Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16


Mungu hakuumba wanadam kama roboti bali viumbe huru
uhuru huo usingekuwepo bila uwezo wa kuchagua jema au baya.
WALAKINI MATUNDA YA UJUZI WA MEMA NA MABAYA MSILE…
Na Petro Tumaini.

NI maneno ambayo yanaweza kuchukuliwa kuwa ya kawaida lakini ni chanzo cha shida na matatizo yote tuyashuhudiayo katika ulimwengu wetu leo…

Mara nyingi huwa ninafikiria, ni nini ambacho kilikuwamo  katika matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Je ni sumu, kemikali au ni nini kilifanya tunda lile lilete laana ya kifo?

Mwanzo 2 :16,17. BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, matunda ya kila mti wa bustani mwaweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile , kwa maana siku utakap[okula matunda ya mti huo utakufa hakika.


Tatizo halikuwa tunda maana tunda ni seheemu ya vile alivyoumba mungu na ambavyo ni vyema sana  Mwanzo 1:31 .

Tatizo lilikuwa ni kuvunja agizo la Mungu, agizo hili lilikuwa ni amri kutoka kwa Mungu kukaidi ilimaanisha kukaribisha laana ya dhambi, shetani kwa kulifahamu hilo alimdanganya Hawa ili avunje amri ya Mungu kwa kula 
tunda Mwanzo 3 :4,5. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo , mtafumbuliwa macho nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Waweza kumlaumu Adam na Hawa kwamba kwanini walikula tunda lakini hata leo yapo matunda mengi ambayo shetani amekushawishi ule nawe umekula…Kumbuka tatizo si tunda bali tatizo ni kutii au kuvunja agizo la Mungu.

Katika kitabu cha Kutoka 20, zipo amri 10 ambazo mungu ameamuru mwanadam yeyote asizivunje, lakini ni mara ngapi watu wamekuwa wakizikaidi bila kutambua kwamba wanaingizwa katika mtego uleule uliojitokeza katika Bistani ya Edeni.

Dhambi ni uasi wa sheria , 1 Yohana 3 :4 Kila atendaye dhambi , afanya uasi ; kwa kuwa dhambi ni uasi.  
Yapo mabo kadhaa ya kujifunza kupitia anguko la Adam na Hawa
  1. Shetani akujaribupo huja kama rafiki mzuri tena alimjaribu kupitia kiumbe kizuri . Mwanzo 3 :1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu… Kabkla ya anguko nyoka alikuwa kiumbe mzuri sana mwenye miguu na mabawa tena hapakuwa na uadui kati ya mwanadam na mnyama yeyote.Kuwa makini sana na vitu uvipendavyo sana kama vile mke, mchumba, rafiki, fedha na kadhalika Shetani atakujia kupitia hivyo. 2 Wakorintho 11 :4 Wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Waepuke sana wachungaji wakuvutiao kwa nguvu ya miujiza wengi ni vibaraka wa shetani
  2. Shetani huja katika namna ya kupendeza kuambatana nae (good company), hata Hawa alipomuona alitumia muda kitambo kufanya nae maongezi alifurahia kampani yake hadi akaingia katika mtego. Shetani akikufuata usikubali kuambatana nae, yawezekana kabisa Eva angekataa kuongea na nyoka angejiepusha na yote yaliyotokea. Ukutanapo na mwanaume muhuni au mwanamke malaya usimpe nafasi ya kuongea na wewe (hata kama wajiona mtakatifu sana) utanaswa.Dawa nzuri ni kukimbia, uonapo picha chafu usikae na kuangalia, mtu akianza kukushawishi kufanya maovu usikubali kuongea nae unampa shetani nafasi
  3. Shetani hujificha, kwa Hawa alitumia umbile la nyoka, leo huja kwa njia nyingi na namna nyingi kupitia ndugu, jamaa na marafiki. Njia rahisi ni kupima kile waongeacho endapo kiko sawa na maandiko.  Isaya 8 :20. Na waende kwa sheria na ushuhuda, ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.
  4. Shetani huficha hila zake, pale alipomjaribu Hawa hakuonyesha kwamba anahitaji Hawa aingie dhambini bali alionyesha kanakwamba kutenda dhambi ni kufunguka na kupata maarifasiku mtakayokula matunda hayo mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. (Mwanzo 3 :5) . Wengi hujaribiwa kuingia dhambini kwa kutaka kujua mambo bila kutambua kwamba kufuata maagizo ya Mungu ndiyo hekima yote…

‘Kumbuka kwamba Mungu kakupatia uwezo wa kutenda upendali, lakini amekukataza kuvunja amri zake na maagizo yake, usalama wako pekee ni pale utakapotumia uhuru huo kufanya yanayompendeza.’’