SOMO HILI LIMEANDALIWA NA PETRO TUMAINI
Email -petro.tumaini@gmail.com
Mtu mmoja aliye na Yesu ni Yote, Kitu cha pekee kuwa na Shauku kwacho ni
uhakika wa Kuwa na Yesu siku zote, kitu cha pekee kuwa na hofu kwacho ni
kutengwa na upendo wa Yesu.
Hakuna jambo
tulitafutalo katika dunia hii ambalo Yesu hawezi kulitimiza. Mtu akimpata Yesu,
amepata yote katika dunia hii na Zaidi Uzima wa milele .
Mathayo 19:29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au
mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na
kuurithi uzima wa milele.
Ukweli
ni kwamba , kama huna Yesu, hata usome elimu yote ya dunia , ufanye kazi kuliko
watu wote duniani, umiliki mali na kuwekeza katika kila nchi duniani, uwe na
fedha katika kila Benki uijuayo chini ya jua, Uwe tajiri wa kwanza duniani, hayo
Yote Bila Yesu ni Bure.
Kama ni
hivyo Basi Swali la Msingi ni hili, Kama nimempata Yesu ni kitu gani chenye
mamlaka ya kunitenga na Kristo? Wapo wanaomwacha Yesu kwasababu ya mali, wapo
watengwao nae kwasababu tofautitofauti. Swali bado linabaki, Je Ni nini Kitakachotutenga na Kristo? Paulo
alijiuliza swali na kutoa majibu katika mafungu yafuatayo.
Warumi 8:35 Ni
nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au
njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
Miongoni mwa Ahadi tamu za Biblia ni Uhakika kwamba
Aliye na Yesu ni Yote. Waati wa Matatizo wengi hutetereka na kudhani kwamba
Yesu kawaacha laini ukweli ni kwamba SHIDA NI NJIA YA KUTUPELEKA KWA YESU MAANA
YEYE NDIYE KIMBILIO LETU
2 Wakorintho 1:3,4 Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana
wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; 4 atufarijiye katika
dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna
zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.
Swali
la Msingi ni hili, Kati ya Mauti na Yesu ni lipi lenye mamlaka na uwezo kuliko
jingine, Jibu rahisi ni Yesu. Yeye aliishinda mauti, wapo ambao wakimfuata Yesu wako tayari
kumwacha ili wasipatwe na mauti ya muda mfupi lakini bbiblia inatupatia tumaini
Mathayo
5:10
10 Heri wenye kuudhiwa (kuuliwa) kwa
ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Ayubu
5:20
20 Wakati wa njaa atakukomboa
na mauti; Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga.
Waebrania
11:4 Kwa
imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo
alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali
akinena.
Yohana 11:25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo,
na uzima. Yeye aniaminiye
mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
Ufunuo wa Yohana 14:13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni
ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam,
asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana
nao.
Yohana 8:51 Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.
Warumi 8:38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya
kwamba, wala mauti,
wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala
yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala
kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika
Kristo Yesu Bwana wetu.
Mungu anamamlaka juu ya hatari zote ziwezazo kutupata
katika duinia hii, Paulo alikutana na hatari karibu aina zote akiwa kwenye kazi
ya ya Mungu kama adhihirishavyo katika
waka ufuatao
2 Wakorintho 11:26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang'anyi; hatari kwa taifa langu; hatari
kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini;
hatari kwa ndugu za uongo;
Pamoja
na hatari zote Paulo alikuwa na tumaini moja na akazishinda
2 Wakorintho 12:9 Naye akaniambia, Neema yangu
yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi
nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
Uwe
katika shida kama Ayubu , uwe katika raha kama Sulemani, katika utajiri kama
Ibrahimu au katika umaskini , katika hali yoyote uliyonayo kumbuka wapo
walioitwa na Mungu katika hali kama Yako . JINSI ULIVYO UWAPO NA YESU HAKUNA LA KUKUTENGA NAE ,NEEMA YAKE YATOSHA .
No comments:
Post a Comment