KWELI 100 KUHUSU SABATO YA BIBLIA
è Kwanini unapaswa kutunza sabato?
è Ni nani unayeabudiwa kaatika siku ya sabato?
è Nani aliiianzisha?
è Ilianzishwa lini na kwaajili ya nani?
è Ni siku gani ambayo ni sabato?
è Wengi hutunza siku ya kwanza ya juma au jumapili je wanamamlaka gani kimaandiko?
è Baadhi hutunza siku ya saba au jumamosi Je wana mamlaka gani ya kimaandiko kwa hilo ?
è Je ibaada ya jumapili ilianza lini, ni nani aliyeianzisha, biblia husemaje kuhusu kuadhimisha siku ya jumapili kama siku ya Ibada?
è Hapa kuna ukweli kuhusu siku hizo zote, kama inavyoelezewa wazi na neno la Mungu.
ZIFUATAZO NI KWELI 100 ZA BIBLIA KUHUSU SABATO.
1)Baada ya kuumba dunia kwa siku sita, Mungu akapumzika siku ya saba. Mwanzo 2:1,3.
2)Jambo hili lilitia muhuri siku hiyo kama Siku ya Mungu ya mapumziko , au siku ya sabato , kama sabato imaanishavyo pumziko. Mtu azaliwapo siku fulani, siku hiyo huwa siku yake ya kuzaliwa (birthday). Kwahiyo Mungu alipopumzika katika siku ya saba, siku hiyo ikawa kumbukumbu ya kuzaliwa/ kuumbwa kwa dunia na vyote vilivyomo au siku ya sabato.
3)Kwahiyo siku ya saba lazima iwe siku yua sabato ya Mungu. Waweza kubadilisha birthday yako kutoka siku ambayo ulizaliwa mpaka siku ambayo hukuzaliwa? Hapana, pia huwezi kubadili siku ya Mungu ya pumziko ikawa siku ambayo mungu hakupumzika. Kwahiyo siku ya saba bado ni sabato ya Mungu.
4)Mungu aliibariki Siku ya Sabato (Mwanzo 2:3.)
5)Mungu aliitakasa Siku ya Sabato. (Kutoka 20:11.)
6)Aliifanya kuwa Siku ya Sabato katika Bustani ya Edeni. (Mwanzo 2:1-3)
7)Ilianzishwa kabla ya anguko, kwahiyo haikuwa kivuli kwa maana vivuli (vielelezo) vilianzishwa baada ya anguko. Kwasababu hiyo haijakomeshwa kwasababu ni kumbukumbu ya uumbaji wa mungu.
8)Mungu alisema ilifanyika kwaajili ya Mwanadam (Marko 2:27.) Hii humaanisha kwa wanadamu wote, kama vile neno mwanadamu hapa halina kikomo; kwahiyo ni kwaajili ya myahudi na mmataifa.
9)Ni kumbukumbu ya uumbaji . (Kutoka 20:11; 31:17.)Kila tupumzikapo siku ya sabato, kama Mungu alivyopumzika tunaadhimisha (sherekea) uumbaji.
10)Ilikabidhiwa kwa Adamu, Baba wa jamii ya wanadam. (Marko 2:27; Mwanzo 2:1-3.)
11)Kwahiyo kupitia kwake, kama Muwakilishi wetu, ni kwa mataifa yote. (Matendo 17:26.)
12)Si siku ya Waayahudi kwani ilianzishwa miaka 2,3000 kabla ya kuwepo Wayahudi.
13)Kamwe Biblia hahiiti sabato ya Wayahudi, lakini mara zote “sabato ya Bwana Mungu wako.” Wanadamu wanapaswa kujihadhari na kuikanyaga sabato ya Mungu
14)Kielelezo cha sabato kama siku ya saba ya wiki , kinawekwa katika kiipindi cha wazee wa imani. (Mwanzo 2:1-3; 10:10,12: 29:27, 28 n.k)
15)Ilikuwa ni sehemu ya Sheria ya Mungu kabla ya Sinai. (Kutoka 16:4, 27-29.)
16)Kisha Mungu akaiwake kama kiini (Moyo) cha sheria yake ya maadili. (Kutoka 20:1-17.) Kwanini aliiweka pale kama haikuwa sawa na amri nyingine tisa ambazo hazibadiliki. Yesu alipoangikwa msalabani hakufuta amri kumi ,ndo maana uzinzi, wizi n.k bado ni dhambi, iweje uvunjaji wa sabato isiwe dhambi?
17)Siku ya saba ya Sabato iliamriwa kwa sauti ya Mungu aliye hai. (Kumbukumbu La Torati 4:12,13.)
18)Kisha Mungu akaandika amri hiyo kwa vidole vyake mwenyewe. (Kutoka 31:18.)
19)Akaitia muhuri katika jiwe lisilofutika, ikiashiria kwamba inaasili ya kutokuharibika. ( Kumbukumbu La Torati 5:22.)
20)Ilitunzwa katika sanduku lilioko Patakatifu Pa Patakatifu. ( Kumbukumbu La Torati 10:1-5.)
21)Mungu alikataza kufanya kazi siku ya sabato, hata katika nyakati ngumu zenye kazi nyingi.(Kutoka 34:21.)
22)Mungu aliwaadhibu wana wa Israeli jangwani kwasababu waliihalifu Sabato.(Ezakieli 20:12,13.)
23)Sabato ni ishara ya Mungu wa kweli, ambaye kupitia hiyo tunamtofautisha na miungu wa uongo. ( Ezekieli 20:20.), Wana wa israeli walipokuwa wakitoka Misri Sabato iliwatofautisha na waabudu miungu, hii inatokana na ukweli kwamba Amri ya nne Kutoka 20:8-...ndiyo amri pekee imtambulishayo Mungu kama muumbaji.
24)Mungu aliahidi kwamba Yerusalemu ingedumu milele endapo wayahudi wangeitunza sabato.(Yeremia 17:24,25.)
25)Mungu aliwaacha (Israeli) utumwani babeli kwasababu waliivunja Sabato. (Nehemia 13:18)
26)Aliiangamiza Yerusalemu kwa kuivunja Sabato.(Yeremia 17:27.)
27)Mungu ameahidi mibaraka maalumu kwa wamataifa na wote watakaoitunza Sabato.(Isaya 56:6,7.)
28)Hii ipo katika unabii , ambayo kwa ujumla inahusu ukristo. (Isaya 56.)
29)Mungu ameahidi kuwabariki wote waitunzao sabato. (isaya 56:2.)
30)Mungu anatuhitaji sisi tuiite siku takatifu ya heshima. (Isaya 58:13.) Iweni na tahadhari ninyi mnaoiita “Sabato ya zamani ya Wayahudi”, “nira ya utumwa.”
31)Baada ya Sabato takatifu kukanyagwa chini “vizazi vingi” itarejeshwa tena katika siku za mwisho. (Isaya 58:12,13.)Hapa Sabato inaelezewa kama mojawapo ya matengenezo ya ibada ya kweli katika siku za mwisho.
32)Manabii wote watakatifu waliitunza Sabato.
33)Mwana wa Adam (Yesu Kristo) alipokuja, aliitunza Sabato maisha yake yote. (Luka 4:16; Yohana 15:10.) Kwa kufanya hivyo alifuata kielelezo cha Baba yake cha uumbaji. Je hatuwezi kuwa salama zaidi kwa kufuata kuelelezo cha Baba na Mwana?
34)Siku ya Sabato ni siku ya Bwana ( Ufunuo 1:10,Marko 2:28, Isaya 58:13; Kutoka 20:10.)
35)Yesu Kristo ni bwana wa sabato (marko 2:28.), hii inamaanisha kuipenda na kuitunza, kama mume ni Bwana wa mke , kwa kumpenda Yesu ambaye ni Mume na kichwa ca kanisa(Waefeso 5:22-27) , tunamtii kwa kuitunza sabato ambayo ni agizo lake (si ombi) kwetu .
36)Yesu aliifunua Sabato kama taasisi ya neema iliyoundwa kwa kumtakia mema mwanadam. (Marko 2:23-28.)
37)Yesu Badala ya kuihalifu sabato , kwa umakini mkubwa alifundisha namna ya kuitunza.(Mathayo 12:1-8,Marko 3:1-5,Luka 14:1-5.),Mafarisayo walifanya sabato kuwa ngumu kwa kuzuia hata shughuli njema zisifanyike,Yesu akasema shughuli njema yaani za kuokoa uhai kama vile kutibu wagonjwa, kumpikia mwenye njaa ni halali kuzifanya Siku ya Sabato (Mmat 12:12.)
38)Yesu aliwafundisha wanafunzi wake wasifanye kitu Siku ya Sabato kilicho kinyume na sheria. (Mathayo 12:12.)
39)Yesu aliwasisitiza wanafunzi wake kwamba waombe baada ya kunyakuliwa kwake hata siku watakapokimbia maangamizi ya Yerusalemu, isiwe sabato maana wangeihalifu.(Mathayo 24:20.)Hili linadhiirisha kwamba hata Yesu alijua kwamba atakapo kufa, atakapo fufuka na kunyakuliwa sabato haitasitishwa.
40)Wanawake walioambatana na Yesu kwa umakini waliitunza sabato baada ya kifo cha Yesu.(Lika 23:56.)
41) Miaka thelathini, baada ya Yesu kunyakuliwa , Roho Mtakatifu kupitia Paulo anaitaja kama “Siku ya Sabato,” (Matendo ya Mitume 13:14.)
42)Paulo, Mtume kwa watu wa mataifa, “aliita Siku ya Sabato” katika mwaka 45.A.D ( Matendo ya Mitume 13:14) Je Paulo hakujua? Au tuwaamini walimu wa sikuhizi wasemao iligongomelewa msalabani yaani iliishia kipindi Yesu aliponyakuliwa Mbinguni?
43)Luka, mwanahistoria wa Kikristo aliyevuviwa, akiandika miaka ya 62 A.D anaiita “Siku ya Ssabato.”(Matendo 15:21.)
44)Waongofu wa mataifa waliita Sabato. (Matendo ya Mitume 13:42.)
45)Katika baraza kubwa la Wakristo mwaka 49 A.D mbele ya mitume na maelfu ya wanafunzi , Yakobo anaiita “Siku ya Sabato.” ( Matendo ya Mitume 15:21)
46)Ilikuwa ni desturi kufanya maombi kufanya kusanyiko la maombi siku hiyo.( Matendo ya Mitume 16:13.)
47)Pauo alisoma maandiko matakatifu katika kusanyiko takatifu katika Siku ya Sabato. ( Matendo ya Mitume 17:2,3.)
48)Ilikuwa ni desturi ya Paulo kuhubiri Siku ya Sabato.( Matendo ya Mitume 17:2,3.)
49)Kitabu cha Matendo ya Mitume kinatoa rekodi ya Paulo kufanya mikutano ya ibada 84, katika siku ya sabato.( Matendo ya Mitume 13:14,44; 16:13 ; 17:2 ; 18:4,11.)
50)Hapakuwa na ugomvi wowote kati ya Wayahudi na Wakristo juu ya Sabato.Huu ni uthibitisho kwamba wakristo waliitunza sabato ileile iliyotunzwa na Wayahudi.
51)Wakristo walipomshtaki Paulo, kamwe hawakumshtaki kwa suala la kutunza Sabato. Kwanini hawakumshtaki kama si kwasabau walikuwa wakiitunza?
52) Lakini Paulo mweyewe alikiri kwamba aliitunza sheria. (Matendo 25:8.) Je hili lawezaje kuwa sahihi kama Paulo hakuitinza Sabato?
53)Sabato hutajwa katika aganojipya mara hamsini na nane,, na marazote kwa heshima ikibeba jina lile lile ililokuwanalo katrika Agano la Kale kama “Siku ya Sabato.”,na matendo ya kupumzika,ibada na matendo mema.Mathayo 10,Marko 11,Luka 18, Yohana 10 na Matendo ya Mitume 9.
54)Katika agano jipya hakuna neno lionyeshalo kuwa Sabato ilisitishwa, kuondolewa, kubadilishwa , au kitu chochote cha aina hiyo.
55)Mungu kamwe hajaruhusu mwanadamu yoyote kufanya kazi katika siku hiyo, ndugu msomaji ni kwa mamlaka ya nani unaitumia siku ya sabato kwa kazi za kawaida?
56)Katika Biblia Hakuna Mkristo katika agano jipya, eidha kabla au baada ya kunyakuliwa kwa Yesu, ambaye alifanya kazi za kawaida Siku ya saba ya Sabato.Kwanini wakristo wa leo hufanya tofauti na Wakristo wa kwenye Biblia?
57)Hakuna rekodi kwamba Mungu ameondoa Mbaraka na Utakaso wa Siku ya Sabato.
58)Kama vile Sabato ilivyotunzwa Edeni kabla ya Dhambi (Anguko), vivyohivyo itatunzwa mbinguni baada ya dhambi kuangamizwa.(Isaya 66:22,23.)
59)Sabato ya Siku ya Saba ilikuwa na nafasi muhimu katika amri kumi za Mungu, kama ilivyotoka katika kinywa cha Mungu, na kuandikwa kwa kidole chake mwenyewe juu ya jiwe pale Sinai (tazama Kutoka 20.) Yesu alipoanza kazi alisema kwa uwazi kabisa Hakuja kuitangua Torati (sheria). “Msidhani ya kwamba nalikuja kuitangua torati, au manabii.” (Mathayo 5:17.)
60)Yesu aliwakemea vikali Mafarisayo kwamba ni wanafiki wakiigiza kama walimpenda Mungu, na bado wakati huohuo wliihalifu sheria moja kati ya Amri kumi za Mungu kwa kufuata mapokeo yao . Uutunzaji wa jumapili kama siku ya Ibada ni mapokeo ya wanadam.
KWELI AROBAINI ZA BIBLIA KUHUSU SIKU YA KWANZA YA JUMA.
61)Kitu cha kwanza kurekodiwa katika Biblia ni kazi iliyofanyika siku ya kwanza ya juma.(Mwanzo 1:1-5.) Muumbaji mwenyewe alifanya hili.Kama Mungu aliiumba dunia siku ya jumapili,je yaweza kuwa dhambi kwa sisi kufanya kazi siku ya jumapili?
62)Mungu huwaamuru wanadamu wafanye kazi siku ya kwanza ya juma.( Kutoka 20:8-11.) Je ni dhambi kumtii Mungu?
63)Hakuna Mzee wa imani aliyeitunza Jumapili kama siku ya Ibada.
64)Hakuna Nabii Mtakatifu aliyeitanza (jumapili) kama siku ya ibada.
65)Kwa maelekezo ya sheria ya Mungu ,kutoka uumbaji hadi kifo cha Yesu watakatifu Wake wameitunza siku ya kwanza ya juma kama siku ya kawaida ya kazi angalau kwa miaka 4,000.
66)Mungu mwenyewe huiita siku ya kazi .(Ezekieli 46:1.)
67)Mungu hakupumzika katika ya kwanza (Jumapili).
68)Mungu hakuibariki siku ya kwanza (Jumapili.)
69)Yesu alikuwa fundi seremala (Marko 6:3) na alifanya biashara yake mpaka alipofikisha miaka 30. Aliitunza sabato na kufanya kazi kwa siku sita za wiki. Kwahiyo alifanya majukumu yake mazito siku ya Jumaapili.
70)Yesu hakupumzika siku hiyo ya jumapili.
71)Mitume walifanya kazi jumapili.
72)Mitume hawakupumzika jumapili.
73)Yesu kamwe hakuibariki.
74)Kamwe haijabarikiwa na Mamlaka Takatifu kutoka Mbinguni.
75)Kamwe haijatakaswa.
76)Hakuna sheria iliyoagiza kuitunza siku ya kwanza ya juma (jumapili) kama siku ya Ibada, kwa hiyo si dhambi kufanya kazi katika siku hiyo. “kwa maana pasipo na sheria, hakuna dhambi .” (Warumi 4:15. Pia 1 Yohana 3:4.)
77)Katika agano jipya hakuna sehemu ikatazayo kufanya kazi siku hiyo.
78)Hakuna adhabu itolewayo kwa kufanya kazi jumapili (ikionyesha kama imehalifiwa.)
79)Hakuna mbaraka ulioahidiwa kwa kuitunza.
80)Hakuna maelezo yaliyotolewa kwamba ni kwa namna gani inapaswa kutunzwa.Je hili lawezekana endapo mungu anekuwa anataka tuitunzw kama siku ya Ibada.
81)Kamwe haijaitwa Sabato ya wakristo.
82)Kamwe haijaitwa Siku ya Sabato.
83)Kamwe haijaitwa siku ya Bwana,wanadam ndio walioiita Siku ya Bwana.
84)Kamwe haijaitwa siku ya pumzinko.
85)Hakuna jina takatifu ililopewa. Sasa kwanini tuiite siku takatifu?
86)Kwa urahisi huitwa “siku ya Kwanza ya juma.”
87)Yesu hakuitaja kwa namna yoyote,kamwe hakulitamka jina la siku hiyo kwa midomo yake, kwa rekodi yote tuliyonayo.
88)Neno jumapili kamwe halionekano kwenye Biblia, labda biblia ya kiswahili cha kisasa, lakini katika Biblia nyingine imetajwa kama siku ya kwanza ya juma.
89)Kamwe Mungu, Yesu , hata waliovuviwa kuandika maandiko ya Biblia hakuna aliyewahi kuongea akiisifia jumapili kama siku ya Ibada.
90)Siku ya kwanza ya juma inatajwa mara nane tu katika Agano Jipya.(Mathayo 28:1, Marko 16:2,9; Luka 24:1. Yohana 20:1,19; Matendo ya Mitume 20:7; 1 Wakorintho 16:2.)
91)Mafungu sita huelezea siku ya kwanza ya wiki.
92)Paulo aliwaagiza watakatifu wajishughulishe na mambo yao katika siku hii ya kwanza ya wiki, (1 Wakorintho 16:2.)
93)Katika agano jipya tuna kumbukumbu ya mkutano mmoja tu wa kiroho uliofanyika katika siku hiyo, nao ulifanyika usiku (matendo 20:5-12.)
94)Hakuna maandiko yaonyeshayo kwamba walikuwa na mkutano kama huo kabla au baada ya hapo.
95)Haikuwa desturi yao kukusanyika katika siku hiyo(jumapili).
96)Hakukuwa na agizo la kuumega mkate katika siku hiyo.
97)Tuna kumbu kumbu ya tukio moja tu ambapo waliumega mkate. (Matendo ya Mitume 20:7.)
98)Tukio hilo lilifanyika usiku wa manane. (Matendo ya Mitume 20:7-11.) Yesu alifanya tukio kama hilo Ijumaa jioni (Luka 22), Na wanafunzi wakati mwingine walilifanya tendo hilo kila siku.(Matendo ya Mitume 2:42-46.) Ingekuwa ni Ibada rasmi ya kielezo kwa kawaida isingefanyika usiku bali kuanzia asubuhi.
99)Kamwe Biblia haijaonyesha sehemu yoyote kwamba jimapili (siku ya kwanza) ni siku ya kukumbuka kufufuka kwa Yesu, Haya ni mapokeo ya wanadam ambayo ni kinyume na neno la Mungu. (Mathayo 15:1-9.)
100)Ubatizo ndiyo tendo litukumbushalokifo na ufufuo wa Yesu. (Warumi 6:3-5.), na jambo jingine ni kitendo cha kuumega mkate (Pasaka ) tofauti na ile ya mwezi wa nne kwasababu pasaka ya biblia na Easter ni vitu viwili tofauti. Yesu aliacha mabo hayo kama vielelezo vya kukumbuka na kuadhimisha ukombozi aliotufanyia na sio kusali siku ya kwanza ya juma.
101)Mwishowe, Agano jipya liko kimya kabisa kuhusu badiliko lolote la siku ya sabato au utakatifu wa siku ya kwanza.
Maelezo zaidi kuhusu Sabato.
ISHARA YA UHUSIANO WETU NA MUNGU.
Sabato ni Ishara ya taifa la Mungu, Kutoka 31:13,17,16.Imeandikwa , 13“Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika sabato zangu kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasae ninyi. 17Ni kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya Mbingu na nchi, akastarehe siku ya saba akapumzika. 16Kwaajili ya hayo wana wa Israeli wataishika sabato katika vizazi vyao vyoyte, ni agano la milele.
Sabato ni ishara kati ya waumini wa Mungu na Mungu iashiriayo kwamba wanamtii na kushika sheria yake.Utunzaji wa sabato ni njia aliyoiweka Mungu ili kutunza maarifa kumhusu Yeye na kutofautisha waumini wanaomtii na wale wavunjaji wa sheria yake. Shetani atafanya kila mbinu kuhakikisha kwamba mafundisho ya Imani iliyokabidhiwa kwa watakatifu hapo mwanzo isilete matokeo kwa watu wa kizazi hiki.
Mungu asingeweza kusema kuwa ni agano lake la milele halafu aje kubadilisha, sabato itaendelea kuwepo milele zote hata katika Mbingu mpya na nchi mpya soma Isaya 66:22,23.
Msomaji yeyote wa Biblia sehemu ya agano jipya, kuanzia mathayo 12:1-13, akifuatilia kila kisemwacho kuhusu sabato na msimamo ambao Yesu na Mitume waliuchukua kuhusu sabato, hatashindwa kutambua kwamba Kanisa la kipindi cha agano jipya lilitunza Sabato kutokana na mfano wa mafundisho ya Yesu mtunzaji wa sabato. “Bwana wa Sabato” alifundisha sehemu yake halisi na tabia ya sabato katika ufalme wake.
IBADA YA JUMAPILI ILIANZA LINI?
Kabla ya yote ikumbukwe kwamba Biblia huitaja siku ya saba (Sabato ) kama siku ya Bwana. Kutoka 20:10. “lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana...”, Marko 2:28. Basi Mwana wa Adam ndiye Bwana wa Sabato.Isaya 58:13...ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima... Baada ya Kostantino kuanzisha Ibada ya jumapili aliita siku hiyo Siku ya Bwana jambo ambalo halina ukweli wa kimaandiko, wote waiitao jumapili siku ya Bwana huo ni uongo wa shetani kuwapofusha wasijue udanganyifu wa sabato bandia aliyoanzisha. Hivyo hata vitabu vya historia huiita sjumapili siku ya Bwana kwa mtazamo huo kama ifuatavyo.
VITABU VISIVYO VYA KISABATO HUELEZEAJE?
Kitabu cha (International Standard Bible Encyclopedia, Vol 3, pg 158, na Vol 4 ukurasa 251,252) kimnaelezea mabo yuafuatayo:-
“Katika Mwaka 321 A.D Costantino, ambaye pia alikuwa na muumini wa mungu-jua, aliifanya siku ya kwanza kuwa siku ya kawaida kwa jamii kupumzika, akisema kwamba, Majaji, watu wa mijini, na wachongaji wapumzike katika siku hii ya mungu jua,lakini aliwaruhusu wakulima kuhudhuria mashambani hali ya hewa ikiruhusu.Sheria hii kwa asili ilisababisha uwepo wa Ibada ya Kikristo.”
Mwaka 363 A.D.Baraza la Laodikea(Council of Laodecia)
Baraza hili lilikataza kupumzika katika siku ya saba (Sabato) na kuagiza watu wapumzike katika siku ya Bwana kama ijulikanavyo kuwa siku mbadala ya Ibada.
Mwaka 451 Baraza la Karthage(Council of Carthage )
Baraza hili lilikaataza watu wasihudhurie katika michezo siku ya Bwana (jumapili.)
Karne ya 16. Baraza la Oreansi (Council of Orleans )
Baraza hili liliongeza sheria ya kukataza watu wasifanye kazi siku ya Bwana.(jumapili).
Pia kitabu cha Roman Katoliki kiitwacho “Historia ya Kanisa Vipindi Vyake saba, kilichoandikwa na F.Potmani. Ukurasa 24, kinaelezea yafuatayo;
Mwaka 306, Kostantino alitangazwa Kaisari wa Magharibi, ilipofika mwaka 312 alimshinda mpinzani wake karibu na Roma. Mwaka 313, Kaisari Kostantino hakukawia kutangaza uhuru wa kanisa kwa “Tangazo la Milano”.Basi Wakristu walipata uhuru uleule wa dini kama wapagani.Walirudishiwa makanisa na mali waliyokuwa wamenyimwa wakati wa udhalimu.Kaisari alitangaza pia jumapili iadhimishwe kama “Siku ya Bwana”, na watu wakumbuke ufufuko wa Kristu wala wasifanye kazi.
Katika maelezo hayo yote ni wazi kwamba kuanzishwa kwa Ibada ya jumapili, kusudi lake na hata muanzilishi wake havitokani na Biblia bali ni sababu za kibinadam. Kostantino alikuwa mpagani muabudu jua, na alipokuwa kaisari aliongoka kiuongo alitaka kupata waumini wa kipagani na kikristo . Kwa hitaji lake aliona njia pekee ya kuwavuta ni kuchanganya ukristo na upagani.
Mchanganyiko huu ulikamilika pale alipoanzisha ibada katika siku ya wapagani ya kuabudu mungu jua (Sun day-sunday/siku ya jua), kwa kuagiza watu wafanye pumziko la sabato aliyoihamisha kinyume na maagizo ya Mungu, kwa kufanya hivyo aliwapata Wakristo na wapagani na kuanzisha Romani Katoliki . Wkristo wasalio Jumapili hufuata amri yakanisa la Roman Catholic kama tutakavyoona.Sababu kwamba Wakristo wafanye Ibada kukumbuka ufufuo wa Yesu si ya kibiblia .Hata yesu mwenyewe hakusema wakristo wafanye ibada siku ya kwanza ya juma wakikumbuka ufufuo wake.
Ilipofika mwaka 1234 A.D . Papa glegory IX aliidhinisha rasmi mapumziko ya siku ya jumapili.
Biblia ilitabiri kuja kwa Uvunjwaji wa sabato
2 Wathesolanike 2:3,4. Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu, akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu. 4 yule mpinzani ajiinuaye juu ya kile kiitwacho Mungu...
Japokuwa fungu hili linamaana nyingine kubwa ila kwa sehemu linazungumzia kitendo cha waanzilishi wa kanisa la Roman catholic walivyobadili sheria ya mungu toka sabato hadi jumapili, hapa walivunja amri ya 4 katika amri 10 za Kutoka 20:8->.Danieli 7:10 Inaitaja dola ya rumi kama pembe iliyoinuka na kunena maneno makuu (Kufuru) neno ambalo pamoja na maana yake kubwa ni kuchukua cheo cha mungu kwa kubadili alichoagiza (Utunzaji wa sabato) na kuweka agizo la kibinadam. (ibada ya Jumapili).
Wakristo wote wasaliojumapili hufuata amri ya Roma si ya Mungu
Hebu tuone kauli za baadhi ya maandishi ya Roman Catholic kuhusu wakristo watunzao jumapili:-
1) Nithibitishie katika bibliapekee kwamba napaswa kuadhimisha jumapili kama siku takatifu.Hakuna sheria kama hiyo katika Biblia.Ni sheria ya kanisa takatifu la Romani Katoliki pekee. Biblia inasema 'Ikumbuke siku ya sabato uitakase.' Kanisa Katoliki linasema, Hapana. Kwa mamlaka yangu tukufu naiondoa sabato na kukuagiza wewe utunze siku ya kwanza ya juma. Na kumbe, Ulimwengu wote uliostaarabika unasujudu kwa kicho ukitii amri ya Kanisa Takatifu Katoliki. - Thomas Enright, CSRR , President, Redemptorist college (Roman Catholic) , Kansas City, MO.,February 18, 1884.
2) Utunzaji wa jumapili kwa Waprotestanti ni gharama wailipayo, badala ya wao wenyewe, kwa mamlaka ya kanisa la Romani Katoliki. - Monsignor Louis Segur , Plain talk About the Protestantism of today (1868),p.213.
3) Kama Waprotestanti wangefuata Biblia, wangepaswa kumuabudu Mungu katika siku ya Sabato (Jumamosi). Kwa kutunza jumapili wanafuata sheria ya Kanisa la Romani Katoliki.-Albert smith, Chancellor of the Archdiocese of Baltimore, replying for Cardinal in a letter of february 10, 1920.
4) Waprotestanti...wanakubali Jumapili kuliko jumamosi kama siku ya ibada ya jumuiya baada ya Kanisa la Romani Katoliki kufanya mabadiliko...lakini akili za Waprotestanti hazionyeshi kutambua kwamba...kwa kuitunza jumapili, wanakubali mamlaka ya mzungumzaji mkuu wa kanisa, Papa.-Our sunday Visitor, February 5, 1950.
Jumapili ni Chapa/Alama ya Romani Katoliki Duniani.
1) Kwa kweli Kanisa la Romani Katoliki linasema kwamba badiliko (Kutoka Jumamosi hadi Jumapili) ni kazi yake.Na kitendo hicho ni CHAPA ya mamlaka yake ya kanisa na mamlaka katika mabo ya kidini.- C.F.Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons.
Onyo la Biblia
Ufunuo 14:9,10...Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama ( hapa anamaanisha Romani Katoliki) na sanam yake (jumapili ni sanam ya sabato iliyosimamishwa na Romani), na kuipokea chapa ,(Kuabudu jumapioli badala ya sabato) katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake. Eye naye atakunywa katika mvinyo wa ghadhabu ya Mungu uliotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji,katika kikombe cha hasira yake;naye atateswa kwa moto na kiberitimbele ya malaikawatakatifu,na mbele za mwana wa mungu.
Kama Yesu mwenyewe alisema Sabato ni siku ya Bwana ni vyema kumfuata maana Yeye ndiye njia ya kweli na Uzima hakuna mtu awezae kumfuata Baba bila kupitia yeye, utajisikiaje kushika kweli zote za Biblia halafu kwa kupuuzia sabato ambayo Mungu ameamuru uitunze ukashindwa kuirithi Mbingu. Kila tufanyalo duniani hutuandaa kuwa watahiniwa wa kuirithi Mbingu, Ibada mbinguni hufanyika na itaendelea kufanyika siku ya sabato. Isaya 66:22,23.Biblia inaonyesha kuwa sabato hata sabato wanadam wote watakaoirithi Mbingu wataenda kuabudu mbele za Bwana.
MUNGU HUTAMBUA MATENGENEZO YA IBADA SIKU ZA MWISHO NI UTUNZAJI WA SABATO.
Ufunuo 14: 6,7. Kisha nikaona malaika mwingine ,akiruka katikati ya mbingu, mwenye injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa nakabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu ,Mcheni mungu, na kumtukuza , kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
Biblia inaposema tumsujudie yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.. Hutupeleka katika amri ya nne (Kutoka 20:8-). Ambayo hutuonyesha tusalipo katika siku ya sabato tunaonyesha kwamba tunamtambua mungu kama Muumbaji, watu wasalio jumapili huungana na Darwin mwanasayansi apingaye uumbaji, Wanadam wote wangekuwa watunzaji wa sabato (Birthday) ya uumbaji wasingesahau kuwa tumeumbwa na mungu.
Sabato ni muhuri chapa ya MUNGU, kwani amri ya 4, jina (maana kwa siku sita mungu…) , hutaja cheo (…Mungu aliziumba mbingu na nchi na bahari..) na Mamlaka (ya mtoaji amri (Muumbaji). Amri ya nne hutia muhuri amri kumi na wote waitunzao hupigwa muhuri ili wasipigwe muhuri wa mrumi au Romani katoliki kwa kutunza jumapili. Utunzaji wa jumapili ni kupokea chapa ya 666 (VICARIUS FELEE DEI /makamu wa Mungu- Cheo cha papa ambacho hesabu yake huleta namba ya 666.) rumi inapanga kutimiza mpango huu kwa kuwalazimisha watu wote kusali jumapili kwasababu kwa kufanya hivyo watapokea chapa ya rumi.
Katika barua ya VATICAN CITY , TAARIFA YA MAENDELEO INAYOLENGA MWAKA 200.ROMA 20/02/199. TAARIFA NO.207.ILIYOFANYIKA MWAKA 1951 MWEZI WAKWANZA. Inanukuu hivi “Madhehebu yote hayana budi kuwa na siku moja ya ibada na hasa Jumapili, ambayo Roman Catholic iliipitisha kwa niaba ya Mungu kwa kubadili kuwa jumapili kutoka jumamosi…Kama biblia ndio mwongozo pekee wa mkristo. Waadventista wasabato wako sahihi kuitunza jumamosi pamoja na wayahudi.
Umeshaona ushahidi wa biblia na vitabu vingine ambavyo havikuandikwa na wasabato vinavyoonyesha kuwa kutunza jumapili kama siku ya ibada si agizo la biblia. Napenda ufahamu kuwa tatizo litakalofanya wengi wapotee ni kuabudu katika mfumo ambao kiasilia huwatendesha watu dhambi. Kusali jumapili ni mfumo ambao huwafanya watu waendelee kuvunja amri ya nne katika kutoka 20:8-.
Je kunausalama kuendelea kuvunja sheria ya mungu huku ukijua , fanya matengenezo. Mungu anatambua kuwa wewe ni muumini mwaminifu kila upatapo ufunuo wa kweli yake, waweza kusema huokolewi kwa kuvunja sheria ya Mungu bali kwa Neema. Kumbuka Sheria Hukuonyesha kuwa umefanya dhambi na Neema ya yesu (damu yake hukupa nafasi ya kufanya marekebisho). Amri ya nne inakuonyesha kuwa umevunja sabato , ukimjia Yesu anakupa nguvu ya kuitunza sabato na namna ya kuitunza.
Warumi 6:1,2.Tuseme nini basi?tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi. Hasha sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
Unachukua uamuzi gani baada ya kutambua kweli 100 za biblia kuhusu sabato ya BWANA , Je msingi wa Imani yako unajengwa kwa kile kisemwacho na Biblia au Mapokeo (Romani Katoliki). Kama Kweli wataka imani yuako ijengwe katika kweli (Mwamba na sio mchanga) Ifuate Ibada inayoonyeshwa wazi na Biblia , IBADA YA SIKU YA SABATO, BWANA AKUBARIKI UFANYAPO MAAMUZI KWAAJILI YA UMILELE WAKO.
Rejea.
Bill Hughes, The Secret Terrorists
F.Potmann.(1999).Historia ya Kanisa Vipindi Vyake Saba.Tanganyika Mission Press Kipalapala
Mark Finley, (2005).The Next Super Power.Review and Herald publishing association
A.H.Lewis D.,A Critical History of the Sabath and The Sunday in the Christian Church
Ellen G White.The Great Controversy.
Ellen g White. Patriachs and Prophets.
Ellen g White .Testimornies for the church Vol
Somo hili limeandaliwa na , Petro Tumaini.
Email -petro.tumaini@gmail.com
Sim.+255712761605
No comments:
Post a Comment