Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16



JINSI MAJASUSI WALIVYOANZISHA MATUMIZI YA VIDONGE
Utumiaji wa vidonge ulianzishwa na majasusi , ili kutengeneza faida
bila kujali kwamba vidonge ni sumu kwa afya ya mtumiaji.

    

    
Miaka ya 1930, Morris A. Bealle aliyekuwa mhariri wa zamani gazeti la Washington Times and Herald nchini marekani,alikuwa msimamizi wa gazeti maarufu ambalo liliingiza mapato makubwa sana kwa matangazo ya Kampuni ya nishati kila wiki.

Katika mapato yaliyokuwa yakikusanywa mwisho wa mwezi, kampuni hiyo ilionekana kama tegemeo kubwa la gazeti hilo.
Siku moja habari za malalamiko ya wananchi dhidi ya huduma mbovu za kumpuni hiyo yalianza kuandikwa na gazeti hilo.

Bealle,  alipata vitisho,vikali kutoka kwa kampuni iliyotengeneza matangazo ya kampuni hiyo ya nishati kuambiwa kama ataendelea kuandika habari “zilizo nje ya mfumo”  wa kampuni hiyo, si kwamba ataondolewa katika mkataba wa matangazo tu, bali kusitishwa katika huduma za kampuni ya gesi na ya huduma za simu.

Hapo ndipo macho ya Bealle yalifunguka kuhusu “uhuru wa vyombo vya habari”,hatimaye akaacha kazi kwasababu alikuwa na uwezo mzuri kiuchumi.

Kupitia uzoefu wake kitaaluma aliamua kufanya utafiti kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na kuja na tafiti kuu mbili
1.   Habari kuhusu Vidonge (The Drug Story)
2.   Nyumba ya Rokifila. (House of Rockefeller)

Kitabu kilichofunua siri kali ,jinsi jamii ya siri ya Majasusiwalivyosambaza
 utumiaji wa madawa ya kisasa (vidonge)ambayo ni hatari kwa afya
 yamwanadam



Pamoja na uzoefu katika ulimwengu wa uhariri  hakuweza kuandika mafunuo yake mpaka alipoanzisha kampuni yake binafsi iliyoitwa Idara ya uchapishaji –Kolombia, Washinton D.C.,mwaka 1949.

Pamoja na kitabu cha Habari kuhusu Vidonge  kuwa katabu cha pekee katika masuala ya Siasa na Afya nchini Marekni, kamwe hakijawahi kupelekwa katika maktaba kuu za vitabu wala kuzungumziwa katika magazeti ya marekani.
Kwa upande wa uuzaji , kitabu hiki pekee kiliuzwa kwa njia ya mizigo iliyosafirishwa kupitia shirika la Posta. Pamoja na hayo , kitabu hiki baada ya kuingia sokoni katika toleo lake la 33 kilikuwa kikitoka katika lebo tofauti kama vile Biworld Publishers, Orem na Utah

Baelle alibainisha kuwa kwa miaka 1960, biashara iliyoingiza faida asilimia sita (6%), ilikuwa ni biashara kubwa sana.

KAMPUNI YA JAMII YA SIRI (MAJASUSI) ILIYOITWA NGOME YA MADAWA YA ROKIFILA (The Rockefeller Drug Empire) iliingiza faida Dolla za marekani Milioni 23.4 baada ya kulipa Kodi katika mali za thamani ya Dola milioni 43.1. sawa na asilimia hamsini na nne (54%) .
Kampuni ya Skwibu (Squib) amayo pia iko chini ya  Rokifila (Kampuni ya majasusi) iliingiza faida ambayo si asilimia 6 bali asilimia 576 (576%) katika thamani
Faida hii ilitokana na juhudi za Daktari mkuu wa Upasuaji  , ofisi ya Jemedari wa jeshi pamoja na Taasisi ya Madawa Na Upareshei ya Navi (Navy Bureau of Medicine and surgery)   Taasisi hizi hasikuwa tu  zikihimiza wattu watumie vidonge, lakini walilazimisha  sumu za vidonge katika damu za Wanajeshu wa Marekani , wasafiri wa majini na mabaharia.
“Je ni ajabu , kwamba Rokifila, na vitengo vyao vya vya biashara (mbovu) ya vyakula na madawa, Jumuiya ya Afya Ulaya, Taasisi Kuu ya Biashara,  Taasisi ya Madawa ya Navi, na maelfu ya maafisa wa dawa nchi nzima , kuunganika na kupinga aina zote za tiba zipingazo matumizi ya vidonge?” Aliuliza baelle.
Baelle aliendelea kubainisha kwamba katika kipindi hicho “Ropoti ya mwisho wa mwaka ya Faundesheni ya Rokifila”, ilionyehsa zawadi (tuzo) ilizotoa katika vyuo na taasisi za umma katika miaka 44 iliyopita, thamani yake ilizidi dola nusu bilioni.
Vyuo hivi vilianza kufundisha ujuzi wa kutumia madawa ambayo Famasi za Rokifila zilihitaji ufundishwe.  Tofauti na hapo hukukuwa na tuzo, kama vile vyuo visivyo vya kawaida 30 katika jumuiya ya Ulaya vilivyokosa tuzo kwa kutofundihsa tiba zilizoegemea katika utumiaji wa vidonge.
Baadhi ya vyuo maarufu vilivyopewa fedha na kampuni hii ya Kijasusi ili kuhimiza utumiaji wa madawa ya kisasa ni:
·       Havadi, pamoja na shule yake ya Tiba ambayo maarufu sana , ilikuwa imepokea  Dola Milioni 8.7 kutoka Taasisi ya Fedha za Madawa ya Rokifila.(Rockefeller’s Drug Trust Money )
·       Yale, chuo kilipewa Dola Milioni 7.9
·       John Hopkinss, kilipokea Dola Milioni 10.4
·       Chuo Kikuu  cha Washintoni huko Mt.Louis, kilipewa Dolla Milioni 2.8
·       Chuo Kikuu cha New York Kolombia , kilipewa Dola Milioni 5.4
·       Chuo Kikuu cha Korneli , kilipokea Dolla Milioni 1.7 n.k
Pamoja na “kugawa” vitita vya fedha kwa vyuo vilivyosambaza propaganda za utumiaji wa vidonge , madhumuni ya Rokifilla yaliendelea kukua katika mtandao wa dunia nzima kuliko mtu yeyote awezavyo kugunda.
Kwa zaidi ya miaka 30, ilikuwa ni kiasi cha kutosha kwa Baelle kugundua Makusudio yaliyoanzishwa na Rokifila, na kuendelezwa katika Kampuni kubwa isiyoweza kufikiriwa namwanadam.
Rokifila inamiliki jumuiya kubwa ya kuzalisha madawa ya kisasa Duniani kote, na hutumia madhumuni yao mengine yote kukuza uuzaji wa madawa. Ukweli kwamba zaidi ya aina 12,000 za madawa tofauti (ya kisasa) katika soko ni sumu, si wazo la wazalishaji wa madawa...
Itaendelea...


MBINU ZA IBILISI KUONDOA MATENGENEZO KWA WAKRISTO
Shabaha Kubwa Ya ibilisi ni kuwaondoa watu katika Utii wa neno la Mungu
kwasababu kutii Biblia ni kiini cha matengenezo, na utakaso . Yohana 17:17. 


Katika biblia, Yuda 1:3 Biblia yasema tuipiganie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara Moja...


Miongoni mwa mambo makubwa aliyhoyafanya Ibilisi, ni kuondoa hali ya matengenezo kwa watu wa Mungu, zifuatazo ni agenda kuu kumi zilizoandaliwa na jamii za siri ili kuwafanya Wakristo wabweteke , na kuachana na juhudi ya kufanya matengenezo. 

Mambo aliyopangilia Ibilisi kupitia kikao cha siri, kama utakavyoyasoma utagundua kwamba ni udhihirisho katika yale yaendeleayo miongoni mwa Wakristo wengi.

Hizi ni agenda za kikao cha siri

  1. Kuzusha magombano baina ya waombezi ili kuwavunja wasiendelee kumtafuta Mungu wao.
  2. Sababisheni hadithi kwa wingi watakapoingia ndani ya makanisa yao wakati wa kuja kumuomba Mungu wao.
  3. Msiwaruhusu kuomba wakati wa kulala kwao (Janatus) maana hamuwezi kuwaona wakifunikwa na nguvu za Mungu wao.
  4. Msiwape nguvu au nafasi ya kusoma Biblia, baadala yake wapeni wakati mwingi wa kusoma magezeti na kuangalia televishini zao.
  5. Sababisheni ufukara, mateso na pesa zao kupotea bila wao kujua ili wasimtolee Mungu wao, na walio na pesa roho ya ubahili ya kutokutoa.
  6. Inueni nguvu za kuzimu makanisani kwao baina ya viongozi na washirika wao na vijana kwa wasichana ili kupata nafasi ya kuzima nguvu zao.
  7. Ibada zao ziwe baridi kabisa ili Roho wa Mungu wao asipate nafasi ya kuongea na kusikia kutoka kwake.
  8. Tumieni ajali maana damu yao tutaitumia katika vikao vyetu.
  9. Akina mama wajawazito wazalishwe kwa operesheni ili kupata damu.
  10. Tumieni Ukimwi wa kutengeneza kama pigo kwao ili kuwamaliza na kuwaletea aibu katika vifo vyao.
  11. Vurugeni umoja wa nyumba zao kati ya mke na mume, wazazi na waatoto wao ili maombi yasipatikane.
Hayo ni Baadhi ya Mambo yhaliyoorodhesha katika barua ya kikao hicho.

Ukristo ni gharama, kujikana nafsi. Je katika hayo ni lipi ambalo walitenda na kumpatia mwanya Ibilisi katika maisha yako? 

Habari njema ni kwamba , ukimtegemea Yesu kwa moyo wote bila kujichanganya na mabo ya dunia ,kwake ushindio ni wa Lazima. 

Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 

Biblia izungumziapo Mbinu za ibilisi dhidi ya wale wamtegemeao Yesu huishia na kauli ya ushindi , hii ni kutokana na Ukweli kwamba KUPITIA KIFO CHA YESU PALE MSALABANI IBILISI ALINYIMWA UWEZO DHIDI YA WOTE WAMTEGEMEAO YESU

Ufunuo 12:11. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakuyapenda maisha yao hata kufa.



KUFUNGA, IBADA ISIYOKWEPEKA KWA

 MKRISTO

“Akafunga siku arobaini mchana na usiku , mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia , Ukiwa ndiwe mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mkate.” Mathayo 4:2,3
“Baadhi wamekweza kitendo cha kufunga kuliko maandiko yote na makusudi; japokuwa , wengine wamepuuzia kitendo hicho.” John Wesley.
KWANINI MUNGU ALILETA WAZO LA KUFUNGA
Kwa Yesu, kama vile kwa ndoa takatifu pale Edeni, tamaa ya chakula kilikuwa ni kigezo cha jaribu kubwa la kwanza. Pale anguko lilipoanzia, kazi ya ukombozi wetu lazima ianzie hapo. Kwa kuendekeza tama ya chakula Adam alianguka, kwahiyo kwa kuikana tamaa ya chakula Yesu lazima ashinde anguko. “Akafunga siku arobaini mchana na usiku , mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia , Ukiwa ndiwe mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mkate.”[1]

JE BIBLIA HUONYESHA KUWA KUFUNGA NI LAZIMA AU UAMUZI.
Japokuwa Biblia haijaonyesha kuwa kufunga ni amri, huonyesha kuwa kufunga ni suala litarajiwalo kwa mfuasi makini wa Mungu .Katika Mathayo 6:17-18 husema “ufungapo” Ysu hakusema “kama ukifunga” badala yake akasema “ufungapo” ili kuonyesha kwamba anatarajia tufunge na kuomba kama kama wafuasi wake.
Kwa nfuasi wa Yesu, swali la kujiuliza si kwamba Je naweza kufunga bali Je nitafunga, na kama nikifunga nifunge vipi?
“Siwezi kusaidia bali kushangaa kwamba matukio makubwa hayawezi kutokea kwasababu tunapuuzia kufunga” K. Neill Foster

Katika biblia suala la kufunga na kuomba, hutajwa mara nyingi sana japokuwa uelewa wa watu kuhusu suala hili nyeti umekuwa ni tofauti na limepuuziwa kuliko Mungu alivyolipa uzito wa Kiroho .Kumekuwa na dhana potofu kuhusiana na ibada ya kufunga.
  • Wapo wadhanio kwamba kufunga ni kuacha kula matokeo yake wanashinda na njaa badala ya kufunga.
  • Wengine hudhani kwamba kwa kuacha kula wanaongeza nafasi ya kupata upendeleo kwa Mungu ili awajibu maombi yao.

Lakini swali bado linabakia:
  • Nini maana ya kufunga?
  • Kwanini maombi ya kufunga husisitizwa sana katika biblia?
  • Kufunga kuna faida gani?
  • Hivi kuna mambo ambayo hatuwezi kuyapata bila kufunga?

Hayo na mengine mengi yatajibiwa katika somo hili “Kufunga na maajabu yake kiroho”

KUFUNGA HUMAANISHA NINI?

Kufunga , ni neno lililotokana na neno la limaanishalo kuacha kula chakula, eidha kwa madhumuni ya kidini au kwasababu ya ukosekanaji wa kiebrania \suÆm, chakula, au kipindi cha kufanya jambo hilo.[2]
Kufunga humaanisha kuweka kando starehe yoyote ile au shughuli ya muhimu kwa kipindi fulani ili kumtafuta Mungu kwa juhudi.

Hapa jambo la msingi tutakaloliangazia ni kufunga kwaajili ya maombi katika Biblia, suala la kufunga huonekana pote katika biblia kuanzia agano la kale hadi agano jipya.

  1. Musa alifunga siku 40 mara mbili hadi uso wake ukabadilika na kuangaza utukufu wa Bwana. (Kumbukumbu la Torati 9:9,18)
  2. Yoshua alifunga baada ya ushindi pale AI.(Yoshua 7:6)
  3. Daudi alifunga kabla ya kuteuliwa kuwa mfalme, wakati mwanae ailpougua, na kwasababu ya dhambi za watu wote (Zaburi 35:13; 69:9-10)
  4. Yehoshafati na watu wake walifunga mpaka Bwana akasema hawatapigana vita  hatimaye wakashinda vita kwa kufunga na kuomba tu (2 Mambo ya Nyakati 20:17)
  5. Danieli alifunga na kuomba mpaka Gabrieli akagizwa kumfariji na kumpatia majibu ya njozi ambayo hakuielewa. (Danieli 9:3,21-23)
  6. Yesu alifunga siku 40 na kupata nguvu ya kumshinda majaribu shetani kwa niaba ya mwanadamu na kuukomboa ulimwengu.

“Kwa Mkristo kufunga si suala la uchaguzi bali la msini.
Ushahidi wa vielelezo hivyo ni udhihirisho kwamba
    • Mungu hupendelea sana watu wamwelekeao kwa maombi wafunge ili kuwa karibu na yeye zaidi.
    • Kuna mambo ambayo wafuasi wa Mungu hawawezi kupata bila kufunga na kuomba kama vile imani. (Mathayo 17:21)
    • Mungu aliona kufunga ni jambo lisilokwepeka kwa kila mfuasi wake kiasi cha kulizungumzia sana katika biblia.
    • Hakuna ushindi wa Dhambi Bila kufunga na kuomba.

Pamoja na wengi kujua umuhimu wa kufunga na kuomba , bado utata umebakia katika namna ya kufunga na kuomba, wapo ambao kiukweli hufunga na kuomba huku wengine hushinda na njaa wakidhani kwamba wamefunga na kuomba. Ili kujua kuwa umefunga sawa na maagizo ya biblia, wapaswa kuelewa maana halisi ya kufunga.

KUFUNGA KULIKO SHAHIHI
  • Kufunga humaanisha kuweka akili na Moyo kwa Mungu na sio katika chakula. “Roho ya kufunga kwa kweli na maombi ni roho iwekayo akili na moyo kwa Mungu[3] Pia humaanisha “kufikiria sana chakula kutoka mbinguni kitakacotoa nguvu na uwezo katika uzoefu wa kidini[4]

“Mfungaji aachapo chakula, ubongo haushughuliki tena na jukumu la kumeng’enya au kufikiria chakula bali unamuelekea Mungu.”

  • Hitaji la Kiroho na vita ya kiroho , kusudi lako la kupatana na Mungu ni zito kiasi  kwamba umeamua uachane na mahitaji ya kimwili ili ujitoe katika maombi na kutafakari. (Zaburi 1:1) Hili ni kutokana na ukweli kwamba kati ya mambo yafanyayo tushindwe kumtafakari Mungu vizuri ni uroho na tama ya ya chakula (kukosa kiasi katia ulaji.)

MBINU SaHIHI ZA KUFUNGA
KAMA tulivyoona kufunga ni kuacha kula kwa madhumuni ya kidini, hii humaanisha kwamba kufunga hakuishii kuacha kula peke yake, bali ni kudhiirisha kwamba Hitaji lako kwa Mungu ni zito kuliko mahitaji uyapenadayo(mf chakula, usingizi n.k). Kwa ukweli huo, zifuatazo ni namna tofauti za kufunga:

  • Kuacha vyakula vya kusisimua (stimulants). “Kufunga kwa kweli kushauriwako kwa wote , ni kuacha kila chakula cha kusisimua, matumizi sahihi ya chakula rahisi, cha lishe ambacho Mungu ametoa kwa wingi. Watu wapaswa kufikiria kidogo kwamba ni nini watakula na kunywa katika chakula cha kupita, na wafikirie zaidi chakula kutoka Mbinguni.[5]
  • Kujinyima (kufunga) usingizi, kujinyima usingizi humaanisha hitaji la kiroho ni zito kuliko usingizi. Mara kadhaa Yesu alijinyima usingizi na kukesha katika maombi, waweza kufunga kwa kuacha kulala kwa sababu zilezile za kuacha kula. (Luka 6:12)

Yakobo katika Mto Jabok alijinyima usingizi usiku kucha akiomba hatimaye ombi lile aliloomba kwa miaka ipatayo 20 likajibiwa usiku ule.

  • Kujitenga na wale au vile uvipendavyo , kuna wakati ambapo waweza kujitenga na ndugu, familia na mazingira uyapendayo sana ili kukutana na Mungu tu. Waweza kwenda mlimani au sehemu ya upekee ili umtafakari Mungu bila muingiliano na jambo lolote. Kuna wakati Yesu alijitenga na jamii (Mathayo 14:23)
  • Kula kidogo chakula rahisi , “Sasa na kuendelea mpaka mwisho wa wakati watu wa Mungu wapaswa kuwa makini sana, wawe macho zaidi, wasitegemee hekima zao wenyewe…Watenge siku kwaajili ya kufunga na kuomba. Kuacha kula kabisa kwaweza kusihitajike, lakini wale kwa kidogo (sparingly) chjakila rahisi.[6]
  • Waweza kuacgha kula kabisa na kunywa, waweza kuacha kula tu ukanywa maji, waweza kuacha chakula ukala matunda.Kwa ujumla kufunga ni kuacha yote tuyapendayo katika dunia hii (vyakula,kazi, matamanio) kwasababu twaelekeza akili katika ulimwengu mwingine  (Mbingu).

AINA ZA KUFUNGA ZIPATIKANAZO KATIKA BIBLIA
  • Kufunga kwa kawaida(Normal Fast), huku ni kuacha vyakula vya aina zote na kunywa maji tu.
  • Kuacha kula kabisa (Absolute Fast) ,ni aina ya kufunga ambapo mfungaji huacha kula na kjunywa kabisa I Wafalme 19:7-10

  • Kufunga kidogo (Partial Fast) , huambatana na kuacha kula vyakula ambavyo wapendelea kuvitumia. Danieli na wenzake walifunga hivi kwa kunywa maji na mtama tu kwa siku kumi.Danieli 1:15. Wakati mwingine danieli alifinga hivi wiki tatu. Danieli10:3.

“Kufunga kwa aina zote tatu kunakubalika mbele za Mungu jambo la msingi ni kuelekeza akili kwa mungu pekee wakati wa mfungo”

YAPO MAMBO AMBAYO KAMWE  HATUWEZI KUFANYA BILA KUFUNGA.
  • Tiba dhidi ya baadhi ya magonjwa, “kula bila kiasi husababisha magonjwa, na asili huhitaji zaidi kupumzishwa kutoka katika mzigo mzito ambao umebebeshwa. Katika matatizo mengi ya magonjwa, tiba ya pekee ni mgonjwa kufunga mlo mmoja au miwili. [7]  
“Wapo wawezao kunufaika zaidi kwa kuacha kula siku moja au mbili kila wiki kuliko …ushauri wa kitabibu. Kufunga siku moja ya wiki kwaweza kuwa ni faida isiyokifani kwao.”[8]   
  • Kuishinda dhambi, “Yesu aliingia katika jaribu juu ya suala la tama ya chakula, na karibia wiki sita alishinda jaribu kwa niaba ya mwanadam. Kule kufunga kurefu katika nyika ni fundisho wakati wote kwa mwanadam aliyeanguka dhambini…Alitoa fundisho mkwa mwanadam kwamba ataanza kazi ya kushinda pale anguko lilipoanzia, katika suala la tama ya chakula.[9]
  • Kuelewa maandiko. “Kuna baadhi ya maandiko na mambo ambayo ni magumu kuelewa…Muda utafika chini ya upaji wa Mungu kwa dunia kujaribiwa kwa ukweli wa wakati huo, akili zitafanyiwa mazoezi kwa Roho Yake ya kuchunguza maandiko hata kwa kufunga na kuomba …kila ukweli unaohitajika haraka kwa wokovu utawekwa wazi kiasi kwamba hakuna atakayehitaji kukosea...[10]
  • Kupata majibu kwa maombi, kuomba pekee hakutoshi kupata majibu kwa mahitaji yote bali baadhi ya mambo hujibiwa kwa njia ya kufunga na kuomba. “Kwa baadhi ya mabo , kufunga na kuomba hushauriwa na ni sahihi.Katika mkono wa Mungu ni njia ya kusafisha moyo na kuhamasisha…mfumo wa akili. Tunapokea majibu kwa maombi yetu kwasababu tumenyenyekeza mioyo yetu kwa Mungu”[11]
  • Maombi ya kufunga pekee yaweza kuwaokoa waliotekwa katika umizimu, “baadhi ya roho zilizoshangazwa na maneno ya kuvutia kutoka kwa walimu wa umizimu, na kufuata msukumo wake, baada ya hapo wakatambua tabia yake ya mauaji, wataacha na kuukimbia, lakini hawataweza.Shetani kawashikilia kwa nguvu zake, na hayuko tayari kuwaachia huru…shetani atawaimarisha malaika wake waovu ambao wamewaendesha watu hawa, lakini kama watakatifu wa Mungu wakifunga na kuomba kwa moyo wa dhati maombi yao yatashinda.Yesu atatuma malaika watakatifu kumpinga shetani...[12]
  • Kutambua mapenzi ya Mungu katika mipango yetu, “kuna nyakati ambapo mkristo anahitaji umakini wa mawazo na uamuzi madhubuti, aweza kuwa na maamuzi muhimu ya kufanya, au anahitaji kutambua zaidi mapenzi ya Mungu. Katika mazingira hayo kufuka kutathibitisha mbaraka mkubwa.kufunga huko kwaweza kusiwe kuacha chakula kabisa, lakini mlo uloandaliwa na virutubisho rahisi kwaajili ya kuendeleza afya na nguvu… (Dan 10:3, Matt. 6:16.)[13]

MAMBO YA KUZINGATIA KUHUSU KUFUNGA
  • Hatupaswi kufunga kwa kujionyesha kwa watu, “kama mtu anafunga ni suala lake binafsi. Kwakweli, msingi wa kufunga ni utambuzi wa hitaji binafsi wa kufanya hivyo.Fundisho la Yesu ni kwamba kufunga kunapaswa kuwa uzoefu binafsi unaofanywa kwasababu ya utambuzi wa hitaji, na sio…kujipatia sifa ya umahiri…”[14] Kufunga ni njia ya kumtafuta mungu na kusogezwa karibu naye
  • Hatupaswi kufunga kama desturi, wapo wanaofunga ili kutimiza wajibu au kutekeleza tu ratiba Fulani na sio kutokana na hitaji, msukumo wa kiroho uletwao na shauku ya kutaka kuwa karibu zaidi na Mungu. Usifunge kwa kufuata tu ratiba iliyopangwa ,huko ni kushinda na njaa, hata kama kuna ratiba sharti uwe na shauku na msukumo wa dhati kufanya hivyo. Kufunga si tendo la neema kwa lenyewe tu, bali lifanywapo katika moyo wa upendo, hitaji na kujitoa huwa mbaraka.
  • Usichukulie kufunga kama kitendo cha kupata upendeleo kutoka kwa Mungu, wengine hudhani akifunga Mungu atasikiliza ombi kwa makini zaidi wanasahau kwamba sikio la mungu liko wazi siku zote.
  •  Kufunga ni kwaajili ya kubadilisha hali zetu na kutubadili sisi, sio kumbadilisha Mungu. (Isaya 58:1-9).
  • Kufunga si mbadala wa utii, wana wa Israeli walizingatia sana kufunga wakapuuzia majukumu yao kiroho na kimwili wakidhani kwamba kufunga kungemfanya Mungu apuuzie Dhambi zao walizoendelea kuzitenda.(Isaya 58:1-11) Mungu aliwadhihirishia kuwa pamoja na kufunga pia huzingatia utii na kujitoa.


“Maombi ya kufunga ni silaha pekee kwa kila mkristo  kwa maana Ukristo ni kuenenda kwa Imani sio kwa kuona tu, na pasipo Imani haiwezekani kumpendeza mungu, na Imani ya kushinda vita ya kiroho hupatikana kwa kufunga pekee.”



[1] Ellen G White.(1898) Tumaini la Vizazi Vyote,uk 117,118.

[2] Horn, Siegfried H., Seventh-day Adventist Bible Dictionary, (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Association) 1979.
[3] Ellen G White(1938) . Counsels on Diet and Foods
[4] Ellen G White (1932). Medical Ministry
[5] Ellen G White(1932) . Medical Ministry,pg 283
[6] Ellen G White (1904) Review and Herald.
[7] Ellen G White (1905) Ministry of Healing.pg 134
[8] Ellen G White (1902) Testimornies for the Church.vol7.pg 134
[9] Ellen G White(1938) . Counsels on Diet and Foods.pg 186
[10] Ellen G White (1870) Testimornies for the Church.vol 2.pg 692
[11] Ellen G White(1938) . Counsels on Diet and Foods. pg 187
[12] Ellen G White (1855-1868) Testimonies For The Church. vol 1, pg
[13]Nichol, Francis D., The Seventh-day Adventist Bible Commentary, (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Association) 1978.
[14]Nichol, Francis D., The Seventh-day Adventist Bible Commentary, (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Association) 1978.