Mavazi ya Kikristo.
By Petro Tumaini.
Watu wengi hudhani kwamba biblia haijawa wazi hususani tunapozuingumzia suala la Mavazi, lakini Miongoni ya mambo aliyo yashughulikia mungu mwenywe likiwamo na na ukombozi wa Mwanadam ni kutengeneza na kuwavika mavazi ya kusetiri mwili adam na Hawa.
Adam na Eva Walijitrambua kuwa wako nuchi, wakajitengenezea Mavazi.
Ø Mwanzo 3:7. Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajiona kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Ni wazi kwamba utukufu wa Mungu uliowafunika Adam na Eva kabla ya dhambi lakini mara tu baada ya kukubali kula tunda la ujuzi wa mea na mabaya alilowakataza Mungu utukufu wa mungu uliwaacha na wakaanza kujisikia aibu kuwa wako uchi wakajitengenezea majani ya mtini ambayo Mungu hakuridhika nayo na kuamua kuwatengenezea vazi yeye mwenyewe.
Ø Mwanzo 3:21. Bwana Mungu akawafanyia Adam na mkewe mavazi ya ngozi akawavika.
Vazi alilowatengenezea Mungu lilikuwa ni ngozi ya kondoo, liliwakilisha Utukufu wa Yesu ambao unatufunika uchi wa dhambi zetu.Mungu aliwavika ngozi kwasababu vazi la majani ya mtini waliyojitengenezea hayakusitiri uchi wao.
“Kitendo cha Mungu kuwatengenezea vazi na kuwavika Adam na Eva kinaashiria namna Mungu anavyozingatia sana umuhimu wa mavazi kwa wafuasi wake.”
Neno la kiebrania lizungumzialo vazi alilotengeneza mungu kwa kutumia ngozi ya kondoo limejengwa kaytika mzizi wa neno ktnvt ambalo humaanisha (to cover), yaani kusitiri au kufunika.
Katika biblia ya kiingereza limetumika vizuri zaidi, limeitwa (tunics), ambalo lilmetokana na neno la kilatini tunicas.
Tunics ni mavazi yaliyovaliwa na wtu wa Mungu tokea agano la kale, yalikuwa ni mavazi marefu yanayofunika mikono , mwili na kufuka chini ya magoti.
Waweza kusema Mungu anaangalia moyo na si mavazi kwahiyo hata nikivaa vazi lisilositiri ni sawa maana moyo wangu utabaki kuwa msafi, neno ambalo limekuwa likisemwa na wengi wanaotetea uvaajio wa nguo za kihuni. Biblia inasema Mungu anataka tuwe safi ndani na nje, yani wasafi wa moyo na mwili pia.
Ø I Wathesolanike 5:23. Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa: na miili yenu muhifadhiwe muwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu yesu krist.
Mwanadamu huona nje, aonaye ndani ya moyo ni mungu peke yake, hata hivyo waweza ukawa msafi nje lakini moyoni ukawa mchafu, lakini huwezi ukawa msafi ndani halafu nje ukwa mchafu. Huwezi kutembea nusu uchi halafu wanadami wakadhania kuwa moyo wako ni msafi.
“Waweza ukawa samba aliyejivija ngozi ya kondoo, lakini huwezi kuwa kondoo halafu ukavaa ngozi ya samba.”
Tokea dhambi iingie mungu hakupenda mwanadam atembee bila kuusitiri mwili wake, hata makuhani waliohudumu hekaluni alitaka wasogee mbele zake wakiwa wamesitiri miili yao.
Ø Kutoka 20:26. Tena hutapanda kwenda madhabahuni kwangu kwa daraja, uchi wako usidhihirike juu yake.
Itaendelea, endelea kutendembelea blog yetu…
No comments:
Post a Comment