Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16



KUFUNGA, IBADA ISIYOKWEPEKA KWA

 MKRISTO

“Akafunga siku arobaini mchana na usiku , mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia , Ukiwa ndiwe mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mkate.” Mathayo 4:2,3
“Baadhi wamekweza kitendo cha kufunga kuliko maandiko yote na makusudi; japokuwa , wengine wamepuuzia kitendo hicho.” John Wesley.
KWANINI MUNGU ALILETA WAZO LA KUFUNGA
Kwa Yesu, kama vile kwa ndoa takatifu pale Edeni, tamaa ya chakula kilikuwa ni kigezo cha jaribu kubwa la kwanza. Pale anguko lilipoanzia, kazi ya ukombozi wetu lazima ianzie hapo. Kwa kuendekeza tama ya chakula Adam alianguka, kwahiyo kwa kuikana tamaa ya chakula Yesu lazima ashinde anguko. “Akafunga siku arobaini mchana na usiku , mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia , Ukiwa ndiwe mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mkate.”[1]

JE BIBLIA HUONYESHA KUWA KUFUNGA NI LAZIMA AU UAMUZI.
Japokuwa Biblia haijaonyesha kuwa kufunga ni amri, huonyesha kuwa kufunga ni suala litarajiwalo kwa mfuasi makini wa Mungu .Katika Mathayo 6:17-18 husema “ufungapo” Ysu hakusema “kama ukifunga” badala yake akasema “ufungapo” ili kuonyesha kwamba anatarajia tufunge na kuomba kama kama wafuasi wake.
Kwa nfuasi wa Yesu, swali la kujiuliza si kwamba Je naweza kufunga bali Je nitafunga, na kama nikifunga nifunge vipi?
“Siwezi kusaidia bali kushangaa kwamba matukio makubwa hayawezi kutokea kwasababu tunapuuzia kufunga” K. Neill Foster

Katika biblia suala la kufunga na kuomba, hutajwa mara nyingi sana japokuwa uelewa wa watu kuhusu suala hili nyeti umekuwa ni tofauti na limepuuziwa kuliko Mungu alivyolipa uzito wa Kiroho .Kumekuwa na dhana potofu kuhusiana na ibada ya kufunga.
  • Wapo wadhanio kwamba kufunga ni kuacha kula matokeo yake wanashinda na njaa badala ya kufunga.
  • Wengine hudhani kwamba kwa kuacha kula wanaongeza nafasi ya kupata upendeleo kwa Mungu ili awajibu maombi yao.

Lakini swali bado linabakia:
  • Nini maana ya kufunga?
  • Kwanini maombi ya kufunga husisitizwa sana katika biblia?
  • Kufunga kuna faida gani?
  • Hivi kuna mambo ambayo hatuwezi kuyapata bila kufunga?

Hayo na mengine mengi yatajibiwa katika somo hili “Kufunga na maajabu yake kiroho”

KUFUNGA HUMAANISHA NINI?

Kufunga , ni neno lililotokana na neno la limaanishalo kuacha kula chakula, eidha kwa madhumuni ya kidini au kwasababu ya ukosekanaji wa kiebrania \suÆm, chakula, au kipindi cha kufanya jambo hilo.[2]
Kufunga humaanisha kuweka kando starehe yoyote ile au shughuli ya muhimu kwa kipindi fulani ili kumtafuta Mungu kwa juhudi.

Hapa jambo la msingi tutakaloliangazia ni kufunga kwaajili ya maombi katika Biblia, suala la kufunga huonekana pote katika biblia kuanzia agano la kale hadi agano jipya.

  1. Musa alifunga siku 40 mara mbili hadi uso wake ukabadilika na kuangaza utukufu wa Bwana. (Kumbukumbu la Torati 9:9,18)
  2. Yoshua alifunga baada ya ushindi pale AI.(Yoshua 7:6)
  3. Daudi alifunga kabla ya kuteuliwa kuwa mfalme, wakati mwanae ailpougua, na kwasababu ya dhambi za watu wote (Zaburi 35:13; 69:9-10)
  4. Yehoshafati na watu wake walifunga mpaka Bwana akasema hawatapigana vita  hatimaye wakashinda vita kwa kufunga na kuomba tu (2 Mambo ya Nyakati 20:17)
  5. Danieli alifunga na kuomba mpaka Gabrieli akagizwa kumfariji na kumpatia majibu ya njozi ambayo hakuielewa. (Danieli 9:3,21-23)
  6. Yesu alifunga siku 40 na kupata nguvu ya kumshinda majaribu shetani kwa niaba ya mwanadamu na kuukomboa ulimwengu.

“Kwa Mkristo kufunga si suala la uchaguzi bali la msini.
Ushahidi wa vielelezo hivyo ni udhihirisho kwamba
    • Mungu hupendelea sana watu wamwelekeao kwa maombi wafunge ili kuwa karibu na yeye zaidi.
    • Kuna mambo ambayo wafuasi wa Mungu hawawezi kupata bila kufunga na kuomba kama vile imani. (Mathayo 17:21)
    • Mungu aliona kufunga ni jambo lisilokwepeka kwa kila mfuasi wake kiasi cha kulizungumzia sana katika biblia.
    • Hakuna ushindi wa Dhambi Bila kufunga na kuomba.

Pamoja na wengi kujua umuhimu wa kufunga na kuomba , bado utata umebakia katika namna ya kufunga na kuomba, wapo ambao kiukweli hufunga na kuomba huku wengine hushinda na njaa wakidhani kwamba wamefunga na kuomba. Ili kujua kuwa umefunga sawa na maagizo ya biblia, wapaswa kuelewa maana halisi ya kufunga.

KUFUNGA KULIKO SHAHIHI
  • Kufunga humaanisha kuweka akili na Moyo kwa Mungu na sio katika chakula. “Roho ya kufunga kwa kweli na maombi ni roho iwekayo akili na moyo kwa Mungu[3] Pia humaanisha “kufikiria sana chakula kutoka mbinguni kitakacotoa nguvu na uwezo katika uzoefu wa kidini[4]

“Mfungaji aachapo chakula, ubongo haushughuliki tena na jukumu la kumeng’enya au kufikiria chakula bali unamuelekea Mungu.”

  • Hitaji la Kiroho na vita ya kiroho , kusudi lako la kupatana na Mungu ni zito kiasi  kwamba umeamua uachane na mahitaji ya kimwili ili ujitoe katika maombi na kutafakari. (Zaburi 1:1) Hili ni kutokana na ukweli kwamba kati ya mambo yafanyayo tushindwe kumtafakari Mungu vizuri ni uroho na tama ya ya chakula (kukosa kiasi katia ulaji.)

MBINU SaHIHI ZA KUFUNGA
KAMA tulivyoona kufunga ni kuacha kula kwa madhumuni ya kidini, hii humaanisha kwamba kufunga hakuishii kuacha kula peke yake, bali ni kudhiirisha kwamba Hitaji lako kwa Mungu ni zito kuliko mahitaji uyapenadayo(mf chakula, usingizi n.k). Kwa ukweli huo, zifuatazo ni namna tofauti za kufunga:

  • Kuacha vyakula vya kusisimua (stimulants). “Kufunga kwa kweli kushauriwako kwa wote , ni kuacha kila chakula cha kusisimua, matumizi sahihi ya chakula rahisi, cha lishe ambacho Mungu ametoa kwa wingi. Watu wapaswa kufikiria kidogo kwamba ni nini watakula na kunywa katika chakula cha kupita, na wafikirie zaidi chakula kutoka Mbinguni.[5]
  • Kujinyima (kufunga) usingizi, kujinyima usingizi humaanisha hitaji la kiroho ni zito kuliko usingizi. Mara kadhaa Yesu alijinyima usingizi na kukesha katika maombi, waweza kufunga kwa kuacha kulala kwa sababu zilezile za kuacha kula. (Luka 6:12)

Yakobo katika Mto Jabok alijinyima usingizi usiku kucha akiomba hatimaye ombi lile aliloomba kwa miaka ipatayo 20 likajibiwa usiku ule.

  • Kujitenga na wale au vile uvipendavyo , kuna wakati ambapo waweza kujitenga na ndugu, familia na mazingira uyapendayo sana ili kukutana na Mungu tu. Waweza kwenda mlimani au sehemu ya upekee ili umtafakari Mungu bila muingiliano na jambo lolote. Kuna wakati Yesu alijitenga na jamii (Mathayo 14:23)
  • Kula kidogo chakula rahisi , “Sasa na kuendelea mpaka mwisho wa wakati watu wa Mungu wapaswa kuwa makini sana, wawe macho zaidi, wasitegemee hekima zao wenyewe…Watenge siku kwaajili ya kufunga na kuomba. Kuacha kula kabisa kwaweza kusihitajike, lakini wale kwa kidogo (sparingly) chjakila rahisi.[6]
  • Waweza kuacgha kula kabisa na kunywa, waweza kuacha kula tu ukanywa maji, waweza kuacha chakula ukala matunda.Kwa ujumla kufunga ni kuacha yote tuyapendayo katika dunia hii (vyakula,kazi, matamanio) kwasababu twaelekeza akili katika ulimwengu mwingine  (Mbingu).

AINA ZA KUFUNGA ZIPATIKANAZO KATIKA BIBLIA
  • Kufunga kwa kawaida(Normal Fast), huku ni kuacha vyakula vya aina zote na kunywa maji tu.
  • Kuacha kula kabisa (Absolute Fast) ,ni aina ya kufunga ambapo mfungaji huacha kula na kjunywa kabisa I Wafalme 19:7-10

  • Kufunga kidogo (Partial Fast) , huambatana na kuacha kula vyakula ambavyo wapendelea kuvitumia. Danieli na wenzake walifunga hivi kwa kunywa maji na mtama tu kwa siku kumi.Danieli 1:15. Wakati mwingine danieli alifinga hivi wiki tatu. Danieli10:3.

“Kufunga kwa aina zote tatu kunakubalika mbele za Mungu jambo la msingi ni kuelekeza akili kwa mungu pekee wakati wa mfungo”

YAPO MAMBO AMBAYO KAMWE  HATUWEZI KUFANYA BILA KUFUNGA.
  • Tiba dhidi ya baadhi ya magonjwa, “kula bila kiasi husababisha magonjwa, na asili huhitaji zaidi kupumzishwa kutoka katika mzigo mzito ambao umebebeshwa. Katika matatizo mengi ya magonjwa, tiba ya pekee ni mgonjwa kufunga mlo mmoja au miwili. [7]  
“Wapo wawezao kunufaika zaidi kwa kuacha kula siku moja au mbili kila wiki kuliko …ushauri wa kitabibu. Kufunga siku moja ya wiki kwaweza kuwa ni faida isiyokifani kwao.”[8]   
  • Kuishinda dhambi, “Yesu aliingia katika jaribu juu ya suala la tama ya chakula, na karibia wiki sita alishinda jaribu kwa niaba ya mwanadam. Kule kufunga kurefu katika nyika ni fundisho wakati wote kwa mwanadam aliyeanguka dhambini…Alitoa fundisho mkwa mwanadam kwamba ataanza kazi ya kushinda pale anguko lilipoanzia, katika suala la tama ya chakula.[9]
  • Kuelewa maandiko. “Kuna baadhi ya maandiko na mambo ambayo ni magumu kuelewa…Muda utafika chini ya upaji wa Mungu kwa dunia kujaribiwa kwa ukweli wa wakati huo, akili zitafanyiwa mazoezi kwa Roho Yake ya kuchunguza maandiko hata kwa kufunga na kuomba …kila ukweli unaohitajika haraka kwa wokovu utawekwa wazi kiasi kwamba hakuna atakayehitaji kukosea...[10]
  • Kupata majibu kwa maombi, kuomba pekee hakutoshi kupata majibu kwa mahitaji yote bali baadhi ya mambo hujibiwa kwa njia ya kufunga na kuomba. “Kwa baadhi ya mabo , kufunga na kuomba hushauriwa na ni sahihi.Katika mkono wa Mungu ni njia ya kusafisha moyo na kuhamasisha…mfumo wa akili. Tunapokea majibu kwa maombi yetu kwasababu tumenyenyekeza mioyo yetu kwa Mungu”[11]
  • Maombi ya kufunga pekee yaweza kuwaokoa waliotekwa katika umizimu, “baadhi ya roho zilizoshangazwa na maneno ya kuvutia kutoka kwa walimu wa umizimu, na kufuata msukumo wake, baada ya hapo wakatambua tabia yake ya mauaji, wataacha na kuukimbia, lakini hawataweza.Shetani kawashikilia kwa nguvu zake, na hayuko tayari kuwaachia huru…shetani atawaimarisha malaika wake waovu ambao wamewaendesha watu hawa, lakini kama watakatifu wa Mungu wakifunga na kuomba kwa moyo wa dhati maombi yao yatashinda.Yesu atatuma malaika watakatifu kumpinga shetani...[12]
  • Kutambua mapenzi ya Mungu katika mipango yetu, “kuna nyakati ambapo mkristo anahitaji umakini wa mawazo na uamuzi madhubuti, aweza kuwa na maamuzi muhimu ya kufanya, au anahitaji kutambua zaidi mapenzi ya Mungu. Katika mazingira hayo kufuka kutathibitisha mbaraka mkubwa.kufunga huko kwaweza kusiwe kuacha chakula kabisa, lakini mlo uloandaliwa na virutubisho rahisi kwaajili ya kuendeleza afya na nguvu… (Dan 10:3, Matt. 6:16.)[13]

MAMBO YA KUZINGATIA KUHUSU KUFUNGA
  • Hatupaswi kufunga kwa kujionyesha kwa watu, “kama mtu anafunga ni suala lake binafsi. Kwakweli, msingi wa kufunga ni utambuzi wa hitaji binafsi wa kufanya hivyo.Fundisho la Yesu ni kwamba kufunga kunapaswa kuwa uzoefu binafsi unaofanywa kwasababu ya utambuzi wa hitaji, na sio…kujipatia sifa ya umahiri…”[14] Kufunga ni njia ya kumtafuta mungu na kusogezwa karibu naye
  • Hatupaswi kufunga kama desturi, wapo wanaofunga ili kutimiza wajibu au kutekeleza tu ratiba Fulani na sio kutokana na hitaji, msukumo wa kiroho uletwao na shauku ya kutaka kuwa karibu zaidi na Mungu. Usifunge kwa kufuata tu ratiba iliyopangwa ,huko ni kushinda na njaa, hata kama kuna ratiba sharti uwe na shauku na msukumo wa dhati kufanya hivyo. Kufunga si tendo la neema kwa lenyewe tu, bali lifanywapo katika moyo wa upendo, hitaji na kujitoa huwa mbaraka.
  • Usichukulie kufunga kama kitendo cha kupata upendeleo kutoka kwa Mungu, wengine hudhani akifunga Mungu atasikiliza ombi kwa makini zaidi wanasahau kwamba sikio la mungu liko wazi siku zote.
  •  Kufunga ni kwaajili ya kubadilisha hali zetu na kutubadili sisi, sio kumbadilisha Mungu. (Isaya 58:1-9).
  • Kufunga si mbadala wa utii, wana wa Israeli walizingatia sana kufunga wakapuuzia majukumu yao kiroho na kimwili wakidhani kwamba kufunga kungemfanya Mungu apuuzie Dhambi zao walizoendelea kuzitenda.(Isaya 58:1-11) Mungu aliwadhihirishia kuwa pamoja na kufunga pia huzingatia utii na kujitoa.


“Maombi ya kufunga ni silaha pekee kwa kila mkristo  kwa maana Ukristo ni kuenenda kwa Imani sio kwa kuona tu, na pasipo Imani haiwezekani kumpendeza mungu, na Imani ya kushinda vita ya kiroho hupatikana kwa kufunga pekee.”



[1] Ellen G White.(1898) Tumaini la Vizazi Vyote,uk 117,118.

[2] Horn, Siegfried H., Seventh-day Adventist Bible Dictionary, (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Association) 1979.
[3] Ellen G White(1938) . Counsels on Diet and Foods
[4] Ellen G White (1932). Medical Ministry
[5] Ellen G White(1932) . Medical Ministry,pg 283
[6] Ellen G White (1904) Review and Herald.
[7] Ellen G White (1905) Ministry of Healing.pg 134
[8] Ellen G White (1902) Testimornies for the Church.vol7.pg 134
[9] Ellen G White(1938) . Counsels on Diet and Foods.pg 186
[10] Ellen G White (1870) Testimornies for the Church.vol 2.pg 692
[11] Ellen G White(1938) . Counsels on Diet and Foods. pg 187
[12] Ellen G White (1855-1868) Testimonies For The Church. vol 1, pg
[13]Nichol, Francis D., The Seventh-day Adventist Bible Commentary, (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Association) 1978.
[14]Nichol, Francis D., The Seventh-day Adventist Bible Commentary, (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Association) 1978.