NI JINSI GANI MUNGU ANAHITAJI
TUMUIMBIE?
- Je biblia humaanisha nini isemapo "tumsifu Mungu kwa matari na kucheza (zaburi 150:4)?
- Je biblia humaanisha nini izungumziapo kucheza?
- Vipi kuhusu wakristo waimbao kwa kucheza, je wanafuata kile Biblia isemacho au wamepotoshwa?
- Ni kanuni gani za kuzingatia ili tuimbe nyimbo zikubalikazo mbele za Mungu?
- Je uimbaji ulianza lini katika Biblia?
- Biblia hutoa muongozo gani kuhusu matumizi ya vyombo vya muziki?
- Kuna usahihi wowote kuwakataza watu wasicheze katika Ibada wakati biblia humuonyesha daudi na wakati Miriam akicheza?
Majibu ya aswali haya na mengine mengi yahusuyo mziki waweza kuyapata katika somo hili, fuatiliasomo hili kwa makini mpaka mwisho na Bwana atakufunulia siri ya pekee sana juu ya muziki ukubalikao mbele zake kwa mujibiu wa Biblia.
Uimbaji ni mojawapo ya huduma
takatifu zinazoendeshwa katika ibada au mikutano ambapo watu hukusanyika ili
kumwabudu Mungu Mwenyenzi aliye mkuu na muumbaji wa vitu vyote vilivyo hai na
visivyo hai hapa duniani na mbinguni. Mungu mwenyewe ametoa miongozo ndani ya
neno lake takatifu ni jinsi gani watu waenende mbele zake wakati wa ibada.
Miongozo hiyo inapaswa iangaliwe na kufuatwa kwa makini sana ili ibada iweze
kupata kibali machoni pa Mungu na hao waabuduo waweze kupata kibali machoni
pake vile vile na Baraka tele. Ibada ni tendo(worship is a verb).
Ibada kamili
lazima iwe na mambo
1. Lazima tujiandae kuabudu
2. Tujiandae kusikia neno la Mungu
3. Kujiandaa kuitikia kile Mungu anacho tuambia na
4. Kukubali kutumwa na Mungu
“Katika
mambo hayo humaanisha kuwa, ibada ni tendo la kumwabudu na kumsifu Mungu;katika
ibada Mungu sharti anenenasi na kutenda nasi;katika ibada huitkia sauti ya
Mungu na kuhudumiana na viumbe wote vyote hujumuika jamopa katika ibada”Robert
W.Webber uk26
Sababu za
Kuimba
Je, umewahi kuketi chini na kutafakari
walao kwa muda wa nusu saa ukitafakari kwa nini unaimba nyimbo za dini? Mtu,
kwaya au kikundi chochote cha uimbaji, kama hawaelewi sababu ya kutunga na
kuimba nyimbo zao, basi ni rahisi sana kuifanya huduma kwa mtazamo na malengo
yote ya uimbaji kinyume na mapezi ya Mungu. Ikumbukwe kwamba ‘katika muziki wa
kidini Mungu ndiye kiini, na sio mambo ya ubinafsi wa mtu. Wazo la kumsifu
Mungu kwa ajili ya kujiburudisha ni wazo geni katika Biblia.’
Vile vile kufanya huduma ya nyimbo kwa madhumini ya kujipatia fedha ni mawazo
potovu yayoiharibu sana huduma hii takatifu sana.
Mfanyieni Bwana kelele za shangwe
Hindu ya rejea kwa sauti kubwa ya muziki
inatukumbusha kuhusu onyo, “mfanyieni Bwana kelele za shangwe.” Usemi
unajitokeza mara kwa mara katika Biblia ya tafsri ya mfalme James (KJV) lakini
kwa tofauti kidogo katika Agano la Kale (Zaburi 66:1; 81:1; 95:1-2; 98:4, 6;
100:1). Mafungu haya ya Biblia yametumiwa mara kwa mara kutetea matumizi ya
sauti ya juu katika muziki wa ‘rock’
(aina ya dansi ya kurukaruka ndani ya kanisa). Man‘ruwa,’-רוע Neno hili halimaanishi
kufanya kelele za juu zisizochaguliwa kwa busara, bali ni kupaza sauti kwa
furaha… mfano mzuri
unapatikana katika kitabu cha Ayubu 38:7 mahali ambapo neno lilo hilo ‘ruwa’-רוע
limetumiwa kuelezea wana wa Mungu ‘walipopaaza sauti kwa
furaha’ baada ya umbaji. Uimbaji wa viumbe vya mbinguni wakati wa
uumbaji hauwezi kabisa kuelezewa kuwa ni kelele za juu kwa sababu kelele
huashiria sauti mbaya.’
Mara nyingi watu wa
Mungu wamekosa mibaraka yake kwa sababu ya vurugu nyingi na ambazo hazina maana
yoyote wanapokuwa mbele za Mungu kwa ajili ya kumwabudu. Uwepo wa Mungu
unakosekana. Ibada na hasa katika uibaji wa kwaya hugeuka kuwa maburudisho yenye
mvuto wa kidunia. Hivyo baraka za Mungu
zinakosekana. Watu hurudi nyumbani kama walivyokuja na pengine hurudi
nyumbani wakiwa wamechanganyikiwa zaidi ya walivyokuwa walipokuwa wakija kwenye
ibada. Mungu hawezi kubariki fujo na machafuko hata siku moja. Kwa maana
‘Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika
makanisa yote ya watakatifu.’ (1Wakorintho 14:33). Kwa sababu hiyo
mashauri yametolewa kwamba ‘Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na
kwa utaratibu (1Wakorintho 14:40).
Ni jambo la muhimu sana
kwa wote waabuduo kukumbuka daima kuwa kama kuna jambo nyeti na lenye uzito wa
pekee ni lile la kwenda kukutana na Mungu katika ibada. Kicho na adabu halisi
vinapaswa kuonekana katika maisha ya waabuduo. Sababu ni kwamba Mfalme Mkuu, ndiyo Mungu mwenye nguvu,
Muumbaji wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo, Mwokozi wetu wa pekee Yesu
Kristo, kwa njia ya Roho wake Mtakatifu anakuwa na watu wake katika ibada. Nao
malaika kutoka mbinguni mahali ambapo uzuri na utaratibu kamili hutawala mile
na hata milele, hujihudhurisha katika mikutano ya watu wa Mungu wakutanapo ili
kutoa sifa na kumwabudu Mfalme wa milele au kufanya jambo lolote lile kwa ajili
yake
Kwanza kabisa
tunaona katika maandiko matakatifu habari ya wanawake wakicheza kwa mara ya
kwanza katika kutoka 15:20, 21. ‘Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni,
akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye
matari na kucheza. Miriamu akawaitikia mwimbieni Bwana, kwa maana ametukuka
sana; farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.’ Tukio hili
lilitokea baada ya Mungu kuwaangamiza Wamisri kwa kuwafunika na maji katika
bahari ya Shamu wakiwa katika harakati za kuwafuatia Wana wa Israeli ili
kuwarudisha utumwani katika nchi ya Misri. Tunaambiwa kuwa Miriamu pamoja na
wanawake wengine walicheza.
Neno la Kiebrania lililotumika hapa ni ‘miholah’ (מְחֹלָה) ambalo humaanisha kutembea katika mduara. Biblia, tafsiri ya KJV hutafsiri
‘dansi’ ya muduara. Lakini maana
yake halisi ni kutembea (matching) katika mduara. Kwa
kufafanua zaidi,
‘miholah’-מְחֹלָה humaanisha kucheza (kutembea) katika mistari miwili, kucheza katika kambi
la jeshi.’ Mara nyingi hueleweka kwamba jeshi au askari wanacheza gwaride. Jeshi Lichezapo gwaride halinengui bali hutembe
katika mwendo maalum ambao hupangiliwa katika mistari miwili au zaid,mwendo huu
huwa katika utaratibu uliokubalkikai. Hivyo wanawake waliomfuata Miriamu nyuma
walikuwa wakienda kwa kumachi (kutembea) na sio kwa kukatika, kurukaruka au
kunengua viuno vyao. Kutafsiri fungu
hili kumaanisha kwamba ilikuwa ni ‘dansi’ ya kukatika au kunengua viuno ni
kulitendea isivyo halali fungu hili la Biblia. Jambo lingine la kuzingatia katika tukio hili la Miriamu na wanawake
wenzake ni kwamba hawakuwa kwenye mkutano wa ibada au mkutano wowote wa
mafundisho ya neno la Mungu. Bali walikuwa safarini kutoka katika nchi ya Misri
kwenda Kanaani na walikuwa jangwani.
Kwa upande mwingine neno hilo hilo ‘mihola’ מְחֹלָה limetumiwa katika
1Samweli 18:6 ambapo tunasoma, ‘hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi
aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya
Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari,
na shangwe, na vinanda.’ Katika Waamuzi 11:34, hapo napo neno ‘mihola’מְחֹלָה
limetumiwa wakati binti wa Yeftha alipotoka kumlaki baba yake alipotoka vitani.
Matukio yote hayo hayawezi kuchukuliwa kama kigezo
cha Wakristo kuimba na kucheza dansi katika mikutano ya ibada. Matukio
hayo hayakuwa ya ibada. Katika matukio yote hayo wanaoonekana wakicheza ni
wanawake peke yao. Siku hizi wanaume katika kwaya mbalimbali wanaonekana wakicheza na
kurukaruka kama wendawazimu.
Katika 2Samueli
6:14 Mfalme Daudi aliopkuwa analileta sanduku la agano katika mji wa Daudi,
yeye alicheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote. Neno la Kiebrania
lililotumika hapo ni ‘kara’ כָּרַר ambalo humaanisha kurukaruka
na kuzungukazunguka (leaping and whirling) na wengine hufasiri kucheza. Hivyo
maana yake halisi ni kwamba, kwanza Daudi alikuwa kwenye msafara wa kulileta
sanduku la Bwana kutoka kwenye nyumba ya Obed-Edom hadi kwenye mji wa Daudi.
Akiwa kwenye msafara huo, Daudi, kwa furaha kubwa alionekana akirukaruka na
kuzunguka zunguka mbele ya sanduku la Bwana.
Mambo ya kuzingatiakatika muktadha wa uchezaji wa Daudi:
1. Daudi
hakuwa na maandalizi yoyote ya namna ya kucheza. Yeye
alizunguka zunguka huko na huko na kuruka kuruka huko na huko jambo ambalo mtu
yeyote anaweza kulifanya apatwapo na furaha isiyo na kifani. Mfano mzuri ni
pale mtoto apatapo matokeo ya mtihani na kuona kuwa amefauru kwa kiwango cha
juu sana. Anaweza kuruka ruka na kucheza cheza bila ya maandalizi yoyote ni
jinsi gani angeruka ruka endapo angefauru vizuri. Na
kucheza kwa Daudi kulikuwa ni tukio la papo hapo. Halikuwa tukio la kuendelea
au mtindo wa ibada ya uimbaji.
2.
Hakuwa na timu au kikundi cha watu
ambacho alifanya nacho maandalizi kwa ajili ya kucheza.
3. Hakuwa
Hekaluni au kwenye mkutano wa ibada au mafundisho yoyote ya neno la Mungu. Alijua wazi
kwamba ndani ya nyumba ya ibada hakuna kurukaruka au kuzunguka zunguka kwa
namna iwayo yote maana imeandikwa, ‘Lakini Bwana yumo
ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake
(Habakuki 2:20).
4. Daudi
hakuwa anacheza kama ni sehemu ya ibada mbele za Mungu aliye hai. Pia hatuoni
kama alikuwa anaimba wimbo wowote wakati alipokuwa anarukaruka na kuzunguka
zunguka mbele ya sanduku la Bwana. Wala
haikuwepo kwaya yoyote ikiimba nyimbo. Kurukaruka na kuzunguka zunguka kwa Daudi
mbele ya sanduku la Bwana au Miriamu
pamoja na wanawake waliomfuata nyuma, hakuwezi kuchuliwa kuwa ni kigezo
cha kuhalalisha dansi katika kanisa la Mungu aliye hai au katika ulimwengu wa
Kikrsito.
Katika Zaburi 149:3 na 150:4, kuna neno jingine la
Kiebrania linalofasiriwa kama ‘dansi’ ambalo ni ‘maholi’- מָחוֹל .
Haya mafungu ya Biblia ni ya muhimu sana kwasababu Ibilisi na makanisa
yachezayo dansi huyatumia kuunga mkono hoja ya watu wengi kuwa ‘dansi’ ni sehemu ya ibada kanisani. Ikiangaliwa kwa makini sana
itaonekana kuwa neno ‘dansi’ katika mafungu haya mawili ya Biblia linabishaniwa
sana na wana-eliungu (Theologians). Baadhi ya wana-eliungu huamini kwamba ‘maholi’-מָחוֹל hutokana na neno ‘chuwl’ amabalo humaanisha
‘fanya uwazi.’ Kwa maelezo hayo inawezekana ni chombo cha muziki chenye uwazi
kama vile bomba. Tafsiri hii yaweza kuwa sahihi kwa sababu ukiangalia kwa
makini sana, tunaweza kuona kuwa ‘maholi’-מָחוֹל ni chombo cha muziki kwa
sababu katika Zaburi 149:3 na 150:4 kuna
mlolongo wa vyombo vya muziki kama ifuatavyo:
Zaburi 150:3-
Kwa mvumo wa baragumu……kwa kinanda na kinubi
150:4-kwa matari na kucheza
(maholi)-מָחוֹל
150:4-Kwa zeze na
filimbi
150:5- Kwa matoazi yaliyao………kwa
matoazi yavumayo
Katika sura hii sehemu zote za mafungu kuna usambamba (parallelism) wa
vyombo vya muziki tu isipokuwa chombo cha muziki ‘matari’ ndiyo huambatanishwa
na kucheza. Msambamba wa vyomvo vya muziki katika sura hii ni wazi kuwa neno lililofasiriwa kama ‘kucheza’ kutoka katika neno la
Kiebrania ‘maholi’-מָחוֹל si sahihi. Neno ‘maholi’-מָחוֹל linaonekana kuwa chombo cha muziki katika
Zaburi 149:3 na Zaburi 150:4. Neno hilo linatokea katika mlolongo wa
vyombo vinavyoweza kutumika katika kumsifu Bwana. Kwa kuwa mtunga zaburi
anaoorodhesha vyombo vyote vinavyoweza kutumiwa katika kumsifu Bwana ni vyema kuelewa kuwa ‘maholi’-
מָחוֹל ni chombo cha muziki, kwa namna yoyote
kinavyoweza kuonekana.
Katika Muongozo wa ‘The Study Bible,’ tafsiri ya Mfalme James, katika
‘footnote,’ inatafsiri neno ‘maholi” מָחוֹל kuwa ni chombo cha muziki aina ya ‘bomba’ (pipe). Zamani, katika shule za msingi, bendi za shule zilikuwa na wapiga filimbi
ambazo zilikuwa ni bomba refu kidogo na matundu kama matano au sita .
Ngoma ilipopigwa na wapiga filimbi walipiga muziki kusindikiza mlio wa ngoma.
Chombo cha jinsi kama hiyo hiyo chaweza kutumika katika kumsifu Mungu. Izingatiwe
kwamba, ‘neno la Kiebrania lilofasiriwa “Zaburi” linatokana na neno la asili
linalomaanisha ‘kuimba kwa kutumia vyombo vya muziki.’
Katika Zaburi 81:2 tunasoma, ‘pazeeni Zaburi (vyombo vya muziki), pigeni
matari, kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda.’ Hapa anataja
kupaza Zaburi ambayo humaanisha chombo chochote kinachoweza kutumiwa katika
kumsifu Mungu. Kwa hiyo dhana ya kwamba Zaburi 150:4 huelekeza watu kucheza
dansi mbele za Mungu ni dhana potofu na tafsiri iliyopotoka.
Bila shaka watu
wengi wanaweza kuibuka na hoja kwamba, ni kweli ‘maholi’-מָחוֹל chaweza kuwa ni chombo cha aina fulani cha muziki na
hasa chombo cha muziki abamcho ni kama aina ya bomba (pipe); lakini je mfalme
Daudi hakuwahi kucheza mbele za Bwana Mungu? Jibu liko wazi kabisa. Ni kweli
aliwahi kucheza. Neno la Kiebrania ‘karar’-כָּרַר lililotumika katika 2Samweli
6:14 kama tulivyoona hapo awali, humaanisha kurukaruka na kuzunguka zunguka.
Davidson anaeleza ‘karar’-כָּרַר kuwa ni kurukaruka. Pia kwamba mwana-kondoo
anaitwa hivyo (karar) kwa sababu ya
kurukaruka kwake.’
Maana halisi ya neno kucheza katika
Biblia
Kwa wale wote wenye
dhana potofu kwamba Daudi alicheza dansi katika 2Sameli 6:14 ;Zaburi 149:3 na
150:4 anasistiza kwamba watu wamwimbie Bwana kwa matari na kucheza, wanapaswa
kuelewa kuwa
:
- Katika 2Samweli 6:14 neno la
Kiebrania lilotumika ni ‘karar’-
כָּרַר humaanisha kurukaruka na kuzunguka
zunguka.
- Katika Zaburi 149:3 na 150:4 neno la Kiebrania
lilotumika ni ‘maholi’ -מָחוֹל humaanisha chombo cha muziki cha aina kama ya bomba
(pipe).
Maneno haya yana maana tofauti na vile watu waelewavyo kuwa ni uchezaji
dansi
- Daudi hakucheza dansi katika 2Samweli 6:14 bali ali-‘karar’-כָּרַר yaani
alirukaruka kama mwana-kondoo aliyenenepeshwa anavyorukaruka akiwa nje ya
zizi. Na wala hakuwa ana- ‘maholi,’-
מָחוֹל yaani akipiga chombo cha muziki.
Mwana-kondoo huwa hana maandalizi au mafunzo ni namna gani arukeruke.
Mwana-kondoo anarukaruka bila ya kufuata mwelekeo wa aina fulani na wala
hafuati mapigo au mudundo fulani. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Daudi.
Hakuwa na muda wa kujifunza na wala hatuambiwi ya kwamba aliwahi kwenda
kwenye shule yoyote ya kujifunza namna ya kucheza mbele za Bwana kwa
ustadi wa mwelekeo fulani kama kwaya nyingi zifanyavyo siku hizi.
- Daudi
hakujikaririsha njia iwayo yote ile kwa ajili ya kurukaruka na kutupa
mikono na miguu huko na huko kama kwaya za leo zifanyavyo kwa kushinda
ndani ya jengo la kanisa au kwenye viwanja fulani na kujikaririsha ni
namna gani wataruka kwa pamoja na kutupa mikono kwa pamoja. Na
ieleweke tu kwamba kwaya za siku hizi hazipo kumwimbia na kumsifu Mungu
bali zipo kwa ajili ya kutimiza kiu yao kali ya dansi ya dunia huku wakiwa
wameivika dansi yao vazi la Kikrsito. Kwa lugha rahisi, kile kinachofanywa
na kwaya za siku hizi ni ‘upagani mambo kikristo.’ Kwa upande mwingine
lazima tukubali kuwa pepo mchafu ameingia katika fani ya uimbaji na muziki
kwa ujumla na ni lazima akemewe kwa nguvu zote ili atoke katika mioyo ya
waimbaji ili wabaki wakimwimbia Bwana na kumtukuza yeye tu.
Mashauri ya nabii Ellen G white kuhusu uimbaji
Makelele na midundo na kucheza ni ishara ya ukaribu
wa kufungwa kwa mlango wa rehema . Mjumbe
wa Mungu anaelezea kile ambacho Bwana alimwonyesha kuhusu ibada ya ghasia na
makele ambazo huonekana katika ibada siku hizi.
‘Mambo yale
umeyaelezea…Bwana amenionyesha kwamba yatatokea tena kabla ya kufungwa kwa
mlango wa rehema. Kutakuwepo na kupiga makelele, pamoja na ngoma, muziki, na
kucheza. Akili za mwanadmu zitachanganyikiwa kiasi cha kwamba hazitaweza
kuaminiwa kufanya maamuzi sahihi.’
White pia
anasema kuwa, ‘Bwana amenionyesha kwamba nadharia na mbinu potovu vitaingizwa
katika makambi yetu, na kwamba historia ya zamani itarudiwa…Mambo yale
yaliyokuweko wakati wa nyuma yatakuwepo siku za mbele (ndio sasa). Shetani
ataufanya muziki kuwa mtego kwa namna unavyoendeshwa. Mungu anawaita watu wake,
amabao wana ushuhuda, kusoma na kutafakari kwa makini, na kuchukua jukumu la
kusikia.’
Ni muhimu kwa
watu wa Mungu kuelewa kuwa uimbaji wajinsi hiyo kamwe hauongozwi na uwezo wa
Mungu Roho Mtakatifu. Mjumbe wa Mungu anasema tena kwamba, ‘Roho Mtakatifu kamwe
hajidhihirishi mwenyewe kwa njia kama hii, katika ghasia za makelele. Huu ni
ubunifu wa shetani ili kufunika werevu wa mbinu zake ili kuufanya ukweli ulio
safi, ulionyoka, wenye kuinua, wenye kunfanya mtu kuwa mungwana, ukweli wenye
kutakasa kwa wakati huu usiwe na matokeo mazuri.
Ni vema kutokuwa na ibada ya Mungu iliyochanganywa na muziki kuliko
kutumia vyombo vya muziki kufanya kazi ambayo mnao January lilionyesha kwangu
kwamba italetwa katika makambi yetu…Ghasia za makelele hushitua akili na
hupotosha kile ambacho kama kingeendeshwa vizuri kingeweza kuwa Baraka…Mambo
yote yaliyokuwepo siku za nyuma yatajitokeza siku za usoni. Shetani ataufanaya
muziki kuwa mtego kwa jinsi uanvyoendeshwa.’
Kucheza, midundo ya muziki na midundo ya ngoma na kadhalika
vimetawala na kuwa chanzo cha machafuko katika ibada.
Mjumbe
wa Mungu anasema kuwa,
‘Roho Mtakatifu hana sehemu yoyote katika
makelele na milio mikubwa kama ilivyopita mbele zangu… Shetani anafanya kazi
katika makelele na machafuko ya muziki, ambao kama uingefanywa kwa usahihi,
ungekuwa ni sifa na utukufu kwa Mungu. Anafanya madhara ya huo muziki kama sumu kali ya nyoka.’
Naliona ya
kwamba utaratibu wa Mungu umebadilishwa, na miongozo yake muhimu imepuuzwa na
wale wote wanaoiga utamaduni wa Amerika. Nilirejeshwa kwa fungu la Kumbukumbu
la Torati 22:5 kwamba mwanamke asivae mavazi yampasyo mwanamume…kumekuwapo na
hali ya wanawake katika mavazi yao na mwonekano wao kuwa karibu sana sawa na
ule wa wanaume kwa kadiri iwezekanavyo, na wanashona mavazi yao karibu sana na
yale ya wanaume, lakini Mungu anasema wazi kuwa hayo ni machukizo.’
1T 457
Wakati kanisa zima au kwaya maalumu inapoimba nyimbo
za kumsifu na kumtukuza Mungu Aliye Mkuu kwa kuimba kwa uzuri , utaratibu na
utakatifu wote, malaika nao huunganika nao katika kumsifu Mungu huku wakivipiga
vinubi vyao Mara nyingi, kwenye mikutano ya jinsi hiyo waabuduo wanatoka wakiwa
wamepata burudiko la Kiroho na ‘ruwa,’-רוע Neno hili halimaanishi
kufanya kelele za juu zisizochaguliwa kwa busara, bali ni kupaaza sauti kwa
furaha…
Katika kitabu cha Ayubu 38:7 mahali ambapo neno lilo
hilo ‘ruwa’-רוע limetumiwa
kuelezea wana wa Mungu ‘walipopaaza sauti kwa furaha’ baada ya umbaji. Uimbaji wa viumbe vya
mbinguni wakati wa uumbaji hauwezi kabisa kuelezewa kuwa ni kelele za juu kwa
sababu kelele huashiria sauti mbaya.’
Waimbaji wapaswa kuadabishwa
E.G.
White alikutana na tatizo hili siku za maisha yake na utumishi akasema ‘lakini wakati mwingine ni vigumu
zaidi kuwaadibisha waimbaji na kuwaweka katika utaratibu wa kazi…Wengi wanataka
kufanya mambo kwa kufuata mtindo wao wenyewe; wanakataa kushauriwa; na hawako
tayari kusikiliza uongozi.’
Mahali na Wakati wa Kuimba
Biblia
haituelekezi tu kuimba katika nyumba ya Mungu, bali pia miongoni mwa
wasioamini, katika nchi za kigeni, na wakati wa mateso, na katikati ya
watakatifu mwandishi wa kitabu cha Waebrania anasema, ‘nitalihubiri jina lako
kwa ndugu zangu; katikati ya kanisa nitakuimbia sifa (Waebrania 2:12).
Mtunga
Zaburi anasisitiza kwa kusema, ‘mwimbieni Bwna wimbo mpya, sifa zake katika
kusanyiko la watauwa (Zaburi 149:1).
Naye mtume Paulo imeandikwa, ‘kwa hiyo
nitakushukuru kati ya mataifa, nami nitaliimbia jina lako (Warumi 15:9).
Katika
kitabu cha nabii Isaya imeandikwa, ‘jangwa na miji yake na ipaze sauti zao,
vijiji vinavyokalia na Kedari, na waimbe wenyeji wa Sela, wapige kelele toka
vilele vya milima, na wamtukuze BWANA, na kutangaza sifa zake visiwani (Isaya
42:11, 12).
Wakiwa gerezani, Paulo na Sila ‘walilkuwa wakimwomba Mungu na
kumwimbia nyimbo za sifa, na wafungwa wengine walikiuwa wakiwasikiliza (Matendo
ya Mitume 16:25).
Kwa mafungu hayo machache ni wazi kuwa nyimbo za kumsifu
Mungu zaweza kuimbwa popote pale. Gerezani, katikati ya mataifa, kanisani na
katika kusanyiko lolote la watakatifu. Mwanadamu anaitwa kumwimbia na kumsifu
Mungu mahali popote pale alipo. Kwamba ana furaha au huzuni, ana njaa au shibe
na amwimbia na kumsifu Mungu Muumbaji.
Hindu za rejea
za mara kwa mara kwa ajili ya kumsifu Mungu miongoni mwa wapagani au watu wa
mataifa (2Samewli 22:50; Warumi 15:9; 108:3) huashiria kuwa uimbaji ulionekana
kuwa njia ya kumshuhudia BWANA kwa watu wasioamini. Hata hivyo hakuna
uthibitisho wowote katika Biblia kwamba Wayahudi au Wakristo wa kwanza
walifuatisha sauti na nyimbo za kidunia ili kuweza kuwahubiri watu wa
mataifa.
Wayahudi na Wakristo wa kwanza waliamini
kuwa muziki wa kidunia ulikuwa hauna nafasi katika nyumba ya ibada.
Mwanzo wa Huduma ya Muziki Katika Biblia:
Kabla ya wana wa Israeli kuingia katika
nchi ya Palestina, huduma ya muziki wakati wa ibada kwa kusudi la kukidhi
mahitaji ya waabuduo haikuwepo. Kabla ya wakati huo hindu za rejea kwa muziki
kimsingi zilihusiana na wanawake kuimba na kucheza kwa ajili ya kusherehekea
tukio fulani maalumu. Mfano wa kwanza kabisa ni ule wa Miriamu akiongoza kundi
la wanawake ambao walikuwa wakiimba na kucheza kwa sababu Bwana Mungu aliwatupa
Wamisri katika bahari ya Shamu na kuwangamiza huku akiwaokoa wana wa Israeli
kwa muujiza wa ajabu kabisa (Kutoka 15:1-2). Pia, wakati Daudi alipomua Goriathi
ambaye alikuwa ni tishio kubwa kwa wana wa Israeli, wanawake walicheza
wakishangilia ushindi huo mkuu (1Samuli 18:6-7). Na mfano mwingine ni ule wa
binti wa Yefta ambaye alimlaki babaye kwa matari na kucheza aliporudi kutoka
vitani (Waamuzi 11:34).
Jambo la kuzingatia hapa ni
kwamba wote hao waliimba na kucheza wakati ambao sio wa ibada na nje ya mahali
pakuabudia au kanisa/hekalu.
Kulingana na taarifa ipatikanayo katika kitabu cha Mambo ya Nyakati
kitabu cha kwanza, mfalme Daudi alianzisha huduma ya uimbaji katika hatua tatu:
1.Aliagiza vichwa
wa familia za Kilawi kuchagua watu wapigao vyombo vya muziki na kwaya kwa ajili
ya kulisafirisha sanduku la Agano kutoka kwa Wafilisti hadi hemani kwake katika
mji wa Yerusalemu (1Nyakati 15:16-24).
2.Hatua ya pili
ilitokea wakati sanduku la Agano lilikuwa limewekwa katika hema lake katika
mahali pake (1Nyakati 8:11), kwaya moja ilikuwa ikiimba chini ya uongozi wa
Asafu mbele ya Sanduku la Agano katika Jerusalemu (1Nyakati 16:37-42).
3.Hatua ya tatu ya
uanzishaji wa huduma ya muziki ilitokea
mwishoni mwa utawala wa mfalme Daudi wakati mfalme alipoandaa kwa undani
kabisa huduma ya muziki ambao ungetumika katika hekalu ambalo Sulemani
angelijenga (1Nyakati 23:2 hadi 26:32). Daudi aliunda kundi la Walawi 4000 kuwa
waimbaji wa pekee (1Nyakati 15:16; 23:5). Kutoka kwenye kundi hili mfalme Daudi
aliunda kwaya ya Kilawi yenye waimbaji 288.
Daudi mwenyewe alihusika pamoja na
maofisa katika kuchagua viongozi 24 kuwa walinzi, kila mmoja alikuwa na
wanamuziki 12. Jumla yao ilikuwa ni wanamuziki 288 (Nyakati 25:1-7). Hao nao
waliajibika katika kuchagua wanamuziki wengine.
Huduma ya Wanamuziki
Ili
kuhakikisha kuwa kusiwepo machafuko au mgongano kati ya huduma ya makuhani na
huduma ya wanamuziki ya Walawi, mfalme Daudi, kwa uangalifu mkubwa sana
alifafanua nafasi, cheo, na kusudi la huduma ya wanamuziki (1Nyakati 23:25-31).
Utendaji wa huduma ya wanamuziki ulikuwa chini ya makuhani (1Nyakati 23:28).
Viongozi wa kwaya au walimu wa kwaya
wanapaswa kuelewa fika utendaji wao ili kusiwepo mgogoro baina yao na
wachungaji.
Ukweli ni kwamba mchungaji ndiye kiongozi wa kwaya. Tatizo kubwa linalojitokeza
katika kanisa ni lile la walimu wa kwaya kutaka kumtawala mchungaji na kutaka
mchungaji akubaliane na kufuata matakwa yao hata kama yako kinyume na neno la
Mungu au kanuni za kanisa. Walimu wa kwaya wengi hukanyaga chini
taratibu za kanisa na kufanya mambo kama wapendavyo kwa ajili ya faida yao
wenyewe na familia zao badala ya kufanya kazi ya uimbaji kwa ajili ya Mungu.
Walimu wengi sana wa kwaya wamejaa
kiburi na ukaidi usio wa kawaida. Wanadharau neno la Mungu, wanadharau uongozi
wa kanisa na taratibu zake zote. Roho hiyo hiyo inaingizwa kwa waimbaji wote
ambao nao hawako tayari kuheshimu wazee wa kanisa na wachungaji. Wanadharau
taratibu zote za kanisa. Kiongozi wa kwaya anageuka kuwa mungu wao. Hili
halikuanza leo. Tangu zamani roho ya ukaidi na kiburi, ikianzia na shetani
mwenyewe kule mbinguni, imeonekana katika maisha ya waimbaji.
Mjumbe wa Mungu E.G. White alikutana na tatizo
hili siku za maisha yake na utumishi na aliandika, ‘lakini wakati mwingine ni vigumu zaidi
kuwaadibisha waimbaji na kuwaweka katika utaratibu wa kazi…Wengi wanataka
kufanya mambo kwa kufuata mtindo wao wenyewe; wanakataa kushauriwa; na hawako
tayari kusikiliza uongozi.’
Hili ni tatizo kubwa ambalo huleta giza
na laana isiyo ya kawaida katika kanisa la Mungu.
· Kwaya nyingi sana zinafanya maamuzi zenyewe ni namna
gani wataimba ili kukidhi haja yao ya muziki wa kidunia ambayo wengi waliipata
kabla ya kuingia kanisani.
· Kwaya haziko tayari kuwasikiliza wazee wa makanisa
labda kama naye mzee awe ametekwa na kuingia katika ukafiri wa jinsi hiyo hiyo.
· Kwaya haziko tayari kusikiliza wachungaji na adui
yao mkubwa ni Roho ya Unabii na Biblia kwa ujumla. Kwaya nyingi zimekuwa ni
mashirika yanayojitegemea ndani ya kanisa. Na wanaofaidika
na kile kinachotokana na uimbaji huo ni wachache sana. Wengine wanakuwa ni
bendera fuata upepo. Pale uongozi unapojaribu kusahihisha na kerekebisha
uimbaji wao, na wakiona mafundisho yanapingana na matakwa yao na maslahi yao
kwa ujumla, utajionea mwenyewe roho ya uasi iliyo ndani yao. Ndipo utajua kuwa
wamevaa ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu wakali mno. Wako tayari
kupigana, kutukana na kubeza uongozi. Kweli hata ibilisi alipoona mambo yake
yanapingwa kule mbinguni, aliazimia kupigana na roho hiyo hiyo imeipandikiza
ndai ya waimbaji na hasa walimu wa kwaya walio wengi (Ufunuo 12:7-12). Ibilisi
hakushinda kule mbinguni. Akatupwa chini. Kama Bwana aishivyo, waimbaji wote
pamoja na walimu wao wanao kaidi neno la Mungu na kushindana na uongozi wa
kanisa, muda si murefu watatupwa chini na wala hawatalishinda neno la Mungu.
VYOMBO VYA MUZIKI NA MATUMIZI YAKE KATIKA AGANO LA
KALE NA JIPYA
Haiwezekani kuongelea habari ya vyombo
vya muziki katka ulinasi wa Kikrisito siku hizi na upigaji wake katika ulinasi
wa Kikrsito wa sasa bila ya kuchunguza katika Agano la Kale kama vilitumikaje.
Kama tulivyokwisha kuona katika sura iliyotangulia, ‘Daudi hakuanzisha tu muda,
mahali, na maneno kwa ajili ya huduma ya kwaya ya Walawi, lakini pia
alitengeneza vyombo vya muziki ili vipate kutumiwa kwa ajili ya huduma yao.
Tunasoma, ‘na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsiu BWANA kwa
vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia (1Nyakati 23:5).
‘Wakasimama makuhani sawasawa na malinzi yao; Walawi nao pamoja na vinanda vya
BWANA, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru BWANA, kwa maana fadhili zake
ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda
mbele yao; nao Israeli wote wakasimama (2Nyakati 7:6). Hii ndiyo sababu
inayofanya viitwe vyomb vya Daudi (2Nyakati 29:26-27).
Kwa mapanda ambayo Bwana aliyaamuru
kupitia Musa, Daudi aliongeza matoazi, vinubi na vinanda (1Nyakati 15:16;
16:5-6). Mapanda yalipigwa na makuhani na idadi yao ilianzia mawili katika
ibada ya kila siku (1Nyakati 16:6; Hesabu 10:2) hadi saba au zaidi wakati wa
matukio maalumu (1Nyakati 15:24; Nehemia 12:33-35; 2Nyakati 5:12).
‘Wakati
wa ibada pale Hekaluni mapanda yaliaashiria kusanyiko la waabuduo kusujudu
wakati wa kutoa sadaka ya kuteketezwa na wakati wa kuitikia (Choral service)
huduma ikiendelea (2Nyakati 5:12; 7:6).’
“Mpangilio huu ulionyesha umuhimu wa wapiga mapanda kutoa ishara kwa
ajili ya mkutano kusujudu na kwaya kuimba.
‘Vyombo vya nyuzi vilitumika sana kusindikiza uimbaji kwani vilikuwa
havifuniki sauti au maneno ya Yehova yaliyokuwa yakiimbwa.’
Uangalifu mwingi ulifanyika ili kuhakikisha kwamba sauti za sifa za kwaya
hazikufunikwa na sauti za vyombo vya muziki.
Kusudi hilo hilo la vyombo kusindikiza
sauti za waimbaji linapaswa kufuatwa kwa makini leo. Lakini kwa bahati mbaya
tena kwa makusudi kabisa vyombo vinapigwa na watu wasio na ujuuzi kabisa kwa
sauti ya juu sana na midundo mizito na kufunika sauti za maneno ya sifa
zinazotolewa na waimbaji hazisikiki na wala kueleweka. Badala ya waabuduo
kutoka katika ibada na Baraka na kicho mbele za Mungu, wanatoka na vichwa
vinavyouma na masikio yanayonyita kwa sababu ya midundo na kelele za juu sana
za vyombo vya muziki tena vinavyopigwa bila utaratibu wala kicho mbele za
Mungu.
Swali linaweza kuulizwa, ‘je tupunguze
sauti za vyombo ili midundo isikike kwa chini kabisa? Jibu liko wazi kabisa.
Sumu ni sumu tu. Kwamba iko kwenye pipa la lita 100 au ipunguzwe hadi kuwa
katika nusu ya kijiko cha chai uwezo wake wa kufiisha uko pale pale. Kama mtu
haelewi hata hilo basi na aelewe kwamba kinyesi ni kinyesi tu. Kwamba
kimechotwa chooni na kuwekwa na kujazwa kwenye debe au kimewekwa kwenye kijiko
cha chai madhara yake ni yale yale. Hivyo ndivyo ulivyo muziki wa midundo.
Kwamaba imepigwa kwa sauti ya chini au ya juu madhara yake ni yale yale. Mungu
haitaki kwa sababu inafiisha hali ya mtu kuyaelewa na kuyapokea mambo ya
kiroho. Inalewesha wale ambao huipenda kiasi cha kwamba hawako tayari kusikia
ushauri wowote utokao kwenye neno la Mungu na Roho ya unabii. Inapumbaza na
kuilaza akili hata isitamani mafundisho yatokayo kwenye neno la Mungu.
Na
izingatiwe kuwa ‘kamwe hakukuwa na vyombo vyovyote vya midundo vilivyoweza
kuruhusiwa kusindikiza nyimbo za kwaya ya Walawi ilipokuwa ikitoa huduma ya
nyimbo Hekaluni au kundi kubwa la wapiga muziki pamoja (Orchestra) pale
Hekaluni (Ezra 3:10; Nehemia 12:27, 36). Waimbaji na vyombo vya muziki pale
Hekaluni vilikuwa tofauti kabisa na vile vilivyotumiwa katika maisha ya kila
siku ya watu.
Kupitia fani ya muziki, laana
na giza limeingia kanisani. Katika ibada nyingi malaika wa Mungu huwa wanaamua
kuondoka pindi wanapoona nyimbo za zisizofaa na muzuki wa usiofaa unapoanza
kupigwa.
Mjumbe wa Mungu White anasema:
Mambo ya milele
yana uzito kidogo sana kwa vijana. Malaika wa Mungu wanatoa machozi
wanapoandika maneno na matendo ya Mkrisito. Malaika wanazunguka zunguka huko na
huko. Vijana wamekutanika pamoja, kuna mlio wa sauti na vyombo vya muziki. Wakrisito
wamekusanyika hapo, lakini ni nini unachokisikia? Ni wimbo, wimbo wa upuuzi,
ufao katika ukumbi wa dansi. Tazama malaika wanaiondoa nuru kutoka kwao, na
giza nene linawagubika wote walio katika eneo hilo. Malaika wanaondoka kutoka
kwenye tukio hilo. Huzuni ijuu ya nyuso zao. Tazama, wanalia. Hili nililiona
likirudiwa mara nyingi katika makundi yote ya watunzao Sabato…muziki ni sanamu
ambayo wengi wa Wakrisito wa wanaokiri kuitunza Sabato. Shetani hana
kipingamizi kwa muziki kama anaweza kuufanya kuwa njia ya kuyafikia mawazo ya
vijana…Vijana wanakutana kuimba, na ingawaje wanakiri kuwa ni Wakristo, mara
kwa mara wanamvujia Mungu heshima na imani yao kwa mazungumuzo ya upuuzi na
uchaguzi wao wa muziki.
Midundo ya muziki wa lege, jazz, rock za
aina zote, na mingineyo, pale tu inapoanza kupigwa, malaika wa Mungu hawabaki
hapo tena. Wanaondoka mara moja kwenye mkutano huo. Ni mkutano wa laana huo. Na
malaika wa Mungu wakiondoka, mara moja shetani na malaika zake huja na kuchukua
nafasi na kuongoza mkutano huo.
Nuru ya Mungu huondolewa kwenye mkutano
huo. Giza nene huwafunika hao waliokusanyika kwa ibada mahali hapo. Badala ya
kuwa mkutano wa Baraka unageuka kuwa mkutano wa laana kubwa ajabu. Rubani wa
mikutano hiyo anakuwa ni ibilisi yule nyoka wa zamani. Je, hapo mahali ambapo
ibilisi anongoza, unategemea waimbaji na wapiga vyombo na hasa keyboard
wataitikia maonyo yoyote? Kamwe hawawezi kusikia maana roho mchafu wa shetani
anakuwa ametawala na kuongoza mkutano huo. Jua wazi kwamba kabla hata malaika
wa Mungu hawajaoondoka, Roho Mtakatifu anakuwa amekwisha ondoka zamani. Pepo
mchafu anakuwa ametawala mkutano au ibada hiyo asili mia moja. Kwa sababu hiyo
kanisa zima linakuwa chini ya chuki ya Mungu kwa sababu tu ya hao wachache
ambao wamekataa neno la Mungu bali hufuata mapenzi yao.
Mungu anawaita watu wake kuwa watulivu
na wenye msimamo. Wanapaswa kuwa waangalifu sana wasije wakamwakilisha vibaya
na kuyavunjia heshima mafundisho makuu ya ukweli kwa njia ya maonyesho ya
kigeni, kwa machafuko na makelele. Kwa haya, wale wasioamini wataongozwa
kufikiri kuwa Waadventista wa Sabato ni kikundi cha ulokole…wakati waumini
wanapohubiri ukweli kama ulivyo katika Yesu, wanadhihirisha utakatifu, utulivu,
na sio dhoruba ya machafuko.
Wote tunajua
kuwa uimbaji wa kilokole ni wa midundo ya ngoma, kucheza na kurukaruka na sauti
ya makelele ya juu sana. Kuna hitaji kubwa kwa mtu yeyote anayeijua kweli
kusimama na kukemea uimbaji huu ambao ibilisi ameuingiza katika kanisa la Mungu
kwa makusudi ya kuwapoteza watu Mungu yamkini hata walio wateule.
Ulokole, mara unapokuwa umeanza na
kuachwa bila ya kuzuiwa, ni vigumu kuuzima kama vile moto ambao tayari unakuwa
umeanza kuteketeza nyumba. Wote ambao wameingia katika hali ya ulokole na
kukuubali huu ulokole, ni vyema sana waingie katika kazi za kidunia; kwa maana
kwa mwelekeo huu wa matendo yasiyo sahihi wanamvunjia heshima Mungu na
kuhatarisha watu wake. Mivuto mingi kama hii itainuka wakati huu, wakati ambapo
kazi ya Bwana ingeinuliwa, iwe safi, bila ya kuchafuliwa na ushirikina na
hadithi. Tunapaswa kuwa waangalifu, kudumisha uhusiano wa karibu pamoja na
Kristo, ili kwamba tusidanganywe na shetani. Mungu anataka utaratibu na nidhamu
katika huduma yake, sio msisimuko na machafuko. Kwa sasa hatuwezi kuelezea kwa
usahaihi matukio ambayo yatatendeka katika ulimwengu wetu huu siku za usoni,
lakini hiki ndicho tunachokijua, kwamba huu ndio wakati ambapo tunapaswa
kukesha katika maombi; kwa maana siku kuu ya Bwana iko karibu sana. Shetani
anaongeza nguvu zake. Tunapaswa kuwa watu makini na watulivu, na kutafakari
kweli za ufunuo. Msisimuko haukubaliki kwa kukua katika neema, usafi wa kweli
na utakaso wa roho.
Dini ya kilokole imeuteka ulimwengu wa Kikristo na
vile vile ulinasi wa kipagani. Sasa pia imeuteka ulimwengu wa Kikristo wa kanisa
la Mungu la Waadvnetista wa Sabato. Ni wapi mtu ataweza kwenda asiweze kukutana
na uimbaji wa midundo ya muziki na kucheza kwa namna ya kilokole? Nenda katika
kanisa Katoliki ambalo miaka ya zamani lilisifika kuwa ma muziki wa dini hasa,
nenda katika kanisa la Lutherani ambao walikuwa ni waimbaji mashughuli katika
ulimwengu wa Kikristo, Moravian, Anglicana, na kadhalika, utakutana na muziki
wa midundo na kucheza na kurukaruka.
Nenda kweye
virabu vya pombe kwamba ni vijijini au mijini utakutana na muziki wa midundo na
kurukaruka iliyoimbwa na wale anaojidai kuwa ni Wakristo na ati wanamwimbia na
kumchezea Yesu. Walevi waliisha acha miuziki ya wapigaji wa kidunia maana hao
hawamdhihaki Yesu na wamegeukia muziki wa upagani mambo kikristo.
Je, Roho ya Unabii inatoa maagizo gani katika
fani ya uimbaji na muziki kwa ujumla?
“‘Watu wengi, vijana kwa wazee, kwa maneno
matamu wanaeleza sababu zao za kutumia muziki bandia…kuwa wanaupenda. Hii ni
tabia ya kuogofya. Wavuta bangi wanaweza kutetea matumizi yao ya dawa za
kulevya kwa maneno hayo hayo, tunaipenda.’ Je, kusema vile kunaweza kuhalalisha
matumizi yao? Je, jema na baya‘Muziki umechukua muda ambao ungetumiwa kwa
maombi. Muziki ndio kinyago kinachoabudiwa na wengi wa Wakristo watunzao
Sabato. Shetani hapingi muziki wowote ikiwa anaweza kupitia hapo kufikia kwenye
mawazo ya vijana. Muziki ukitumiwa vibaya huongoza moyo kuwa na kiburi, upuuzi
na upumbavu. Muziki kama huo ni laana ya kutisha.’
‘Mara nyingi nimeumia moyoni kusikia sauti
kali za juu mno zikiharibu maneno matakatifu ya nyimbo za sifa. Sauti kali
zinazokwaruza hazifai kabisa katika ibada yenye furaha mbele za . nilitaka
kuziba masikio au kukimbia kutoka mahali hapo.’
‘Muziki unaweza
kuwa na uwezo mkubwa sana kwa wema ingawa hatutumii uwezo huo wote upasavyo
kama sehemu ya ibaada. Mara nyingi uimbaji hutendwa kutokana na hisia au
kukidhi malengo maalum na nyakati zingine waimbaji huachwa kusitasita hatimaye
muziki huwa na matokeo mabaya katika mawazo ya wasikilizaji. Lakini wakati
mwingine huwa vigumu zaidi kudhibiti waimbaji na kuwa fanya wafuate utaratibu
kuliko kuboresha mazoea ya maombi. Wengi wa waimbaji hupenda kufanya vitu
katika mitindo yao wenyewe, hukataa kushauriwa wala hawavumilii kutawaliwa.’
‘Mazoea mabaya
na mwelekeko wa dhambi hutiwa nguvu na kuimarishwa na burudani hizi. Nyimbo za
dunia, kuyumbisha sehemu fulani za mwili kunakoashiria hisia za msisimko wa
mapenz, maneno na mwelekeo mwovu uaathiri mawazo na kushusha maadili. Kila
kijana mwenye mazoea ya kuhudhuria matamasha kama hayo tabia zao huchafuliwa.
Katika nchi yetu [Marekani] hakuna kitu kingine chenye mvuto mkubwa kinachotia
sumu mawazo yanayoharibu moyo wa kupenda mambo ya kiroho na kupunguza hamu ya
utulivu na furaha ya kweli maishani kama tamasha la burudani.’
‘Shetani anaelewa ni kiungo gani cha mwili cha
kushitua ili mwili wote usisimke na kuchangamsha akili kisha Kristo hatamaniki
tena moyoni.’
‘Muziki mbaya
hujaa lugha isiyoeleweka na sauti zisizolingana. Mungu hapendezwi na
mvurugano.’
‘Nawezaje kuvumilia fikira hii ati “wengi wa vijana
wetu wa kizazi hiki hawatafikia uzima wa milele. Oh! Ningalipenda kuwa hizo sauti za vyombo vya muziki zikome ili vijana
wasiendelee kutumia muda wa thamani kubwa kwa kujifurahisha tu.’
‘Malaika wanavinjari karibu na
nyumba ambamo vijana wanakutana. Kuna mvumo wa sauti za vyombo vya muziki.
Wakriso wanakutana pale, lakini unasikia kitu gani pale? Ni nyimbo za pambio za
kipuuzi tu zisizositahili kuimbwa katika ukumbi wa ibaada. Tazama malaika
watakatifu hukunja mbawa zao karibu nao, ndipo wale walio nyumbani hufunikwa
gizani, kasha malaika huondoka pale, nyuso zao zikijaa huzuni, wanalia. Haya
niliyaona mara nyingi yakitokea kati ya makundi ya watunzao Sabato.’
‘Katika uzoefu wa wale ambao
maisha yao hutawaliwa na nyimbo za “pop”, “Regge”, nk. Swala la mema na mabaya
hufikiriwa juu juu tu.’
‘Muziki mbaya huimbwa na kwaya za
kidunia ambazo hutegemea kupata fedha.’
‘Kujionyesha sio dini wala utakaso.
Hakuna kinachomchukiza Mungu kulko muziki ambao unaotolewa na vyombo wakati
ambapo wanaopiga vyombo hivyo hawakujitoa kamili kwa Mungu.’
‘Mtindo wa mavazi yavutiayo sana, nyimbo
zisizo fuata taratibu za maadili ya uimbaji, hazikaribishi kwaya za malaika wa
mbinguni makanisani namachini pa Mungu, vitu hivi vyote ni matawi ya mtini
usiozaa matunda bali majani mabichi tu.’
Samuele Bacchocch, The Chrsitian and the Rock Music:
A Study on Biblical Principles of Music, ‘Biblical Principles of Music, p. 193.
Samuele Bacchiocchi,
The Christian and the Rock Music: A Study on Biblical Pricinciples of
Music, Biblical Pricnicples of Music, pp 194-5 cf. Bible Works; Benjamin
Davidson, The Analytical Hebrew and Chaldee Lexcon (Grand Rapids, Michigan:
Zondervan Publishing House, 1993), p. 679
Samuelle Bacchiocchi, p. 223.
King James Version, The Study Bible Presenting The
Old and The New Testament in the E.G. White Scripture Comments (Maryland: Review and Herald
Publishing Association, 1993), p. 670.
Rosalie H. Zinke, Adult Teachers Sabbath School Bible
Study Guide: Worship in the Psalms, Lesson 7, p. 77.
Ellen G. White, Selected Messages (3Vols, Washington,
D.C.: Review and Herald Publishing Association, 1958), vol. 2, p. 36.
Ellen G. White, Selectd Messages, vol. 2, p. 37, 38.
Ellen G. White, Selected Messages, vol. 2, p. 37.
Ellen G. White, Testimonies for the Church (9Vools,
Cal: Pacific Press Publishing Association, 1948), vol. 1, p.457
Samuele Bacchiocchi,
The Christian and the Rock Music: A Study on Biblical Pricinciples of
Music, Biblical Pricnicples of Music, pp 194-5 cf. Bible Works; Benjamin
Davidson, The Analytical Hebrew and Chaldee Lexcon (Grand Rapids, Michigan:
Zondervan Publishing House, 1993), p. 679
Samuele Bacchiocchi, The Christian and the Rock Music:
A Study on Biblical Principle of Music, Biblical Principles of Music, p. 201-2.
Samuelle Bacchiocchi,
p. 206
John W. Kleinig, p. 80 (Samuelle Bacchiocchi p. 206).
Samuelle Bacchiocchi, p. 206.
Garen L. Wolf, Music of the Bible in Christian
Perspective (Salem, OH, 1996), p. 287 cf. Samuelle Bacchiocchi, p. 207.
Samuelle Bacchocchi, p. 207.
Samuelle Bacchiocchi, p. 208.
Ellen G. White, Testimonies for the Church (9Vols,
Cal. : Pacific Press Publishing Association, 19480, VOL. 1, 506.
Ellen G. White, Selected Messages, vol. 2, p. 36.
Ellen G. White, Selected Messages, vol. 2, p. 35.
Ellen G. White, Testimonies for the Church (9vols, ),
vol. 1, p. 506.
Ellen G. White, Evangelism, p. 508.
Ellen G. White, Evangelsim, pp 507-8
Ellen G. White, Testimonies for the Church (9vols, ),
vol. 4, p. 653.
Ellen G. White, Testimonies for the Church (9
vols, ), vol. 1, p. 497.
Ellen G. White, Evangelism, p.510.
Ellen G. White, Testimonies for the Church
(9vols, ), vol. 2, p. 144.
Ellen G. White, Messages to Young People, p. 97, 297.
Review and Herald, Decewmber 2, 1972.
Ellen G. White, Evangelism, p. 509.
Ellen G. White, Evangelism, p. 510.
Ellen G. White, Evangelism, p. 511.