitunza Jumapili kama siku ya Ibada.
64)Hakuna Nabii Mtakatifu aliyeitanza (jumapili) kama siku ya ibada.
65)Kwa maelekezo ya sheria ya Mungu  ,kutoka  uumbaji hadi kifo cha Yesu watakatifu Wake wameitunza siku ya kwanza ya juma kama siku ya kawaida ya kazi angalau kwa miaka 4,000.
66)Mungu mwenyewe huiita siku ya kazi .(Ezekieli 46:1.)
67)Mungu hakupumzika katika ya kwanza (Jumapili).
68)Mungu hakuibariki siku ya kwanza (Jumapili.)
69)Yesu alikuwa fundi seremala (Marko 6:3) na alifanya biashara yake mpaka alipofikisha miaka 30. Aliitunza sabato na kufanya kazi kwa siku sita za wiki. Kwahiyo alifanya majukumu yake mazito siku ya Jumaapili.
70)Yesu hakupumzika siku hiyo ya jumapili.
71)Mitume walifanya kazi jumapili.
72)Mitume hawakupumzika jumapili.
73)Yesu kamwe hakuibariki.
74)Kamwe haijabarikiwa na Mamlaka Takatifu kutoka Mbinguni.
75)Kamwe haijatakaswa.
76)Hakuna sheria iliyoagiza kuitunza siku ya kwanza ya juma (jumapili) kama siku ya Ibada, kwa hiyo si dhambi kufanya kazi katika siku hiyo. “kwa maana pasipo na sheria, hakuna dhambi .” (Warumi 4:15. Pia 1 Yohana 3:4.)
77)Katika agano jipya hakuna sehemu ikatazayo kufanya kazi siku hiyo.
78)Hakuna adhabu itolewayo kwa kufanya kazi jumapili (ikionyesha kama imehalifiwa.)
79)Hakuna mbaraka ulioahidiwa kwa kuitunza.
80)Hakuna maelezo yaliyotolewa kwamba ni kwa namna gani inapaswa kutunzwa.Je hili lawezekana endapo mungu anekuwa anataka tuitunzw kama siku ya Ibada.
81)Kamwe haijaitwa Sabato ya wakristo.
82)Kamwe haijaitwa Siku ya Sabato.
83)Kamwe haijaitwa siku ya Bwana,wanadam ndio walioiita Siku ya Bwana.
84)Kamwe haijaitwa siku ya pumzinko.
85)Hakuna jina takatifu ililopewa. Sasa kwanini tuiite  siku takatifu?
86)Kwa urahisi huitwa “siku ya Kwanza ya juma.”
87)Yesu hakuitaja kwa namna yoyote,kamwe hakulitamka jina la siku hiyo kwa midomo yake, kwa rekodi yote tuliyonayo.
88)Neno jumapili kamwe halionekano kwenye Biblia, labda biblia ya kiswahili cha kisasa, lakini katika Biblia nyingine imetajwa kama siku ya kwanza ya juma.
89)Kamwe Mungu, Yesu , hata waliovuviwa kuandika  maandiko ya Biblia hakuna aliyewahi kuongea akiisifia jumapili kama siku ya Ibada.
90)Siku ya kwanza ya juma inatajwa mara nane tu katika Agano Jipya.(Mathayo 28:1, Marko 16:2,9; Luka 24:1. Yohana 20:1,19; Matendo ya Mitume 20:7; 1 Wakorintho 16:2.)
91)Mafungu sita huelezea siku ya kwanza ya wiki.
92)Paulo aliwaagiza watakatifu wajishughulishe na mambo yao katika siku hii ya kwanza ya wiki, (1 Wakorintho 16:2.)
93)Katika agano jipya tuna kumbukumbu ya mkutano mmoja tu wa kiroho uliofanyika katika siku hiyo, nao ulifanyika usiku (matendo 20:5-12.)
94)Hakuna maandiko yaonyeshayo kwamba walikuwa na mkutano kama huo kabla au baada ya hapo.
95)Haikuwa desturi yao kukusanyika katika siku hiyo(jumapili).
96)Hakukuwa na agizo la kuumega mkate katika siku hiyo.
97)Tuna kumbu kumbu ya tukio moja tu ambapo waliumega mkate. (Matendo ya Mitume 20:7.)
98)Tukio hilo lilifanyika usiku wa manane. (Matendo ya Mitume 20:7-11.) Yesu alifanya tukio kama hilo Ijumaa jioni (Luka 22), Na wanafunzi wakati mwingine walilifanya tendo hilo kila siku.(Matendo ya Mitume 2:42-46.) Ingekuwa ni Ibada rasmi ya kielezo kwa kawaida isingefanyika usiku bali kuanzia asubuhi.
99)Kamwe Biblia haijaonyesha sehemu yoyote kwamba jimapili (siku ya kwanza) ni siku ya kukumbuka kufufuka kwa Yesu, Haya ni mapokeo ya wanadam ambayo ni kinyume na neno la Mungu. (Mathayo 15:1-9.)
100)Ubatizo ndiyo tendo  litukumbushalokifo na ufufuo wa Yesu. (Warumi 6:3-5.), na jambo jingine ni kitendo cha kuumega mkate (Pasaka ) tofauti na ile ya mwezi wa nne kwasababu pasaka ya biblia na Easter ni vitu viwili tofauti. Yesu aliacha mabo hayo kama vielelezo vya kukumbuka na kuadhimisha ukombozi aliotufanyia na sio kusali siku ya kwanza ya juma.
101)Mwishowe, Agano jipya liko kimya kabisa kuhusu badiliko lolote la siku ya sabato au utakatifu wa siku ya kwanza.

Maelezo zaidi kuhusu Sabato.
                  ISHARA YA UHUSIANO WETU NA MUNGU.
                  Sabato ni Ishara ya taifa la Mungu, Kutoka 31:13,17,16.Imeandikwa , 13“Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika sabato zangu kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasae ninyi. 17Ni kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya Mbingu na nchi, akastarehe siku ya saba akapumzika. 16Kwaajili ya hayo wana wa Israeli wataishika sabato katika vizazi vyao vyoyte, ni agano la milele.
                  Sabato ni ishara kati ya waumini wa Mungu na Mungu iashiriayo kwamba wanamtii na kushika sheria yake.Utunzaji wa sabato ni njia aliyoiweka Mungu ili kutunza maarifa kumhusu Yeye na kutofautisha waumini wanaomtii na wale wavunjaji wa sheria yake. Shetani atafanya kila mbinu kuhakikisha kwamba mafundisho ya Imani iliyokabidhiwa kwa watakatifu hapo mwanzo isilete matokeo kwa watu wa kizazi hiki.              
                  Mungu asingeweza kusema kuwa ni agano lake la milele halafu aje kubadilisha, sabato itaendelea kuwepo milele zote hata katika Mbingu mpya na nchi mpya soma Isaya 66:22,23.
                  Msomaji yeyote wa Biblia sehemu ya agano jipya, kuanzia mathayo 12:1-13, akifuatilia kila kisemwacho kuhusu sabato na msimamo ambao Yesu na Mitume waliuchukua kuhusu sabato, hatashindwa kutambua kwamba Kanisa la kipindi cha agano jipya lilitunza Sabato kutokana na mfano wa mafundisho ya Yesu mtunzaji wa sabato. “Bwana wa Sabato”  alifundisha sehemu yake halisi na tabia ya sabato katika ufalme wake.

IBADA YA JUMAPILI ILIANZA LINI?
     
                  Kabla ya yote ikumbukwe kwamba Biblia huitaja siku ya saba (Sabato ) kama siku ya Bwana. Kutoka 20:10. “lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana...”, Marko 2:28. Basi Mwana wa Adam ndiye Bwana wa Sabato.Isaya 58:13...ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima... Baada ya Kostantino kuanzisha Ibada ya jumapili aliita siku hiyo Siku ya Bwana jambo ambalo halina ukweli wa kimaandiko, wote waiitao jumapili siku ya Bwana huo ni uongo wa shetani kuwapofusha wasijue udanganyifu wa sabato bandia aliyoanzisha. Hivyo hata vitabu vya historia huiita sjumapili siku ya Bwana kwa mtazamo huo kama ifuatavyo.

VITABU VISIVYO VYA KISABATO HUELEZEAJE?
                  Kitabu cha (International Standard Bible Encyclopedia, Vol 3, pg 158, na Vol 4 ukurasa 251,252) kimnaelezea mabo yuafuatayo:-
                             
                  “Katika Mwaka 321 A.D Costantino, ambaye pia alikuwa na muumini wa mungu-jua, aliifanya siku ya kwanza kuwa siku ya kawaida kwa jamii kupumzika, akisema kwamba, Majaji, watu wa mijini, na wachongaji wapumzike katika siku hii ya mungu jua,lakini aliwaruhusu wakulima kuhudhuria mashambani hali ya hewa ikiruhusu.Sheria hii kwa asili ilisababisha uwepo wa Ibada ya Kikristo.”

Mwaka 363 A.D.Baraza la Laodikea(Council of Laodecia)
                  Baraza hili lilikataza kupumzika katika siku ya saba (Sabato) na kuagiza watu wapumzike katika siku ya Bwana  kama ijulikanavyo kuwa siku mbadala ya Ibada.

Mwaka 451 Baraza la Karthage(Council of Carthage)
                  Baraza hili lilikaataza watu wasihudhurie katika michezo siku ya  Bwana (jumapili.)

Karne ya 16. Baraza la Oreansi (Council of Orleans) 
                  Baraza hili liliongeza sheria ya kukataza watu wasifanye kazi siku ya Bwana.(jumapili).

                  Pia kitabu cha Roman Katoliki kiitwacho “Historia ya Kanisa Vipindi Vyake saba, kilichoandikwa na F.Potmani. Ukurasa 24, kinaelezea yafuatayo;
                  Mwaka 306,  Kostantino alitangazwa Kaisari wa Magharibi, ilipofika mwaka 312 alimshinda mpinzani wake karibu na Roma. Mwaka 313, Kaisari Kostantino hakukawia kutangaza uhuru wa kanisa kwa “Tangazo la Milano”.Basi Wakristu walipata uhuru uleule wa dini kama wapagani.Walirudishiwa makanisa na mali waliyokuwa wamenyimwa wakati wa udhalimu.Kaisari alitangaza pia jumapili iadhimishwe kama “Siku ya Bwana”, na watu wakumbuke ufufuko wa Kristu wala wasifanye kazi.

                  Katika maelezo hayo yote  ni wazi kwamba kuanzishwa kwa Ibada ya jumapili, kusudi lake na hata muanzilishi wake havitokani na Biblia bali ni sababu za kibinadam. Kostantino alikuwa mpagani muabudu jua, na alipokuwa kaisari aliongoka kiuongo alitaka kupata waumini wa kipagani na kikristo . Kwa hitaji lake aliona njia pekee ya kuwavuta ni kuchanganya ukristo na upagani.
                  Mchanganyiko huu ulikamilika pale alipoanzisha ibada katika siku ya wapagani ya kuabudu mungu jua (Sun day-sunday/siku ya jua), kwa kuagiza watu wafanye pumziko la sabato aliyoihamisha kinyume na maagizo ya Mungu, kwa kufanya hivyo aliwapata Wakristo na wapagani na kuanzisha Romani Katoliki . Wkristo wasalio Jumapili hufuata amri yakanisa la Roman Catholic kama tutakavyoona.Sababu kwamba Wakristo wafanye Ibada kukumbuka ufufuo wa Yesu si ya kibiblia .Hata yesu mwenyewe hakusema wakristo wafanye ibada siku ya kwanza ya juma wakikumbuka ufufuo wake.
                  Ilipofika mwaka 1234 A.D . Papa glegory IX aliidhinisha rasmi mapumziko ya siku ya jumapili.
Biblia ilitabiri kuja kwa Uvunjwaji wa sabato
                  2 Wathesolanike 2:3,4. Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu,  akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu. 4 yule mpinzani ajiinuaye juu ya kile kiitwacho Mungu...
                  Japokuwa fungu hili linamaana nyingine kubwa ila kwa sehemu linazungumzia kitendo cha waanzilishi wa kanisa la Roman catholic walivyobadili sheria ya mungu toka sabato hadi jumapili, hapa walivunja amri ya 4 katika amri 10 za Kutoka 20:8->.Danieli 7:10 Inaitaja dola ya rumi kama pembe iliyoinuka na kunena maneno makuu (Kufuru) neno ambalo pamoja na maana yake kubwa ni kuchukua cheo cha mungu kwa kubadili alichoagiza (Utunzaji wa sabato) na kuweka agizo la kibinadam. (ibada ya Jumapili).

Wakristo wote wasaliojumapili hufuata amri ya Roma si ya Mungu
                              Hebu tuone kauli za baadhi ya maandishi ya Roman Catholic kuhusu wakristo watunzao jumapili:-
1)      Nithibitishie katika bibliapekee kwamba napaswa kuadhimisha jumapili kama siku takatifu.Hakuna sheria kama hiyo katika Biblia.Ni sheria ya kanisa takatifu la Romani Katoliki pekee. Biblia inasema 'Ikumbuke siku ya sabato uitakase.' Kanisa Katoliki linasema, Hapana. Kwa mamlaka yangu tukufu naiondoa sabato na kukuagiza wewe utunze siku ya kwanza ya juma. Na kumbe, Ulimwengu wote uliostaarabika unasujudu kwa kicho ukitii amri ya Kanisa Takatifu Katoliki. - Thomas Enright, CSRR , President, Redemptorist college (Roman Catholic) , Kansas City, MO.,February 18, 1884.
2)      Utunzaji wa jumapili kwa Waprotestanti ni gharama wailipayo, badala ya wao wenyewe, kwa mamlaka ya kanisa la Romani Katoliki. - Monsignor Louis Segur , Plain talk About the Protestantism of today (1868),p.213.
3)      Kama Waprotestanti wangefuata Biblia, wangepaswa kumuabudu Mungu katika siku ya Sabato (Jumamosi). Kwa kutunza jumapili wanafuata sheria ya Kanisa la Romani Katoliki.-Albert smith, Chancellor of the Archdiocese of Baltimore, replying for Cardinal in a letter of february 10, 1920.
4)      Waprotestanti...wanakubali Jumapili kuliko jumamosi kama siku ya ibada ya jumuiya baada ya Kanisa la Romani Katoliki kufanya mabadiliko...lakini akili za Waprotestanti hazionyeshi kutambua  kwamba...kwa kuitunza jumapili, wanakubali mamlaka ya mzungumzaji mkuu wa kanisa, Papa.-Our sunday Visitor, February 5, 1950.

                        Jumapili ni Chapa/Alama ya Romani Katoliki Duniani.                             
1)      Kwa kweli  Kanisa la Romani Katoliki  linasema kwamba badiliko (Kutoka Jumamosi hadi Jumapili) ni kazi yake.Na kitendo hicho ni CHAPA ya mamlaka yake ya kanisa na mamlaka katika mabo ya kidini.- C.F.Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons.
Onyo la Biblia
                  Ufunuo 14:9,10...Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama ( hapa anamaanisha Romani Katoliki) na sanam yake (jumapili ni sanam ya sabato iliyosimamishwa na Romani), na kuipokea chapa ,(Kuabudu jumapioli badala ya sabato) katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake. Eye naye atakunywa katika mvinyo wa ghadhabu ya Mungu uliotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji,katika kikombe cha hasira yake;naye atateswa kwa moto na kiberitimbele ya malaikawatakatifu,na mbele za mwana wa mungu.
                  Kama Yesu mwenyewe alisema Sabato ni siku ya Bwana ni vyema kumfuata maana Yeye ndiye njia ya kweli na Uzima hakuna mtu awezae kumfuata Baba bila kupitia yeye, utajisikiaje kushika kweli zote za Biblia halafu kwa kupuuzia sabato ambayo Mungu ameamuru uitunze ukashindwa kuirithi Mbingu. Kila tufanyalo duniani hutuandaa kuwa watahiniwa wa kuirithi Mbingu, Ibada mbinguni hufanyika na itaendelea kufanyika siku ya sabato. Isaya 66:22,23.Biblia inaonyesha kuwa sabato hata sabato wanadam wote watakaoirithi Mbingu wataenda kuabudu mbele za Bwana.

MUNGU HUTAMBUA MATENGENEZO YA IBADA  SIKU ZA MWISHO NI UTUNZAJI WA SABATO.
Ufunuo 14: 6,7. Kisha nikaona malaika mwingine ,akiruka katikati ya mbingu, mwenye injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa nakabila na  lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu ,Mcheni mungu, na kumtukuza , kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
 Biblia inaposema tumsujudie yeye  aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.. Hutupeleka katika amri ya nne (Kutoka 20:8-). Ambayo hutuonyesha tusalipo katika siku ya sabato tunaonyesha kwamba tunamtambua mungu kama Muumbaji, watu wasalio jumapili huungana na Darwin mwanasayansi apingaye uumbaji, Wanadam wote wangekuwa watunzaji wa sabato (Birthday) ya uumbaji wasingesahau kuwa tumeumbwa na mungu.
                             
                  Sabato ni muhuri chapa ya MUNGU, kwani amri ya 4, jina (maana kwa siku sita mungu…) , hutaja cheo (…Mungu aliziumba mbingu na nchi na bahari..) na Mamlaka (ya mtoaji amri (Muumbaji). Amri ya nne hutia muhuri amri kumi na wote waitunzao hupigwa muhuri ili wasipigwe muhuri wa mrumi au Romani katoliki kwa kutunza jumapili. Utunzaji wa jumapili ni kupokea chapa ya 666 (VICARIUS FELEE DEI /makamu wa Mungu- Cheo cha papa ambacho hesabu yake huleta namba ya 666.) rumi inapanga kutimiza mpango huu kwa kuwalazimisha watu wote kusali jumapili kwasababu kwa kufanya hivyo watapokea chapa ya rumi.
                  Katika barua ya VATICAN CITY, TAARIFA YA MAENDELEO INAYOLENGA MWAKA 200.ROMA 20/02/199. TAARIFA NO.207.ILIYOFANYIKA MWAKA 1951 MWEZI WAKWANZA. Inanukuu hivi “Madhehebu yote hayana budi kuwa na siku moja ya ibada na hasa Jumapili, ambayo Roman Catholic iliipitisha kwa niaba ya Mungu kwa kubadili kuwa jumapili kutoka jumamosi…Kama biblia ndio mwongozo pekee wa mkristo. Waadventista wasabato wako sahihi kuitunza jumamosi pamoja na wayahudi.

                  Umeshaona ushahidi wa biblia na vitabu vingine ambavyo havikuandikwa na wasabato vinavyoonyesha kuwa kutunza jumapili kama siku ya ibada si agizo la biblia. Napenda ufahamu kuwa tatizo litakalofanya wengi wapotee ni kuabudu katika mfumo ambao kiasilia huwatendesha watu dhambi. Kusali jumapili ni mfumo ambao huwafanya watu waendelee kuvunja amri ya nne katika kutoka 20:8-.
                  Je kunausalama kuendelea kuvunja sheria ya mungu huku ukijua , fanya matengenezo.    Mungu anatambua kuwa wewe ni muumini mwaminifu kila upatapo ufunuo wa kweli yake, waweza kusema huokolewi kwa kuvunja sheria ya  Mungu bali kwa Neema. Kumbuka Sheria Hukuonyesha kuwa umefanya dhambi na Neema ya yesu (damu yake hukupa nafasi ya kufanya marekebisho). Amri ya nne inakuonyesha kuwa umevunja sabato , ukimjia Yesu anakupa nguvu ya kuitunza sabato na namna ya kuitunza.
Warumi 6:1,2.Tuseme nini basi?tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi. Hasha sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?

            Unachukua uamuzi gani baada ya kutambua kweli 100 za biblia kuhusu sabato ya BWANA , Je  msingi wa Imani yako unajengwa kwa kile kisemwacho na Biblia au Mapokeo (Romani Katoliki). Kama Kweli wataka imani yuako ijengwe katika kweli (Mwamba na sio mchanga) Ifuate Ibada inayoonyeshwa wazi na Biblia , IBADA YA SIKU YA SABATO, BWANA AKUBARIKI UFANYAPO MAAMUZI KWAAJILI YA UMILELE WAKO.




            Rejea.

            Bill Hughes, The Secret Terrorists
           
F.Potmann.(1999).Historia ya Kanisa Vipindi Vyake    Saba.Tanganyika Mission Press         Kipalapala

Mark Finley, (2005).The Next Super Power.Review and Herald publishing association

A.H.Lewis D.,A Critical History of the Sabath and The Sunday in the Christian Church

Ellen G White.The Great Controversy.

Ellen g White. Patriachs and Prophets.

Ellen g White .Testimornies for the church Vol


  Somo hili limeandaliwa na , Petro Tumaini.
Sim.+255712761605

SHETANI ATUMIAVYO MASTAA KUKUANDAA KWA MOTO WA MILELE.

Maburudisho tupatayo kupitia vyombo vya Habari hutumiwa sana na shetani
kuondoa hali ya matengenezo ya kiroho kwa Wakristo.
   
JIEPUSHE  NA UCHAWI WA BABELI
Mbinu za shetani kuua hali ya kiroho kupitia Maburudisho.
By Petro Tumaini.

lWafuasi wake hupatikana Jiji la malaika waliopotea (lossangeles) -Lost Angels.

lWana msukumo mkubwa kupitia vyombo vya habari.

lHufanya kazi kama wasanii nyota (mastaa).

lHawana tofauti na theluthi ya nyota (malaika wapotevu) waliotupwa pamoja na shetani kutoka mbinguni.


    Ufunuo 18: 23 . Wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala saauti ya Bwana harusi na bibi harusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa, maana hao wafanyabiashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.

SHETANI ameweka nguvu yake kubwa sana nyuma ya vyombo vya habari (Televisheni, Magazeti, Mikanda, Intaneti n.k) ili kuhakikisha anawaandaa watu kwa moto wa milele ambao Mungu ameuandaa kwaajili ya ibilisi na wale wanaomfuata. Hebu tuchunguze Biblia tuone imelizungumziaje suala hili.

Wanadam wengi hutumia sehemu kubwa ya maisha kwa kujishughulisha namaburudisho (entertainment).
· Vijana wengi hutegemea maburudisho kama vile;
     · Muziki.
     · Mpira.
     · Maigizo.
     · Riadha.n.k.
·Kwa madhumuni ya;
ØKufahamika
ØKupata hela
ØKuburudika
 Hebu tutazame kitabu cha Ufunuo wa Yohana, ambacho hukusanya kwa pamoja maneno ya Mbinguni, Duniani na hata yale ya shetani kikionyesha vita ya mwisho baina ya wema na uovu kikitumia picha halisi na alama,vitu vya kawaida na vya kiroho ili kutupatia ujumbe uliotoka kwa Mungu mwenyewe.
MADHUMUNI HAYA YAMEJENGWA KATIKA NENO LIITWALO UCHAWI, KAMA FUNGU LIFUATALO LIONYESHAVYO.
Ø Ufunuo 18:21-23. 21 Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe , kama vile jiwe kubwa ka kusagia, akalitupa katika bahari, akisema , kama hivi, kwa nguvu nyingi , utukufu wa Babeli, mji ule mkuu , wala hautaonekana tena kabisa. 22 Wala sauti ya wapiga vinanda na ya wapiga zumari, na ya waapiga filimbi, na ya wapiga baragumu , haitasikiwa ndani yako tena kabisa, wala fundi awaye yote hataonekana tena ndani yako kaabisa,wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa. 23 Wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala saauti ya bwana harusi na bibi harusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa, maana hao wafanyabiashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.
                                                                                               
KUNA MAMBO MAKUBWA MAWILI YA KUWEZA KUFAHAMU;
Ø Maana ya Babeli, ambayo inahusika kuondolewa utukufu.
ØMaana Uchawi , ambao kwa huo Babeli imedanganya mataifa yote.
MAANA YA BABELI
Ujenzi wa mnara wa babeli uliositishwa na mungu kule shinari, huwakilisha
machafuko yanayoletwa na shetani ili kupinga maagizo ya mungu.
ØMwanzo 11:2. Ikawa  watu waliposafiri wakaona nchi tambarare katika nchi ya Shinari, wakakaa huko.

Baada ya watu kuanzisha makazi wakaamua kujenga mnara mrefu sana kwa sabau kuu nyingi zikiwemu kubwa mbili zifuatazo.
(1) Kujiepusha na gharika endapo kama mungu angeleta gharika nyingine kama ile ya kipidi cha Nuhu.
(2)Kujitukuza nafsi.
(3)Wasipate kutawanyika usoni pa nchi.

Mungu akaingilia kati baada ya kuona jamii hii ya wanadamu wanataka kufanya yaliyo tofauti na mpango wake, akawachafulia lugha, wakashindwa kuendelea na ujenzi na hatimaye wakatawanyika usoni pa dunia kila watu kwa kadri walivyelewana kutokana na lugha zilizoibuka katika machafuko hayo.

ØMwanzo 11:9. Kwasababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipochafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi.
   
Kwahiyo maana ya babeli ni machafuko, watu wa babeli walipotawanyika usoni pa dunia walisanbaza dini ya upagani wa kuabudu miungu na kufanya yote yaliyo kinyume na maandiko. Tokea hapo Babeli ni dini ya  kupenda dunia ambayo na kumuacha Yesu Huleta uchawi wake ili iwapotoshe watu wote wa dunia hii endapo tu hawatajikita kwa Yesu Kristo, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.

Dini ifundishayo kuwa wanadam hawaokolewi kwa kushika sheria, mwaadam akifa rho inaendelea kuishi inajenga mnara wa mafunzo ambayo kupitia hayo inawadanganya watu kwamba wataokolewa lakini kiukweli watapotea kupitia mafundisho hayo.

MAANA YA NENO UCHAWI LILILOTUMIKA KATIKA UFUNUO 18:23.
  Neno uchawi katika fungu hili limetokana na neno la kigiriki Famacia ambalo kwa kiingereza pia ni Phamacy. Kwa kawaida famacy ni sehemu ambayo madawa huuzwa. Madawa  yatumikapo bila utaratibu huwa ni sumu na mengine hulewesha na kuharibu akili.
  Maana ya neno famacia ni kitu chochote kichanganyacho au kupumbaza akili na kufanya isiweze kutii au kufuata mapenzi ya Mungu au sheria yake.

KWA MUJIBU WA KICHWA CHA SOMO HILI WAWEZA KUJIULIZA MASWALI YAFUATAYO.
(1)Je Pombe yaweza kupumbaza akili isiweze kutii amri na maagizo ya mungu?
(2)Je televisheni yaweza kupumbaza akili isiweze kufuuata , kutii au kusoma neno la mungu?
(3)Je Mpira waeza kupumbaza akili isipate nafasi na mda wa kutafakari neno la mungu?
(4)Je muziki (hasa hasa wa kidunia) waweza kupumbaza akili isifuate , na kutii neno la Mungu

 Shetani ameweka hazina kubwa ya uchawi wake kupitia kiwanda cha maburudisho (Entertainment industry). Huu ndio uchawi anaotumia kuwapotosha mataifa na kwa namna moja au nyingine ndio utajwao na kitabu cha ufunuo . Kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako. 
   Tunapozungumzia Kiwanda cha maburudisho, tunazungumzia:
(1)Pombe.
(2)Muziki
(3)Michezo.
(4)Filamu
(5)Maigizo.n.k

  Haya yate hutimiza kile kinachoelezea neno Famacia au uchawi wa babeli ambao kwa huo shetani kuwafanya watu wapuuzie kusali, kusoma neno la Mungu, kulitafakari na hata mda wa kushuhudia kweli ya biblia.
Maana ya neno ENTERTAINMENT (maburudisho).
  Neno hili limejengwa na maneno matatu
(1)ENTER-Kuingia (coming in)
(2)TAIN- kumiliki (posses)
(3)MENT- kuendelea kumiliki.(Keep on the state of possesion)
 Kwa ujumla inamaanisha kuingia, kumiliki na kuendelea kuweka katika hali ya kumiliki. (coming in, posses and keep on the state of possesion.)

Je umewahi kutambua kwamba, kupitia entertainment industry (kiwanda cha maburudisho) ambayo mengi ni ya kidunia shetani huingia akilini mwako, hukumiliki na kuendelea kukumiliki kifikra?”

Waebrania 13:1, 2. 1 Upendano wa ndugu na udumu. 2 Msisahau kuwafadhili (entertain) wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika bila kujua.

Kama inawezekana kuwakaribisha (entertain) malaika wa nuru  yaani waingie, kumiliki na kuweka katika hali ya kumiliki nyumba zetu na akili zetu. Je si rahisis zaidi kuwakaribisha malaika waovu nao wafanye makao yao majumbani kwetu na akilini mwetu kupitia maburudisho tunayoyapendelea?

“Ukijishughukisha na maburudisho ya kiroho/kikristo (spiritual entertainment) utakuwa makao ya Roho wa Mungu, vivyo hivyo ukijishughulisha na maburudisho ya kidunia (wordly entertainment) utakuwa makao ya shetani.”
  Ni kwa namna hii Ufunuo 18:23 inatoa kifungu cha maneno Kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako (entertainment). 
  Shetani ametupofusha akili tushindwe kuelewa kina
cha uchawi uzungumziwao na Biblia kwa kutupatia dhana finyu, yaani kila tusikiapo neno uchawi tuwaze tu watu wanaowanga usiku, waganga wa kienyeji wapigao ramli.

   “Laiti kama tungejua shetani hutuloga na kutupotosha kwas uchawi wake (famacia) kupitia kiwanda cha maburudisho (entertainment), tungegesali kuliko kawaida.”
   Katika Biblia wapo watu wsaliojioepusha na uchawi huu na hatimaye walichukuliwa kwenda Mbinguni kama henoko.
   Henoko (Mwanzo 5:21-23), alitembea na Mungu kwa muda wa miaka mia tatu. Yaani alimtafakari mungu na mabo ya kimbingu, hakutumia mda wake kwa kuijazaakili na mabo ya dunia, hatimaye Mungu akaamua kumchukua mbinguni.

Wale wajiitao mastaa katika entertainment indusry ni wakala wa Malaika wa Shetani waliotupwa toka mbinguni.
Ufunuo 12: 9, 4. 9 Yule joka akatupwa, yule mkkubwa , nyoka wa zamani, aitwae Ibilisi na Shetani, audanganyae ulimwengu wote , akatupwa hata nchi na malaika zake pamoja nae. 4 Na mkia wake ukakokota theluthi ya nyota za Mbinguni, na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
Baada ya kuleta uasi wa kutaka kufanana na Mungu
Malaika mkuu Lusifa (kwa sasa ni shetani) alitupwa
na theluthi ya malaika waliofuata uongo wake.
Ni nini kilichomfanya Shetani na theluthi ya nyota (malaika) watupwe.
Ukisoma Isaya 14 utagundua yafuatayo.

(1)Alitaka kuwa kama Mungu.
(2)Aliwashawishi malaika wamuunge mkono akimshutumu mungu kama dikteta.
(3)Alitaka kuwa zaidi ya mungu, yaani alitaka kuwa maarufu (famous) kuliko Mungu.
   Kwa kadri Muda ulivyozidi kwenda uongo wa shetani ulijulikana akatupwa kutoka mbinguni na kuhamishia mashambulizi yake duniani.
   Alipofika duniani alimdanganya Hawa kwa kutumia medium (mfumo) wa nyoka, leo hii hutumia media (mass media) yaani vyombo vya habari kwa ujumla.
  Wafuasi wa shetani ambao kwa sehemu kubwa hutumia media (mass media) vyombo vya habari nao hufanya kazi wakiongozwa na madhumuni hayo hayo ya kutaka kuwa maarufu, na kuwaburudisha (entertain) watu.
  Wanafanya kazi ya kuwahimiza watu nao waitwe nyota (mastaa), na hivyo si kazi kuona matokeo ya kazi zao. Ukiona mtu anafanya kazi akidhamiria kuwa staa, kuwa maarufu ni msukumo uleule wa shetani.
Watu wafanyao kazi kwa madhumuni ya kuwa masupastaa kama wale wa mieleka
huongozwa na roho ya kujikweza iliyomfanya shetani atupwe kutoka mbinguni.
Mungu hajaagiza ufanye kazi kwa mashindano Wafilipi 2

  Ndiyo maana tuna mastaa wa aina nyingi;
(1)Mastaa wa filamu.
(2)Mastaa wa mpira.
(3)Mastaa wa ngumi.
(4)Mastaa wamuziki.
(5)Mastaa wa michezo mbali mbali.
   Siku kwa siku tunaabudu mastaa bila kujua na wakati mwingine tunajua, na kiukweli kupitia maburudisho shetani huwatumia kutu entertain ( kuingia, kutumiliki ,na kutuweka katika hali ya kutumiliki.)
   baada ya siku chache tunajikuta.
(1)Tunaongea kama mastaa.
(2)Tunatembea kama mastaa.
(3)Tunavaa kama mastaa. Mabinti huvaa vimini kwasababu ya msukumo wa mastaa, vijana huvaa milege kwasababu ya msukumo wa mastaa. Huu ndiyo uchawi wa Babeli ufanyavyo kazi.                                                        

   “Mahali walipoweka ngome malaika wa shetani (NYOTA. Ufunuo 12:4  Na mkia wake ukakokota theluthi ya nyota za Mbinguni...”)
   Bila shaka theluthi hii ya malaika hupatikana mahali ambapo ngome ya mastaa (nyota) wa maburudisho duniani hupatikana. Na sehemu hii Hujulikana kama Hollywood hasa katika jiji la Losangeles lililoko  California. Hapa ndipo wapatikanapo mastaa wa movies na maburudisho ya aina zote duniani , tena hutumia media kuwafikia mashabiki wao.
   Majina tu ya sehemu hizo yanadhihirisha kuwa hizo ni ngome za sheta. HOLLYWOOD, LOSANGELES. Je umewahi kutafakari maana ya majina haya.
   HOLYWOOD, jina hili limetokana na jina HOLLY TREE mojawapo ya miti ya nguvu za giza na ulikuwa na matunda ya kuvutia ambayo ni sumu , ulikuwa ikitumika kuwafanya watu wafikie kifo bilo tabu.
   Je haiwezekani pia kupitia hiollywood shetani huwaloga watu kwa uchawi wa wanamaburudisho kuwafanya watu wafe kiroho kwa kile wanachoshabikia au kutazama kama kitu cha kuvutia na kupendeza ?

   LOSANGELES, jina la jiji hili waishio mastaa wakubwa wenye msukumo sana dunia nzima limetokana nna neno la kiingereza (LOST ANGELS) LIMAANISHALO MALAIKA WALIOPOTEA.

Hapa tunapata jambo moja la uhakika, malaika (nyota) waliodanganywa na shetani na hatimae kutupwa kutoka mbinguni pamoja na shetani hata kama si wote basi kwa sehemu kubwa sana waliangukia katika jiji hili lililoitwa kwa jina lao.(Loss angeles-lost angels au malaika waliopotea).

MAANENO YAONYESHAYO KAZI YA SHETANI KUPITIA MABURUDISHO
­
AMUSE

Kama litumikavyo katika filam likimaanisha kuonyesha mambo ya  kushangaza . Neno hili linamaanisha kudangaanya kwa kupindisha ukweli, bahati mbaya wengi hupenda kutazamba mambo ya kushangaza bila kutambua kuwa shetani  anawadanganya maana ni kanuni ya kazi zake.
Ufunuo 12:9. Yule Joka aaakatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwae Ibilisi na shetani, audanganyae ulimwengu wote, akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.
“Asilimia kubwa ya Filamu , vipindi na program zote zifuraishazo na kushangaza zimejengwa katika kanuni ya Uongo (yaana kanuni ya shetani)”
Maana ya CHANELLING

The ability to communicate with evil spirits through medium, (uwezo wa kuwasiliana na roho waovu/wachafu kupitia mfumo au chombo fulani).

Uwashapo TV ilkiyounganishwa na kebo, dishi (satelite), unakuta chaneli nyingi. Hapo shetani shetani ameweka mawasiliano yake kupitia chombo hicho ili unapoendelea kuchaneli japokuwa kuna baadhi ni za mabo ya Mungu. Tabia yake anaihamishia kwako kupitia chaneli mbaya uzitazamazo.
“By beholding we become changed ( Ellen G white), yaani anamaanisha kwa kutazama tunabadilishwa.”

“Kama tunavyobadilishwa kwa kumtazama Yesu, kwa kutazama chaneli za shetani tunafanana na shetani mwenyewe na ndo maana ana mawasiliano ya kula aina katika chaneli.”
lKuchochea ugomvi anachaneli ya ngumi
lKukuchochea uzini ana chaneli za Ngono “X”
lKuchochea kanuni ya kujikweza ana chaneli za Muzinki wa kidunia n.k.

KUPROGRAM (PROGRAMING)
   Ni kuendesha au kuunda kitu unavyo taka wewe, shetani pia hutuunda atakavyo kupitia program mbali mbali za TV, Redio, Intaneti n.k.

Remote control (Kuendesha kwa limonti)
   Neno hili tunalitumia sana tubadilidhapo program za redio na TV bila kuigusa tukitumia kifaa cha rimonti. Remote inamaanisha mbali.
   Shetani hutuendesha (control) bila sisi kujua maana hutumia mawakala ambao wako mbali (remote) hata yeye yuko mbali na hivyo si rahisi kujua kama huna Roho wa Mungu. Na hii ndiyo maana ya Remote Control kaatika uchawi wa shetani (Babeli).

   Matokeo yake tunaanza kufanya mambo ambayo hakuna aliyetwambia tufanye ila kwasababu tumevutiwa na program za shetani, na anatuendesha  tunajikuta tunafanya tu. Kuvuta sigara, kuivaa nguo fupi (Vimini).

 HIPNOSISI.
  
Maana ya neno hioli ni akili ya mtu mmoja kuendesha akili ya mtu mwingine haaatimmaye anayeendesha anajikuta anaenenda katika tabia na mtindo ambao si wake.
lMfano- Vijana wengi tokea utotoni huwa wanatenbea vizuri na kuongea vizuri lakini waanzapo kuangalia filamu za muziki na hata zile za kizungu wanaanza kuongea kizungu (what's up man,) na hata mwendo hubadilika na kuwa wa mdundo wengine kama wamevaa viatu vyenye spiringi.
   Akili zao zinaanza kuendeshwa na mastaa (malaika wa shetani) kwa hiyo kila kitu wanachofanya wanataka wawe mastaa.
Shetani hutumia muvi kutuhamisha kututawala fikra na
kutupotezea muda katika kutazama yasiyo na maana.

Muvi (Movie,Emotion)
  Emotion ni neno ka kiingereza litumikalo kuelezea mweneno wa mwanadamu. Movie inamaanasha kuhamisha na limetokana na neno move ambalo halina tofauti na e-motion.Hata neno Cinema limetokana na neno la Kigiriki Kinema limaanishalo kuhamisha (to move)
 “Shetani hutumia movie kutuhamiosha na kunadilisha miendendo(e-motion) kwa kutugeuza tabia”.

Wakolosai 1:23. Mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa  na kuliacha tumaini la injili mliyosikia habari zake...
  
Dhumuni la Mungu iu kwamba tusiondolewe klatika injili, dhumuni la shetani ni kutuondoa (move) katika injili.
 Msipogeuzwa
   Neno la Paulo msipogeuzwa limetokana na neno la kigiriki limaanishalo kuhamisha,, hata neno Sinema limetokana na neno Kinema-Kinein limaanishalo kuhamisha.
 
   Unapoangalia movie unahamishwa kutoka sehemu mojaa hadi nyingine, staa akiumizwa unaumia, akifurahi unafurahi, akitaka kuua unafurahia. Kwa njia hiyo shetani anmatubadilisha tofauti na mungu alivyokusudia kuwa tusibadilishwe kutoka katika tumaini letu la Kikristo.


Video Game zimejengwa katika kanuni ya ukatili ili kutuweka
katika hatia ya dhambi ya mauaji na chukui. 

VIDEO GAME
   Video game nyingi zimejengwa kaatika kanuni ya  hasisra na ukatili, yaani mauaji na ushindani. Kanuni hizi huunda tabiaa ya shetani.
lUkiua katika video game Mungu unahesabiwa na hatia ya mauaji. Dhambi haaihesabiwi hadi ufanyapo tendo bali huanzia katika fikra. Yesu alisema yeyote amtazamae Mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini nae.
“Shetani hucheza na fikra zetu ili ahakikishe kwamba kwa namna yoyote ziko katika hatia. Hata kipindi cha Nuhu fikra za wanadamu zilikuwa zimejaa dhambi ndo maana Mungu akaleta gharika.”
Mwanzo 6:5 . BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwaduniani na kwamba kila kusudi alilowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote . Soma pia Isaya 23:6

Muziki humiliki sehemu kubwa ya mawazo na tabia.

   TABIA NA MUZIKI
   TABIA HUUNDWA NA MAMBO MAWILI

lMawazo (feelings)
lMwenendo (Emotions)

MUZIKI HUUNDWA NA MABO MAWILI

lManeno- ambayo huelezea mawazo (feelings)
lMuziki-ambao huelezea mwenendo (emotions)

   “Muziki ni silaha kubwa atumiayo shetani kubadili tabia zetu, yaani kupitia muziki wa kidunia (blues, rnb, hip hop, bongo fleva, taarabu n.k) shetani hubadili mawazo yetu na mwenendo.”

   Muziki wa kidunia umeingizwa mpaka kanissani, siku hizi tuna muziki wa injili au disko la yesu , ikumbukwe kuwa shetani ana kanuni mooja kubwa sana ya kuwateka wakristo. Kila akitaka kuingiza kitu chake katika ukristi huongezea neno kristo mbele. Ndio maana zamani tulikuwa na disko sikuhizi tuna Disko la Yesu. Vitu vingi huvibadilisha kwa njia hii.
 

 DHUMUNI LA MUZIKI NI KUTUKUMBUSHA UTAKATIFU SI MABURUDISHO.

   Russano (2000) alisema, Muziki unamiliki kiwango cha maadili na unaweza kumuathiri msikilizajitabia na mwenendo... miziki unawakilisha shauku ya moyo kama vile hamasa, hasira, kiasi, na kinyume na hayo.
    Aliendelea kusema kuwa “muziki unaowakilisha shauku fulani pia unaamsha shauku hiyo kwa msikilizaji.aina mbaya ya muziki inakufanya uwe mtu mbaya na aina nzuri inakufanya uwe mtu mzuri.
 katika Karne ya 15 makanisa na wanafalsafa walikataa wazo kwamba muziki lazima ufurahiwe kwa jinsi unavyochezwa na sauti...bila kupinga uzuri wa sauti walisema...
      
      (1)Vitu vizuri vipo kutukumbusha juu ya utukufu na uzuri wa mungu.
(2)Siyo kufurahisha furaha binafsi.

Nyimbo nyingi tunazosikiliza kanisani hutufurahisha nafsi zetu na hazitukumbushi utukufu wa mungu hivyo tumetanga mbali na kusudi la mungu katika Muziki na kuingiza uchawi wa babeli (Machafuko kanisani).
 Muziki wa unaoingizwa katika makanisa mengi ya kikristo sasa umejengwa katika kanuni za kishetani.
(1)Mkazo mkubwa uko kwenye kucheza (kudansi) na sio kumsifu mungu katika heshima na kicho. Husababisha kujitukuza nafsi,
(2)Midundo huchochea msisimko nambao hufukuza uwepo wa malaika wa mungu.
(3)Makelele na fujo huondoa kabisa uwepo wa Mungu.
 
Shetani amefanya yote hayo kwasababu muziki ndiyo njia pekee ambayo binadamu anaweza kuitumia kuweka kumbu kumbu ya maneno na mawazo yoyote yale kwa kuyakariri.

Yawekana katika yote  haya umetambua kwamba wewe ni miongoni mwa waliokamatwa na uchawi wa babeli, usalama pekee ni kuachana na yote uonayo kwamba yatakupoteza na kumtazama Yesu tu.   Wakolosai 1:23. Mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa  na kuliacha tumaini la injili mliyosikia habari zake...

Kusudi la Yesu ni kumtazama Yeye pekee ili atubadilishe, kusudi la shetani ni kutugeuza pale tu tunapoacha kumtazama yesu na kutazama mambo ya dunia hii.

“Yeye ambaye macho yake humtazama Yesu tu ataacha yote, ataifia nafsi. Ataamini neno la Mungu kama lilivyo”

“Katika msalaba mvutano huishia pale na kutoka pale msukumo wote husambaa, nio kituo kikuu cha mvuto na kutoka hapo msukumo wote husambaa.



   Rejea
èBarnaba R. Hanning.(2000). Concise History of Western music.2nd Ed
èEllen g white, Counsels on Music.
èDVD - Escape From the Black Hole (Agujero Negro). 
èSDA Bible commentary .Vol 6,pg1113.

   
­