Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16

MUNGU ATABIRI ANGUKO LA SHETANI




Adam na hawa walijikuta katika uadui na Mungu baada ya kufuata
udanganyifu wa shetani badala ya kushikiia ahadi za Mungu





SHETANI APONDWA KICHWA
By Petro Tumaini.
Akiwa amefanikiwa kumdanganya Hawa na Hatimaye Adam, ni ndani ya muda mfupi tu uongo wake ulioneka wazi.Kifuatacho ni kiini cha uongo aliotamka shetani akimshawishi Eva kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya:-

Ø    Mwanzo 3:4. Nyoka akamwambia Mwanamke, Hakika hamtakufa

Baada ya  Eva kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya na hatimaye mumewe Adam kushawishika kula tunda hili kwa kumhurumia mkewe, kwa mara ya kwanza Mungu akatamka sentesi ya kifo ,kauli iliyoanika uongo wa ibilisi alioutumia akimshawishi Eva kula tunda alilokataza Mungu.

AKIDHIIRISHA UONGO WA IBILISI HIVI NDIVYO MUNGU ALIVYOSEMA
Ø    Mwanzo 3:19. Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini nutarudi.

Laana kubwa iliyoletwa na dhambi ni kifo, lakini ni dhumuni la shetani kuwadanganya wanadamu hasa katika siku hizi za mwisho kwamba watakapotenda dhambi hakika hawatakufa, kama alivyomdanganya Hawa .

Fundisho la kwanza ambalo kwalo shetani alilitumia kumdanganya Eva ndilo fundisho kuu atumialo kuwadanganya waumini wengi katika siku hizi za mwisho, nalo “Mwanadamu akifa rho yake huendelea kuishi”.Ili utambue kuwa fundisho hili limekubaliwa na jopo kubwa la jamii ya wanadamu ni rahisi tu hudhuria misiba mingi nawe utasikia kauli hii “Mungu ailaze pema roho ya marehemu”. Huu ni uongo usio na chembe ya ukweli ndani yake.

Ø    Mwanzo 3:4,5. Nyoka akamwambia mwanamke, hakika hamtakufa. Kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakapokula matunda ya mti huo,mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na Mabaya.

Udanganyifu wa shetani atumiao kuudanganya ulimwengu watu wa leo hauna tofauti na ule wa pale edeni, hujaribu kuonyeshadhambi kama kitu kizuri kana kwamba mtu atendapo dhambi anafumbuliwa macho na kuwa na uelewa mpana zaidi jambo ambalo si la ukweli.

Wakati huohuo humuweka Mungu katika sura ambayo humfanya aeleweke vibaya, na ndo maana alimwambia Eva kuwa Mungu kwa kuwakataza wasile mti wa ujuzi wa mema na mabaya aliwafumba macho, si jambo la kushangaza kuona leo vijana wakidanganyana kufanya uzinzi ili kupata maarifa ya ndoa na uzoefu wa maisha hayo.

Aidha shetani huwashawishi watu kunywa pombe ili kuchangamsha akili, kiukweli haya yote yanatudhihirishia kuwa historia inajirudia, Adam na Hawa walipokula tunda la ujuzi wa mema na mabaya walifumbuliwa macho na kuona mabo ya kusikitisha na kuumaza.

Hili lilidhiirisha kwamba Mungu hakuwa na nia mbaya alipowakataza wasile tunda la ujuzi wa mema na mabaya, kwanza walijitambua kuwa wako uchi. Utukufu wa Mungu uliowasitiri hapo mwanzo uliwatoka baada tu ya kutenda dhambi.

Wakati huo huo hofu na uoga uliwaingia, tofauti na walivyozoea kuzungumza na Mungu ana kwa ana hatimaye walianza kumkimbia mungu.

Baya zaidi ni Pale Mungu alipozungumza kwa mara ya kwanza sentensi ya kifo kwa wanadamu ambao alikusudia waishi milele katika maoisha ya furaha yasiyo na kifo, huzuni , uadui wala magonjwa.

Ø    Warumi  6:23. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

“Ikumbukwe kwamba lilikuwa ni kusudi la mungu mwanadamu aendelee kukua kiakili na kimwili endapo tu asingekubali kujiingiza katika mtego wa kutenda dhambi baada ya kushawishiwa na shetani.”

Kwa Kuwadanganya Adam na Hawa shetani alifanikiwa kuingiza laana ya kifo katika jamii ya wanadamu. Ni kama vile alionekana kupata ushindi juu ya wanadamu kwa kuwaweka chini ya laana hiyo kwa kuvunja maagizo na namri za Mungu ambazo ni ufunuo wa mapenzi yake na Msingi wa serikali yake Mbinguni.

MUNGU ATANGAZA VITA NA NAMNA YA KUPATA USHINDI.

Akizungumza laana ya dhambi juu ya Mwanamke, Mwanaume , Shetana na Ardhi katika kitabu cha MWanzo 3:13-19. Mungu alionyesha Tumaini la Pekee kwa wanadam ambao tayari walijiingiza katika laana ya dhambi ambayo ni kifo.

TUMAINI LILIONEKANA MUNGU ALIPOTANGAZA VITA KUU KATI YA  SHETANI NA KANISA LA MUNGU.


Shetani alipondwa kichwa (alimalizwa nguvu na kushindwa) kupitia kifo cha
Yesu pale msalabani.(Warumi 16:20)


Ø    Mwanzo 3:14,15. BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwasababu umefanya hayo,umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko Mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa nawe utamponda kisigino.

UADUI GANI ULITANGAZWA.

Ø    Bila shaka huu ni uadui kati ya nyoka ( Ibilisi ) na kanisa la Mungu (MWanamke.)

NI MBINU GANI ATUMIAYO SHETANI KATIKA VITA BAINA YAKE NA KANISA LA MUNGU?

Ø    KItabu cha Ufunuo wa Yohana kinatupa picha zaidi kuhusu nyoka na mbinu atumiayo kushinda vita.

NI UDANGANYIFU / UONGO
Ø    Ufunuo 3:9. Yule joka akatupwa, nyoka wa zamani ,aitwae Ibilisi na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.

Ø    Kanuni kuu aitumiayo shetani ni kudanganya, yani kila jambo aliloagiza Mungu yeye huwashawishi wanadamu kutenda kinyume, pale Edeni Mungu aliwaambia Adam na Hawa  wasile tunda la ujuzi wa mema na Mabaya shetani yeye akawaambia wale hatimaye walipo kula kwa njia hiyo shetani akapata ushindi wa mda mfupi.

KATIKA BIBLIA MWANAMKE HUWAKILISHA NINI?

Ø    Waefeso 5:22,23. Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana Mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.


Ø    Kwahiyo hii ni vita baina ya shetani na kanisa la Mungu, kwa kuwa Mpaka kiipindi hiki kanisa la Mungu lilisha ingia katika laana ya dhambi kwa kukutwa na kifo Mungu alitengeneza mpango wa kuweza kumponda shetani kwa kuleta Mkombozi ambaye katika Mwanzo 3:15 ametajwa kama uzao wa mwanamke.


Ø    Ufunuo 12:11, Nao wakamshinda kwa kwa Damu ya Mwana- Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.


Ø    Sheria ya Mungu iliyovunjwas pale edeni ni takatifu kama Mungu aliyeitoa kwa hiyo kiumbe kilichopaswa kuja kufanya ukombozi ni lazima kiwe na hali ya Uungu, ndiyo maana mungu alimtuma Yesu kuja kufanya ukombozi hakutuma viumbe wengine walioko mbinguni kama vile malaika.


Ø    Mungu ameliahidi kanisa lake kumshinda Ibilisi kwanza kwa  DAMU YA MWANA KONDOO  , halafu  na kwa NENO LA USHUHUDA WAO.


Ø    Ni kupitia kifo cha Yesu pale msalabani, mwanadamu anapomwamini Yeye na kupmpokea anajiweka katika mpango wa kurejeshewa uzima wa milele hapa ndipo Mwananamu au wanadamu wanaounda kanisa la Mungu wanamshinda Ibilisi kwa DAMU YA MWANAKONDOO ..


Ø    Yohana 3;16. Kwa maana jinsi hii Mungu alliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.     


Ø    Yesu ni mwanakondoo aliyemwaga damu kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu wote.


Ø    Yohana 1:36. Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama Mwana-konoo wa Mungu.

NENO LA USHUHUDA WAO

Ø     Ufunuo 12:11 imetaja kitu kingine kinachofanya kanisa la Mungu kumshinda Ibilisi nacho ni NENO LA USHUHUDA WAO , tena fungu la mbele limeenda mbali zaidi


Ø     Ufunuo 12:17.Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao Amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.


Ø     Ushuda wao, au ushuhuda wa Yesu ni Maandiko matakatifu ( Biblia) kwasababu hiyo ndiyo imuonyeshayo mwanadamu yeyote ukombozi.Wanadamu wanateseka tu kwasababu hawajamjua Yesu, wanadamu hawajamjua Yesu kwasababu hawayajayajua maandiko eidha kwa kuyasoma au kufundishwa.


Ø    Akiongea na mafurisayo ambao walikuwa wachunguzaji wazuri sana wa maandiko Yesu alisema maneno yafuatayo.


Ø    Yohana  5:39. Mwayachunguza maandiko , kwasababu mnadhani ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.


Ø    Hata Nabii Yohana katika kitabu ncha ufunuo alifunuliwa zaidi na mjumbe kutoka Mbunguni kuhusu maana ushuhuda wa Yesu


Ø    Ufunuo 19:10, Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudu; akaniambia, angalia ,usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie  Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio Roho ya unabii.



POTE KATIKA BIBLIA TOKEA MWANZO MPAKA UFUNUO MAANDIKO MATAKATIFU HUMSHUUDIA YESU AMBAYE KWA KIFO CHAKE ALIMPONDA SHETANI KICHWA NA  KUFUMBUA FUMBO LA MAUTI

Ø    Jambo baya na la kusikitisha zaidi ni mbinu atumiayo shetani  ambayo ni kufundisha maandiko nusunusu, hawafundishi wanadamu kuzishika amari za Mungu kwasababu Uadui wake upo dhidi ya kanisa lizishikazo amri za Mungu na kuwa na Imani ya Yesui.


Ø    Waweza kudhani kwamba mtu yeyote ashikae Biblia na kuhubiri ni mtumishi wa Mungu la hasha, hata shetani hutumia biblia lakini jhutumia vifungu vya bibilia kutetea hoja zake na siyo Biblia nzima ionyeshe uhalisia wa hoja mbali mbali.


Ø    Watumishi wa Mungu hutumia Mafungu na vitabu vya kutosha katika biblia ili kuonyesha msimamo wa maandiko kuhusiana na hoja mbalimbali badala ya kujetretea kwa kusimamia kifungu kimoja tu cha biblia.
 

 
KITAMBULISHO CHA  KANISA LA  MUNGU LINALOCHUKIWA NA SHETANI NI LILE LISHIKALO AMRI ZOTE KUMI ZA MUNGU NA KUWA NA IMANI YA YESU
Ø   Je wew ni miongoni kanisa la mungu lizishikazo amri kumi za mingu?
Ø   Je unasoma maandiko ili upate kujua mbinu za shetani katika vita hii ili umshinde?
Ø   Ili kuzijua amri kumi za Mungu soma Kutoka 20.Mungu akubariki.
Ø   Kwa ukweli zaidi tembelea kanisa lolote la WAADVENTISTA WASABATO LILILOPO JIRANI NA MAHALI UISHIPO.

Endelea kutembelea blog yetu upate kujua mengi zaidi…

Silaha kubwa ya vita ya shetani kuwaongoza wanadam kuvunja eidha
amri moja au zaidi katika amri kumi za Mungu.

No comments:

Post a Comment