Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16


MAMBO SABA AMBAYO NI LAZIMA TUFANYE ILI KUMWAGIWA MVUA YA MASIKA

IMEKUSANYWA NA KUFASIRIWA PETRO TUMAIN

Kuna mambo saba ambayo hayakwepeki kwa mtu yeyote anayetarajia kumwagiwa mvua ya Masika. Masharti haya yako saba, hii inamaana kwamba ni lazima msafiri wa kwenda mbinguni awe nayo yote au akose yote.

1)                     Watu waliopata nuru (Enlightened)

2)                     Watu walioshinda.(Victory Over Sin)

3)                     Watu wenye upendo.

4)                     Watu wa maombi.

4)                    Watu wafanyao kazi.

6)                     Watu wenye kiasi.

7)                     Watu watunzao sabato

Ni muhimu tuzingatie haya haya masharti saba kwa maombi . hapa mni mkusanyiko wa nukuu za kalamu ya uvuvio zenye kudhihirisha uhalisia wa maswala yaliyoorodheshwa hapo juu.

 

 

 

 

 

 

1.                      WATU WALIOPATA NURU.

Kabla ya kusoma ifahamike kwamba , swala la kupata nuru ni SHARTI LA KUWA MWANAFUNZI MAKINI SANA WA MAANDIKO HUSUSANI VITABU VYA UNABII (DANIELI NA UFUNUO)

“Kumwagwa kwa Roho wa Mungu ambaye huiangaza dunia kwa nuru yake, hakuwezi  kuja mpaka tuwe na watu walioelimika na kupata nuru”

 

 

“Sisi , pamoja na faida zetu za kidini,twapaswa kujua zaidi leo kuliko tujuavyo.” TM 116.

“Pale vitabu vya Danieli na ufunuo vitakaeleweka vizuri, waumini watakuwa na uzoefu tofauti kabisa wa  kidini” TM114

“Pale kama ninadu tutakapoelewa kitabu hiki (Kitabu cha Ufunuo)kinamaana gani kwetu,kutaonekana kati yetu uasho mkuu.” TM 113

“wale ambao wanaula mwili na  na kunywa damu ya Yesu watatoa katika vitabu vya  Danieli na Ufunuo ukweli ambao umevuviwa na Roho Mtakatifu .Wataanza katika nguvu kazi ambazo haziwezi kuzuiliwa.” TM 116

 

2.                      WATU WASHINDI (WASHINDI WA DHAMBI)

Jambo la msingi kujua tofauti na dhana potofu iliyosambaa, kila mtu atakaemwagiwa mvua ya masika ni LAZIMA MVUA YA VULI IWE IMEMWEZESHA KUSHINDA KILA AINA YA DHAMBI MAISHANI MWAKE. Ili kuelewa vyema somo la kushinda dhambi fuatilia somo la SAYANSI YA KUSHINDA DHAMBI SHE YA 1 -4 , IMANI RAHISI INAPATIKANA HIVI, USIANZE SAFARI YA KUSHINDA DHAMBI KABLA YA KUELEWA HILI…n.k…Katika YOUTUBE ACOUNT YA PETRO TUMAINI TV. Pia waweza kupata series ya vitabu vya haki kwa Imani kwa kuwasiliana na namba 0754202021. Ifahamike kwamba hakuna kitu tunachohitaji sana sasa kama ushindi dhidi ya dhambi.

Ni wale Waadndventista wa Sabato tu waishio leo ambao (1)watapokea kwa moyo wote ushuhuda ulionyooka-kuzingatia ushuhuda wa Shahidi wa Kweli (Yesu) uliopo katika Ufunuo 3:14-22 (2) wapokeao wingi wa mvua ya vuli, na (3)kushinda kila dhambi inayowakabili (besetting sin) na kuakisi kikamilifu sura ya Kristo,watapokea mvua ya Masika.

 

 

“Ujumbe wa malaika wa tatu umefungamanishwa (swelling)  katika kilio kiluu, na haupaswi kujisikia huru kupuuzia jukumu la sasa,na kuendelea kukaribisha wazo kwamba wakati flani huko baadae utakuwa mpokeaji wa mbaraka mkuu, ni wakati gani ambapo bila juhdi yoyote kwa upande wako uamsho wa ajabu utatokea... Leo wapaswa kuwa na chombo chako kimetakaswa tayari kwa kupokea manyunyu ya mvua ya masika, kwa kuwa mvua ya masika itakuja, ma mibaraka ya Mungu itajaza kila Roho ambayo imetakaswa kutoka katika kila uchafu. Ni kazi yetu leo kujitoa roho zetu kwa Yesu, ili kwamba tuweze kunufaika wakati wa kuburudishwa kwa uwepo wa Bwana- tayari kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu.” RH March 22, 1892;Ilinukuliwa katika 1 SM 190,191

“Wale ambao (1) huinula katika kila jaribu na (2) hushinda kila jaribu na (3) kushinda, iwe kwa gharama yoyote, wamesikia ushaur wa shahidi wa kweli na watapokea  mvua ya masika na hivyo kufanywa wafae kwa kunadilishwa  (translation)” 1T 187 (msisitizo umeongezwa)

 

 

Ushuhuda ulionyooka ni nini (Straight Testimony) ? Ushuhuda wa shaihidi wa kweli ni nini?

1)                     “kuinuka katika kila jaribu”(Come up to every point)

2)                     “kushinnda kila jaribu”

3)                     Na  “kushinda (kila dhambi), iwe kwa gharama yoyote.”

 

 

 

Hii si jumla ya “Ushuhuda ulionyooka” na “ushauri wa shahidi mwaminifu.” Pia kuna dhahabu (Imani na Upendo), vazi jeupe (Vazi la tabia ya haki ya Kristo) na dawa ya macho (utambuzi wa Kiroho wa Roho Mtakatifu). Ushuhuda ulionyooka huitaja dhambi kwa jina lake na huwapa mwito watu wa Mungu  kutubu na kuacha dhambi zote. Kufikia juu ya kiwango.

 

3.                      WATU WENYE UPENDO- UPENDO WA NDUGU-UMOJA-MPATANO-KITU KIMOJA

“Roho hawezi kumwagwa wakati utofauti na chuki dhidi ya mmoja na mwingine vinaendekezwa na washiriki wa kanisa. Kinyongo,Wivu, majungu/ maneno maovu (evil-surmising), ni ya shetani na kwa kweli yanazuia njia ya utendaji kazi wa Roho Mtakatifu.” 6T 42

“ Hebu Wakristo waweke kando tofauti zote, wajitoe kwa Bwana kwaajili ya kuwaokoa waliopotea. Hebu waombe kwa imani ahadi ya ya mbaraka ulioahidiwa, nao utakuja. Kumwagwa kwa Roho siku za mitume iliuwa ni ‘Mvua ya Vuli,’na utukufu ilikuwa ni matokeo.Lakini mvua ya masika itakuwa nyingi zaidi” 8T . 21

MUNGU ANATUPIMA UPENDO WETU KWAKE KWA NAMNA TUNAVYO TENDEANA MMOJA NA MWINGINE

“Pale mvua ya masika itakapomwagwa, kanisa litavikwa uwezo kwa kazi yake; lakini kaniza kama lilivyo kwa ujumla kamwe halitapokea mvua hii mpaka waumini wake waweke kando wivu, majungu/mazungumzo mavu (evil summisings). Wale wanaoendekeza dhambi hizi hawajui uzoefu wa mbaraka wa upendo.; hawajaamka katika ukweli kwamba Bwana  anaujaribu na kuuthibitisha upendo wao kwaajili yake kwa mtazamo wauonyeshao kila mmoja kwa mwenzake ,Yesu atwambia , ‘Amri mpya...pendaneni.’ Amri hii inapoheshimiwa, wivu , mawzo maovu,na mawazo maovu hayataendekezwa; havitakuwa na nafasi katika kuitengeneza tabia.” (RH Oct 6, 1986.) Msisitizo umeongezwa

 

4.                      WATU WA MAOMBI

“Lakini ni lazima Mungu aamuru mvua inyeshe. Kwahiyo hatupaswi kuwa wazembe katika kuomba.” TM 590. Msisitizo umeongezwa

“Hebu sote kwa mioyo mikunjufu, tuombe kwa juhudi kwamba sasa, katika wakati wa mvua ya masika , manyunyu ya neema yaanguke juu yetu.” TM 590.

Twapaswa kuomba kwa juhudi kwaajili yakushuka kwa Roho Mtakatifu kama wanafunzi walivyoomba katika siku ya Pentekoste. Kama walimuhitaji katika wakati ule, tunamhitaji zaidi leo... Bila msaada wa Roho , juhudi zetu kufikisha ukweli mtakatifu zitakuwa ni bure.” R Aug.25,1896. Msisitizo umeongezwa

 

5.                      WATU WAFANYAO KAZI

Ni vyema na hili niliweke bayana kabla ya kutazama kile asemacho nabii wa Mungu, swala kuu linalozungumziwa hapa NI KUFANYA KAZI YA MUNGU KATIKA NA MNA SAHIHI. HII INAMAANA WATU WASIOJIHUSISHA NA UMISHENARI HAWATAMWAGIWA MVUA YA MASIKA.

Mvua ya masika kamwe haiwezi kumwagwa kwa Wakristo wavivu, wasiofanya kazi. Kwavile Mvua ya Masika hutolewa kwa madhumuni ya ushuhudiaji, itamwagwa kwa wale tu ambao wanaingia kikamilifu katika kazi ya Mungu kwa ubora wa uwezo wao.

“Makanisa yanapokuwa hai, makanisa yafanyayo kazi, Roho Mtakatifu atatolewa kama jibu kwa maombi yao ya dhati. Kisha ukweli  wa neno la Mungu utazingatiwa kwa shauku mpya...Kisha watasihi pamoja na roho za wengine na hawataweza kuziliwa. Kisha madirisba ya mbinguni yatafunguliwa kwa manyunyu ya mvua ya masika.” RH Feb.25,1890 Msisitizo umeongezwa

 

“Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu kukuu, ambako kutaiangaza dunia yote kwa utukufu wake, hakutatokea mpaka tuwe na watu walioangazwa, kwamba kujua kwa uzoefu wa kimatendo inamaana gani kuwa watendakazi na Mungu. Kwa ujumla tutakapokuwa, tumejitoa kwa moyo wote katika huduma ya Kristo,   Mungu atatambua ukweli huu kwa kumwaga Roho wake bila kipimo; lakini hili haliwezi kutokea wakati sehemu kubwa ya kanisa si watendakazi pamoja na Mungu” CS 253;Ev 699 Msisitizo umeongezwa

 

“Wakati uendekezaji (reproach) wa uvivu (indolence) na uzembe (sloghtfulness) vitakapo ondolewa mbali na kanisa, Roho wa Mungu atadhihirishwa kwa utukufu. Nguvu za Mungu zitafunuliwa. Kanisa litaona msaada wa utendaji kazi wa Bwana wa Majeshi. Nuru ya kweli itaangaza kwa uwazi, miale imara, na kama ilivyokuwa wakati wa mitume, roho nyingi zitageuka toka kwenye uwongo kwenda kwenye ukweli.Dunia itaangazwa na utukufu wa Mungu.” 9T 46. Msisitizo umeongezwa

 

 

 

KAZI YA UMISHENARI HUAMSHA ROHO NA KUMLETA ZAIDI ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA

“Sheria ya kujitumikia ni sheria ya kujiangamiza. Sheria ya kujitoa dhabihu ni sheria ya kujitunza.”DA 623,624

Uwezo wa kupokea hutunzwa tu kwa kutoa (Imparting). Hatuwezi kuendelea kupokea hazina ya Mbinguni bila kuiwasilisha kwa wale wanaotuzunguka” COL 143

“Roho inayokataa kufundisha (imparting) itapotea. “ DA 417 Msisitizo umeongezwa

 

“Msaada wa pekee ambao wachungaji waweza kuutoa kwa washiriki wa makanisa yetu si kuhubiri,lakini ni kuwapangia kazi. Mpatie kila mmoja kitu cha kufanya kwaajili ya wengine...Kama wakiwekwa kazini,punde wanyonge watasahau unyonge wao (despondency), wadhaifu watakuwa na nguvu, wajinga watakuwa na akili, na wote wataandaliwa kuufikisha ukweli kama ulivyo kwa Yesu.” 9T 82.

“Tulijazwa Roho Mtakatifu kwa kadri tulivyoenda na kuihubiri sabato kwa uwazi.” EW 85

Ni kanuni ya jumla (universal principle) kwamba kila mara mtu anapokataa kutumia  nguvu alizopewa na Mungu, ngvu huoza na kupotea. Ukweli usiotendewa kazi maishani, ambao haufundishwi, hupoteza nguvu yake yenye kutoa uhai maishani.” AA 206 Msisitizo umeongezwa

 

 

HAKUNA KITU KIITWACHO WAKRISTO WASIO HAI. KAMA MTU SI HAI SI MKRISTO. BALI NI ALIYERUDI NYUMA, HALI YA UPOTEVU!

“Hebu wachungaji wafundishe washiriki wa kanisa kwamba ili wakue kiroho, ni lazima wabebe mzigo ambao Bwana ameuweka juu yao,-mzigo wa kuziongoza Roho kwenye ukweli.” GW 200;CS 69,70 Msisitizo umeongezwa

 

“Wale watakaokuwa washindi ni lazima wavutwe kutoka katika nafsi zao na kitu pekee kitakachofanya kazi hii kuu ni kuwa na shauku sana ya wokovu wa wengine.” MH 90.

“Nguvu yako Kiroho na mibaraka vitawiana na kazi ya upendo na kazi nzuri unazofanya.” 3T 526

“Mungu hawezi kutupatia uwezo tusionao kwa miujiza, lakini wakati tukitumia uwezo tulionao, tafanya kazi nasi kuongeza na kuimarisha kila uwezo; nguvu zetu zilizolala zitaamshwa, nguvu ambazo kwa muda mrefu zilizimwa (Palsied) zitapewa maisha mapya.” 5T 459

“Nilionyeshwa watu wa Mungu wakisuburi badiliko fulani liweze kuwatokea. Lakini watahuzunishwa kwasababu wamekosea. Lazima wafanye kitu. Lazima wafanye kazi wenyewe. 1T 261. Msisitizo umeongezwa

 

 

 

 

 

Hatuwezi kukutana na Uumgu bila kukutana na Ubinadamu.. ("We can not come in touch with Divinity without coming in touch with humanity") . COL 384

 

 

 

 

 

Maana ya maneno hayo ni kwamba hatuwezi kukutana na na Mungu isispokuwa tuwe tayari kukutana na ubinadamu katika huduma ya UPENDO na matendo ya huruma. Kimsingi huduma hiyo ni sehemu ya utakaso pia, ni huduma inayopaswa kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila Siku "SI KAMA TUNAVYOITEKELEZA KIPROGRAM" Wengi huduma hii kwetu sio sehemu ya maisha ila tunafanya kama tu program ya kanisa, nah ii ni hatari sana. Ni lazima huduma ya kuleta unafuu kwa binadamu wenzetu iwe sehemu ya maisha yetu SI MATUKIO YA TAREHE MAALUMU ZA PROGRAM ZA KIKANISA AMBAZO TUNATAKA KUTANGAZWA NA VYOMBO VYA HABARI.

 

 

 

 

NYONGEZA

UHUSIANO -> ROHO MTAKATIFU -> KUVIKWA UTAKATIFU NA BADILIKO LA TABIA -> KUKAMILISHWA

 

KUKAMILISHWA TABIA HUKUA KUTOKA KATIKA MAHUSIANO YA KUSHIRIKI, KUSHUHUDIA NA HUDUMA YA KIKRISTO.

 

 

 

HUDUMA

 Kufanana na Mungu kitabia , umoja nae katika utakatifu , huruma pamoja nae katika upendo, shauku pamoja nae katika ukweli, na shaku ya Mungu kwaajili ya wokovu wa roho, hauji katika moyo kwa kukaa nyumbani na kuomba na kusoma biblia zetu na kuimba ya mbinguni. Hapana, haya yote ni ya muhimu na yana msaada, lakini hayatoshelezi kwa yenyewe. Kitu zaidi kinahitajika.

 

 

Kwa nyongeza pamoja na yaliyoorodheshwa hapo juu ambayo ni ya lazima,  kile ambacho ni muhimu kutuleta katika upatano na Mungu ni kushuhudia -Christian Service.

“Sheria ya kujitumikia ni sheria ya kujiangamiza. Sheria ya kujitoa dhabihu ni sheria ya kujitunza.” DA 623,624 Msisitizo umeongezwa.

“Roho ikataayo kufundisha itapotea.” DA 417 Msisitizo umeongezwa.

Nguvu za kiroho zitazidi kuwa dhaifu na kufa kama hazifanyiwi mazoezi katika uongoaji roho kwa Yesu.” 9T 106

UMISHENARI NDIYO FURSA YA KUTEMBEA NA YESU

“Wale wanaopuuzia fursa ya kutembea na Yesu katika huduma , hukataa mafunzo pekee  ambayo huleta kufaa kwa kushirikiana nae katika utukufu.” ED 264. Msisitizo umeongezwa

“Ni kanuni ya jumla (universal PRINCIPLE) kwamba kila mara mtu anapokataa kutumia  nguvu alizopewa na Mungu, nguvu huoza na kupotea. Ukweli usiotendewa kazi maishani, ambao haufundishwi, hupoteza nguvu yake yenye kutoa uhai maishani.” AA 206 Msisitizo umeongezwa

“Wakati ambapo hakuna utendaji kazi hai kwaajili ya wengine, upendo hupoa, na umani hufifia.” DA 825

“Hatuwezi kuokolewa kwa kukaa kizembe na bila kazi. Hakuna kitu kama mtu aliyeongoka kiukweli na kuishi maisha yasiyo na msaada. Haiwezekani kwetu kuangukia (drift) mbinguni.” COL 282

 

 

 

 

MAAMUZI YA UTEKELEZAJI HAYAKWEPEKI NA NI MUHIMU

“Nilionyeshwa watu wa Mungu wakisuburi badiliko fulani liweze kuwatokea.Lakini watahuzunishwa kwasababu wamekosea. Lazima wafanye kitu. Lazima wafanye kazi wenyewe. 1T 261. Msisitizo umeongezwa

TIBA (CURE).

“Ipo lakini tiba moja tu ya uhakika kwa uvivu wa kiroho, na hiyo ni, fanya kazi, fanya kazi kwa roho zinazohitaji msaada wako.” 4T 236,CS 106,107. Msisitizo umeongezwa

 

DAWA

“Hii ni dawa ambayo Kristo ameiandika kwaajili ya mwenye moyo-unaozimia, mashaka, roho inayotetemeka. Hebu wenye huzuni , watembeao kwa maombolezo mbele za Bwana, waamke na kumsidia mtu anayehitaji msaada.” 6T 266 Msisitizo umeongezwa

 

MANENO MATATU YA KUTAZAMWA NA MKRISTO

“Yapo maneno matatu ya kutazamwa katika maisha ya mkristo , ambayo ni lazima yazingatiwe kama hatutaki shetani kuiba ushindi (match) kati yetu,yaitwayo, kuwa macho, omba, kazi.” 2T 283 Msisitizo umeongezwa

 

 

DAWA

“Kwa waliokata tamaa ipo dawa moja ya uhakika-Imani, maombi, kazi.”PK 164,165 Msisitizo umeongezwa

“Kubeba msalaba hukata ubinafsi kutoka katika Roho.” 5BC 1090

 

 

NAFASI YETU

“Tukiwa waaminifu katika kufanya sehemu yetu, katika kushirikiana nae, Mungu atafanya kazi kupitia sisi kutekeleza starehe njema ya mapenzi yake. Lakini Mungu hawezi kufanya kazi kupitia sisi kama hatufanyi juhudi yoyote. Kama tunapata uzima wa milele, ni lazima tufanye lazi, na tufanye kazi kwa juhudi...Tabia tuziundazo hapa zitaamua mwisho wetu wa milele. Sehemu yetu ni kuondolea dhambi mbali, tutafute kwa kunuia ukamilifu wa tabia. Kwa kadri tufanyavyo hivyo, Mungu hushirikiana nasi kutufanya tufae kwaajili ya nafasi katika ufalme wake...

Kuyafanya mapenzi ya Mungu ni muhimu kama tutakuwa na  maarifa yanayoongezeka kumhusu yeye. Hebu tusidanganywe na na dhana zitajwazo mara kwa mara,  ‘chote upaswacho kufanya ni kuamini.’ Imani na matendo ni makasia mawili (oars) ambayo ni lazima tuyatumie kwa usawa kama tunasukuma njia yetu kupanda mkondo wa maji dhidi ya wimbi la kutokuamini. ‘Imani, kama haina matendo,imekufa, kwa yenyewe.’ Mkristo ni mtu wa kufikiri na kutenda. Imani yake ikiwa imekita mizizi kwa Kristo. Kwa imani na matendo mema hutunza hali yake ya kiroho kuwa imara na yenye afya,na nguvu  zake kiroho huongezeka kadri anavyokazana kufanya kazi za Mungu.” RH June 11,1901. Msisitizo umeongezwa

NJIA PEKEE YA KUKUA KATIKA NEEMA

Njia pekee ya kukua katika neema ni kufanya kwa shauku kazi ambayo Kristo alituagiza, kuifanya kwa kiwango cha uwezo wetu, katika kusaidia na kubariki wale wanaohitaji msaada tuwezao kuwapa.” SC 86. Msisitizo umeongezwa

“Wale ambao watapata zaidi uzoefu wa utakaso wa kweli katika roho zao, wapaswa kufiksha kweli kwa wale ambao ni wajinga wa huo. Kamwe hawawezi kuwa na kazi kubwabzaidi yenye kuinua,na kuimarisha.

 

 

Those who would experience more of the sanctification of the truth in their own souls, should present the truth to those who are ignorant of it. Never will they find a more elevating, ennobling work. . . .  {5MR 346.1}

Wale ambao watapata Zaidi uzoefu wa utakaso wa ile kweli katika roho zao, watapaswa kuuwasilisha ukweli kwa wale ambao ni wajinga wa huo. Kamwe hawatapata kazi ya kukweza, na uwezo….{5MR 346.1}

 “Nguvu yako Kiroho na mibaraka vitawiana na kazi  ya upendo na kazi nzuri unazofanya.” 3T 526....

Nguvu ya kushinda dhambi hupatikana vizuri kwa kuwa na shauku katika huduma. (Strength to resist evil is best gained by aggressive service.)--The Acts of the Apostles, p. 105.  {ChS 100.5}  Msisitizo umeongezwa

 

Tunakuwa washindi kwa kuwasaidia wengine kushinda.”7BC 974

Hakuna kitakachokupa mifupa, na misuli katika  wito wako kama kutumika kuendeleza kazi ambayo unadai kuipenda. “Northing will give bone and sinew to your piety like working to advance the cause you profess to Love.” 4T 236. Msisitizo umeongezwa

 

“Mungu Angefikia dhumuni katika kuokoa wadhambi bila msaada wetu, lakini ili kukuza tabia kama ya Kristo kazima tushiriki katika kazi yake.”DA 142

“Nilionyeshwa watu wa Mungu wakisuburi badiliko fulani liweze kuwatokea.Lakini watahuzunishwa kwasababu wamekosea. Lazima wafanye kitu. Lazima wafanye kazi wenyewe. 1T 261. Msisitizo umeongezwa.

 

Roho ya unabii pia huelezea kwamba hatuwezi kukutana na Uungu kama hatuwezi kugusana na binadamu.

Yule akataae kufundisha atapotea.Hakuna kitu  kiitwacho mkristo mzembe asiye hai.

 

 

6.                      WATU WENYE KIASI

Kwamba Mungu anajihusisha na afya yetu na furaha  hapa duniani vilevile na ukuaji WA Tania yetu na hatima ya milele, no ukweli WA kuvutia.  Kiasi inamaanisha kutotumia kabisa kilichokatazwa, na kutumia kwa wastani kilichoruhusiwa. Hapa ndipo huja umuhimu wa somo la matengenezo ya afya kama linavyofundishwa na Biblia na Roho ya unabii, kwa wengi limechukuliwa kama somo lisilo na uzito LAKINI HAPA UTAGUNDUA LINA ATHARI KATIKA UMILELE WETU.

 

Ujumbe wa afya ni zawadi ya pekee sana kwa kanisa la masalio . Utoaji wa ujumbe huu ni mojawapo ya mambo makubwa sana ambayo Bwana amefanya kwaajili yetu. Kwakweli ni kipaumbele cha pekee kuwa na maelekezo ambayo Mungu amefunua kwetu kuhusu uhusiano kati ya mtindo wa kiafya na ukuaji wa tabia.

3 Yohana 1:2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

 

 

 

Kadri utakavyosoma nukuu hizi, nikusihi usome sana kitabu cha MINISTRY OF HEALING, COUNSELS ON DIET AND FOODS kwa upande wa Kiswahili pitia KUTAYARISHA NJIA SEHEMU YA KWANZA SURA TATU ZA MWISHO.

Ni kupitia usomaji wa nukuu zifuatazo BWANA ALINIWEZESHA KUPATA NGUVU YA KUFANYA MATENGENEZO YA AFYA NA KUACHA UTUMIAJI WA NYAMA. NINAAMINI ROHO WA KRISTO HATAKUACHA VILE VILE UMALIZAPO KUSOMA NUKUU HIZI

Hebu daima tukumbuke Kwamba " Ilikuwa no kwa upendo Baba yetu wa mbinguni Alituma nuru ya matengenezo ya afya ili kutulinda dhidi ya maovu yanayotokana na kuendekeza uchu wa chakula usio dhibitiwa. " (CDF 243) Msisitizo umeongezwa.

"Dhumuni lake no kupata maendeleo makuu ya mwili, akili na roho." (CDF 457)

"...kuutibu mwili kuna kila kitu kinachoshughulika na nguvu na usafi wa akili na moyo."  7BC 909

Kama ujumbe huu umetolewa kwetu kupitia mafunuo, je hatupaswi kuuzingatia sana kuliko sasa?

Wengi wa Waadventista wa sabato wanakufa kila Siku kutokana na kukosa maarifa ya kuishi kwa afya, wengi wanachimba makaburi yao kwa midomo yao,  wanajinyonga kwa mpango wa awamu - kwa mienendo isiyo sahihi ya kula na kunywa. Wengi zaidi wanaenda kinyume na mapenzi ya Mungu, na badala ya kukamilishwa Tabia zifanane na Kristo , wanazidi kunajisika na kudhoofika na kujimaliza kwasababu hawasomi Roho ya unabii.

Kiasi na kuishi maisha ya kuzingatia kanuni za afya ni mambo ya muhimu sana kwasababu mienendo sahihi ya kiafya husaidia katika kukuza tabia ya Kristo ndani yetu wakati mitindo mibaya ya afya hupambana dhidi ya kukuza Tabia ya Kristo.

"Wale wanaougua katika mwili kwa ni karibu mara zote huumwa katika roho , na roho inapougua na mwili hufanywa uugue pia." MS 62, 1900 Msisitizo umeongezwa.

Tunajua kuna muuunganiko na uhusiano usioweza kutenganishwa kati ya mienendo ya kuafya na ukuaji wa Mkristo. Haiwezekani kwa mtu asiye na kiasi kukuza Tabia ya Kristo , kipengele hiki kuhusu afya kimebeba kauli za muhimu kuhusu afya ambazo Waadventista wa Sabato wengi hawajui kwamba zipo katia roho ya unabii.

 

 

Kwasababu ujumbe WA afya na Tabia vinahusiana moja kwa Moja na kutegemeana, ni athari gani kimoja huwa nazo kwa kingine. Kila Mwadventista wa Sabato aliyesoma vizuri anajua kuna kanuni nane za afya.

"(1) Hewa safi, (2) mwamga wa jua, (3) Kujizuia (4) Pumziko (5) Mazoezi, (6) Mlo sahihi (7) Matumizi ya maji (8) Kutumaini katika nguvu za Mungu, hizi ni Tina asili (Natural Remedies)." (MH 127) Msisitizo umeongezwa.

Hapa nitaielezea moja tu kwasababu imepuuziwa sana na Waadventista wa Sabato - ile ihusuyo kula- hususani- kula vyakula vya nyama.Wale wanaokula hivyo hawatambui umuhimu wa kula na kunywa kwa utukufu wa Mungu. (1 Kor 10:21)

 

Waadventista wa Sabato hawaachi kula nyama hususani kutokana na msimamo wa kiafya- vilevile kwasababu mtu anajiingiza katika hatari ya kula nyama zenye magonjwa , na vile vile kwasababu sio chanzo bora cha protini, bali ni kwasababu ulaji wa nyama hufanya iwe vigumu kukuza tabia ya kufanana na Kristo.

Vyakula vya nyama hufanya iwe vigumu kuwa mvumilivu na mwema, mwenye upendo na afananae na Kristo. Waadventista WA Sabato hawatambui mwamba ulaji WA nyama una msukumo ule ule katika mielekeo ya kitabia (disposition) ya mwanadamu kama ilivyo ya mnyama - kuwafanya wasiwe wavumilivu, wenye hasira za haraka (irritable), wagomvi (cantankerous) , waovu (vicious). Hili limethibitishwa kisayansi tena na tena.

 

"Wapo wachache wanaoelewa wapaswavyo kuelewa ni kwa vipi mienendo yao kiafya ya ulaji inahusiana na afya yao, Tabia, na kutumika kwao katika dunia hii, na matokeo yao ya milele." PP 599

 

Ulaji wa vyakula vya nyama (1) huwanyang'anya watu upendo na huruma, (2) hufanya asili iwe ya kinyama , (3) huweka sumu katika mfumo wadamu, (4) huwasha hisia Kali za mapenzi , (5) huharibu huruma na kupendana (6) hudhibiti utambuzi na hamasa za kiroho, (7) humfanya mtu awe so mvumilivu na mwenye ugonjwa WA hasira (ill-tempered) , na (8) hupotosha hamu ya chakula.

"Kwa kutumia vyakula vya nyama (1) asili ya kinyama huimarishwa na (2) asili ya kiroho hudhoofishwa…" CDF 383. Msisitizo umeongezwa.

 

Nimepewa maelekezo kwamba chakula cha nyama kinatabia ya kufanya asili iwe ya kinyama (animalize the nature) , kuwanyang'anya wanaume na wanawake ule upendo na huruma ambavyo wanapaswa kuhisi kwa kila mmoja, na kufanya tamaa za chini kuendesha nguvu za juu za utu. Kama ulaji wa nyama ungekuwa ni afya, si salama sasa. Saratani, uvimbe , na magonjwa ya mapafu kwa sehemu kubwa husababishwa na ulaji WA nyama." 9T 159 Msisitizo umeongezwa.

He hii yaweza kuwa sababu no kwanini hakuna tena upendo  katika Makanisa ya Wadventista wa Sabato? Je hili laweza kuelezea no kwanini baadhi ya Waadventista wa Sabato wameacha kukua Kiroho- miaka 10, 20, 30 imepita - na bado no baridi wasioelewa, wenye kiburi na tamaa, na pia wagomvi?Je, hili laweza kuelezea no kwanini wengi bado no watoto katika Kristo, wana akili za kidunia, wenye tamaa ya vitu na wasioridhika ? Je hili laweza kutupa sababu ni kwanini baadhi ya makanisa huundwa na washiriki vuguvugu, wasioelewa na hata washiriki wenye uadui? Je Mungu anaweza akawa akiendelea kuzuia mvua ya masika kwa Manisa kutokana na sababu hii? Ni nini kilitokea kwa wana WA Israeli waliotamani mabakuli ya nyama za Misri?

1 Wakorintho 9:25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.

"Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipinganazo na roho." (1 Petrol 2:11)

"Afya... yapaswa kulindwa kwa utakatifu kama Tabia." CT 294

"Mwili ni mfumo pekee ambao kupitia huo akili na roho hukuzwa kwa kuijenga Tabia juu." MH 130

“Ubongo ni makao makuu ya mwili . Kama nguvu za utambuzi zikidhoofishwa kupitia kukosa kiasi kwa aina yoyote, mambo ya umilele hayawezi kutambuliwa." Ukombozi au Kujaribiwa kwa Kristo katika Jangwa, uk . 56. (Redemption or The Temptation of Christ in the Wilderness, p. 56)

“Ubongo huharibiwa kutokana na hali ya tumbo," 7T 257.

“Kukosa kiasi ni dhambi." CDF 43 Msisitizo umeongezwa.

 

Ni dhambi kubwa kuvunja sheria za uhai wetu (Laws of our being) kama kuvunja moja ya amri kumi, kwasababu hatuwezi kufanya mojawapo bila kuvunja amri za Mungu." 2T 70 Msisitizo umeongezwa.

 

"Kuvunja sheria za kimwili (physical law as) ni kuvunja amri za Mungu…" CDF 43. Msisitizo umeongezwa.

 

"Kila kitendo ambacho huharibu nguvu za mwili, akili, na roho no dhambi." MH 113 Msisitizo umeongezwa.

MAANA NZURI YA DHAMBI

“Chochote kinacho dhhofisha uwezo wetu wa kufikiri, hudhohofisha uwezo wa utambuzi wetu, hudhohofisha hali yetu ya kumtambua Mungu, au kuondoa shauku ya mambo ya kiroho, kwa kifupi chochote kinachoongeza mguvu ya mwili wako juu ya akili, kitu hicho ni dhambi kwako haijalishi kiwe kizuri kiasi gani kwa chenyewe." Susanna Wesley (Mama yake John Wesley)

"Ujinga katika somo hili (matengenezo ya afya) la muhimu, ni dhambi..." CH 40 Msisitizo umeongezwa. Msisitizo umeongezwa.

" Yule anaebakia katika katika uovu unaotokana na ujinga wa kanuni za afya na uzima , na ambae kwa maamuzi yake huvunja kanuni hizi, hutenda dhambi dhidi ya Mungu. " CT 295. Msisitizo umeongezwa.

 

"Chochote kinachodhohofisha afya , si kwamba hudhohofisha nguvu za mwili tu, lakini pia huwa na tabia ya kudhohofisha nguvu za kiakili na kimaadili pia." MH 128 Msisitizo umeongezwa.

"...Utumiaji wa vyakula vya nyama...Je hatupaswi kubeba ushuhuda wa maamuzi dhidi ya kuendekeza hamu ya chakula iliyopotoshwa?" 9T 159 Msisitizo umeongezwa.

"Kama tumbo halitunzwi vizuri, uundwaji wa tabia nyoofu, ya kimaadili utazuiliwa." 9T 160. Msisitizo umeongezwa.

"Lakini wale ambao ni watumwa wa tamaa ya chakula watashindwa katika kukamilisha tabia ya Kikristo." 3T 492. Msisitizo umeongezwa.

"Haiwezekani kwa wale wanaoendekeza tamaa ya chakula kupata ukamilifu wa Kikristo (Christian Perfection)." 2T 400

"Ukamilifu wa tabia hauwezi kupatikana wakati sheria za asili zinavunjwa; kwa kuwa huku ni kuvunja sheria ya Mungu." OHC 266

"Huwezi kupata ukamilifu wa Kikristo isipokuwa umepata udhibiti mkamilifu wa roho yako." 2T 311

"...chakula kimwili huathiri akili na tabia/ silika ya moyo (disposition)." AH 252.

"Wengi hudhohofisha tabia zao kwa kula bila utaratibu."  CDF. 126 Msisitizo umeongezwa.

"Kiasi katika ulaji ni lazima kifanyiwe mazoezi kabla hujawa mtu mvumilivu." 2T 405 Msisitizo umeongezwa.

"Mungu hawezi kuruhusu Roho Wake Mtakatifu juu ya wale ambao... (kwa kujua) hodhohofisha  akili na mwili." CDF 55. Msisitizo umeongezwa.

"Hatma ya umilele wetu hutegemea katika msimamo thabiti wa kiasi katika mienendo  ya afya,..." 3T 489.

"Tumaini letu pekee katika uzima wa milele ni kupitia kuleta tamaa ya chakula na tamaa za mwili kwa kuzisalimisha chini ya mapenzi ya Mungu." DA 122

"Kila uvunjaji wa kanuni katika ulaji au unywaji, huondoa makali ya viungo vya fahamu, kufanya isiwezekane kwavyo kukubali au kuweka thamani halisi katika mambo ya milele." CH 38

"Unywaji wa chai na kahawa ni dhambi." (CDF 425.)

"Kila shilingi iliyotumika kwaajili ya Chai, kahawa , na nyama ni mbaya kuliko iliyopotezwa ...(Every penny expended for tea, coffee, and flesh meat is worse than wasted); kwa kuwa vyakula hivi huzuia maendeleo ya nguvu za  kimwili, kiakili na kiroho. " CDF 402. (See also CDF 381; 9T 153,154)

USHAURI WA SHETANI

Baadhi hudhani kwamba hawawezi kufanya matengenezo, kwamba afya itatolewa kafara kama wakijaribu kuacha matumizi ya chai, tumbaku, na nyama. Huu ni ushauri wa shetani. Ni hivi visisimuo vya kudhuru ambavyo kwa hakika huharibu mwili na kuuandaa mfumo wake kwa magonjwa makali  , kwa kudhohofisha mashine bora ya asili na kuangusha chini nguvu zilizosimamishwa dhidi ya magonjwa na kuoza mapema.(premature decay).... {CTBH 153.1}

 

Some think they cannot reform, that it would ruin their health to leave off the use of tea, tobacco, and flesh-meats. This is a suggestion of Satan. These hurtful stimulants will surely undermine the constitution, and prepare the system for acute disease; for they impair nature's delicate machinery, and batter down the fortifications she has erected against disease and premature decay.  {CTBH 153.1}

Utumiaji wa visisimuo visisvyo vya asili ni uharibifu kwa afya, na wenye msukumo wa kudhohofisha katika ubongo, kufanya isiswezekane kuyakubali mambo ya umilele. Wale wanaoendekeza miungu hiyo hawawezi kuweka thamani kwa usahihi katika wokovu ambao Kristo ameutoa kwaajili yao kwa maisha ya kujikana, sadaka ya daima, na maonyo, na hatimaye kwa kujitoa maisha take yasiyo na dhambi kuokoa mwanadamu anaepotea toka kwenye kifo.

 

"Mlo wa nyama ni swami makini. Je wanadamu waishi kwa nyama ya wanyama waliokufa? Jibu kutoka kwa nuru ambayo Mungu ametoa ni, HAPANA, hapana thabiti (decidedly no) ....wanyama wachache sana wako huru mbali na magonjwa." CDF 388; MS 3, 1897. Msisitizo umeongezwa

 

"Magonjwa katika wanyama yanongezeka kwa uwiano na kuongezeka kwa maasi katika wanadamu." CDF 366 (Na Je jamii ya wanadamu haijakaribia kukijaza kikombe chake cha uovu?)

"Imekuwa ikionyeshwa kwangu kwa uwazi kabisa kwamba watu wa Mungu wanapaswa kuchukua msimamo thabiti dhidi ya ulaji wa nyama. Je Mungu Angewapa watu wake kwa miaka 30 kwamba ili wawe na damu safi na akili safi, ni lazima waache kula nyama, kama hakuwataka kuzingatia ujumbe wake?" Notebook Leaflets, Elmshaven Leaflets, Vol 1, No. 35, p.2 Msisitizo umeongezwa

 

"Kwanini baadhi ya ndugu zetu wachungaji hudhihirisha shauku ndogo katika matengenezo ya afya? Hakuna mtu apaswae kutengwa kama mwalimu wa watu wakati kielelezo chake kama mfundishaji kinapingana na ushuhuda ambao Mungu amewapa watumishi wake kuubeba kuhusiana na ulaji, kwakuwa hili litaleta mkanganyiko (confusion). Upuuziaji wake wa matengenezo ya afya utamfanya asifae kusimama kama mjumbe wa Mungu." 6T 378

"Hebu hata mmoja wa wachungaji wetu asitoe mfano mwovu kwa  ulaji wa nyama." CDF 399

 

Hawana cha kujitetea hata kidogo kwa kula nyama ya wanyama waliokufa... Je twaweza kuwa na imani katika wachungaji ambao, katika meza ambazo nyama huletwa, huungana na wengine katika kuila?" (Pacific Union Recorder, Oct 9, 1902; MS 3, 1897. Tazama pia CDF 402. Msisitizo umeongezwa

Oh Bwana tupatie wachungaji ambao ni watiifu kwa mashauri yako. Tupatie wchungaji ambao utawajaza Roho . Tupatie wachungaji ambao tutawaamini.

"Maelekezo yametolewa kwangu kwamba matabibu ambao wanatumia nyama na kuiandika itumiwe na wagonjwa , hawapaswi kuajiriwa na taasisi zetu." CDF 290 Msisitizo umeongezwa

"Ulaji wa nyama haupaswi kuja katika maelekezo ya kitabibu kwaajili ya mtu yeyote kutoka kwa Tabibu yeyote toka kwa wale wanaoelewa mambo hayo. Magonjwa katika wanyama yanafanya ulaji wa nyama kuwa jambo la hatari.... Hivyo mambo hata yasiruhusiwe kwa maelekezo ya tabibu yeyote ambae ana ujuzi wa ukweli wa wakati huu. Hakuna usalama katika ulaji wa nyama ya wanyama waliokufa, na katika wakati mfupi itakuwa si salama kutumia chochote ambacho hutoka kwa viumbe wanyama." CDF 441. Msisitizo umeongezwa

 

"Katika nafaka, matunda, mboga , na jamii ya karanga zapaswa kuonekana kuwa aina zote za vyakula tunavyohitaji." CDF 310

WALE WANAOJIANDAA KUNYAKULIWA WATAACHA ULAJI WA VYAKULA VYA NYAMA .

“Miongoni mwa wale am,bao sasa wanangojea kurudi kwa Bwana, ulaji wa nyama hatimaye utaachwa kabisa; nyama itaacha kuunda sehemu ya lishe yao.” CDF 380, 381. Msisitizo umeongezwa

 

 

WAADVENTISTA WENGI WANAONG’ANG’ANIA KULA NYAMA WATAPOTEA

"Wale ambao sasa wameongoka nusunusu katika swala la ulaji wa nyama wataachana na watu wa Mungu na hawataambatana nao tena." CDF 382; RH May 27, 1902; H 575.

"Ushahidi wa hali ya juu wa ubora wa Mkristo ni kujidhibiti-nafsi." DA 301.

NENO LA KUTIA MOYO

"Kama ukitafuta msaada toka kwa Mungu, nguvu Yake itendayo kazi ndani yako itazileta katika udhaifu nguvu zote zinazopinga, na utaweza kutakaswa kupitia ukweli." RH June 16, 1891. Msisitizo umeongezwa

 

"Atakubadili , kwa ajabu atabadili mwonekano usio na matumaini kabisa wenye kukatisha tamaa." PK 260.

 

"Je mlo waweza kifanya Nini nasi? Kila kitu , kama tuko tayari kusalimisha vyote." OHC 19.

 

TWAWEZA KUSHINDA TAMAA KWA KUJIZUIA KABISA

"Kwa kujizuia kabisa atashinda tamaa yake ya kuendekeza vitu vinavyoharibu afya." (EV 264.)

"Yeu aweza kukupa nguvu ya kushinda. Kwa msaada wake waweza kuharibu kikamilifu mzizi wa ubinafsi." 7T 49

 

"Wale wore wanaotumia nyama wanapuuzia maonyo yote ambayo Mungu ametoa kuhusu swala hili. Hawana ushahidi kwamba wanatembea katika njia  salama. Hawana utetezi hata kidogo." Pacific Union Recorder, Oct. 9,1902. Msisitizo umeongezwa

"Swala la matengenezo ya afya halitiliwi mkazo ipaswavyo na inavyotakiwa kuwa." CDF.304.

"Kuwa makini sasa unajiweka katika pingamizi la kazi ya matengenezo ya afya. Itasonga mbele...." CDF.38.

MAAMUZI YETU

Mungu kazungumza nasi katika Biblia na Roho ya Unabii. " Nyakati za hatari ziko mbele yetu....ni lazima tufuate maelekezo yaliyotolewa kupitia Roho ya Unabii.... Kama tukiyapuuzia, tutatoa utetezi gani?" 8T 298. Msisitizo umeongezwa

Swali ni kwamba , Je tutafuata mashauri yaliyotolewa katika Biblia na Roho ya Unabii? Kwasababu tunampenda Bwana, tuitikie, "Bwana amenena: nasi tutatii!"

 

 

7.                      WATU WANAOITUNZA SABATO

 

VILELE VIKUU VIWILI VYA MLIMA

Umewahi kujiuliza swali hili makini sana "Je Mimi ni MSABATO au ni MWADVENTISTA WA SABATO? Haya majina mawili yana tofauti sana.

 

Kama vilele vikuu viwili vya milima vilivyosimama juu ya vingine vyote, vionekanavo juu katika anga, vivyo hivyo na matukio makuu mawili katika historia ya dunia yetu.

Text Box: UUMBAJI

UKOMBOZI

 
Kwa kujua zaidi namna ya kutunza sabato, kasome Shuhuda kwa Kanisa, Gombo la Sita, sura inayoeleza utunzaji wa SABTO

 

 

 

 

Haya ni mtukio makubwa mawili uumbaji na ukombozi. Haya ni matukio mawili makuu kuliko yote katika historia ya dunia yenye manufaa kuyajua. Kwa kulinganisha matukio Haya matukio mengine yote yanakosa umuhimu.

 

 

UUMBAJI

Katika mwanzo wa historia ya dunia yetu hii, baada ya kuiumba dunia Mungu aliumba wazazi wetu wa kwanza kwa mfano wake, kimwili, kiakili na Kiroho. Mungu aliumba jamii ya wanadamu kuikuza mbingu. Ni tukio kubwa kiasi gani lisilo na ubinafsi. Tusingekuwa hapa leo kama isingekuwa kwa kitendo hicho kikuuu cha upendo toka kwa Mungu.

UKOMBOZI

Pale jamii ya wanadamu ilipotenda dhmbi na kuanguka kutoka katika hadhi yake ya juu ya kufanana na Mungu, Mungu alimkomboa na kumuumba upya mwanadamu kwa sura yake, kwa kumfia pale msalabani, kilikuwa ni kitendo kikuu jinsi gani cha kujitoa kafara. Tungekuwa ni wa kupotea milele bila tumaini la wokovu, kama isinge kuwa kwa tendo hili kuu la upendo wa Mungu.

 

 

 

MUUMBAJI WETU

Na ni nani muumbaji wetu? Biblia husema kwamba Mungu alituumba kupitia Yesu.

"Mungu Baba aliviumba vitu vyote kupitia Yesu Kristo." Waefeso 3:9

"Katika yeye (Yesu Kristo) vitu vyote viliumbwa" Wakolosai 1:16

"Vyote vilifanyika kwa Huyo ; wala pasipo yeye hakikufanyka chochote kilichofanyika" Yohana 1:3

 

Uweza uliotumiwa na Mungu katika Uumbaji ndiyo uliotumiwa nae katika ukombozi. Uweza Huo hudhihirishwa au kuwasilishwa kwa Ishara ya sabato. Kwa maelezo Zaidi ya mambo makuu matatu yawasilishwayo mna sabato fuatilia somo “UNAFANYA HAYO KWA UWEZA WA NANI,MAANA YA KINA YA PUMZIKO” KATIKA YOUTUBE ACOUNT YA PETRO TUMAINI TV. Kwa maelezo Zaidi kuhusu kupata kitabu kinachoelezea kwa kina Zaidi habari hizi wasiliana nasi kwa email- petro.tumaini@gmail.com au simu 0754202021. Bwana akubariki unapoendelea kuyafanyia kazi mambo hayo na kuwafundisha wengine