Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16

BIBLIA IZUNGUMZIAVYO NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KATISA NA UTUME.

KWANINI TUNACHAGUA WAZEE WA KANISA WA KIUME TU, HATUCHAGUI NA WA KIKE.
By Petro Tumaini

Ofisi ya kanisa la agano jipya inataja vyeo vikubwa viwili vya uongozi wa kanisa amabavyo ni mashemasi na wazee wa kanisa. Umuhimu wa ofisi hizi unaelezewa kwa kiwango cha hali ya juu ya kiroho na kimaadili kwa wale watakiwao kushikilia nafasi hizi.

Kanisa linatambua utakatifu kwa  wito wa utume huu kwa kuwekea mikono na ndiyo maana baada ya kanisa la Mitume kuanzishwa na kupata viongozi ambao ni Stefano, Filipo, Prokoro, Nikanori , Timothi, Parmena, na Nikolao  waliwekewa mikono .
Tokea agano la kale Mungu aliwaweka wakfu wanaume waweze kufanya kazi katika Hekalu lake takatifu, lakini bado kuna kazi za kiroho zilifanywa na wa wanawake kama vile kazi ya nabii.

Mwanamke aliumbwa kama msaidizi (ezer-help) hii humaanisha mtendakazi pamoja na mwanaume wa Mwanaume na si wa kukanyagwa.

Jambo hili halikumtenga na shughuli za kanisa, japokuwa kunashughuli zilizofanywa na wanaume tu hekaluni na kanisani kama tutakavyoona, lakini hebu tuangalie shughuli walizoshiriki wanawake tokea agano la kale.

Nafasi ya Mwanamke kanisani
ØNabii.Wanawake walishiriki katika nafasi ya kuzungumza na Mungu tokea agano la kale hadi Jipya (Manabii)

ØMiriam

Kutoka 15:20. Na Miriam Nabii mke Ndugu yake Haruni, , akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.

ØDebora
Waamuzi 4:4. Basi Debora, nabii mke , mkewe  Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.

ØMke wa Isaya

Isaya 8:3. Nami nikamwendea Huyo nabii Mke, naye akapata miimba, akazaa motto mwanamume. Kisha nikamwambia Mwite jina lake Maher- Shalal-Hash-Bazi.

ØWatoto wa Filipo

MAtendo 21:9. Mtu huyu alikuwa na binti wane, mabikira waliokuwa wakitabiri.(whp prophesized NKJV)

ØKatika huduma (Ibada) .
Wao walifika kusikiliza tu neno la Mungu.
ØNehemia 8:2-3

Ø    Muziki

ØKutoka 15:20-21

Ø1 Nyakati 25:5




Wakati wowote tokea anguko mwananamke aliwekwa kuwa chini ya mwanaume , ni kusudi la Mungu mwanamke atawaliwe ,na mdiyo maana katika Biblia mwanamke aliyetaka kumtawala mwanaume ilikuwa ni hukumu.

ØIsaya 3:12. Katika habari za watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.


Kwa kifupi ,majuikumu ya mwanamke tokea dhambi iingie,  dhambi iliingilia kupitia kwake- vilevile mkombozi alizaliwa kupitia mwanamke mwaminifumwaminifu - huyo pia alishiriki katika kuomba ujio wa Roho mtakatifu matendo 1:13-14, Lidya alimkarimu Paulo Mdo 16:14, mwongofu wa Kwanza Ulaya ni mwanamke .

Paulo alipopata maono kumwendea mtu wa mataifa alikuta wanawake wakisali, kwahiyo tokea agano la kale hadi agano jipya wanawake wameshiriki kikamilifu katika huduma za kanisa na ukombozi .

Pamoja na hayo yote bado kuna mipaka ya huduma za wanawake katika kanisa. Kwa mfano Paulo na wazee wenzake walisaidiwa na wanawake katika huduma, hii haimaanishi kwamba wanawake walichukua vyeo vya wazee hao.

ØWarumi 16:6. Nisalimieni Mariamu, aliyejitaabisha sana kwaajili yetu.

ØWarumi 16:3 Nisalimieni Prisca na akila, watenda kazi pamoja nami katika kristo Yesu.

ØWarumi 16:1-2. Namkabidhi kwenu Fibi, ndugu yetu, ndiye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea. Neno mhudumu lililotumika hapa limetokana na neon DEACENESS ambaye ni mtumishi wa kawaida wa kanisa yaani shemasi.


Shughuli Zilizofanywa na wanaume tu
Ø    Ukuhani.
Ø Hesabu 28:1 Nawe umlete Haruni ndugu yakokaribu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Haruni na Nadabu, na Abihu, na Eliazari, na Ithamari, wana wa Haruni.  Mafungu Mengine kuhusu kazi hii ni Hesabu 18:1-7.

ØWazee (maaskofu)

Ni wazee waliowahi kuhudumu kama waamuzi, viongozi wa familia

Matendo 6:6. ambao akawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.

Matendo 13:2,3. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwna ibada na kufunga, Roho Mtakatifu  akasema , Nileteeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba , wakaweka mikono yao juu yao , wakawaacha waende zao. Pia waweza kusoma  1 Timotheo 4:14; 5:22


Uongozi wa Kanisa unawekwa na Mungu kwahiyo hata viongozi wake ni sharti watimize maagizo na kanuni zilizowekwa na Mugu japokuwa huchaguliwa na wanadamu .

Nafasi ya wazee ambao leo tunawatambua kama maaskofu au wazee wa kanisa ni nafasi inayotajwa kushikiliwa na wanaume tu pote katika Biblia , hii ndiyo sababu hata katika kanisa letu leo hatuchagui wazee wa kanisa wa kike.


MAANA YA MZEE WA KANISA

Biblia katika agano jipya iliandikwa katika ligha ya kigiriki, kwa lugha hii neno wazee limetokana na neno presbuteros au askofu( bishop). Linamaanisha mtu  mzee au mwenye mamlaka nah ii ni kwasababu biblia inamfananisha na mtu anayelisimamia kanisa kwahiyo ni mtu wa kuheshimiwa sawasawa na jina lake linavyomaanisha.

Neno askofu (Bishop) pia lilimaanisha mtawala na Paulo aliyatumia maneni yote mawili kwambadilishano.

Matendo 20:17,28. Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa. 

Tito 1:5,7 .Kwasababu hii nilikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru . Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshtakiwa neno , kwa kuwa ni wakili wa mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu.

Katika kanisa lililounwa upya Mzee wa kanisa  kilikuwa ni cheo cha kiofisi halafu askofu ikamaanisha majukumu ya ofisisi.

SIFA ZA MZEE WA KANISA
Hizi ni sifa za kiroho , na wala si sifa za kimwili kama zitumiwazo kuwachagua Viongozi wa kidunia.  Zinatajwa katika kitabu vifuastavyo 1Timotheo 3:1-7. Tito 1:5-9.

Ni wazi kabisa kutokana na sifa ambazo Biblia imeziainisha kuhusiana na mzee wa kanisa zinadhihirisha wazi kwamba Mungu alikusudia wazee wa kanisa kuwa Wanaume na ndio maana katika msingi wa  mafungu hayo hapo juu tunapata sifa zifuatazo.

1)Asiyelaumika.
2) Mume wa mke mmoja na sio mke wa mume mmoja.
3)Mwenye kiasi na busara
4)Mwenye kiasi, utaratibu.
5)Mkarimu.
6) Asiyezoea ulevi  watu hutumia usemi huu kumaanisha kuwa askofu awe mtu mlevi lakini asijizoeshe ulevi lakini  Tito anasema asiwe mlevi wala mgomvi..
7)Mpole.n.k

Pote ambapo eidha wazee wanachaguliwa, au sifa za mzee wa kanisa zinatajwa zinadhiirisha kwamba nafasi hii ni ya kushikiliwa na wanaume tu.

ØKUFUNDISHA KANISANI(SPIRITUAL AUTHORITY).

1 Timotheo  2:11-12.Mwanamke na ajifunze kwa utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha wala kumtawala mwanaume bali awe katika utulivu. Kwa maana Adam ndiye aliyeumbwa kwanza na Hawa baadae. Wala Adam hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali yua kukosa.

1 Kor 14:34-35.  Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa ya kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neon lolote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu mwanamke kunena katika kanisa.

Wanazuoni wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na Ayah hii..

1)Paulo alikuwa analenga kwa wanawake wa Efeso ambao walikuwa wanashuhudia  wanawake wa kipagani wakiendesha Ibada katika hekalu la atemi na hivyo aliwaonya wanawake wa Efeso ili wasiende katika mahekalu hayo na wasilete utamaduni huo. Upungufu unaonekana pale anapowaandikia na wakorintho kwahiyo pamoja na kwamba hoja inaweza kuwa na ukweli bado inamapungufu.

SDA Bible commentary ukurasa wa 792 . Inaelezea kama ifuatavyo..


Fungu hili limeunganishwa na fungu la 33 ambalo linasomeka hivi  “Kwa maana Mungu si Mungu wa macahafuko, bali wa amani, vilevile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu…Kutokana na maelezo hayo wanawake kunyamaza kimya inaonyeshwa kuwa si msimamo uliosababishwa na mmatatizo ya sehemu mahalia tu , lakini ni kuakisi utaratibu wa jumla katika makanisa yote. Ili kutdhihirisha kuwa huo ni msimamo wa makanisa yote   inaonekana pia katika  2 Timotheo 2:11,12.

Katika fungu la timotheo Paulo anatoa katazo bila kutaja kanisa moja na kusema   “Mwanamke na ajifunze kwa utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha wala kumtawala mwanaume bali awe katika utulivu”

Wengi wamepata ugumu kuelewa fungu hili si kwasababu tu ya nafasi aliyonayo mwanamke katika kanisa la leo bali pia nafasi na huduma ya Mwanamke katika historia.

ØWaamuzi 4:4
Ø2 Wafalme 22:14
ØLika 2:36,37
ØMatendo 21:9

KAMA VILE INENAVYO TORATI

Maandiko yanafundisha kwamba , kwa upande wa mwanamke katika anguko, mwanamke amepewa jukumu na Mungu kuwa na nafasi ya kuwa chini ya (subordination) na Mwanaume.

ØMwanzo 3:6,16
ØWaefeso 5:22-24
Ø1 Timotheo 2:11
ØTito 2:5
Ø1 Petro 3:1,5,6

“Kwa kujisababishia kubadilisha asili yake kwa kuleta uzoefu wa dhambi katika maisha yake, maisha ya amani ambayo mwanadam aliyajua hapo mwanzo yalifikia mwisho. Haikuwezekana tena kiutendaji kwa mwanaume na mwanamke kuwa na usawa katika uongozi wa nyumbani, na mungu alichaguwa kuweka kwa mwanaume jukumu la kufanya maamuzi ya familia yake.


AU JE NENO LA MUNGU LILITOKA KWENU

Kanisa la wakorintho halikuwa la kwanza kuanzisha bali miongoni mwa makanisa ya mwisho, hivyo halikutakiwa kuanzisha taratibu zake kama linavyjitakia bali lilitakiwa kufuata taratibu zinazotumiwa na makanisa mengine katika utaratibu wa kuendesha Ibada.

Kanisa lilianzisha taratibu zisizo zakawaida , kama vile kumruhusu mwanamke kuonekana katika huduma za jumuiya bila kufunika kichwa.

1 Wakorintho 11:5,16. Bali kila mwanamke asalipo au anapohutubu, bila kufunikwa kichwa, yuaibisha kichwa chake: kwa maana ni sawasawa na yule saliyenyolewa.  Maana mtu yeyote akitaka kuleta fitina sisi hatuna desturi hiyo wala makanisa ya mungu.

Wanawake walikuwa na kawaida ya kutoa unabii tokea agano la kale, ilifikia hatua wanawake wa Korintho walitaka wanapotoa unabii wasifunike vichwa kama wanaume.. 1 Kor 11:4.
Agenda ya idara ya wanawake ni  mbinu atumiayo shetani kufanya kanisa la Mungu likiuke maagizo ya biblia na roho ya Unabii.
Katika taarifa ya mkutano wa Vatikan City  uliofanyika tar 28/02/1999, ukiwa na wajumbe 1000 na viongozi wa serikalini 3000 ambao miongoni mwa wajumbe wake walikuwemo Roman Catholic,Lutheran church,Seventh Day Adventist Church.Jehova’s Wtness, Church of jesus Christ of latter dat saints (mormons), All Pentecostal Churches,Brethren Assemblies, Salvation Army, Church of England (Anglican), Presbyterian Church, London Missionary Society, Baptist church, Methodist Church.
Katika agenda ya MUUNGANO WA MAKANISA, moja ya dondoo za barua imenukuliwa kama ifuatavyo. “Makanisa katoliki yametenga mfuko wa kuendesha chombo kinachoitwa Davidian movement ndani ya kanisa ili kuwasaidia akina mama makanisani, nakwahiyo jina dorkas halina budi kubadilishwa na kuitwa huduma za akina mama kanisani (Women’s Ministry).
Kwa mujibu wa kikao hicho inamaanisha agenda ya idara ya wanawake ni fundisho kutoka rumi na si la biblia wala roho ya unabii.
JE NABII ELLEN G WHITE ALISEMAJE KUHUSU KUPIGANIA HAKI ZA WANAWAKE KANISANI?
  (1T,page 421… Those who feel called out to join the movement in favor of woman's rights and the so-called dress reform might as well sever all connection with the third angel's message. The spirit which attends the one cannot be in harmony with the other. The Scriptures are plain upon the relations and rights of men and women…)
Maana yake “wale wanaojisikia kwamba wanaitwa kuungana na wapiganiaji wa haki za wanawake na na kile kiitwacho matengenezo ya mavazi wanapaswa pia kuuondoa muungano ujumbe wa malaika watat. Roho ijihudhurishayo kwa mmoja haiwezi kufungamana na nyingine.Maandiko yako wazi juu ya mahusiano ya mwqanaume na mwanamke.”( Shuhuda kwa Kanisa, Gombo la kwanza uk 421.)


Mwanamke kwa mtazamo wa kibliblia hawezi kushikilia wadhifa kama mzee wa kanisa, askofu au mchungaji kama ijulikanavyo leo. Hii haimaanishi kwamba hawapaswi kushiriki katika uinjilisti, bali katika kushughulika kwao waweza kufanya majulumu mengine ya kanisa lakini wadhifa na majukumu ya mzee wa kanisa, askofu na wachungaji biblia huonyesha kwamba ni ya wanaume tu.

No comments:

Post a Comment