Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16


NI NANI WA KUTUTENGA NA YESU?


SOMO HILI LIMEANDALIWA NA PETRO TUMAINI


Mtu mmoja aliye na Yesu ni Yote, Kitu cha pekee kuwa na Shauku kwacho ni uhakika wa Kuwa na Yesu siku zote, kitu cha pekee kuwa na hofu kwacho ni kutengwa na upendo wa Yesu.  
 Hakuna jambo tulitafutalo katika dunia hii ambalo Yesu hawezi kulitimiza. Mtu akimpata Yesu, amepata yote katika dunia hii na Zaidi Uzima wa milele .
Mathayo 19:29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
Ukweli ni kwamba , kama huna Yesu, hata usome elimu yote ya dunia , ufanye kazi kuliko watu wote duniani, umiliki mali na kuwekeza katika kila nchi duniani, uwe na fedha katika kila Benki uijuayo chini ya jua, Uwe tajiri wa kwanza duniani, hayo Yote Bila Yesu ni Bure.
Kama ni hivyo Basi Swali la Msingi ni hili, Kama nimempata Yesu ni kitu gani chenye mamlaka ya kunitenga na Kristo? Wapo wanaomwacha Yesu kwasababu ya mali, wapo watengwao nae kwasababu tofautitofauti. Swali bado linabaki,  Je Ni nini Kitakachotutenga na Kristo? Paulo alijiuliza swali na kutoa majibu katika mafungu yafuatayo.
Warumi 8:35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?

Je ni dhiki au shida ?

Miongoni mwa Ahadi tamu za Biblia ni Uhakika kwamba Aliye na Yesu ni Yote. Waati wa Matatizo wengi hutetereka na kudhani kwamba Yesu kawaacha laini ukweli ni kwamba SHIDA NI NJIA YA KUTUPELEKA KWA YESU MAANA YEYE NDIYE KIMBILIO LETU
2 Wakorintho 1:3,4 Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; 4 atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.

Je Ni Mauti ?

Swali la Msingi ni hili, Kati ya Mauti na Yesu ni lipi lenye mamlaka na uwezo kuliko jingine, Jibu rahisi ni Yesu. Yeye aliishinda mauti,  wapo ambao wakimfuata Yesu wako tayari kumwacha ili wasipatwe na mauti ya muda mfupi lakini bbiblia inatupatia tumaini

Mathayo 5:10
10 Heri wenye kuudhiwa (kuuliwa) kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Ayubu 5:20
20 Wakati wa njaa atakukomboa na mauti; Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga.

Waebrania 11:4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.

Yohana 11:25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
Ufunuo wa Yohana 14:13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Yohana 8:51 Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.
Warumi 8:38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Je  ni hatari ?

Mungu anamamlaka juu ya hatari zote ziwezazo kutupata katika duinia hii, Paulo alikutana na hatari karibu aina zote akiwa kwenye kazi ya  ya Mungu kama adhihirishavyo katika waka ufuatao
2 Wakorintho 11:26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang'anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;
Pamoja na hatari zote Paulo alikuwa na tumaini moja na akazishinda
2 Wakorintho 12:9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

Uwe katika shida kama Ayubu , uwe katika raha kama Sulemani, katika utajiri kama Ibrahimu au katika umaskini , katika hali yoyote uliyonayo kumbuka wapo walioitwa na Mungu katika hali kama Yako . JINSI ULIVYO  UWAPO NA YESU HAKUNA LA KUKUTENGA NAE ,NEEMA YAKE YATOSHA .