KANUNI NANE ZA MAOMBI YAJIBIWAYO NA MUNGU
Petro Tumaini
Maombi ni silaha kubwa ya kutupatia ushindi katika vita iendeleayo baina ya wema na uovu. |
MUONGOZO KWA MAOMBI YANAYOJIBIWA NA MUNGU
ØMaombi ni nini?
ØKwanini wapaswa kusli kama Mungu amekusudia mema kwa kila mwanadam?
Ø Ni kanuni gani za kuzingatia ili maombi yako yajibiwe?
ØJe Mungu hujibu kila tumuombalo?
Endelea Kusoma jarida hili mpaka mwisho ili upate majibu ya maswali yote yaliyoorodheshwa hapo , Mungu akubariki unapoendelea kumtafuta kupitia maandiko matakatifu
DUKUDUKU kubwa ambalo huzuka kwa waKristo wafikiriapo upaji wa Mungu na jukumu la maombi katka mpango wa Mungu ni;
vKama Mungu amempangia mema kila mwanadam na mipango yake haibadiliki, Je kunahaja ya Kusali?
vKama maombi huleta matokeo kwa lolote litokealo basi inaweza kifikiriwa kwamba mapenzi ya Mungu hayakupangwa hapo mwanzo.
Ifahamike kwamba utoaji wa Mungu hutegemea sana na husukumwa na jinsi na namna mtu aombavyo.
vBiblia hufundisha kwamba mipango ya Mungu ni thabiti na haipo chini ya badiliko lolote.
vYakobo 5:16, inaatuonyesha na kutuhimiza kuomba “…kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana…”
KWANINI TUOMBE KAMA MIPANGO YA MUNGU NI THABITI.
Neno maombi limetiokana na neon la kiebrania tephillah, limaanishalo ombi au zaburi za kusifu, vile vile kwa kigiriki huitwa deeµsis, ikimaanisha “kusihi,” “ombi,” na proseuche, “ombi,” “ungano.” Muungano na Mungu huhusisha kisifu, shukrani na kusihi. Maombi hujengwa na Imani kwamba Mungu husikia, hujali, na ni “mtoaji kwa wale wamtafutao kwa bidii. (Waebrania 11:6). Hudumisha na kurejesha mahusiano na Mungu.
“Maombi ni pumzi ya nafsi hai…Maombi ni Mkono ambao kupitia huo m,wanadam hushikilia nguvu ya upendo wa Mungu usio na kifani.”(Gospel Workers uk, 254, 259.)
Mungu hufanya kazi katika ubia na mwanadam, Mungu hafanyi kitu kama mwanadamu hafanyi sehemu yake. Yesu alitembea katika miji ya Nazareti lakini si wanazareti wote walioponywa bali ni wale tu waliojinyenyekeza kwake kwa kuonyesha hitaji kwake na kuwa na imani. Katika miujiza na uponyaji wote alioufanya Yesu,imani ilihoitajika na imani hiyo ilikosekana Nazareti (Mathayo 14:22-23.)
Mungu amempangia mema kila mwanadam lakini mema hayo hayapatikani endapo mtu anakaa bila kuonyesha hitaji lolote, njia pekee ya kufikia mema ambayo Mungu anakusudia kila mwanadamu ayapate ni maombi .
Petro alimuomba Yesu kutembea juu ya maji na alitembea, kimsingi wanafunzi wote wa Yesu wangeweza kutembea juu ya maji lakini hawakuweza kwasababu hawakumwambia Yesu kuwa wanahitaji kutembea juu ya maji.
Mtumishi wa Akida aliponywa kwa sababu Akida alipeleka hitaji lake kwa Yesu (Mathayo 8:5-13), Binti aliyefariki alifufuliwa kwasababu mzazi wake alionyesha hitaji hilo na kuamini kwamba Yesu atamfufua (mathayo 9:18-22)
Mungu anapokusudia hitimisho (hasa katika maswala ya Uponyaji), pia hukusudia namna ya kutimiza kusudi hilo (kuonyesha hitaji la kuponywa jambo ambalo lahitaji imani.)Maombi hayabadili mpango wa Mungu bali hufanya kusudi la Mungu litimie. Maombi hutengeneza mazingira mazuri ya jinsi na namna tunavyofikiria mipango ya Mungu kwetu, kwa njia hiyo mhumuunganisha Mwanadamu na Mbingu wakati wote.
Maombi ni ufunguo wa mibaraka mingi ambayo Mungu amenuia kumpatia kila mwanaadamu, ni njia ya pekee ambayo mwanadamu hupata nafasi ya kufunua moyo wake kwa Mungu.
Ikumbukwe kwamba tunaposali tunavyotwa karibu zaidi na Mungu, Viumbe ambao hawajaanguka dhambini yaani malaika hujisikia kuwa karibu na Mungu mda wote wakimsujudu jambo ambalo ni msingi wa furaha yao, ni wazi kabisa kuwa malaika hushangaa sana waonapo wanadam wanakaa bila Roho matakatifu kwa njia ya maombi ya kudumu.
Giza na wimbi la dhambi huwa karibu sana na watu wote wapuuziaao maombi, bila maombi ya kudumu na mara kwa mara tunajiweka katika hatari ya kuiacha nuru na kutembea gizani.
MAMBO YATUTHIBITISHIAYO KUWA MUNGU ATAJIBU MAOMBI YETU
1)Wapaswa kukiri kuwa wahitaji msaada wa Mungu, wale wote wenye njaa na kiu ya haki ya kumtafuta Mungu Biblia inathibitisha kuwa watajibiwa. Moyo lazima uwe tayari kwa msukumo wa Roho wa Mungu tofauti na hapo maombi hayatajibiwa.
a.Isaya 44:3 . Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu;nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu ya utakao wazaa.
b.Hitaji letu ni kithibitisho tosha cha kumfanya Mungu atufungulie mibaraka tele.Mathayo 7:7.Ombeni, nanyi mtapewa;tafuteni, nanyi mtaona;bisheni; nanyi mtafunguliwa. Warumi 8.32,Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwaajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirfimia mambo yote pamoja naye?
2)Acha maisha ya dhambi ukishikilia dhambi yoyote uijuayo maishani mwako Mungu kamwe hatosikia maombi yeko lakini ukiungama na kuiacha kwa kumuendea Mungu kwa moyo uliopondeka maombi yeko yatasikiwa. Ni haki na damu ya Yesu pekee itupatiayo ukubali mbele za Mungu.
3) Kuwa na Imani, ni kipengele kingine muhimu sana kwa maombi yenye mafanikio.
a. Waebrania 11:6. Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
b. Marko 11;24. Kwasababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, amini ya kwamba mtayapokea, nayo yatakuwa Yenu. Ni udhihirisho kwetu kwamba Mungu hana mipaka kwa yeyote amjiae kwa imani, lakini kuna nyakati ambapo waweza kuomba halafu usipate majibu papo hapo jambo la kuzingatia ni kuendelea kudai ahadi za Mungu na kuwa mvumilivu. Wakati mwingine waweza kuomba jambo ambalo Mungu anaona si mbaraka kwako hivyo waweza usijibiwe na badala yake Mungu akakupatia linalokufaa zaidi. Mungu huzingatia muda kwa kila alifanyalo hivyo waweza kuomba jambo ambalo Mungu anaona si wakati wake kukupatia wewe endelea kudumu katika maombi saa na wakati utakapofika utajibiwa.
4)Kuwa mwepesi wa kuwasamehe waliokukosea, ukiwa na moyo mgumu kuwasamehe wale wakukoseao kumbuka kwamba unaweka kikwazo cha maombi yako kutokujibiwa. Kama upendavyo kusamehewa na Mungu vivyohivyo wapaswa kuwasamehe wote wakukoseao.
a.Mathayo 6:12. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
5)Uvumilivu, katika maombi hii ni kanuni ya pekee sana ya maombi yanayo jibiwa. Wapaswa kuwa mvumilivu kwa kuzingatia yafuatayo. Uvumilivu katika maombi hudhihirisha kwamba ombi lako ni la muhimu kwako kama lilivyo la muhimu kwa Mungu. Lakini pia si kila ombi lijibiwalo kama utarajiavyo katika 2 Cor 12:9-10 Paulo alimuomba Mungu amuondolee muiba uliomsumbua maishani mwake lakini Mungu hakujibu ombi hilo kwa faida ya Paulo.
a. Wapaswa kuwa mtu wa maombi na kudumu katika maombi huku ukitoa shukrani. Warumi 12:12. kwa Tumaini, mkifurahi; katika dhiki , mkisubiri; katika kusali mkidumu. Wakolosai 4:2. Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; 1 Petro 4:7 Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia ; basi iweni na akili, mkeshe katika sala. Wafilipi 4:6, Msijisumbue kwa neno lolote; Bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane kwa Mungu. Yuda 1: 20,21. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu, jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.
b.Maombi yasiyokoma ni muungaano usiovunjika kati ya roho na Mungu, ili kwamba uzima kutoka kwa Mungu ububujike katika maisha yetu, na kutoka katika maisha yetu usafi na utakatifu umrudie Mungu. Kuna umuhumu wa kudumu katika maombi, usiruhusu kitu chochote kikuzuie, fanya kila juhudi kudumisha mawasiliano kati ya moyo wako na Yesu Kristo…twapaswa kusali katika familia na juu ya yote tusipuuzie maombi ya siri kwasababu huu ndiyo uzima wa nafsi(SC, pg 98)
c.Kwa maombi ya moyoni Enoko alitembea na Mungu na kamwe shetani hakufanikiwa kumdanganya na kumwangusha katika hila zake kwasababu shetani hana nguvu kwa mtu ambaye moyo wake umeunganishwa na Mungu mda wote kwa njia ya maombi. Hakuna wakati ambao utashindwa kusali kwa Mungu wetu,iwe ni mitaani ,safarini na mahali popote pale ukiwa na hulka ya kuomba komoyomoyo utadumu katika muungano na Mungu siku zote.
6) Weka mahitaji yako, huzuni , furaha, dukuduku kwa Mungu na kamwe huwezi kumpa mzigo wala kumchosha.
a. Yakobo 5:11, Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri.Mmesikia subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya Kwamba Bwana ni mwingi wa rehema mwenye huruma . Hakuna ukurasa wa maisha wetu ambao ni mgumu kusomwa na Mungu na wala hakuna tatizo kubwa kwa yeye kushindwa kulitatua
7) Omba kwa jina la Yesu, hii ni kwasababu Yesu ndiye njia na kweli na uzima na hakuna mtu awezaye kwenda kwa Baba bila kupitia kwa Yesu. Yeye alimwakilisha Mungu hapa duniani na pia anamwakilisha kila mwanadamu mbinguni mbele ya Mungu Baba.
a.Yohana 16:26,27. Na siku ile matomba kwa jina langu, wala siwaambii ya kwamba mimi ntawaombea kwa Baba. Nalitoka kwa Baba nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba. Yohana 15:16. Si ninyi mlionichagua mimi ,bali ni mimi niliyewacahgua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda , na matunda yenu yapate kukaa, ili kwamba lolote mmwombalo baba kwa jina langu awapeni. Tuangaze macho yetu Mbinguni na kumtazama Yesu amabaye “Naye ,kwasababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote ili awaombee.(Waebrania 7:25.)
8)Mtukuze Mungu kwa wema aliokutendea na uwe mtu wa kutoa shukrani
a.Zaburi 107:8. Na wamshukuru BWANA , kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.
Kumbuka, maombi mengi huambatana na mafanikio mengi, maombi kidogo mafanukio kidogo , vilevile pasipo maombinb hakuna mafanikio. Mungu anahitaji kwamba kupitia somo hili awe amekufungua akili kutambua njia na ufunguo pekee wa mafaniko ambao yawezekana haukuujua hapo mwanzo, dumu katika maombi.
Rejea
Bob Pritchett & Kiernon Reiniger. (1991) SDA Bible Dictionary. Logos Research Systems Inc.USA
Bob Pritchett & Kiernon Reiniger. (1991)SDA Encyclopedia. Logos Research Systems Inc.USA
Millard J. Erickson.(1991) Christian Thology. Borker Book house Company Inc.USA
Ellen G White. (1893) Steps to christ. Review and Herald Inc USA
Ellen G White. (1915)Gospel Workers. Review and Herald Inc USA
No comments:
Post a Comment