Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16

KIKAO CHA SHETANI NA AGENDA ZAKE.

MUNGU AMEAMUA KUFICHUA SIRI ZA KIKAO CHA IBILISI ILI UOKOLEWE

MKUTANO WA SIRI WA SHETANI NA WAJUMBE WAKE
ADHAMIRIA KUKOMESHA WATAKATIFU ( WAKRISTO )  DUNIANI

  • MIKAKATI 12 YA KUUA UKRISTO YAJADILIWA.
  • WAKRISTO WASIOSHIKA AMRI KUMI WANASWA
JE UMEISHANASWA?
MWENDEE YESU KWA NJIA  YA TOBA NAYE ATAKUSAMEHE.
  
         Shetani aliitisha mkutano wake wa siri ambao wajumbe wake walihudhuria ili kufanya namna  ya kukomesha  kazi ya watakatifu duniani.Mkutano huu ulikua ni wasiri sana, nahakuna Malaika wa Mungu aliye ruhusiwa kusikia kinacho zungumziwa. Lakini Mungu alijua na akamutuma YESU  iliamtume malaika ambaye alimpa taarifa  mmoja wa wajumbe wa Mungu, nabii,Ellen  G.  White mwaka 1884.

 MIKAKATI 12 YA SHETANI DHIDI YA WATAKATIFU(WAKRISTO)
1.Kadri watu wa Mungu wanavyokaribia dhoruba kuu ya siku za mwisho, Shetani anaitisha mashauri nyeti na malaika wake ilikuweka mipango ya mafanikio zaidi ilikupindua imani zao. Anaona kwamba makanisa  mashuhuri yanayopendwa na watu  tayari yameshalala kutokana na nguvu ya udanganyifu wake. Kwa mbinu ya vivutio na kuyatia kwenye miujiza anaweza kuyafanya yaendelee chini ya utawala wake, kwahiyo anawaelekeza malaika wake waweke mitego yao hasa kwa wale wanao tazamia kurudi kwa  Yesu mara ya pili, kuwaharibu ili wasiweze kuzitunza amri zote za Mungu.


2.Alisema mdanganyifu  mkuu huyo,“Lazima tuwachunge sana walewanao waita nakuwavuta watu kwa sabatoya yehova. Watawaongoza wengi waweze kuona umuhimu wa sheria ya Mungu; nakwa nuru hiyo, inayofunua sabato ya kweli, inafunua pia huduma ya kristo yapatakatifu Mbingini, na kuonyesha kuwa kazi ya mwisho ya wokovu wa mwanadamu inasonga mbele. Shikilieni mawazo ya watu gizani hadi kazi imalizike, natutawaletea mambo ya dunia na kanisa tuyachanganye pamoja pia."


3.Sabato ndio swala kuu  litaloamua  mwelekeo wa  roho za watu . lazima tuitie nguvu ibada ya kuabudu jumapili tulioianzisha  tuliyoianzisha. Tumefanya ipokelewe na watu wa dunia na washiriki wa kanisa ; sasa kanisa lazima . lielekeze kuungana na   dunia kwa kupewa misaada . Ni lazima tufanye kazi kwa kutumia ishara na miujiza ili tuyafumbe   macho yao  juu ya   ukweli ,na tuwavute ili waachane na maswali juu ya ukweli na wasimwogope Mungu ili wafuate mila na desturi

4.Nitawatumia wachungaji mashuhuri wenye mvuto   ili  waupindue mvuto wa wasikilizaji wao   ili  kuwatoa kwenye  amri za Mungu .mahali ambapo maandiko matakakatifu yanaikiri sheria kamili ya uhuru itaonyeshwa kama ni nira ya utumwa. Watu wanayapokea maelezo ya maandiko matakatifu yanayotafsiriwa na wachungaji wao , na huwa hawasomi ili kuchunguza wenyewe. Kwa hiyo kwa kutumia wachungaji nita watawala watu kama nipendavyo .

5"Lakini hasa , kusudi letu kuu ni kulinyamazisha dhehebu hili la watunza sabato. Lazima tuanzishe chuki kuu kinyume chao tutawatafuta watu mashuhuri na wenye hekima  ili  wawe upande wetu ;  halafu na kuwapitisha ili wawe na madaraka ili waweze kutekeleza makusudi yetu ndipo ibada ya jumapili niliyoianzisha italazimiswa kwa sheria zilizokali na zilizokazwa .Wale watakao zivunja watafukuzwa watoke katika miji, navijiji na kuwafanya wateseke kwa njaa na umaskini . Mara tutakaposhika madaraka tutawaonyesha jinsi ya kuwatenda wale ambao watakuwa bado hawajakana utiifu wa kanuni za Mungu. Tumelitumia kanisa la Rumi kuwa kamata na kuwafunga, kuwatesa na kuwauwa wale waliyokataa kujisalimisha chini ya sheria zake, na sasa  tunayaleta makanisa ya kiprotestant  yafanane na dunia, maana huu ndiyo mkono wetu ; Wakulia wenye nguvu mwishoni tutaweka sheria ya kuwaangamiza wale wote watakaokataa kujisalimisha chini ya mamlakan yetu. Wakati adhabu ya kifo itakapoitishwa  kwa watakaoivunja sheria ya kuabudu jumapili tulioianzisha , ndipo wengi walio katika  nyadhifa  za washikao amri watakimbilia upande wetu .

6."Lakini kabla hatujachukua hatua kali hizo, lazima tutumie hekima  ya juu kuwadanganya na kuwanasa wale wanaoitunza sabato ya kweli. Tunaweza kuwatenga wengi kutoka kwa kristo ikiwa tutawaletea mambo ya kidunia , tamaa na majivuno. Watajidhania    wenyewe wako salama kwasababu wanaamini ukweli  kwakuzama katika  tama ya uchu wa kula na misisimko vitawachanganya ili wasiweze kupambanua na kuharibu uchaguzi mzuri na ndipo wengi tutawasababisha waanguke

7."Nendeni wafanyeni wale waliona fedha na mashamba walewe na masumbuko ya maisha yao. Wapatieni dunia iwe kitu chenye nuru ya kuvutia    zaidi ili waweze  kuleta hazina zao hapa , na waweze kukaza makusudi yao juu ya vitu vyakidunia tu.lazima tuwa chunge kwa hali zote wale wanaomtumikia mungu ili  wasiwe na mali yoyote  itakayosaidia kuwapatia njia kinyume chetu .Ziwekeni fedha mikononi mwa watu wakubwa walio upande wetu.  Kadri wanavyopata  mali zaidi na ndivyo watakavyo uharibu ufalme wetu kwa  kutuchukulia watu na vitu vyetu . wafanyeni wapende fedha zaidi ya kuujenga ufalme wa kristo na kueneza ukweli ambao tunauchukia, nahatuhitaji kuogopa mvuto wao ; maana     kila mbinafsi mchoyo ataanguka chni ya nguvu zetu , na hatimaye atatengwa na watu wa Mungu.

8.Wale waliomfano wa utauwa , lakini hawajui nguvu zozote za Mungu, tunaweza kuwatumia wengi ili walete madhara makubwa kwa adui zetu. Wapenda anasa kuliko kumpenda mungu , hawa ni wasaidizi wetu mashuhuri kuliko wote hawa waliomo kwenye kundi hili tuta watumia kama vibaraka wetu ,  maana wana akili na hekima ili kuwavuta wenzao waangukie mitego yetu. Wengi hawataogopa mvuto wao kwasababu wanaiamini na kushiriki imani moja ndipo tutakapowavuta wengi waamini na kuamini kuwa sheria za kristo sio ngumu kulingana na  mafundisho waliyofundiswa hapo mwanzo na kwa kufanana na dunia watawajaza makanisa  mvuto mkuu wa mambo ya kidunia . Ndvyo watakavyo tengana na kristo na hapo hawatakuwa na nguvu za kupingana na nguvu zetu , na hatimaye watakuwa tayari kurudia  udhaifu walioukuwa nao zamani na kuto kuomba

9.Hapo ndipo tutakapotia pigo letu la mwisho; juhudi zetu za kupambana na washikao sheria zifanywe bila kuchoka. Lazima tuhudhulie mikutano yao inapokusanyika.Hasa katika mikutano mikubwa itasababisha hasara sana kwetu, na lazima tupeleke upinzani mkubwa, na tuweke mambo yatakayozuia  roho zao zisiusikie ukweli utakao wavutia.

10.Nitajipatia watu wawe ni watumishi wangu wa siri, wale walio tayari kupokea mafundisho ya uongo na ukweli wa kutosha, wauchanganye ili kuzidanganya roho za watu. Pia nitawatumia watu wasio amini miongoni mwao wawe pale, watakao elezea na kuleta mashaka juu ya ujumbe wa Bwana wenye onyo kwa kanisa lake. Kama watu watasoma na kuamini maonyo hayo basi tutakuwa na matumaini kidogo sana ya kuwashinda. Kama tutaupindua mvuto wao wasifuatilie maonyo haya watabaki kwenye giza la nguvu zetu za ujinga na kutoamini na hatimaye tutawapatia nafasi na vyeo vyetu mwishowe.

11.Mungu hataruhusu maneno yake kuchanganywa na takataka kama tutazivuta roho za watu gizani, baada ya muda Fulani, rehema ya Mungu itawaacha na hapo ndipo atatuachia uwezo kamili ili tuwatawale.

12. Lazima tusababishe ugomvi na mgawanyiko. Lazima taharibu ile kiu ya kupenda mambo ya kiroho, ili tuwafanye wawe wabishi, wagomvi, kushitakiana na kuhukumina ili wadumishe uchoyo na uadui. Na dhambi hizo Mungu alitufukuza mbele zake na wote watakao fuata mfano wetu yatawapata yaleyale yaliyo tupata.




Rejea :
Ellen. G . White, Testimonies to Ministers uk  472 – 475
Spirit of Prophecy, volume 4, 1884, uk 337-340
The great  Controversy, 1884 Sura ya 27 uk 337- 340.

Imeandaliwa na George  Masambu
george.joseph45@yahoo.com
+255759366966 au +255719048480