Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16

NJIA TATU ZINAZOELEKEA  MBINGUNI

 JE ZOTE ZINAFIKA?

(1) IJUMAA :- WANAYOPITA WAISLAMU
(2)JUMAMOSI – WANAYOPITA WAADVENTISTA – WASABATO
(3)JUMAPILI – MADHEHEBU ZOTE ZA JUMA PILI?

Je , Mungu anazikubari zote?
Zakaria 12:6 “Siku hiyo itawafanya wakuu wa Yuda kuwa kama Kigae chenye  moto katika kuni na kama kinga cha moto katika miganda ; Nao watatekeleza watu kila kabila wazungukao pande zote, upande wa mkono wa kuume na upande wa mkono wa kushoto ; Na baada ya hayo Yerusalem utakaa mahali pake, naam Hapo Yerusalem”

-          Njia ya kwanza Jumamosi (sabato):- ilianza kupitika  mnamo tarehe ya 7/1/1 wa uumbaji Mwanzo 2:1-3 “Basi mbingu na Nchi zikakamilika . Na siku ya saba Mungu alimaliza akaibariki siku ya saba akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe” (mwanzo – 2: 1- 3)
-          Yuda 1:3 Njia hii ilitolewa Mara moja tu. “Wapenzi nilipokuwa nikifanya bidii kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia ili niwaonye kwamba Muishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. (Yud 1:3) Imani hii ilitolewa na Mungu mara moja “kama mlivyoitwa katika tumaini moja la mwito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. (Efe. 4: 4 – 6). njia ya kwanza ni sabato (jumamosi) ambaye mwanzilishi wake ni Yesu kristo “Akamwambia sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu . Basi mwana wa Adamu ndiye bwana wa sabato pia. “Marko 2:27-28) yeye huyu Yesu anao uhakika wa kuwafikisha watu mbignuni ndio maana anasema “Msifadhaike mioyoni mwenu; Mnamwamini Mungu niaminini na mimi, Nyumbani kwa Baba yangu mna makao mengi kama si hivyo ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia makao. Basi mimi nikienda na kuwaandalia makao nitakuja tena niwakaribishe kwangu ili nilipo mimi nanyi muwepo. (Yoh. 14:1-3) “Yesu akamwambia Mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi. (Yoh14:6.) Hivyo anawaalika wote kupita katika njia hii. “Na kondoo wengine ninao ambao si wazizi hili, Na hao nao imenipasa kuwaleta na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako na kundi moja na mchungaji mmoja (Yoh 10:16) watu wote hata wewe msomaji mnaitwa kupita njia hii.

Hata katika kitabu cha Mkusanyiko wa madhehebu ya kiprotestandi kiitwacho METHODIST. Kinasomeka:- “Madhehebu sio ya Mungu, hayajawahi kuwa na hayawezi kuwa kamwe , ni roho mbaya anaewatenganisha watu wa mungu katika madaraja ya makasisi na washiriki.
Kwa hiyo basi ni roho mbaya anayewabagua watu wa watu .
Hivyo ndivyo shirika na Madhehebu yafanyavyo. Katika kujiundia madhehebu . wao hujitenga na neno la mungu na kujiingiza katika uzinzi wa kiroho na kulikataa neno la kiroho (Methodist Uk 197 aya 2.


Askofu Peter Kitura wa AIC katika kitabu cha Jumapili au Jumamosi ameandika. “Neno sabato /shabath kwa kiebrania au sabatoo kwa kiyunani lina maana ya mapumziko au siku ya mapumziko asili ya mapumziko yaani sabato haya ni katika kitabu cha mwanzo (Mwanzo 2: 1-3. kama tulivyosoma hapo kwanza ) anaendelea kwa nuru ya mistari hii Mungu mwenyewe alipumzika alihitaji siku moja ya kustarehe baada ya kazi yake ya uumbaji iliyomchukua siku sita. Kutokana umuhimu wa kupumzika kwake akaitakasa siku hiyo ya saba . Neno takasa lina maana ya kuweka wakifu au kutenga kwa ajili ya matumizi matakatifu, yaani matumizi maalum yanayokusudiwa na Mungu au kuondoa unajisi (sura 1 aya 1)
Yeye mwenyewe nalielewa ingawa najaribu kutafuta sababu za kukwepa.
Si wakiristo tu walijua hii lakini hata katika vitabu wa ndugu zetu waislamu limeandikwa.
Njia ya kwanza ya sabato ya J.mosi koroani sura 4 aya 4 (4:47) “Enyi mliopewa kitabu Aminini tuliyowatelemshia yanayosadikisha yaliyondani kabla hatujazigeuza nyuso zenu tukazipeleka kisogoni au kabla ya kuwalaani kama tulivyowalaani watu walioharibu utukufu wa J.mosi na amri ya mwenyezi Mungu ni lazima kufanywa. Ingawa ndugu zetu Waislamu hili hawajalitii (koroani sura 4:154 ufafanuzi ‘c’ ) Na baada  ya kutoka katika hiyo miji na vijiji ya shamu waliambiwa waazimishe hiyo siku ya jumamosi kuwa waifanye kuwa siku ya Ibada na siku ya kufanya kazi”
Hata waislamu wameagizwa kutii Amri hii ya kutofanya kazi siku ya sabato (Jumamosi) “Na kwa yakini mmekwisha kujua habari za wale walioasi miongoni mwenu katika Amri ya kuheshimu Jumamosi. Basi tukawaambia kuweni manyani madhabilifu (koroani 2:65)
Hivyo kwa mujibu wa koroani wale wote wasioiheshimu Amri ya kuitunza Jumamosi ni manyani wasio na akili. Siamini nawe mpendwa kama unaridhika kuwa hivyo. Njoo ujiunge na wasafiri waendao mbunguni.

NJIA YA PILI : JUMA PILI
Njia hii ilitumika mwaka 150 B.K. Dondoo  kutoka katika kitabu cha Muongozo wa wakatoriki.
Misala ya Waumini yana msingi wake katika maandiko ya Mtakatifu Yustino Mzaliwa wa Nchi ya Siria, ambaye alikuwa Mwalimu wa Filosofia katika muji wa Roma. Ndiye yeye aliyeeleza mkutano wa siku ya bwana ndio Dominica au Jumapili mnamomwaka 150 B.K

Mimi  ndimi njia na kweli na uzima”
Maelezo haya yanaonyesha dhahili hakuna ukubali wa Biblia juu ya Ibada ya jumapili isipokuwa ni mapokeo kutoa kwa watu huku akijiita ndiye njia.
Tazama ushahidi mwingine katika kitabu cha AIC Jumapili au J,mosi Uk.45.
“Siku ya sabato au Jumamosi yesu alikuwa kaburini. Siku ya kwanza ya juma Yaani Jumapili alifufuka kutoka kwa wafu. Kwa kuwa sabato ilikuwa Jumamosi kwa kalenda ya kiyahudi siku ya pili yake iliyotengwa na Mungu kuwa siku ya Pentekoste ilikuwa siku ya  Jumapili. Wayahudi walijijua hivyo na kanisa linajua hivyo. Huko Troa Wakristo walianza kuabudu siku ya kwanza ya juma (Juma pili) pamoja na kumsikiliza Paulo akihubiri neno la Mungu walikuwa na Ibada ya ushirika kwa kusema, hata tulipokuwa tumekutana hata kuumega mkate mwandishi wa kitabu cha matendo ya mitume Luka alionyesha ilikuwa siku ya ibada haikuwa siku ya kuagana tu kama Wakristo wenzetu Wasabato wanavyodai” Nukuu hii ni katika kutafuta namna ya kutafuta kupindisha maandko matakatifu. Hebu tuangalie katika Biblia Luka ameandika nini? “jumamosi jiono tulikutana ili kuumega mkate, kwa vile Paulo alikuwa amekusudia kkusafiri kesho yake; aliendelea kuwahutubia watu hata usiku na kuendelea kuongea nao hadi usiu wa manane” Mat 20:7. (Kiswahili cha kisasa) hii inaonyesha kuwa  ilikuwa ni ibada ya kuhitimisha siku ya Sabato. Wala haikuwa jumapili bali siku ya jumamosi.
Jumapili ni siku ya kwanza ya juma, siku ya kufanya kazi wala sio siku ya Ibada. “Naye alipofufuka siku ya kwanza yajuma alimtokea kwanza Mariamu Magdarena ambaye hapo kwanza alimtoa pepo saba, huyo akashika njia akawapasha habari wale aliokuwa pamoja naenao wakali wanaomboleza na kulia. Lakani hao waposikia kwamba yu hai hawakusadiki. Baada ya hayo aliwatoke watu wawili miongoni mwao akiwa na sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shambani” Mark. 16:9-16. (Kiswahili cha kisasa.)  hivyo ni dhahili kuwa jumapili ni siku ya kufanya kazi ndio maana hata hawa wanafunzi wa yesu walikuwa wanakweda shambani.
Lakini Jumapili inaonekana kushamili sana siku za leo kama siku ya Ibada, chini ya kiongozi wa Madhehebu zote za j,pili. Kamusi ya Kiswahili  sanifu inasomeka hivi. “mtaguso: mkutano maalumu wa wakuu wa kanisa la katoriki ambao unawea kubadiri sheria kwa ruhusa maalum ya papa.” Uk. 327.
Papa anayetajwa hapa ndiye kiongozi wa kanisa Katoriki. Kitabu cha muongozo wa kanisa katori; Katekisimu ndogo uk. 26. “Siku hizi nanai ni mwandamizi wa viongozi hao? Jibu: Papa… Askofu wa Roma ndiye mwandamizi wa mtume Petro na maasikofu ndio waandamizi wa Mitume.”
Kiongozi wa wakatoriki wote ni Papa na ndiye amekuwa mstari wa mbele katika kupindua na kupotosha maandiko Matakaatifu.tazama jinsi anavyojichukulia cheo cha Mungu Mkuu. Katika kitabu cha Papa ni nani? Uk.26. kinasomeka “Kwa kuwa Askofu wa Roma kwa haki ya kimungu anao Ukuu wa kitume na kanisa zima tunafundisha hivyona kutangaza yey ndiye  hakimu mkuu wa waumini wote. Ambaye kwake rufaa ya mambo yote yaliyo katika uchaguzi wa kanisa yanaweza kufanywa. Hukumu ya papa haina rufaa, kwa kuwa mamlaka iliyo kuu zaidi”  Je, mpendwa neon hili ni dogo na jepesi kiasi cha kutolitafakali vuzuri? Kitendo cha mwanadamu mwenye kufikiwa na kifo kujitangaza kama hakimu mkuu. Nafasi  na cheo cha Mungu aliye BWANA pekee?
Hii ndio sababu hata ya kudiriki mkubadil sheria takatifu za Mungu. Amri ya NNE ya Mungu inatutaka kuitakasa na kuitunza sabato ya jumamosi wao wakatangaza ibada ya jumapili kinyume na Mungu.
Kitabu cha Wakatoriki. Misale ya waumini uk.1) “… kwa hiyo tangu siku ile aliyofufuka bwana kanisa linatuita siku ya kwanza ya juma ndiyo dominika” maana yake siku ya bwana j,pili.
Wameliacha Kanisa la BWANA na Amri zake nakugeukiaka miungu mingine ya jua na sanamu. “Ndipo akanileta mpaka mlangoowa kuingilia katika nyumba ya BWANA, uliolekea upande wa Kaskazini, na tazama wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi. Akaniambia mwanadamu umeyaona haya? Utaona tena machukizo makubwa kuliko hayo. Akaniletaa mpaka hua wa ndani wa nyumba ya BWANA, na tazama mlango pa Hekalu la BWANA, kati ya ukumbi na Madhabahu, walikuwapo watu kama ishirini na watanowamelipa kisogo Hekalu la BWANA, na nyuso zao wameelekeza upande wa mashsriki, nao wanaliabudu jua, kwa kuelekea upande wa mashariki. BAsi akaniambia umeyaona haya Ee, mwanadamu? … wafanye machukizo wanayofanya hapo? Kwa maana wameijaza nchi hii kwa udhalimu, tena wamerejea nyuma ili kunikasirisha; na tazama wanaliweka tawi puani. Kwa sababu hiyo Mimi nami nitatenda kwa ghadhabu; jicho langu halitachilia wala sitaona huruma, na wajapolia, na wajapolia masikioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikia.” Eze. 8:14-18.
Maneno haya ya Biblia yako wazi yakionyesha jinsi gain watu wameacha maagizo ya Mungu na kugeukia ibada za miungu. Tazamaa kitabu hiki cha Wakatoriki (Katekisimu kubwa uk.484.) kinavyosomeka. “Sisi sote tunakkusanyika siku ya jua, ndio siku ya kwanza baada ya Sabato ya Kiyahudi lakini pia siku ya kwanza ya juma.”
Nji hii inayoongozwa na Papa ambaye hana hatima ya wafuasi wake ila katika hukumu ya milele, maana ndio mwisho wa njia yake. Kitabu cha Wakatoriki (Mungu na Wanadamu toleo la pili. Uk.195. “Kanisa katoriki litadumu  mpaka lini? Jibu: litadumu mpaka mwisho wa Dunia.” Mwanzilishi wa njia hii ni mroma na ndiye anaye elezea mwisho wa njia yake kuwa ni pale Yesu atakaporudi mara pili, wala haitaingia mbinguni wala haitakuwepo tena.  Unajua kwa nini? Kwa sababu hata mafundisho yake ni ya mapokeo ya wanadamu yaliyochanganywa na Neno la Mungu kidogo ili kuwapumbaza watu Kitabu cha mwongozo wa wakatoriki, (katekisimu ndogo. Uk. 12) “Kanisa Katoriki uchota mafundisho ya Mungu wapi? Jibu: Kanisa katori uchota mafundish ya Mungu :-
1: Maandiko matakatifu.
2: Na katika mapokeo.

Uf. 22:18 inasomeka “Namshhudia kila anayesikia maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu yeyote akiyaongeza Mungu atamwongezea, hayo mapigo yaliyoandikwa kitabu hiki. Na mtu yeyote akiondoa lolote katika neon la unabii wa kitabu hiki Mungu atamwondolea sehemu yake katika mti wa uzima, na katika ule Mji mtakatifu ambao habari zake azimeandikwa katika kitabu hiki.
Wameacha Neneo la Mungu wameandama Mapokeo yaliyo maneno ya wanadamu. Nao wamelitimiza neneo la BWANA alilonena kwa kinywa cha Nabii Isaya. “Wawaambiao waonaji msione; na manabii msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo.” Isa. 30:10.
“Maana utakuja wakati watakapo yakataa mafundisho yenye uzima; Ila kwa kufuata nia zao wenyewe watajipatia walmu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao wataiepusha wasisikie yaliyo kweli; na kuzigeukia hadithia zaz uongo.” 2Tim. 3:3-4.
Hii ndio njia ya pili. Juma pili inayobebamafundisho ya mapokeo ya watu (viongozi wa dini) Nao wanawapeleka watu katika upotevu. “kwa maana wawaongozao ndio wawakoseshao, na hao waliongozwa na waatu hao wameangamia.” Isa.9:16.

NJIA YA TATU IJUMAA-WAISLAMU.
Njia hii ya alah nayo inaelekea mbinguni, na watuwanaoipitia wanamfuata mtume Mahamad.
Njia imejikita katika Mafundisho ya watu. Maana Muhamad mwenyewe hakuwa anajua kusoma wala kuandika. Basi alitoa wapi mafundisho yake. “Na wakasema ni ni visa vya watu wa zamani alivyo viandikisha Muhamad kwani yeye mwenyewe hajui kuandika wala kusoma hajui. Alivyosimuliwa asubuhi na jioni kasha yeyeanawasimulia watu akisema ,ameyatelemsha haya yule ajuaye siri za mbinguni na ardhini. Bila shaka yeye ni mwingi wa msamaa.’ Koroani sura 25 aya5-6. “ Ambao wanamfuata mtume. Nabii aliye Umi(maamuma) asiyejua kusoma wala kuandika , na juu ya hili atafundisha mafundisho mafundisho  hayo ya ajabu ya iuslamu.” (koroan. Sura 7 aya 157.)
 Njia hii ilianza kufuatwa mwaka wa 610 B.K. “Tarehe 17 mwezi 12 mwaka 610. Utume uliletwa.” (kitabu cha maisha ya nabii Muhamad Uk 1). Utume huu uliletwa kwa mtu huyu ili awaongoze wanaojua kusoma na kuandika wala hawazingatii kuchunguza kile wanachoagizwa kukifuata. Yako maneno ambayo yako wazi wala hayahitaji Elimu kubwa kuyaelewa, kama hapa. “Je, nimfanye mola wangu asiye kuwa mwenyezi Mungu, ambaye ni muumba wa mbungu na ardhi ambaye ulisha wala harishwi? Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu. Na nikaambiwa nisiwe miongoni mwao wanaomshirikisha  Mwenyezi Mungu.”  Je, mtu huyu awezakuwa kweli nabii wa BWANA Mungu aliye muumba wa mbingu na nchi? Ikiwa hana uhusiano naye tena amezuiwa kumshirikisha yeye aliye Mola? Mmu! Inatia shaka.
“Kwa maana kuna wengi wasiotii wenye maneno yasiyo na maana., wadanganyaji, na hasa wale wa tohara ambao yapaswa wazibwe vinywa vyao. Wao wanapindua watu wa nyumba zima, wakifundisha yasiyo pasa kwa mapato ya aibu, mtu wa kwao nabi wao wenyewe… Wanakili kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao wana kana: ni wenye machukizo, waasi wala kwa kila tendo jema hawafai.” Tit. 1:10-12,16. Kwa namna hii hata mafundisho yao hayatokani na MUNGU.
“Na wengi kati yao hawamwamini Mwenyezi Mungu, isipokuwa na huku wanatia ushirikina. (ufafanuzi: Na haya hata hapa petu tunayo japo tunafuata uislam lakini lakini tunatia ushirikina pia, tunakwenda makaburini tukayaambia Ee, bwana nimezongwa na …… ukinifungua ….. nitaleta hapa pesa au kombe la harua. Anasikia wapi huyu maiti?...”) koroani. Sura 12 aya 106.
“wala hawawi sawa walio hai na wafu. Kwa yakini mwenyezi Mungu umsikilizisha yeye amtakaye, na wewehuwezi kuwasikilizisha waliomom makaburini, na hao kama wamekufa wamo makaburini.” Koroan. Sura 35 aya 22.
Kumbuka mpendwa mtu yule asiyejua kuandika wala kusoma ndiye aliyeandikisha haya iili wale wanajua kusoma na kuandika wasome. Je, litakuwa kosa lake au kosa la waliandikiwa kutosoma na kutafakali hayo waaliyoandikiwa? Ili wajiepushe hata kujiponya nafsi dhidi ya udanganyifu mkubwa huu wa kumtumainia mungu asiyekuwa muumba wa mbingu na nchi. Maana mungu huyo wanayeelekezwa kumuabudu ni mungu wa mji wa dunia hii ya dhambi tu. “Bila sha nimeamlishwa nimwabudu mola wamji huu wa Maka.” Koroan. Sura27aya91.
Lakini Mungu wa kweli yeye yko Mbinguni. “Lakini MUNGU wetu yuko Mbinguni, alitakalo lote amelitenda.” Zab.115:3.
Ujajua Muhamad hata ukitafuta katika Koroan hakuna maali alipoitwa na Mungu kuwa nabii il yeye ndiye anajita kwa nabii. Lakini Manabii wa Mungu waliitwa na Mungu.
“…Ambao wanamfuata nabii aliye umi (maamuma) asiyejua kusoma wala kuandika na juu ya haya atafundisha mafundisho hayo ya ajabu ya uislamu.” Koroan. Sura 7aya157. Mafundisho yasiyokuwa na wokovu maana hayafundi kumtii Mungu wa Mbinguni, leea aya tuliyoisoma katika koroan hapo nyuma.
Ukisoma katika Koran sura ya 3aya ya 19. wanasema kuwa dini ya haki ni Uislam (wa ijumaa). Lakini ni nani aliyeanzisha dini hii. “Hawaabudu baada ya kumuacha Mwenyezi Mungu, ila waungu wanawakw.Wala hawamuabudu (Mungu) ila Shetani asianayewaanzishia hayo., ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani. Naye shetani alisema kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa hakika niashika sehemu maalum katika waja wako na nitawapoteza nanitawatumainisha na nitawwaaminisha ninavyotaka mimi. Basi watakata masikio ya wanyama wawafanye kuwa wanyama watukufu. (kama wanavyofanya ngamia waislamu) nitawaamuru pia, nao wataibadii dini yako Mwenyezi Mungu.” Koroan. Sura 4aya117-121. sasa unaweza kujua kuwa watu hawa wamebadilishwa na Shetani hata kuacha kumuabudu Mungu wa Mbinguni Katika dini yake na kutunza utakatifu wa sabato (jumamosi) na kugeukia ijumaa. Na hapa wamejipatia mafundisho ya uongo ili kuwapoteza. “Na miongoni mwao kuna baadhi yao wanaopinda ndimi zao kwa kusoma vitabu ili mppate kuyafikiri maneno yao hayo kuwa ni ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, … kumbe si sio kitabu cha Mwenyezi Mungu, wanasema haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu kumbe hayatoki kwa Mwenyezi Mungu. Wanamsingizia … uongo na hali wanajua kwamba huo ni uongo.” Koroan. Sra3aya78. Je, ni uongo gain wanaoufanya.  “Yeye Alah ndiye aliyetelemsha kitabu. Ndani yake zimo aya mukamu(nyepesi kufaamika) na zipo nyinine stashabiha yaani za kubabaishia, kama habari za ahela na za peponi na za motoni na mengineyo yanayohusika na roho. Wale ambao moyoni mwao mna upotovu wanafuata wanafuata zile ambazo zinababaishia. Kwa kutaka kuwaharibu watu…” koroan. Sura 3aya 7.
Je, unajua huko peponi na ahela ni wapi? Au ni mbinguni Ebu tuone koroani inatuambiaje!
Tuanze kungalia Peponi: Mfano wa pepo walioahidiwa Wacha mungu ni itakuwa hivi. Imo mito ya maji yasiyovunda na mito ya maziwa yasiyoharibika radha yake na mito ya ulevi yenye radha kwa wanywao na mitoya Asali iliyosafishwa, tena humo watapata matunda ya kila namna na zamaradi kuttoka kwa mola wao. Basi wale watakuwa sawa na walio motni na kunyweshwa maji yachemkayo. Koroan. Sura 47aya15.
 Ooh! Nmna hiihakuna hja ya kusumbuka kuifuata njia hii maana ni kujitesa bule na mwisho ni adhabu sawa na watenda dhambi wengine.
Habari gain kuhusu Ahela. (‘fafanuzi: jehanamu ni jina la moto maalumu huko ahela)” koroani sura 78aya 21. basi kama  ahela kuna moto wa jehanamu  hukumu ya hao watakkao kuwa huko itakuwa kuangamia kwa moto wa huo. Kwa hakika hakuna tumaini la wokovu kwa wanao ifuata njia hii maana ni njia ya uangamivu. Maana ikiwa uko usawa kati ya wadhambi na wema siku ya hukumu, njia gain hiii kuifuata isiyo na tumaini la Uzima.
Unafahamu hili kuwa hata Mtume muhamad hakujua hatima ya njia aliyoinzisha. “Mimi sio kiloja mpya katika mitume, wala sijui nitakavyofanywa mimi  wala sijui mtakavyo fanywa ninyi.” Koroani. Sura 4 6aya 9.
Kwa kuwa hajui hatima yake kama Mitume wa Yesu walivyojua. Ni nini hatima yautume wake? Maana Mitume wa Yesu wao walijua hatima yao “ Kwa maana Mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumalliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki ambayo BWANA mhukumu wa haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu na watu wote waliopenda kufunuliwa kwake. 2Tim.4:6-8.
Lakini tazama tumaini la Mhamad aliye mtume wa uislam: “Lakini wanangojea jingine la kuwajia mfano wa siku za adhabu zilizowafika watu aliopita kabla yenu. Basi mimi nami niko pamoja nanyi katika wanaongojea.” Koroani sura10aya 102. Kwa nini wanangojea adhabu? … Hakika adhabu ya kuivunja taadhima ya Jumamosi iliwekwa juu ya wale waliohitarafiana kwa ajili ya hiyo Jumamosi na kwa hiyo Mola wako atahukumu baina yao siku ya kiyama.” Koroan. Sura 16 aya 124.  Kwa sababu ya kuikataa sheria aliyopewa Musa Nabii wa Mungu, ingawa waliijua.
“Amekupeni shria ya dini ile ile aliyomhusia Nuhu na tuliyokufunulia wewe na tliyomhusia Irahimu na Musa na Isa, kwa simamisheni dini wala msifarakane kwayo.” Koroani sura 42aya13. Lakini rafiki unajua kuwa hata Alah mungu wa Waislamu atachomwa katika moto wa jehanamu? Tazama kitabu cha waislam cha Hadthi za mtume: uk.1071. “ … Jehanamu itaendelea kusema, je, kuna nyongeza? Mpaka alah subuana wataalaatakapoweka mguu wake na hapo atasema  inatosha? Inatosha na hapa kwa nguvu yako na zile sehemu zake nyingine zitakaribiana.” Ikiwa yeye aliye mungu wao ataangamia katika moto wa milele?! Si zaidi hao wafuasi wake? Njoo kwa Yesu yeye amekwenda kuwaandalia makao wote wamchao na kutoka huko atakuja kuwachukua akaishi nao milele zote.
Lakini habari gain kuhusu Jumapili? Katika kitabu cha muunganiko wa Madhehebu ya kipentekoste, kiitwacho: METHODIST. Uk.191 na 192. kinasomeka hivi:- “Unajua nini tunaelekea katika upande huo leo. Kanisa Katoriki la Rumi ujiita kanisa mama; linajiita kanisa la kwanza ama kanisa la awalli. Hivyo ni kweli tupu. Lilikuwa ndilo kanisaasi la kwanza la Rumi llililoanguka na kuuingia dhambini, lilikuwa la kwanza  ambalo liliunda madhehebu  ndani yake kulionekana matendo ya Wanilolai na aadae mafundisho ya wanikolai.
Hakuna mtu anaweza kukana kuwa ndilo mama. Hilo ni mama na llimeza mabinti, basi binti utokana na mwanamke. Mwanamke aliyevaa mavazi ya nyekundu na anketi juu ya vilima saba. Yeye ni kahaba na amezaa mabinti (Ufu. 17:3-5akanichukua katika roho hata jangwani nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru menye vichwa saba na pembe kumi. Na mwanamke yule likuwa amevikwa nguo za rangi ya Zambarau, na nyekundu… alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake klichojawa na machukizo . na katika kipaji cha uso wake aliuwa na jina lililoandikwa kwa siri, BABELI MKUU, MAMA WA MACHUKIZO NA MACHUKIZOYA NCHI.)  Mabinti hao ni makanisa ya kiprotestanti yalitoka kwake  a kasha yakarudi moja kwa moja kwenye Madhehebu ya wanikolai. Mama huyu wa makanisa binti anaitwa kahaba, huyo ni mwanamke ambaye hakuwa mwaminifu kwanadhiri yake ya ndoa, aliolewa na Mungu alafu akaenda kufanya uasherati na Ibirisi. Na katika uasherati wake amezaa mabinti walio kama yeye kabisa. Muungano huu wa mama na binti  ni upinga Neno, upinga Roho, kwa sababu hii ni upinga kristo.
            … Kabla sijaendelea mbali nataka kusema kwamba. Hawa Maaskofu wa mwanzo walidhani kuwa wao walikuwa  juu ya neon wao waliwambia watu kuwa wao waliweza kuwasamehe dhambi zao. Hiyo haikuwa kweli Walianza kubatiza watoto wachanga katika karne ya pili. Si ajiabu watu leo hii wamechanganyikiwa, ikiwa walikuwa wamechanganyikiwa  namna hiyo wakati huo karibu sana na wapentekoste wamo katika hali mbaya sana sasa kuliko nyakati zilizopita  wakiwa umbali yapata kama miaka 2000, kutoka kwake wakiwa wameacha ile kweli ya asisli.
 Hivyo ndivyo hasa kanisa katoriki lilivyo fanya wao waliwaua wale ambao wangektaa kutii utawala wa kipapa. Wale waliotaka maneno ya Mungu badala ya maneno ya watu, waliwaua mara nyingi kwa njia za kikatili. Lakini Kanisa hili ambalo lilishughulika na Mauaji lilikuwa lenyewe llimekufa na halikuwamo na uhai ndani yake wala ishara lililopata kufuatana nayo.
Sura hii inaonyesha nguvu ya kanisa Katoriki la Rumina yale litakayoyafanya kwa kupitia kwenye Shirika.  Kumbuka huu ndio ule mzabibu wa uogo  acha ulitaje tu jina la BWANA. Wanafanya hivyo kwa uongo, uongozi wao ni wake sio wa BWANA bali ni wa Shetani.” Methodist. Uk.191-2.
Kurasa hizi zinaeleza ukweli wa kile ambacho kwa wale wenye nia ya kutafutaa wokovu wataona sababu ya kuiangalia njia ya kweli. Unajua nini, kwamba ni kweli kuwa madhehebu zote za Kiprotestanti tayali zimekwisha jiunga na umoja wa Makanisa, ambayo muu wao ni Papa yule waiyetoka kwake na sasa wamerudi na kuwa nchini yake. Pengine ndio maana Mwandishi anasema wamekwisha rudi kwa mama yao. Ingawa wameziba masikio wasisikie wala kuwaambia watu wanaowaongoza juu ya hatari iliyo juu yao. “Watu wangu wamekuwa Kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani wamekwenda toka mlima hadi kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika (Raha). Yer.50:6. Raha yao iko wapi? “Basi, imesalia Raha ya Sabato kwa Watu wa Mungu.” Ebr.4:9.
Je, njia ipi itaingia Mbinguni?
“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazo zifanya, zitakavyokaa mbele zangu asema BWANA wa, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato,wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.” Isa. 66:22-23.
Mpendwa Sabato ya siku ya saba (jumamosi) ndiyo njia ya kweli na sahii  ya kukufikisha Mbinguni, ungu mwenyewe ndiye mwanzilishi wake, Yeye ni msabato, Malaika zake ni wasabato, Manabii Musa, Eliya, Nuhu, mitume wa Yesu ni wasabato kama Yesu alivyokuwa.  Mbinguni wote ni wasabato. Njoo ujiunge na kundi la watunza sabato uwe nawe kundla Mungu.