Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16


JE UMEMPENDA AU UMEMTAMANI
Na Petro tumaini 
Tofauti kati ya upendo na tamaa ni dhahiri, zingatia haya ili ujenge mahusiano yenye afya.

Kati ya changamoto zitukumbazo vijana ni kukurupuka katika mahusiano bila kuelewa ni nini tunafanya. Kwa upande wa wanandoa changamoto nyingi huwapata kwasababu wameingia katika mahusiano na watu waliodhani wanawapenda kumbe wamewatamani.

Kati ya mambo yasumbuayo katika mahusiano ni watu kudhani upendo ni ngono , lakini ukweli ni kwamba ngono ni sehemu ndogo sana ihusikayo katika upendo kwa wanandoa. Wengi wamevunja ndoa zao kwasababu wameingia katika mahusiano wakidhani kuwa ngono ni kila kitu kumbe kuna majukumu makubwa katika ndoa kuliko ngono.

UPENDO HUUNDWA NA PANDE KUU TATU 
Kwa mujibu wa mwanasaikolojia Robert Stenberg, ili watu wafikie katika mahusiano sahihi ya ndoa ni lazima wapitie hatua tatu
Upendo sahihi katika mahusiano huanza na Mawasiliano (Intimacy), maamuzi ya kufunga ndoa (
                                               Commitment ) na hatimaye tendo la ndoa (Passion)
  1. Intimacy , hii ni sehemu ya mahusiano iundwayo na ukaribu wa kimawasiliano. Kubadilishana mawazo , kufanya kazi pamoja , kufahamiana ,kusaidiana katika shida na raha  .
  2. Commitment , ni sehemu ya pili ya upendo inayohusiana na kuweka mkataba wa makubaliano ya kuwa wachumba mtakaooana na kufikia hatua ya kula kiapo (comitment) ya kuishi pamoja hata mauti itakapowatenga.
  3.  Passion , ni sehemu ya tatu ya upendo ambayo huundwa na mahusiano ya kimwili ambayo  ambayo kilele chake huwa ni tendo la ndoa.

Kumekuwa na kampeni ambazo ni kinyume cha maandiko matakatifu , ikiwamo ''Kampeni ya kucheza ngono salama" , Kibliblia hakuna ngono salama , aziniye baada ya kuthibitisha afya yake na mwenzi wake au kwa kutumia mpira Biblia humuhesabu kama mzinzi / mwasherati. 

KANUNI ZA BIBLIA KUHUSU NGONO KABLA YA NDOA

1 Wakorintho 6:18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 

2 Timotheo 2:22 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. 

Kutoka 20:14 Usizini.


Kumbukumbu la Torati 5:18 Wala usizini  

INFATUATION(KUGHURIKA)
Jambo lipaswalo kufanywa wakati wa uchumba ni , mawasiliano (intimacy) , ya ukaribu  kufahamiana na kusaidiana katika mambo ya kawaida (si matakwa ya ashiki za ngono). 

Jambo la Pili katika mahusiano ya uchumba ni kufanya makubaliano ya kuoana na kufunga ndoa (commitment).

Baada ya kupitia hayo mawili ( 1-Intimacy, 2- commitment ) ndipo wanandoa hufaidi mbaraka wa tendo la ndoa (Passion). Wachumba waingiao katika maghusiano bila kupitia hatua hizo tatu hutafuta laana katika ndoa yao watakayo funga.

HATUA ZA UCHUMBA MPAKANDOA YENYE MBARAKA
  1. Intimacy
  2.  Commitment.
  3. Passion.
HATUA ZA UCHUMBA MPAKA KWENYE NDOA YENYE LAANA
  1. Intimacy
  2. Passion
  3. Commitment

 AU

  1. Passion
  2. Intimacy
  3. Commitmet
Kama wewe ni kijana mwenye mchumba , zingatia kanuni za kibiblia ili ndoa yako iwe nyenye mbaraka . Bwana akubariki.