MAMBO SABA AMBAYO NI LAZIMA TUFANYE ILI KUMWAGIWA MVUA YA
MASIKA
IMEKUSANYWA NA KUFASIRIWA PETRO TUMAIN
Kuna mambo saba
ambayo hayakwepeki kwa mtu yeyote anayetarajia kumwagiwa mvua ya Masika.
Masharti haya yako saba, hii inamaana kwamba ni lazima msafiri wa kwenda
mbinguni awe nayo yote au akose yote.
1)
Watu
waliopata nuru (Enlightened)
2)
Watu
walioshinda.(Victory Over Sin)
3)
Watu
wenye upendo.
4)
Watu
wa maombi.
4) Watu
wafanyao kazi.
6)
Watu
wenye kiasi.
7)
Watu
watunzao sabato
Ni muhimu
tuzingatie haya haya masharti saba kwa maombi . hapa mni mkusanyiko wa nukuu za
kalamu ya uvuvio zenye kudhihirisha uhalisia wa maswala yaliyoorodheshwa hapo
juu.
1.
WATU
WALIOPATA NURU.
Kabla ya kusoma
ifahamike kwamba , swala la kupata nuru ni SHARTI LA KUWA MWANAFUNZI MAKINI
SANA WA MAANDIKO HUSUSANI VITABU VYA UNABII (DANIELI NA UFUNUO)
“Kumwagwa kwa
Roho wa Mungu ambaye huiangaza dunia kwa nuru yake, hakuwezi kuja mpaka tuwe na watu walioelimika na
kupata nuru”
“Sisi , pamoja
na faida zetu za kidini,twapaswa kujua zaidi leo kuliko tujuavyo.” TM 116.
“Pale vitabu vya
Danieli na ufunuo vitakaeleweka vizuri, waumini watakuwa na uzoefu tofauti
kabisa wa kidini” TM114
“Pale kama
ninadu tutakapoelewa kitabu hiki (Kitabu cha Ufunuo)kinamaana gani
kwetu,kutaonekana kati yetu uasho mkuu.” TM 113
“wale ambao
wanaula mwili na na kunywa damu ya Yesu
watatoa katika vitabu vya Danieli na
Ufunuo ukweli ambao umevuviwa na Roho Mtakatifu .Wataanza katika nguvu kazi
ambazo haziwezi kuzuiliwa.” TM 116
2.
WATU
WASHINDI (WASHINDI WA DHAMBI)
Jambo la msingi
kujua tofauti na dhana potofu iliyosambaa, kila mtu atakaemwagiwa mvua ya
masika ni LAZIMA MVUA YA VULI IWE IMEMWEZESHA KUSHINDA KILA AINA YA DHAMBI
MAISHANI MWAKE. Ili kuelewa vyema somo la kushinda dhambi fuatilia somo la
SAYANSI YA KUSHINDA DHAMBI SHE YA 1 -4 , IMANI RAHISI INAPATIKANA HIVI, USIANZE
SAFARI YA KUSHINDA DHAMBI KABLA YA KUELEWA HILI…n.k…Katika YOUTUBE ACOUNT YA PETRO TUMAINI TV. Pia waweza
kupata series ya vitabu vya haki kwa Imani kwa kuwasiliana na namba 0754202021.
Ifahamike kwamba hakuna kitu tunachohitaji sana sasa kama ushindi dhidi ya
dhambi.
Ni wale
Waadndventista wa Sabato tu waishio leo ambao (1)watapokea kwa moyo wote
ushuhuda ulionyooka-kuzingatia ushuhuda wa Shahidi wa Kweli (Yesu) uliopo
katika Ufunuo 3:14-22 (2) wapokeao wingi wa mvua ya vuli, na (3)kushinda kila
dhambi inayowakabili (besetting sin) na kuakisi kikamilifu sura ya
Kristo,watapokea mvua ya Masika.
“Ujumbe wa
malaika wa tatu umefungamanishwa (swelling)
katika kilio kiluu, na haupaswi kujisikia huru kupuuzia jukumu la
sasa,na kuendelea kukaribisha wazo kwamba wakati flani huko baadae utakuwa
mpokeaji wa mbaraka mkuu, ni wakati gani ambapo bila juhdi yoyote kwa upande
wako uamsho wa ajabu utatokea... Leo wapaswa kuwa na chombo chako kimetakaswa
tayari kwa kupokea manyunyu ya mvua ya masika, kwa kuwa mvua ya masika itakuja,
ma mibaraka ya Mungu itajaza kila Roho ambayo imetakaswa kutoka katika kila
uchafu. Ni kazi yetu leo kujitoa roho zetu kwa Yesu, ili kwamba tuweze
kunufaika wakati wa kuburudishwa kwa uwepo wa Bwana- tayari kwa ubatizo wa Roho
Mtakatifu.” RH March 22, 1892;Ilinukuliwa katika 1 SM 190,191
“Wale ambao (1)
huinula katika kila jaribu na (2) hushinda kila jaribu na (3) kushinda, iwe kwa
gharama yoyote, wamesikia ushaur wa shahidi wa kweli na watapokea mvua ya masika na hivyo kufanywa wafae kwa
kunadilishwa (translation)” 1T 187
(msisitizo umeongezwa)
Ushuhuda
ulionyooka ni nini (Straight Testimony) ? Ushuhuda wa shaihidi wa kweli ni
nini?
1)
“kuinuka
katika kila jaribu”(Come up to every point)
2)
“kushinnda
kila jaribu”
3)
Na “kushinda (kila dhambi), iwe kwa gharama
yoyote.”
Hii si jumla ya
“Ushuhuda ulionyooka” na “ushauri wa shahidi mwaminifu.” Pia kuna dhahabu
(Imani na Upendo), vazi jeupe (Vazi la tabia ya haki ya Kristo) na dawa ya
macho (utambuzi wa Kiroho wa Roho Mtakatifu). Ushuhuda ulionyooka huitaja
dhambi kwa jina lake na huwapa mwito watu wa Mungu kutubu na kuacha dhambi zote. Kufikia juu ya
kiwango.
3.
WATU
WENYE UPENDO- UPENDO WA NDUGU-UMOJA-MPATANO-KITU KIMOJA
“Roho hawezi
kumwagwa wakati utofauti na chuki dhidi ya mmoja na mwingine vinaendekezwa na
washiriki wa kanisa. Kinyongo,Wivu, majungu/ maneno maovu (evil-surmising), ni
ya shetani na kwa kweli yanazuia njia ya utendaji kazi wa Roho Mtakatifu.” 6T
42
“ Hebu Wakristo
waweke kando tofauti zote, wajitoe kwa Bwana kwaajili ya kuwaokoa waliopotea.
Hebu waombe kwa imani ahadi ya ya mbaraka ulioahidiwa, nao utakuja. Kumwagwa
kwa Roho siku za mitume iliuwa ni ‘Mvua ya Vuli,’na utukufu ilikuwa ni
matokeo.Lakini mvua ya masika itakuwa nyingi zaidi” 8T . 21
MUNGU ANATUPIMA
UPENDO WETU KWAKE KWA NAMNA TUNAVYO TENDEANA MMOJA NA MWINGINE
“Pale mvua ya
masika itakapomwagwa, kanisa litavikwa uwezo kwa kazi yake; lakini kaniza kama
lilivyo kwa ujumla kamwe halitapokea mvua hii mpaka waumini wake waweke kando
wivu, majungu/mazungumzo mavu (evil summisings). Wale wanaoendekeza dhambi hizi hawajui uzoefu wa mbaraka wa
upendo.; hawajaamka katika ukweli kwamba Bwana
anaujaribu na kuuthibitisha upendo wao kwaajili yake kwa mtazamo
wauonyeshao kila mmoja kwa mwenzake ,Yesu atwambia , ‘Amri
mpya...pendaneni.’ Amri hii inapoheshimiwa, wivu , mawzo maovu,na mawazo maovu
hayataendekezwa; havitakuwa na nafasi katika kuitengeneza tabia.” (RH Oct 6,
1986.) Msisitizo umeongezwa
4.
WATU WA MAOMBI
“Lakini ni
lazima Mungu aamuru mvua inyeshe. Kwahiyo hatupaswi kuwa wazembe katika kuomba.”
TM 590. Msisitizo umeongezwa
“Hebu sote kwa
mioyo mikunjufu, tuombe kwa juhudi kwamba sasa, katika wakati wa mvua ya masika
, manyunyu ya neema yaanguke juu yetu.” TM 590.
“Twapaswa
kuomba kwa juhudi kwaajili yakushuka kwa Roho Mtakatifu kama wanafunzi
walivyoomba katika siku ya Pentekoste. Kama walimuhitaji katika wakati ule,
tunamhitaji zaidi leo... Bila msaada wa Roho , juhudi zetu kufikisha ukweli
mtakatifu zitakuwa ni bure.” R Aug.25,1896. Msisitizo umeongezwa
5.
WATU WAFANYAO KAZI
Ni vyema na hili
niliweke bayana kabla ya kutazama kile asemacho nabii wa Mungu, swala kuu
linalozungumziwa hapa NI KUFANYA KAZI YA MUNGU KATIKA NA MNA SAHIHI. HII
INAMAANA WATU WASIOJIHUSISHA NA UMISHENARI HAWATAMWAGIWA MVUA YA MASIKA.
Mvua ya masika
kamwe haiwezi kumwagwa kwa Wakristo wavivu, wasiofanya kazi. Kwavile Mvua ya
Masika hutolewa kwa madhumuni ya ushuhudiaji, itamwagwa kwa wale tu ambao
wanaingia kikamilifu katika kazi ya Mungu kwa ubora wa uwezo wao.
“Makanisa yanapokuwa
hai, makanisa yafanyayo kazi, Roho Mtakatifu atatolewa kama jibu kwa maombi yao
ya dhati. Kisha ukweli wa neno
la Mungu utazingatiwa kwa shauku mpya...Kisha watasihi pamoja na roho za
wengine na hawataweza kuziliwa. Kisha madirisba ya mbinguni yatafunguliwa kwa
manyunyu ya mvua ya masika.” RH Feb.25,1890 Msisitizo umeongezwa
“Kumwagwa kwa
Roho Mtakatifu kukuu, ambako kutaiangaza dunia yote kwa utukufu wake,
hakutatokea mpaka tuwe na watu walioangazwa, kwamba kujua kwa uzoefu wa
kimatendo inamaana gani kuwa watendakazi na Mungu. Kwa ujumla
tutakapokuwa, tumejitoa kwa moyo wote katika huduma ya Kristo, Mungu atatambua ukweli huu kwa
kumwaga Roho wake bila kipimo; lakini hili haliwezi kutokea wakati sehemu kubwa
ya kanisa si watendakazi pamoja na Mungu” CS 253;Ev 699 Msisitizo umeongezwa
“Wakati uendekezaji (reproach) wa
uvivu (indolence) na uzembe (sloghtfulness) vitakapo ondolewa mbali na kanisa,
Roho wa Mungu atadhihirishwa kwa utukufu. Nguvu za Mungu zitafunuliwa. Kanisa
litaona msaada wa utendaji kazi wa Bwana wa Majeshi. Nuru ya kweli itaangaza kwa uwazi, miale imara, na
kama ilivyokuwa wakati wa mitume, roho nyingi zitageuka toka kwenye uwongo
kwenda kwenye ukweli.Dunia itaangazwa na utukufu wa Mungu.” 9T 46. Msisitizo
umeongezwa
KAZI YA UMISHENARI HUAMSHA ROHO NA KUMLETA ZAIDI
ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA
“Sheria ya
kujitumikia ni sheria ya kujiangamiza. Sheria ya kujitoa dhabihu ni sheria ya
kujitunza.”DA 623,624
“Uwezo wa kupokea hutunzwa tu kwa kutoa
(Imparting). Hatuwezi kuendelea kupokea hazina ya Mbinguni bila kuiwasilisha
kwa wale wanaotuzunguka” COL 143
“Roho inayokataa kufundisha (imparting) itapotea. “ DA 417 Msisitizo umeongezwa
“Msaada wa pekee
ambao wachungaji waweza kuutoa kwa washiriki wa makanisa yetu si kuhubiri,lakini
ni kuwapangia kazi. Mpatie kila mmoja kitu cha kufanya kwaajili ya
wengine...Kama wakiwekwa kazini,punde wanyonge watasahau unyonge wao (despondency),
wadhaifu watakuwa na nguvu, wajinga watakuwa na akili, na wote wataandaliwa
kuufikisha ukweli kama ulivyo kwa Yesu.” 9T 82.
“Tulijazwa Roho Mtakatifu kwa kadri tulivyoenda na
kuihubiri sabato kwa uwazi.” EW 85
“Ni kanuni ya jumla
(universal principle) kwamba kila mara mtu anapokataa kutumia nguvu alizopewa na Mungu, ngvu huoza na
kupotea. Ukweli usiotendewa kazi maishani, ambao haufundishwi, hupoteza nguvu
yake yenye kutoa uhai maishani.” AA 206 Msisitizo umeongezwa
HAKUNA KITU
KIITWACHO WAKRISTO WASIO HAI. KAMA MTU SI HAI SI MKRISTO. BALI NI ALIYERUDI
NYUMA, HALI YA UPOTEVU!
“Hebu wachungaji wafundishe
washiriki wa kanisa kwamba ili wakue kiroho, ni lazima wabebe mzigo ambao Bwana
ameuweka juu yao,-mzigo wa kuziongoza Roho kwenye ukweli.” GW 200;CS 69,70 Msisitizo umeongezwa
“Wale
watakaokuwa washindi ni lazima wavutwe kutoka katika nafsi zao na kitu
pekee kitakachofanya kazi hii kuu ni kuwa na shauku sana ya wokovu wa wengine.” MH 90.
“Nguvu yako
Kiroho na mibaraka vitawiana na kazi ya upendo na kazi nzuri unazofanya.” 3T
526
“Mungu hawezi
kutupatia uwezo tusionao kwa miujiza, lakini wakati tukitumia uwezo tulionao,
tafanya kazi nasi kuongeza na kuimarisha kila uwezo; nguvu zetu zilizolala
zitaamshwa, nguvu ambazo kwa muda mrefu zilizimwa (Palsied) zitapewa maisha
mapya.” 5T 459
“Nilionyeshwa
watu wa Mungu wakisuburi badiliko fulani liweze kuwatokea. Lakini
watahuzunishwa kwasababu wamekosea. Lazima wafanye kitu. Lazima
wafanye kazi wenyewe. 1T 261. Msisitizo umeongezwa
Hatuwezi
kukutana na Uumgu bila kukutana na Ubinadamu.. ("We can not come in touch
with Divinity without coming in touch with humanity") . COL 384
Maana
ya maneno hayo ni kwamba hatuwezi kukutana na na Mungu isispokuwa tuwe tayari
kukutana na ubinadamu katika huduma ya UPENDO na matendo ya huruma. Kimsingi
huduma hiyo ni sehemu ya utakaso pia, ni huduma inayopaswa kuwa sehemu ya
maisha yetu ya kila Siku "SI KAMA TUNAVYOITEKELEZA KIPROGRAM" Wengi
huduma hii kwetu sio sehemu ya maisha ila tunafanya kama tu program ya kanisa,
nah ii ni hatari sana. Ni lazima huduma ya kuleta unafuu kwa binadamu wenzetu
iwe sehemu ya maisha yetu SI MATUKIO YA TAREHE MAALUMU ZA PROGRAM ZA KIKANISA
AMBAZO TUNATAKA KUTANGAZWA NA VYOMBO VYA HABARI.
NYONGEZA
UHUSIANO -> ROHO MTAKATIFU -> KUVIKWA
UTAKATIFU NA BADILIKO LA TABIA -> KUKAMILISHWA
KUKAMILISHWA TABIA HUKUA KUTOKA KATIKA MAHUSIANO YA
KUSHIRIKI, KUSHUHUDIA NA HUDUMA YA KIKRISTO.
HUDUMA
Kufanana na Mungu kitabia , umoja nae katika
utakatifu , huruma pamoja nae katika upendo, shauku pamoja nae katika ukweli,
na shaku ya Mungu kwaajili ya wokovu wa roho, hauji katika moyo kwa kukaa
nyumbani na kuomba na kusoma biblia zetu na kuimba ya mbinguni. Hapana, haya
yote ni ya muhimu na yana msaada, lakini hayatoshelezi kwa yenyewe. Kitu zaidi
kinahitajika.
Kwa nyongeza
pamoja na yaliyoorodheshwa hapo juu ambayo ni ya lazima, kile ambacho ni muhimu kutuleta katika upatano
na Mungu ni kushuhudia -Christian Service.
“Sheria ya kujitumikia
ni sheria ya kujiangamiza. Sheria ya kujitoa dhabihu ni sheria ya kujitunza.” DA 623,624 Msisitizo umeongezwa.
“Roho ikataayo
kufundisha itapotea.”
DA 417 Msisitizo
umeongezwa.
“ Nguvu
za kiroho zitazidi kuwa dhaifu na kufa kama hazifanyiwi mazoezi katika uongoaji
roho kwa Yesu.” 9T 106
UMISHENARI NDIYO FURSA YA KUTEMBEA NA YESU
“Wale
wanaopuuzia fursa ya kutembea na Yesu katika huduma , hukataa mafunzo pekee ambayo huleta kufaa kwa kushirikiana nae
katika utukufu.” ED 264. Msisitizo umeongezwa
“Ni kanuni ya
jumla (universal PRINCIPLE) kwamba kila mara mtu anapokataa kutumia nguvu alizopewa na Mungu, nguvu huoza na
kupotea. Ukweli usiotendewa kazi maishani, ambao haufundishwi, hupoteza nguvu
yake yenye kutoa uhai maishani.” AA 206 Msisitizo umeongezwa
“Wakati ambapo
hakuna utendaji kazi hai kwaajili ya wengine, upendo hupoa, na umani hufifia.”
DA 825
“Hatuwezi
kuokolewa kwa kukaa kizembe na bila kazi. Hakuna kitu kama mtu aliyeongoka kiukweli
na kuishi maisha yasiyo na msaada. Haiwezekani kwetu kuangukia (drift)
mbinguni.” COL 282
MAAMUZI YA UTEKELEZAJI
HAYAKWEPEKI NA NI MUHIMU
“Nilionyeshwa
watu wa Mungu wakisuburi badiliko fulani liweze kuwatokea.Lakini watahuzunishwa
kwasababu wamekosea. Lazima wafanye
kitu. Lazima wafanye kazi
wenyewe. 1T 261. Msisitizo umeongezwa
TIBA (CURE).
“Ipo lakini tiba moja
tu ya uhakika kwa uvivu wa kiroho, na hiyo ni, fanya kazi, fanya kazi kwa roho
zinazohitaji msaada wako.”
4T 236,CS 106,107. Msisitizo
umeongezwa
DAWA
“Hii ni dawa
ambayo Kristo ameiandika kwaajili ya mwenye moyo-unaozimia, mashaka, roho
inayotetemeka. Hebu wenye huzuni , watembeao kwa maombolezo mbele za Bwana, waamke na
kumsidia mtu anayehitaji msaada.” 6T 266 Msisitizo umeongezwa
MANENO MATATU YA
KUTAZAMWA NA MKRISTO
“Yapo maneno
matatu ya kutazamwa katika maisha ya mkristo , ambayo ni lazima yazingatiwe
kama hatutaki shetani kuiba ushindi (match) kati yetu,yaitwayo, kuwa
macho, omba, kazi.” 2T 283 Msisitizo umeongezwa
DAWA
“Kwa waliokata
tamaa ipo dawa moja ya uhakika-Imani, maombi, kazi.”PK 164,165 Msisitizo umeongezwa
“Kubeba msalaba
hukata ubinafsi kutoka katika Roho.” 5BC 1090
NAFASI YETU
“Tukiwa
waaminifu katika kufanya sehemu yetu, katika kushirikiana nae, Mungu atafanya
kazi kupitia sisi kutekeleza starehe njema ya mapenzi yake. Lakini Mungu
hawezi kufanya kazi kupitia sisi kama hatufanyi juhudi yoyote. Kama
tunapata uzima wa milele, ni lazima tufanye lazi, na tufanye kazi kwa juhudi...Tabia
tuziundazo hapa zitaamua mwisho wetu wa milele. Sehemu yetu ni kuondolea dhambi
mbali, tutafute kwa kunuia ukamilifu wa tabia. Kwa kadri tufanyavyo hivyo, Mungu hushirikiana nasi kutufanya tufae
kwaajili ya nafasi katika ufalme wake...
Kuyafanya
mapenzi ya Mungu ni muhimu kama tutakuwa na
maarifa yanayoongezeka kumhusu yeye. Hebu tusidanganywe na na dhana
zitajwazo mara kwa mara, ‘chote
upaswacho kufanya ni kuamini.’ Imani na
matendo ni makasia mawili (oars) ambayo ni lazima tuyatumie kwa usawa kama
tunasukuma njia yetu kupanda mkondo wa maji dhidi ya wimbi la kutokuamini.
‘Imani, kama haina matendo,imekufa, kwa yenyewe.’ Mkristo ni mtu wa kufikiri na
kutenda. Imani yake ikiwa imekita mizizi kwa Kristo. Kwa imani na matendo mema
hutunza hali yake ya kiroho kuwa imara na yenye afya,na nguvu zake kiroho huongezeka kadri anavyokazana
kufanya kazi za Mungu.” RH June 11,1901. Msisitizo umeongezwa
NJIA PEKEE YA KUKUA KATIKA NEEMA
“Njia
pekee ya kukua katika neema ni kufanya kwa shauku kazi ambayo Kristo alituagiza,
kuifanya kwa kiwango cha uwezo wetu, katika kusaidia na kubariki wale
wanaohitaji msaada tuwezao kuwapa.” SC 86. Msisitizo umeongezwa
“Wale ambao
watapata zaidi uzoefu wa utakaso wa kweli katika roho zao, wapaswa kufiksha
kweli kwa wale ambao ni wajinga wa huo. Kamwe hawawezi kuwa na kazi kubwabzaidi
yenye kuinua,na kuimarisha.
Those who would
experience more of the sanctification of the truth in their own souls, should
present the truth to those who are ignorant of it. Never will they find a more
elevating, ennobling work. . . . {5MR
346.1}
Wale ambao
watapata Zaidi uzoefu wa utakaso wa ile kweli katika roho zao, watapaswa
kuuwasilisha ukweli kwa wale ambao ni wajinga wa huo. Kamwe hawatapata kazi ya
kukweza, na uwezo….{5MR 346.1}
“Nguvu yako Kiroho na mibaraka vitawiana na
kazi ya upendo na kazi nzuri
unazofanya.” 3T 526....
“Nguvu ya kushinda dhambi
hupatikana vizuri kwa kuwa na shauku katika huduma. (Strength to resist
evil is best gained by aggressive service.)--The Acts of the Apostles, p.
105. {ChS 100.5} Msisitizo umeongezwa
“Tunakuwa washindi kwa
kuwasaidia wengine kushinda.”7BC 974
Hakuna kitakachokupa mifupa, na misuli katika wito wako kama kutumika kuendeleza kazi
ambayo unadai kuipenda. “Northing will give bone and sinew to your piety
like working to advance the cause you profess to Love.” 4T 236. Msisitizo umeongezwa
“Mungu Angefikia
dhumuni katika kuokoa wadhambi bila msaada wetu, lakini ili kukuza tabia kama
ya Kristo kazima tushiriki katika kazi yake.”DA 142
“Nilionyeshwa
watu wa Mungu wakisuburi badiliko fulani liweze kuwatokea.Lakini watahuzunishwa
kwasababu wamekosea. Lazima wafanye
kitu. Lazima wafanye kazi
wenyewe. 1T 261. Msisitizo umeongezwa.
Roho ya unabii
pia huelezea kwamba hatuwezi kukutana na Uungu kama hatuwezi kugusana na
binadamu.
Yule akataae
kufundisha atapotea.Hakuna kitu
kiitwacho mkristo mzembe asiye hai.
6.
WATU WENYE KIASI
Kwamba
Mungu anajihusisha na afya yetu na furaha
hapa duniani vilevile na ukuaji WA Tania yetu na hatima ya milele, no
ukweli WA kuvutia. Kiasi inamaanisha
kutotumia kabisa kilichokatazwa, na kutumia kwa wastani kilichoruhusiwa. Hapa
ndipo huja umuhimu wa somo la matengenezo ya afya kama linavyofundishwa na
Biblia na Roho ya unabii, kwa wengi limechukuliwa kama somo lisilo na uzito
LAKINI HAPA UTAGUNDUA LINA ATHARI KATIKA UMILELE WETU.
Ujumbe
wa afya ni zawadi ya pekee sana kwa kanisa la masalio . Utoaji wa ujumbe huu ni
mojawapo ya mambo makubwa sana ambayo Bwana amefanya kwaajili yetu. Kwakweli ni
kipaumbele cha pekee kuwa na maelekezo ambayo Mungu amefunua kwetu kuhusu
uhusiano kati ya mtindo wa kiafya na ukuaji wa tabia.
3
Yohana 1:2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama
vile roho yako ifanikiwavyo.
Kadri
utakavyosoma nukuu hizi, nikusihi usome sana kitabu cha MINISTRY OF HEALING,
COUNSELS ON DIET AND FOODS kwa upande wa Kiswahili pitia KUTAYARISHA NJIA
SEHEMU YA KWANZA SURA TATU ZA MWISHO.
Ni
kupitia usomaji wa nukuu zifuatazo BWANA ALINIWEZESHA KUPATA NGUVU YA KUFANYA
MATENGENEZO YA AFYA NA KUACHA UTUMIAJI WA NYAMA. NINAAMINI ROHO WA KRISTO HATAKUACHA
VILE VILE UMALIZAPO KUSOMA NUKUU HIZI
Hebu
daima tukumbuke Kwamba " Ilikuwa no kwa upendo Baba yetu wa mbinguni Alituma
nuru ya matengenezo ya afya ili kutulinda dhidi ya maovu yanayotokana na
kuendekeza uchu wa chakula usio dhibitiwa. " (CDF 243) Msisitizo
umeongezwa.
"Dhumuni
lake no kupata maendeleo makuu ya mwili, akili na roho." (CDF 457)
"...kuutibu
mwili kuna kila kitu kinachoshughulika na nguvu na usafi wa akili na
moyo." 7BC 909
Kama
ujumbe huu umetolewa kwetu kupitia mafunuo, je hatupaswi kuuzingatia sana
kuliko sasa?
Wengi
wa Waadventista wa sabato wanakufa kila Siku kutokana na kukosa maarifa ya
kuishi kwa afya, wengi wanachimba makaburi yao kwa midomo yao, wanajinyonga kwa mpango wa awamu - kwa
mienendo isiyo sahihi ya kula na kunywa. Wengi zaidi wanaenda kinyume na
mapenzi ya Mungu, na badala ya kukamilishwa Tabia zifanane na Kristo , wanazidi
kunajisika na kudhoofika na kujimaliza kwasababu hawasomi Roho ya unabii.
Kiasi
na kuishi maisha ya kuzingatia kanuni za afya ni mambo ya muhimu sana kwasababu
mienendo sahihi ya kiafya husaidia katika kukuza tabia ya Kristo ndani yetu
wakati mitindo mibaya ya afya hupambana dhidi ya kukuza Tabia ya Kristo.
"Wale
wanaougua katika mwili kwa ni karibu mara zote huumwa katika roho , na roho
inapougua na mwili hufanywa uugue pia." MS 62, 1900 Msisitizo
umeongezwa.
Tunajua
kuna muuunganiko na uhusiano usioweza kutenganishwa kati ya mienendo ya kuafya
na ukuaji wa Mkristo. Haiwezekani kwa mtu asiye na kiasi kukuza Tabia ya Kristo
, kipengele hiki kuhusu afya kimebeba kauli za muhimu kuhusu afya ambazo
Waadventista wa Sabato wengi hawajui kwamba zipo katia roho ya unabii.
Kwasababu
ujumbe WA afya na Tabia vinahusiana moja kwa Moja na kutegemeana, ni athari
gani kimoja huwa nazo kwa kingine. Kila Mwadventista wa Sabato aliyesoma vizuri
anajua kuna kanuni nane za afya.
"(1)
Hewa safi, (2) mwamga wa jua, (3) Kujizuia (4) Pumziko (5) Mazoezi, (6) Mlo
sahihi (7) Matumizi ya maji (8) Kutumaini katika nguvu za Mungu, hizi ni Tina asili
(Natural Remedies)." (MH 127) Msisitizo umeongezwa.
Hapa
nitaielezea moja tu kwasababu imepuuziwa sana na Waadventista wa Sabato - ile
ihusuyo kula- hususani- kula vyakula vya nyama.Wale wanaokula hivyo hawatambui
umuhimu wa kula na kunywa kwa utukufu wa Mungu. (1 Kor 10:21)
Waadventista
wa Sabato hawaachi kula nyama hususani kutokana na msimamo wa kiafya- vilevile
kwasababu mtu anajiingiza katika hatari ya kula nyama zenye magonjwa , na vile
vile kwasababu sio chanzo bora cha protini, bali ni kwasababu ulaji wa nyama
hufanya iwe vigumu kukuza tabia ya kufanana na Kristo.
Vyakula
vya nyama hufanya iwe vigumu kuwa mvumilivu na mwema, mwenye upendo na afananae
na Kristo. Waadventista WA Sabato hawatambui mwamba ulaji WA nyama una msukumo
ule ule katika mielekeo ya kitabia (disposition) ya mwanadamu kama ilivyo ya
mnyama - kuwafanya wasiwe wavumilivu, wenye hasira za haraka (irritable),
wagomvi (cantankerous) , waovu (vicious). Hili limethibitishwa kisayansi tena
na tena.
"Wapo
wachache wanaoelewa wapaswavyo kuelewa ni kwa vipi mienendo yao kiafya ya ulaji
inahusiana na afya yao, Tabia, na kutumika kwao katika dunia hii, na matokeo
yao ya milele." PP 599
Ulaji
wa vyakula vya nyama (1) huwanyang'anya watu upendo na huruma, (2) hufanya
asili iwe ya kinyama , (3) huweka sumu katika mfumo wadamu, (4) huwasha hisia
Kali za mapenzi , (5) huharibu huruma na kupendana (6) hudhibiti utambuzi na
hamasa za kiroho, (7) humfanya mtu awe so mvumilivu na mwenye ugonjwa WA hasira
(ill-tempered) , na (8) hupotosha hamu ya chakula.
"Kwa
kutumia vyakula vya nyama (1) asili ya kinyama huimarishwa na (2) asili ya
kiroho hudhoofishwa…" CDF 383. Msisitizo umeongezwa.
“Nimepewa
maelekezo kwamba chakula cha nyama kinatabia ya kufanya asili iwe ya kinyama
(animalize the nature) , kuwanyang'anya wanaume na wanawake ule upendo na
huruma ambavyo wanapaswa kuhisi kwa kila mmoja, na kufanya tamaa za chini
kuendesha nguvu za juu za utu. Kama ulaji wa nyama ungekuwa ni afya, si salama sasa. Saratani, uvimbe ,
na magonjwa ya mapafu kwa sehemu kubwa husababishwa na ulaji WA nyama."
9T 159 Msisitizo umeongezwa.
He
hii yaweza kuwa sababu no kwanini hakuna tena upendo katika Makanisa ya Wadventista wa Sabato? Je
hili laweza kuelezea no kwanini baadhi ya Waadventista wa Sabato wameacha kukua
Kiroho- miaka 10, 20, 30 imepita - na bado no baridi wasioelewa, wenye kiburi
na tamaa, na pia wagomvi?Je, hili laweza kuelezea no kwanini wengi bado no
watoto katika Kristo, wana akili za kidunia, wenye tamaa ya vitu na
wasioridhika ? Je hili laweza kutupa sababu ni kwanini baadhi ya makanisa
huundwa na washiriki vuguvugu, wasioelewa na hata washiriki wenye uadui? Je
Mungu anaweza akawa akiendelea kuzuia mvua ya masika kwa Manisa kutokana na
sababu hii? Ni nini kilitokea kwa wana WA Israeli waliotamani mabakuli ya nyama
za Misri?
1
Wakorintho 9:25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi
hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji
isiyoharibika.
"Wapenzi,
nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipinganazo na
roho." (1 Petrol 2:11)
"Afya...
yapaswa kulindwa kwa utakatifu kama Tabia." CT 294
"Mwili
ni mfumo pekee ambao kupitia huo akili na roho hukuzwa kwa kuijenga Tabia
juu." MH 130
“Ubongo
ni makao makuu ya mwili . Kama nguvu za utambuzi zikidhoofishwa kupitia kukosa
kiasi kwa aina yoyote, mambo ya umilele hayawezi kutambuliwa." Ukombozi au
Kujaribiwa kwa Kristo katika Jangwa, uk . 56. (Redemption or The Temptation of
Christ in the Wilderness, p. 56)
“Ubongo
huharibiwa kutokana na hali ya tumbo," 7T 257.
“Kukosa kiasi ni dhambi."
CDF 43 Msisitizo umeongezwa.
“Ni
dhambi kubwa kuvunja sheria za uhai wetu (Laws of our being) kama kuvunja moja
ya amri kumi, kwasababu hatuwezi kufanya mojawapo bila kuvunja amri za Mungu."
2T 70 Msisitizo umeongezwa.
"Kuvunja
sheria za kimwili (physical law as) ni kuvunja amri za Mungu…" CDF
43. Msisitizo umeongezwa.
"Kila
kitendo ambacho huharibu nguvu za mwili, akili, na roho no dhambi." MH 113
Msisitizo umeongezwa.
MAANA NZURI YA DHAMBI
“Chochote
kinacho dhhofisha uwezo wetu wa kufikiri, hudhohofisha uwezo wa utambuzi wetu,
hudhohofisha hali yetu ya kumtambua Mungu, au kuondoa shauku ya mambo ya
kiroho, kwa kifupi chochote kinachoongeza mguvu ya mwili wako juu ya akili,
kitu hicho ni dhambi kwako haijalishi kiwe kizuri kiasi gani kwa chenyewe."
Susanna Wesley (Mama yake John Wesley)
"Ujinga
katika somo hili (matengenezo ya afya) la muhimu, ni dhambi..." CH
40 Msisitizo umeongezwa. Msisitizo umeongezwa.
"
Yule
anaebakia katika katika uovu unaotokana na ujinga wa kanuni za afya na uzima ,
na ambae kwa maamuzi yake huvunja kanuni hizi, hutenda dhambi dhidi ya Mungu.
" CT 295. Msisitizo umeongezwa.
"Chochote
kinachodhohofisha afya , si kwamba hudhohofisha nguvu za mwili tu, lakini pia
huwa na tabia ya kudhohofisha nguvu za kiakili na kimaadili pia."
MH 128 Msisitizo umeongezwa.
"...Utumiaji
wa vyakula vya nyama...Je hatupaswi kubeba ushuhuda wa maamuzi dhidi ya
kuendekeza hamu ya chakula iliyopotoshwa?" 9T 159 Msisitizo
umeongezwa.
"Kama tumbo
halitunzwi vizuri, uundwaji wa tabia nyoofu, ya kimaadili utazuiliwa."
9T 160. Msisitizo umeongezwa.
"Lakini wale ambao ni watumwa wa tamaa ya chakula watashindwa katika
kukamilisha tabia ya Kikristo." 3T 492. Msisitizo
umeongezwa.
"Haiwezekani kwa wale wanaoendekeza tamaa ya chakula kupata ukamilifu wa
Kikristo (Christian
Perfection)." 2T 400
"Ukamilifu
wa tabia hauwezi kupatikana wakati sheria za asili zinavunjwa; kwa kuwa huku ni
kuvunja sheria ya Mungu." OHC 266
"Huwezi
kupata ukamilifu wa Kikristo isipokuwa umepata udhibiti mkamilifu wa roho
yako." 2T 311
"...chakula
kimwili huathiri akili na tabia/ silika ya moyo (disposition)." AH 252.
"Wengi hudhohofisha tabia zao kwa kula bila utaratibu." CDF. 126 Msisitizo umeongezwa.
"Kiasi
katika ulaji ni lazima kifanyiwe mazoezi kabla hujawa mtu mvumilivu." 2T
405 Msisitizo umeongezwa.
"Mungu
hawezi kuruhusu Roho Wake Mtakatifu juu ya wale ambao... (kwa kujua) hodhohofisha akili na mwili." CDF 55. Msisitizo
umeongezwa.
"Hatma ya umilele wetu hutegemea katika
msimamo thabiti wa kiasi katika mienendo
ya afya,..." 3T 489.
"Tumaini letu pekee katika uzima wa milele ni kupitia kuleta tamaa ya
chakula na tamaa za mwili kwa kuzisalimisha chini ya mapenzi ya Mungu."
DA 122
"Kila
uvunjaji wa kanuni katika ulaji au unywaji, huondoa makali ya viungo vya fahamu,
kufanya isiwezekane kwavyo kukubali au kuweka thamani halisi katika mambo ya
milele." CH 38
"Unywaji
wa chai na kahawa ni dhambi." (CDF 425.)
"Kila shilingi iliyotumika
kwaajili ya Chai, kahawa , na nyama ni mbaya kuliko iliyopotezwa ...(Every
penny expended for tea, coffee, and flesh meat is worse than wasted); kwa kuwa
vyakula hivi huzuia maendeleo ya nguvu za
kimwili, kiakili na kiroho. " CDF 402. (See also CDF 381; 9T
153,154)
USHAURI WA SHETANI
Baadhi
hudhani kwamba hawawezi kufanya matengenezo, kwamba afya itatolewa kafara kama
wakijaribu kuacha matumizi ya chai, tumbaku, na nyama. Huu ni ushauri wa
shetani. Ni hivi visisimuo vya kudhuru ambavyo kwa hakika huharibu mwili na
kuuandaa mfumo wake kwa magonjwa makali
, kwa kudhohofisha mashine bora ya asili na kuangusha chini nguvu
zilizosimamishwa dhidi ya magonjwa na kuoza mapema.(premature decay).... {CTBH
153.1}
Some
think they cannot reform, that it would ruin their health to leave off the use
of tea, tobacco, and flesh-meats. This is a suggestion of Satan. These hurtful
stimulants will surely undermine the constitution, and prepare the system for
acute disease; for they impair nature's delicate machinery, and batter down the
fortifications she has erected against disease and premature decay. {CTBH 153.1}
Utumiaji
wa visisimuo visisvyo vya asili ni uharibifu kwa afya, na wenye msukumo wa
kudhohofisha katika ubongo, kufanya isiswezekane kuyakubali mambo ya umilele.
Wale wanaoendekeza miungu hiyo hawawezi kuweka thamani kwa usahihi katika
wokovu ambao Kristo ameutoa kwaajili yao kwa maisha ya kujikana, sadaka ya
daima, na maonyo, na hatimaye kwa kujitoa maisha take yasiyo na dhambi kuokoa
mwanadamu anaepotea toka kwenye kifo.
"Mlo wa nyama ni swami makini. Je
wanadamu waishi kwa nyama ya wanyama waliokufa? Jibu kutoka kwa nuru ambayo
Mungu ametoa ni, HAPANA, hapana thabiti (decidedly no) ....wanyama
wachache sana wako huru mbali na magonjwa." CDF 388; MS 3, 1897. Msisitizo
umeongezwa
"Magonjwa
katika wanyama yanongezeka kwa uwiano na kuongezeka kwa maasi katika
wanadamu." CDF 366 (Na Je jamii ya wanadamu haijakaribia kukijaza kikombe
chake cha uovu?)
"Imekuwa
ikionyeshwa kwangu kwa uwazi kabisa kwamba watu wa Mungu wanapaswa kuchukua
msimamo thabiti dhidi ya ulaji wa nyama. Je Mungu Angewapa watu wake kwa miaka 30 kwamba ili wawe na damu safi na
akili safi, ni lazima waache kula nyama, kama hakuwataka kuzingatia ujumbe
wake?" Notebook
Leaflets, Elmshaven Leaflets, Vol 1, No. 35, p.2 Msisitizo umeongezwa
"Kwanini baadhi ya ndugu zetu
wachungaji hudhihirisha shauku ndogo katika matengenezo ya afya? Hakuna mtu
apaswae kutengwa kama mwalimu wa watu wakati kielelezo chake kama mfundishaji
kinapingana na ushuhuda ambao Mungu amewapa watumishi wake kuubeba kuhusiana na
ulaji, kwakuwa hili litaleta mkanganyiko (confusion). Upuuziaji wake
wa matengenezo ya afya utamfanya asifae kusimama kama mjumbe wa Mungu." 6T
378
"Hebu hata mmoja wa
wachungaji wetu asitoe mfano mwovu kwa
ulaji wa nyama." CDF 399
Hawana cha kujitetea hata
kidogo kwa kula nyama ya wanyama waliokufa... Je twaweza kuwa na imani katika
wachungaji ambao, katika meza ambazo nyama huletwa, huungana na wengine katika
kuila?" (Pacific Union Recorder, Oct 9, 1902; MS 3, 1897.
Tazama pia CDF 402. Msisitizo umeongezwa
Oh
Bwana tupatie wachungaji ambao ni watiifu kwa mashauri yako. Tupatie wchungaji
ambao utawajaza Roho . Tupatie wachungaji ambao tutawaamini.
"Maelekezo yametolewa kwangu kwamba matabibu
ambao wanatumia nyama na kuiandika itumiwe na wagonjwa , hawapaswi kuajiriwa na
taasisi zetu." CDF 290 Msisitizo umeongezwa
"Ulaji wa nyama haupaswi
kuja katika maelekezo ya kitabibu kwaajili ya mtu yeyote kutoka kwa Tabibu
yeyote toka kwa wale wanaoelewa mambo hayo. Magonjwa katika wanyama yanafanya
ulaji wa nyama kuwa jambo la hatari.... Hivyo mambo hata yasiruhusiwe
kwa maelekezo ya tabibu yeyote ambae ana ujuzi wa ukweli wa wakati huu. Hakuna usalama katika ulaji
wa nyama ya wanyama waliokufa, na katika wakati mfupi itakuwa si salama kutumia
chochote ambacho hutoka kwa viumbe wanyama." CDF 441. Msisitizo
umeongezwa
"Katika
nafaka, matunda, mboga , na jamii ya karanga zapaswa kuonekana kuwa aina zote
za vyakula tunavyohitaji." CDF 310
WALE WANAOJIANDAA
KUNYAKULIWA WATAACHA ULAJI WA VYAKULA VYA NYAMA .
“Miongoni
mwa wale am,bao sasa wanangojea kurudi kwa Bwana, ulaji wa nyama hatimaye
utaachwa kabisa; nyama itaacha kuunda sehemu ya lishe yao.” CDF 380, 381. Msisitizo umeongezwa
WAADVENTISTA WENGI WANAONG’ANG’ANIA
KULA NYAMA WATAPOTEA
"Wale
ambao sasa wameongoka nusunusu katika swala la ulaji wa nyama wataachana na
watu wa Mungu na hawataambatana nao tena." CDF 382; RH May 27, 1902; H
575.
"Ushahidi
wa hali ya juu wa ubora wa Mkristo ni kujidhibiti-nafsi." DA 301.
NENO LA
KUTIA MOYO
"Kama ukitafuta msaada toka
kwa Mungu, nguvu Yake itendayo kazi ndani yako itazileta katika udhaifu nguvu
zote zinazopinga, na utaweza kutakaswa kupitia ukweli." RH June
16, 1891. Msisitizo umeongezwa
"Atakubadili
, kwa ajabu atabadili mwonekano usio na matumaini kabisa wenye kukatisha
tamaa." PK 260.
"Je
mlo waweza kifanya Nini nasi? Kila kitu , kama tuko tayari kusalimisha
vyote." OHC 19.
TWAWEZA
KUSHINDA TAMAA KWA KUJIZUIA KABISA
"Kwa
kujizuia kabisa atashinda tamaa yake ya kuendekeza vitu vinavyoharibu
afya." (EV 264.)
"Yeu
aweza kukupa nguvu ya kushinda. Kwa msaada wake waweza kuharibu kikamilifu
mzizi wa ubinafsi." 7T 49
"Wale wore wanaotumia nyama
wanapuuzia maonyo yote ambayo Mungu ametoa kuhusu swala hili. Hawana ushahidi kwamba
wanatembea katika njia salama. Hawana
utetezi hata kidogo." Pacific Union Recorder, Oct. 9,1902. Msisitizo
umeongezwa
"Swala
la matengenezo ya afya halitiliwi mkazo ipaswavyo na inavyotakiwa kuwa." CDF.304.
"Kuwa
makini sasa unajiweka katika pingamizi la kazi ya matengenezo ya afya. Itasonga
mbele...." CDF.38.
MAAMUZI
YETU
Mungu kazungumza nasi katika
Biblia na Roho ya Unabii. " Nyakati za hatari ziko mbele yetu....ni lazima
tufuate maelekezo yaliyotolewa kupitia Roho ya Unabii.... Kama tukiyapuuzia,
tutatoa utetezi gani?" 8T 298. Msisitizo umeongezwa
Swali
ni kwamba , Je tutafuata mashauri yaliyotolewa katika Biblia na Roho ya Unabii?
Kwasababu tunampenda Bwana, tuitikie, "Bwana amenena: nasi tutatii!"
7.
WATU WANAOITUNZA SABATO
VILELE
VIKUU VIWILI VYA MLIMA
Umewahi
kujiuliza swali hili makini sana "Je Mimi ni MSABATO au ni MWADVENTISTA WA
SABATO? Haya majina mawili yana tofauti sana.
Kama
vilele vikuu viwili vya milima vilivyosimama juu ya vingine vyote, vionekanavo
juu katika anga, vivyo hivyo na matukio makuu mawili katika historia ya dunia
yetu.
|
Haya
ni mtukio makubwa mawili uumbaji na ukombozi. Haya ni matukio mawili makuu
kuliko yote katika historia ya dunia yenye manufaa kuyajua. Kwa kulinganisha
matukio Haya matukio mengine yote yanakosa umuhimu.
UUMBAJI
Katika
mwanzo wa historia ya dunia yetu hii, baada ya kuiumba dunia Mungu aliumba
wazazi wetu wa kwanza kwa mfano wake, kimwili, kiakili na Kiroho. Mungu aliumba
jamii ya wanadamu kuikuza mbingu. Ni tukio kubwa kiasi gani lisilo na ubinafsi.
Tusingekuwa hapa leo kama isingekuwa kwa kitendo hicho kikuuu cha upendo toka
kwa Mungu.
UKOMBOZI
Pale
jamii ya wanadamu ilipotenda dhmbi na kuanguka kutoka katika hadhi yake ya juu
ya kufanana na Mungu, Mungu alimkomboa na kumuumba upya mwanadamu kwa sura yake,
kwa kumfia pale msalabani, kilikuwa ni kitendo kikuu jinsi gani cha kujitoa
kafara. Tungekuwa ni wa kupotea milele bila tumaini la wokovu, kama isinge kuwa
kwa tendo hili kuu la upendo wa Mungu.
MUUMBAJI
WETU
Na
ni nani muumbaji wetu? Biblia husema kwamba Mungu alituumba kupitia Yesu.
"Mungu
Baba aliviumba vitu vyote kupitia Yesu Kristo." Waefeso 3:9
"Katika
yeye (Yesu Kristo) vitu vyote viliumbwa" Wakolosai 1:16
"Vyote
vilifanyika kwa Huyo ; wala pasipo yeye hakikufanyka chochote
kilichofanyika" Yohana 1:3
Uweza
uliotumiwa na Mungu katika Uumbaji ndiyo uliotumiwa nae katika ukombozi. Uweza
Huo hudhihirishwa au kuwasilishwa kwa Ishara ya sabato. Kwa maelezo Zaidi ya
mambo makuu matatu yawasilishwayo mna sabato fuatilia somo “UNAFANYA HAYO KWA UWEZA WA NANI,MAANA YA KINA
YA PUMZIKO” KATIKA YOUTUBE ACOUNT YA PETRO TUMAINI TV. Kwa maelezo Zaidi
kuhusu kupata kitabu kinachoelezea kwa kina Zaidi habari hizi wasiliana nasi
kwa email- petro.tumaini@gmail.com
au simu 0754202021. Bwana akubariki unapoendelea kuyafanyia kazi mambo hayo na
kuwafundisha wengine
No comments:
Post a Comment