Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16

SHETANI ATUMIAVYO MASTAA KUKUANDAA KWA MOTO WA MILELE.

Maburudisho tupatayo kupitia vyombo vya Habari hutumiwa sana na shetani
kuondoa hali ya matengenezo ya kiroho kwa Wakristo.
   
JIEPUSHE  NA UCHAWI WA BABELI
Mbinu za shetani kuua hali ya kiroho kupitia Maburudisho.
By Petro Tumaini.

lWafuasi wake hupatikana Jiji la malaika waliopotea (lossangeles) -Lost Angels.

lWana msukumo mkubwa kupitia vyombo vya habari.

lHufanya kazi kama wasanii nyota (mastaa).

lHawana tofauti na theluthi ya nyota (malaika wapotevu) waliotupwa pamoja na shetani kutoka mbinguni.


    Ufunuo 18: 23 . Wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala saauti ya Bwana harusi na bibi harusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa, maana hao wafanyabiashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.

SHETANI ameweka nguvu yake kubwa sana nyuma ya vyombo vya habari (Televisheni, Magazeti, Mikanda, Intaneti n.k) ili kuhakikisha anawaandaa watu kwa moto wa milele ambao Mungu ameuandaa kwaajili ya ibilisi na wale wanaomfuata. Hebu tuchunguze Biblia tuone imelizungumziaje suala hili.

Wanadam wengi hutumia sehemu kubwa ya maisha kwa kujishughulisha namaburudisho (entertainment).
· Vijana wengi hutegemea maburudisho kama vile;
     · Muziki.
     · Mpira.
     · Maigizo.
     · Riadha.n.k.
·Kwa madhumuni ya;
ØKufahamika
ØKupata hela
ØKuburudika
 Hebu tutazame kitabu cha Ufunuo wa Yohana, ambacho hukusanya kwa pamoja maneno ya Mbinguni, Duniani na hata yale ya shetani kikionyesha vita ya mwisho baina ya wema na uovu kikitumia picha halisi na alama,vitu vya kawaida na vya kiroho ili kutupatia ujumbe uliotoka kwa Mungu mwenyewe.
MADHUMUNI HAYA YAMEJENGWA KATIKA NENO LIITWALO UCHAWI, KAMA FUNGU LIFUATALO LIONYESHAVYO.
Ø Ufunuo 18:21-23. 21 Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe , kama vile jiwe kubwa ka kusagia, akalitupa katika bahari, akisema , kama hivi, kwa nguvu nyingi , utukufu wa Babeli, mji ule mkuu , wala hautaonekana tena kabisa. 22 Wala sauti ya wapiga vinanda na ya wapiga zumari, na ya waapiga filimbi, na ya wapiga baragumu , haitasikiwa ndani yako tena kabisa, wala fundi awaye yote hataonekana tena ndani yako kaabisa,wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa. 23 Wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala saauti ya bwana harusi na bibi harusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa, maana hao wafanyabiashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.
                                                                                               
KUNA MAMBO MAKUBWA MAWILI YA KUWEZA KUFAHAMU;
Ø Maana ya Babeli, ambayo inahusika kuondolewa utukufu.
ØMaana Uchawi , ambao kwa huo Babeli imedanganya mataifa yote.
MAANA YA BABELI
Ujenzi wa mnara wa babeli uliositishwa na mungu kule shinari, huwakilisha
machafuko yanayoletwa na shetani ili kupinga maagizo ya mungu.
ØMwanzo 11:2. Ikawa  watu waliposafiri wakaona nchi tambarare katika nchi ya Shinari, wakakaa huko.

Baada ya watu kuanzisha makazi wakaamua kujenga mnara mrefu sana kwa sabau kuu nyingi zikiwemu kubwa mbili zifuatazo.
(1) Kujiepusha na gharika endapo kama mungu angeleta gharika nyingine kama ile ya kipidi cha Nuhu.
(2)Kujitukuza nafsi.
(3)Wasipate kutawanyika usoni pa nchi.

Mungu akaingilia kati baada ya kuona jamii hii ya wanadamu wanataka kufanya yaliyo tofauti na mpango wake, akawachafulia lugha, wakashindwa kuendelea na ujenzi na hatimaye wakatawanyika usoni pa dunia kila watu kwa kadri walivyelewana kutokana na lugha zilizoibuka katika machafuko hayo.

ØMwanzo 11:9. Kwasababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipochafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi.
   
Kwahiyo maana ya babeli ni machafuko, watu wa babeli walipotawanyika usoni pa dunia walisanbaza dini ya upagani wa kuabudu miungu na kufanya yote yaliyo kinyume na maandiko. Tokea hapo Babeli ni dini ya  kupenda dunia ambayo na kumuacha Yesu Huleta uchawi wake ili iwapotoshe watu wote wa dunia hii endapo tu hawatajikita kwa Yesu Kristo, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.

Dini ifundishayo kuwa wanadam hawaokolewi kwa kushika sheria, mwaadam akifa rho inaendelea kuishi inajenga mnara wa mafunzo ambayo kupitia hayo inawadanganya watu kwamba wataokolewa lakini kiukweli watapotea kupitia mafundisho hayo.

MAANA YA NENO UCHAWI LILILOTUMIKA KATIKA UFUNUO 18:23.
  Neno uchawi katika fungu hili limetokana na neno la kigiriki Famacia ambalo kwa kiingereza pia ni Phamacy. Kwa kawaida famacy ni sehemu ambayo madawa huuzwa. Madawa  yatumikapo bila utaratibu huwa ni sumu na mengine hulewesha na kuharibu akili.
  Maana ya neno famacia ni kitu chochote kichanganyacho au kupumbaza akili na kufanya isiweze kutii au kufuata mapenzi ya Mungu au sheria yake.

KWA MUJIBU WA KICHWA CHA SOMO HILI WAWEZA KUJIULIZA MASWALI YAFUATAYO.
(1)Je Pombe yaweza kupumbaza akili isiweze kutii amri na maagizo ya mungu?
(2)Je televisheni yaweza kupumbaza akili isiweze kufuuata , kutii au kusoma neno la mungu?
(3)Je Mpira waeza kupumbaza akili isipate nafasi na mda wa kutafakari neno la mungu?
(4)Je muziki (hasa hasa wa kidunia) waweza kupumbaza akili isifuate , na kutii neno la Mungu

 Shetani ameweka hazina kubwa ya uchawi wake kupitia kiwanda cha maburudisho (Entertainment industry). Huu ndio uchawi anaotumia kuwapotosha mataifa na kwa namna moja au nyingine ndio utajwao na kitabu cha ufunuo . Kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako. 
   Tunapozungumzia Kiwanda cha maburudisho, tunazungumzia:
(1)Pombe.
(2)Muziki
(3)Michezo.
(4)Filamu
(5)Maigizo.n.k

  Haya yate hutimiza kile kinachoelezea neno Famacia au uchawi wa babeli ambao kwa huo shetani kuwafanya watu wapuuzie kusali, kusoma neno la Mungu, kulitafakari na hata mda wa kushuhudia kweli ya biblia.
Maana ya neno ENTERTAINMENT (maburudisho).
  Neno hili limejengwa na maneno matatu
(1)ENTER-Kuingia (coming in)
(2)TAIN- kumiliki (posses)
(3)MENT- kuendelea kumiliki.(Keep on the state of possesion)
 Kwa ujumla inamaanisha kuingia, kumiliki na kuendelea kuweka katika hali ya kumiliki. (coming in, posses and keep on the state of possesion.)

Je umewahi kutambua kwamba, kupitia entertainment industry (kiwanda cha maburudisho) ambayo mengi ni ya kidunia shetani huingia akilini mwako, hukumiliki na kuendelea kukumiliki kifikra?”

Waebrania 13:1, 2. 1 Upendano wa ndugu na udumu. 2 Msisahau kuwafadhili (entertain) wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika bila kujua.

Kama inawezekana kuwakaribisha (entertain) malaika wa nuru  yaani waingie, kumiliki na kuweka katika hali ya kumiliki nyumba zetu na akili zetu. Je si rahisis zaidi kuwakaribisha malaika waovu nao wafanye makao yao majumbani kwetu na akilini mwetu kupitia maburudisho tunayoyapendelea?

“Ukijishughukisha na maburudisho ya kiroho/kikristo (spiritual entertainment) utakuwa makao ya Roho wa Mungu, vivyo hivyo ukijishughulisha na maburudisho ya kidunia (wordly entertainment) utakuwa makao ya shetani.”
  Ni kwa namna hii Ufunuo 18:23 inatoa kifungu cha maneno Kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako (entertainment). 
  Shetani ametupofusha akili tushindwe kuelewa kina
cha uchawi uzungumziwao na Biblia kwa kutupatia dhana finyu, yaani kila tusikiapo neno uchawi tuwaze tu watu wanaowanga usiku, waganga wa kienyeji wapigao ramli.

   “Laiti kama tungejua shetani hutuloga na kutupotosha kwas uchawi wake (famacia) kupitia kiwanda cha maburudisho (entertainment), tungegesali kuliko kawaida.”
   Katika Biblia wapo watu wsaliojioepusha na uchawi huu na hatimaye walichukuliwa kwenda Mbinguni kama henoko.
   Henoko (Mwanzo 5:21-23), alitembea na Mungu kwa muda wa miaka mia tatu. Yaani alimtafakari mungu na mabo ya kimbingu, hakutumia mda wake kwa kuijazaakili na mabo ya dunia, hatimaye Mungu akaamua kumchukua mbinguni.

Wale wajiitao mastaa katika entertainment indusry ni wakala wa Malaika wa Shetani waliotupwa toka mbinguni.
Ufunuo 12: 9, 4. 9 Yule joka akatupwa, yule mkkubwa , nyoka wa zamani, aitwae Ibilisi na Shetani, audanganyae ulimwengu wote , akatupwa hata nchi na malaika zake pamoja nae. 4 Na mkia wake ukakokota theluthi ya nyota za Mbinguni, na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
Baada ya kuleta uasi wa kutaka kufanana na Mungu
Malaika mkuu Lusifa (kwa sasa ni shetani) alitupwa
na theluthi ya malaika waliofuata uongo wake.
Ni nini kilichomfanya Shetani na theluthi ya nyota (malaika) watupwe.
Ukisoma Isaya 14 utagundua yafuatayo.

(1)Alitaka kuwa kama Mungu.
(2)Aliwashawishi malaika wamuunge mkono akimshutumu mungu kama dikteta.
(3)Alitaka kuwa zaidi ya mungu, yaani alitaka kuwa maarufu (famous) kuliko Mungu.
   Kwa kadri Muda ulivyozidi kwenda uongo wa shetani ulijulikana akatupwa kutoka mbinguni na kuhamishia mashambulizi yake duniani.
   Alipofika duniani alimdanganya Hawa kwa kutumia medium (mfumo) wa nyoka, leo hii hutumia media (mass media) yaani vyombo vya habari kwa ujumla.
  Wafuasi wa shetani ambao kwa sehemu kubwa hutumia media (mass media) vyombo vya habari nao hufanya kazi wakiongozwa na madhumuni hayo hayo ya kutaka kuwa maarufu, na kuwaburudisha (entertain) watu.
  Wanafanya kazi ya kuwahimiza watu nao waitwe nyota (mastaa), na hivyo si kazi kuona matokeo ya kazi zao. Ukiona mtu anafanya kazi akidhamiria kuwa staa, kuwa maarufu ni msukumo uleule wa shetani.
Watu wafanyao kazi kwa madhumuni ya kuwa masupastaa kama wale wa mieleka
huongozwa na roho ya kujikweza iliyomfanya shetani atupwe kutoka mbinguni.
Mungu hajaagiza ufanye kazi kwa mashindano Wafilipi 2

  Ndiyo maana tuna mastaa wa aina nyingi;
(1)Mastaa wa filamu.
(2)Mastaa wa mpira.
(3)Mastaa wa ngumi.
(4)Mastaa wamuziki.
(5)Mastaa wa michezo mbali mbali.
   Siku kwa siku tunaabudu mastaa bila kujua na wakati mwingine tunajua, na kiukweli kupitia maburudisho shetani huwatumia kutu entertain ( kuingia, kutumiliki ,na kutuweka katika hali ya kutumiliki.)
   baada ya siku chache tunajikuta.
(1)Tunaongea kama mastaa.
(2)Tunatembea kama mastaa.
(3)Tunavaa kama mastaa. Mabinti huvaa vimini kwasababu ya msukumo wa mastaa, vijana huvaa milege kwasababu ya msukumo wa mastaa. Huu ndiyo uchawi wa Babeli ufanyavyo kazi.                                                        

   “Mahali walipoweka ngome malaika wa shetani (NYOTA. Ufunuo 12:4  Na mkia wake ukakokota theluthi ya nyota za Mbinguni...”)
   Bila shaka theluthi hii ya malaika hupatikana mahali ambapo ngome ya mastaa (nyota) wa maburudisho duniani hupatikana. Na sehemu hii Hujulikana kama Hollywood hasa katika jiji la Losangeles lililoko  California. Hapa ndipo wapatikanapo mastaa wa movies na maburudisho ya aina zote duniani , tena hutumia media kuwafikia mashabiki wao.
   Majina tu ya sehemu hizo yanadhihirisha kuwa hizo ni ngome za sheta. HOLLYWOOD, LOSANGELES. Je umewahi kutafakari maana ya majina haya.
   HOLYWOOD, jina hili limetokana na jina HOLLY TREE mojawapo ya miti ya nguvu za giza na ulikuwa na matunda ya kuvutia ambayo ni sumu , ulikuwa ikitumika kuwafanya watu wafikie kifo bilo tabu.
   Je haiwezekani pia kupitia hiollywood shetani huwaloga watu kwa uchawi wa wanamaburudisho kuwafanya watu wafe kiroho kwa kile wanachoshabikia au kutazama kama kitu cha kuvutia na kupendeza ?

   LOSANGELES, jina la jiji hili waishio mastaa wakubwa wenye msukumo sana dunia nzima limetokana nna neno la kiingereza (LOST ANGELS) LIMAANISHALO MALAIKA WALIOPOTEA.

Hapa tunapata jambo moja la uhakika, malaika (nyota) waliodanganywa na shetani na hatimae kutupwa kutoka mbinguni pamoja na shetani hata kama si wote basi kwa sehemu kubwa sana waliangukia katika jiji hili lililoitwa kwa jina lao.(Loss angeles-lost angels au malaika waliopotea).

MAANENO YAONYESHAYO KAZI YA SHETANI KUPITIA MABURUDISHO
­
AMUSE

Kama litumikavyo katika filam likimaanisha kuonyesha mambo ya  kushangaza . Neno hili linamaanisha kudangaanya kwa kupindisha ukweli, bahati mbaya wengi hupenda kutazamba mambo ya kushangaza bila kutambua kuwa shetani  anawadanganya maana ni kanuni ya kazi zake.
Ufunuo 12:9. Yule Joka aaakatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwae Ibilisi na shetani, audanganyae ulimwengu wote, akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.
“Asilimia kubwa ya Filamu , vipindi na program zote zifuraishazo na kushangaza zimejengwa katika kanuni ya Uongo (yaana kanuni ya shetani)”
Maana ya CHANELLING

The ability to communicate with evil spirits through medium, (uwezo wa kuwasiliana na roho waovu/wachafu kupitia mfumo au chombo fulani).

Uwashapo TV ilkiyounganishwa na kebo, dishi (satelite), unakuta chaneli nyingi. Hapo shetani shetani ameweka mawasiliano yake kupitia chombo hicho ili unapoendelea kuchaneli japokuwa kuna baadhi ni za mabo ya Mungu. Tabia yake anaihamishia kwako kupitia chaneli mbaya uzitazamazo.
“By beholding we become changed ( Ellen G white), yaani anamaanisha kwa kutazama tunabadilishwa.”

“Kama tunavyobadilishwa kwa kumtazama Yesu, kwa kutazama chaneli za shetani tunafanana na shetani mwenyewe na ndo maana ana mawasiliano ya kula aina katika chaneli.”
lKuchochea ugomvi anachaneli ya ngumi
lKukuchochea uzini ana chaneli za Ngono “X”
lKuchochea kanuni ya kujikweza ana chaneli za Muzinki wa kidunia n.k.

KUPROGRAM (PROGRAMING)
   Ni kuendesha au kuunda kitu unavyo taka wewe, shetani pia hutuunda atakavyo kupitia program mbali mbali za TV, Redio, Intaneti n.k.

Remote control (Kuendesha kwa limonti)
   Neno hili tunalitumia sana tubadilidhapo program za redio na TV bila kuigusa tukitumia kifaa cha rimonti. Remote inamaanisha mbali.
   Shetani hutuendesha (control) bila sisi kujua maana hutumia mawakala ambao wako mbali (remote) hata yeye yuko mbali na hivyo si rahisi kujua kama huna Roho wa Mungu. Na hii ndiyo maana ya Remote Control kaatika uchawi wa shetani (Babeli).

   Matokeo yake tunaanza kufanya mambo ambayo hakuna aliyetwambia tufanye ila kwasababu tumevutiwa na program za shetani, na anatuendesha  tunajikuta tunafanya tu. Kuvuta sigara, kuivaa nguo fupi (Vimini).

 HIPNOSISI.
  
Maana ya neno hioli ni akili ya mtu mmoja kuendesha akili ya mtu mwingine haaatimmaye anayeendesha anajikuta anaenenda katika tabia na mtindo ambao si wake.
lMfano- Vijana wengi tokea utotoni huwa wanatenbea vizuri na kuongea vizuri lakini waanzapo kuangalia filamu za muziki na hata zile za kizungu wanaanza kuongea kizungu (what's up man,) na hata mwendo hubadilika na kuwa wa mdundo wengine kama wamevaa viatu vyenye spiringi.
   Akili zao zinaanza kuendeshwa na mastaa (malaika wa shetani) kwa hiyo kila kitu wanachofanya wanataka wawe mastaa.
Shetani hutumia muvi kutuhamisha kututawala fikra na
kutupotezea muda katika kutazama yasiyo na maana.

Muvi (Movie,Emotion)
  Emotion ni neno ka kiingereza litumikalo kuelezea mweneno wa mwanadamu. Movie inamaanasha kuhamisha na limetokana na neno move ambalo halina tofauti na e-motion.Hata neno Cinema limetokana na neno la Kigiriki Kinema limaanishalo kuhamisha (to move)
 “Shetani hutumia movie kutuhamiosha na kunadilisha miendendo(e-motion) kwa kutugeuza tabia”.

Wakolosai 1:23. Mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa  na kuliacha tumaini la injili mliyosikia habari zake...
  
Dhumuni la Mungu iu kwamba tusiondolewe klatika injili, dhumuni la shetani ni kutuondoa (move) katika injili.
 Msipogeuzwa
   Neno la Paulo msipogeuzwa limetokana na neno la kigiriki limaanishalo kuhamisha,, hata neno Sinema limetokana na neno Kinema-Kinein limaanishalo kuhamisha.
 
   Unapoangalia movie unahamishwa kutoka sehemu mojaa hadi nyingine, staa akiumizwa unaumia, akifurahi unafurahi, akitaka kuua unafurahia. Kwa njia hiyo shetani anmatubadilisha tofauti na mungu alivyokusudia kuwa tusibadilishwe kutoka katika tumaini letu la Kikristo.


Video Game zimejengwa katika kanuni ya ukatili ili kutuweka
katika hatia ya dhambi ya mauaji na chukui. 

VIDEO GAME
   Video game nyingi zimejengwa kaatika kanuni ya  hasisra na ukatili, yaani mauaji na ushindani. Kanuni hizi huunda tabiaa ya shetani.
lUkiua katika video game Mungu unahesabiwa na hatia ya mauaji. Dhambi haaihesabiwi hadi ufanyapo tendo bali huanzia katika fikra. Yesu alisema yeyote amtazamae Mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini nae.
“Shetani hucheza na fikra zetu ili ahakikishe kwamba kwa namna yoyote ziko katika hatia. Hata kipindi cha Nuhu fikra za wanadamu zilikuwa zimejaa dhambi ndo maana Mungu akaleta gharika.”
Mwanzo 6:5 . BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwaduniani na kwamba kila kusudi alilowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote . Soma pia Isaya 23:6

Muziki humiliki sehemu kubwa ya mawazo na tabia.

   TABIA NA MUZIKI
   TABIA HUUNDWA NA MAMBO MAWILI

lMawazo (feelings)
lMwenendo (Emotions)

MUZIKI HUUNDWA NA MABO MAWILI

lManeno- ambayo huelezea mawazo (feelings)
lMuziki-ambao huelezea mwenendo (emotions)

   “Muziki ni silaha kubwa atumiayo shetani kubadili tabia zetu, yaani kupitia muziki wa kidunia (blues, rnb, hip hop, bongo fleva, taarabu n.k) shetani hubadili mawazo yetu na mwenendo.”

   Muziki wa kidunia umeingizwa mpaka kanissani, siku hizi tuna muziki wa injili au disko la yesu , ikumbukwe kuwa shetani ana kanuni mooja kubwa sana ya kuwateka wakristo. Kila akitaka kuingiza kitu chake katika ukristi huongezea neno kristo mbele. Ndio maana zamani tulikuwa na disko sikuhizi tuna Disko la Yesu. Vitu vingi huvibadilisha kwa njia hii.
 

 DHUMUNI LA MUZIKI NI KUTUKUMBUSHA UTAKATIFU SI MABURUDISHO.

   Russano (2000) alisema, Muziki unamiliki kiwango cha maadili na unaweza kumuathiri msikilizajitabia na mwenendo... miziki unawakilisha shauku ya moyo kama vile hamasa, hasira, kiasi, na kinyume na hayo.
    Aliendelea kusema kuwa “muziki unaowakilisha shauku fulani pia unaamsha shauku hiyo kwa msikilizaji.aina mbaya ya muziki inakufanya uwe mtu mbaya na aina nzuri inakufanya uwe mtu mzuri.
 katika Karne ya 15 makanisa na wanafalsafa walikataa wazo kwamba muziki lazima ufurahiwe kwa jinsi unavyochezwa na sauti...bila kupinga uzuri wa sauti walisema...
      
      (1)Vitu vizuri vipo kutukumbusha juu ya utukufu na uzuri wa mungu.
(2)Siyo kufurahisha furaha binafsi.

Nyimbo nyingi tunazosikiliza kanisani hutufurahisha nafsi zetu na hazitukumbushi utukufu wa mungu hivyo tumetanga mbali na kusudi la mungu katika Muziki na kuingiza uchawi wa babeli (Machafuko kanisani).
 Muziki wa unaoingizwa katika makanisa mengi ya kikristo sasa umejengwa katika kanuni za kishetani.
(1)Mkazo mkubwa uko kwenye kucheza (kudansi) na sio kumsifu mungu katika heshima na kicho. Husababisha kujitukuza nafsi,
(2)Midundo huchochea msisimko nambao hufukuza uwepo wa malaika wa mungu.
(3)Makelele na fujo huondoa kabisa uwepo wa Mungu.
 
Shetani amefanya yote hayo kwasababu muziki ndiyo njia pekee ambayo binadamu anaweza kuitumia kuweka kumbu kumbu ya maneno na mawazo yoyote yale kwa kuyakariri.

Yawekana katika yote  haya umetambua kwamba wewe ni miongoni mwa waliokamatwa na uchawi wa babeli, usalama pekee ni kuachana na yote uonayo kwamba yatakupoteza na kumtazama Yesu tu.   Wakolosai 1:23. Mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa  na kuliacha tumaini la injili mliyosikia habari zake...

Kusudi la Yesu ni kumtazama Yeye pekee ili atubadilishe, kusudi la shetani ni kutugeuza pale tu tunapoacha kumtazama yesu na kutazama mambo ya dunia hii.

“Yeye ambaye macho yake humtazama Yesu tu ataacha yote, ataifia nafsi. Ataamini neno la Mungu kama lilivyo”

“Katika msalaba mvutano huishia pale na kutoka pale msukumo wote husambaa, nio kituo kikuu cha mvuto na kutoka hapo msukumo wote husambaa.



   Rejea
èBarnaba R. Hanning.(2000). Concise History of Western music.2nd Ed
èEllen g white, Counsels on Music.
èDVD - Escape From the Black Hole (Agujero Negro). 
èSDA Bible commentary .Vol 6,pg1113.

   
­