Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16


NINI TUPATACHO KWA MASTAA?

   
JIEPUSHE  NA UCHAWI WA BABELI
Mbinu za shetani kuua hali ya kiroho kupitia Maburudisho.
By Petro Tumaini.

lWafuasi wake hupatikana Jiji la malaika waliopotea (lossangeles) -Lost Angels.

lWana msukumo mkubwa kupitia vyombo vya habari.

lHufanya kazi kama wasanii nyota (mastaa).

lHawana tofauti na theluthi ya nyota (malaika wapotevu) waliotupwa pamoja na shetani kutoka mbinguni.

Nini maana ya neno babeli
Wafuatao madanganyo ya Babeli hujiandaa kwa moto wa milele
Ujenzi wa mnara wa babeli uliositishwa na Mungu kule shinari, huwakilisha
machafuko yanayoletwa na shetani ili kupinga maagizo ya Mungu.

Babeli ni neno la kigiriki lililotokana na neno (ba\'be¬l) au kwa kiebrania huitwa (Babel.) Kwa mujibu wa Mwanzo 11:9 Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo BWANA alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo BWANA akawatawanya katika uso wa dunia yote. .’’ (Kiswahili cha kisasa)
Kimsingi  neno babeli humaanisha machafuko kwasababu ya ukweli kwamba kitenzi cha Kiebrania Balal  ambalo humaanisha "kuleta machafuko" japokuwa Wakazi wa mji huo waliuita BaÆbilu wakimaanisha "lango la dhahabu" au BaÆbiÐilaÆni (lango la miungu).
Jina hutokana na neno asilia la "kiebrania babalu" "kutawanya"  au "Kupotea" ; watu wa Babeli wasingeweza kujivunia asili ya jina la mji wao na ndio maana wakauita kwa jina litokanalo na majina Mawili "babu" yaani "geti au lango"  na "ilu" likimaanisha "muungu".
Mji huu huanzia mapema kwa wakazi wa mesopotamia , mwanzo wa utawala wa Nimrodi, ilikuwa nai enzi yake Mwanzo 10:8-10 . Kushi alikuwa baba yake Nimrodi, akakua akawa mtu shujaa mwenye nguvu duniani. 9Alikuwa mwindaji hodari mbele za BWANA. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za BWANA.’’ 10Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari

Bahati mbaya sana jina hili husimama katika siku za mwisho likiwakilisha dini ya uongo, na Biblia huonyesha kuwa mji wa babeli utaanguka na kuangamizwa, Ufunuo 14:8. Ukitafuta katika ramani ya dunia huwezi kukuta mji waishio watu uitwao babeli, hivyo jina hili ni kiwakilishi au alama (symbol) ya dini ya uongo na madanganyo yote ya shetani kwa jamii ya wanadam ambao huwalenga ili waangamizwe pamoja na yeye.

Ufunuo 14:8 Malaika wa pili akafuata akisema, “Ameanguka! Ameanguka Babeli aliye mkuu, yeye aliyeyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.’’ (Kiswahili cha kisasa)

Ufunuo 18: 2 . Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema: ‘‘Umeanguka! Umeanguka Babeli ulio mkuu!
Umekuwa makao ya mashetani na makazi ya kila pepo mchafu, makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye .

Ni watu gani watakaoanguka pamoja na babeli
Ufunuo 18:3.Kwa maana mataifa yote yamekunywa mvinyo wa uasherati wake, nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye, nao wafanyi biashara wa dunia wametajirika kutokana na wingi wa utajiri wake.’’ (Kiswahili cha kisasa)

Watu watakaopotea na babeli ni wale walionyweshwa  mvinyo wa ghadhabu yake...Labda waeza ukasema hujawahi kunywa wala kunyweshwa mvinyo wa Babeli au , wawezaje kunyweshwa mvinyo wakati wewe hutumii pombe kabisa.

Maana ya Mvinyo wa uasherati ni nini?
 
Neno hili limetokana na ukweli kwamba nabii Yeremia aliambiwa hivi katika Yeremia  25:15 .Hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli, aliloniambia: “Chukua kutoka mkononi mwangu kikombe hiki kilichojaa mvinyo ya ghadhabu yangu na kuyanywesha mataifa yote ambayo ninakutuma kwao.  Si dhumuni la shetani (Babeli kuwanywesha mataifa mvinyo wa uasherati wake ili wapaate ghadhabu bali shetani hudai kwamba katika mvinyo wake hupatikana amani.

Kwa kawaida mtu anywapo mvinyo hulewa, kunyweshwa mvinyo na shetani au Babeli ni kufuata mafundisho ya uongo ya Shetani ambayo ni kinyume na maagizo ya Mungu kwahiyo huleta ghadhabu ya Mungu.

Shetani huwanywesha mvinyo watu kwa kuwaloga au kwa kutumia mbinu nyingi aikiwamo mbinu ya uchawi, ufunuo 18 huweka bayana kwamba watu wengi duniani wataangamia kwasababu wamedanganywa na uchawi wa babeli.

Ufunuo 18:23.Mwanga wa taa hautaangaza tena ndani yako. Wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi kamwe haitasikiwa ndani yako. Kwa kuwa wafanyi biashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia na mataifa yote yalidanganyika kwa uchawi wako.

Ufunuo 18: 23 . Wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala saauti ya Bwana harusi na bibi harusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa, maana hao wafanyabiashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.

Re 18:23 And <kai> the light <phos> of a candle <luchnos> shall shine <phaino> no more <ou me> at all <eti> in <en> thee <soi>; and <kai> the voice <phone> of the bridegroom <numphios> and <kai> of the bride <numphe> shall be heard <akouo> no more <ou me> at all <eti> in <en> thee <soi>: for <hoti> thy <sou> merchants <emporos> were <en> the great men <megistanes> of the earth <ge>; for <hoti> by <en> thy <sou> sorceries <pharmakeia> were <planao> all <pas> nations <ethnos> deceived <planao>. (KJV)
Shetani huwaloga watu  ambao wasipoibadilika kwa kupitia njia walizofunguliwa na Mungu ikiwa pamoja na somo hili watangamizwa, kwa kuwafanya wasimuabudu Mungu wa kweli bali wa muabudu yeye kupitia vitu anavyoviweka.
Ni jambo la kushangaza , neno famacia (uchawi) pamoja na mkaana yake kubwa , humaanisha "kitu chochote kugeuzacho akili isiweze kufuata na kutii neno na sheria ya Mungu"
KWANINI TUNAFANYA IBADA  -  MUNGU AMETUWEKEA KILA MMOJA TAMANIO LA KUABUDU
Mwanzo tu wa historia shetani anatajwa kama mpiganaji mashuhuri wa kuwaondoa watu toka kwenye Ibada ya Mungu wa kweli ili aabudiwe yeye.
Mfano wa kuhuzunisha sana juu ya ibada ya sanamu (miungu) unapatikana katika Danieli 3 ipatikanapo habari ya Shedraki, Meshaki na Abednego . Mfalme wa Taifa ambalo vijana hawa watatu wa Kiyahudi  walitekwa alisimamisha sanamu kubwa ya dhahabu, aliagiza kwamba kila mtu lazima asujudu sanam hiyo tofauti na hapo atauwawa. Shedraki, Meshaki na Abednego walikataa kuisujudukwasababu walimwabudu Mungu wa kweli, matokeo yake walitupwa katika tanuru liwakalo moto Mungu akawaokoa hawakuteketea hata kidogo.
TWAWEZA KUPATA MIFANO HALISI YA IBADA YA SANAMU LEO?

Mwaka 2006 katika tamasha la Emmy Awards, mwanavichekesho  Stephen Colbert aliita Hollywood kama “Tumabo la mnyama” na watu waliohusika kama “wanasodoma wasiomcha Mungu”. Japokuwa Colbert alizungumza kwa utani, maneno yake yana uhalisia  wa kutisha.
TUMESHASIKIA KUHUSU UCHAWI WA ZAMANI.

Yawezekana uchawi upo katika jamii zetu leo na tumewekwa chini ya ngome za uchawi? Kama wana wa Israeli walivyokamatwa katika uchawi wa dini zilizowazunguka hata sisi tunakamatwa leo kwa namna hiyo. Katika 1 Timotheo 4:1
Pamoja na uchawi wa zamani tuliousikia Je yawezekana ukawa hai katika jamii zetu leo na sisi tunawekwa chini yake?

Kama wana wa Israeli walivyonaswa na mtego wa uchawi wa mataifa yaliyowazunguka , ndivyo tunavyonaswa leo hii kuikataa imani yetu…
Katika 1 Timotheo 4:1, Paulo anamuonya Timotheo na kanisa juu ya uchawi ambao ulishaeenea tokea enzi zake.
1 Timotheo 4:1 Basi roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafindisho ya mashetani.

Strongs Greek dictionary-Wakisikiliza (Gr prosecho-kubeba akilini, kuhamisha umakini, kujitoa au “apply oneself to”)

Historia ya Hollywood kuhusu wasanii Nyota (stars) wakubwa wanonyeshwa wakiwa wamoja kabisa na “roho zidanyganyazo”

 SHETANI ameweka nguvu yake kubwa sana nyuma ya vyombo vya habari (Televisheni, Magazeti, Mikanda, Intaneti n.k) ili kuhakikisha anawaandaa watu kwa moto wa milele ambao Mungu ameuandaa kwaajili ya ibilisi na wale wanaomfuata. Hebu tuchunguze Biblia tuone imelizungumziaje suala hili.

Wanadam wengi hutumia sehemu kubwa ya maisha kwa kujishughulisha namaburudisho (entertainment). Shetani amegeuza entertainment kuwa sehemu ya uangusha ibada ya Mungu na kufanya iwe Ibada ya Kumuabudu yeye kupitia mastaa, huwaloga watu kupitia entertainment.

v Vijana wengi hutegemea maburudisho kama vile;
            · Muziki.
            · Mpira.
            · Maigizo.
            · Riadha.n.k.
v Kwa madhumuni ya;
     ØKufahamika
     ØKupata hela
     ØKuburudika

Hebu tutazame kitabu cha Ufunuo wa Yohana, ambacho hukusanya kwa pamoja maneno ya Mbinguni, Duniani na hata yale ya shetani kikionyesha vita ya mwisho baina ya wema na uovu kikitumia picha halisi na alama,vitu vya kawaida na vya kiroho ili kutupatia ujumbe uliotoka kwa Mungu mwenyewe.

Tokea zamani Babeli ni dini ya  kupenda dunia ambayo na kumuacha Yesu Huleta uchawi wake ili iwapotoshe watu wote wa dunia hii endapo tu hawatajikita kwa Yesu Kristo, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.

Dini ifundishayo kuwa wanadam hawaokolewi kwa kushika sheria, mwaadam akifa rho inaendelea kuishi inajenga mnara wa mafunzo ambayo kupitia hayo inawadanganya watu kwamba wataokolewa lakini kiukweli watapotea kupitia mafundisho hayo.
Kama tulivyoona neno uchawi  au sorcery limetokana na neno la kigiriki famakeia limaanishalo kitu chochote kichanganyacho au kupumbaza akili na kufanya isiweze kutii au kufuata mapenzi ya Mungu au sheria yake.

KWA MUJIBU WA KICHWA CHA SOMO HILI WAWEZA KUJIULIZA MASWALI YAFUATAYO.
(1)Je Pombe yaweza kupumbaza akili isiweze kutii amri na maagizo ya Mungu?
(2)Je televisheni yaweza kupumbaza akili isiweze kufuuata , kutii au kusoma neno la Mungu?
(3)Je Mpira waeza kupumbaza akili isipate nafasi na mda wa kutafakari neno la Mungu?
(4)Je muziki (hasa hasa wa kidunia) waweza kupumbaza akili isifuate , na kutii neno la Mungu

 Shetani ameweka hazina kubwa ya uchawi wake kupitia kiwanda cha maburudisho (Entertainment industry). Huu ndio uchawi anaotumia kuwapotosha mataifa na kwa namna moja au nyingine ndio utajwao na kitabu cha ufunuo . Kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako. 
   Tunapozungumzia Kiwanda cha maburudisho, tunazungumzia:
(1)Pombe.
(2)Muziki
(3)Michezo.
(4)Filamu
(5)Maigizo.n.k

  Haya yate hutimiza kile kinachoelezea neno Famacia au uchawi wa babeli ambao kwa huo shetani kuwafanya watu wapuuzie kusali, kusoma neno la Mungu, kulitafakari na hata mda wa kushuhudia kweli ya biblia.
Maana ya neno ENTERTAINMENT (maburudisho).
  Neno hili limejengwa na maneno matatu
  • (1)ENTER-Kuingia (coming in)
  • (2)TAIN- kumiliki (posses)
  • (3)MENT- kuendelea kumiliki.(Keep on the state of possesion)
 Kwa ujumla inamaanisha kuingia, kumiliki na kuendelea kuweka katika hali ya kumiliki. (coming in, posses and keep on the state of possesion.)

Je umewahi kutambua kwamba, kupitia entertainment industry (kiwanda cha maburudisho) ambayo mengi ni ya kidunia shetani huingia akilini mwako, hukumiliki na kuendelea kukumiliki kifikra?”

Waebrania 13:1, 2. Upendo wa kidugu na udumu. 2Msisahau kuwakaribisha wageni, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, watu wengine waliwakaribisha malaika pasipo kujua.
Kifungu cha maneno Kuwakaribisha wageni katika biblia ya kuiingereza hutamkwa Entertain strangers, ambalo limetokana na neno entertainment.
Kama inawezekana kuwakaribisha (entertain) malaika wa nuru  yaani waingie, kumiliki na kuweka katika hali ya kumiliki nyumba zetu na akili zetu. Je si rahisis zaidi kuwakaribisha malaika waovu nao wafanye makao yao majumbani kwetu na akilini mwetu kupitia maburudisho tunayoyapendelea?

“Ukijishughukisha na maburudisho ya kiroho/kikristo (spiritual entertainment) utakuwa makao ya Roho wa Mungu, vivyo hivyo ukijishughulisha na maburudisho ya kidunia (wordly entertainment) utakuwa makao ya shetani.”
 
Ni kwa namna hii Ufunuo 18:23 inatoa kifungu cha maneno Kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako. 

Shetani ametupofusha akili tushindwe kuelewa kina cha uchawi uzungumziwao na Biblia kwa kutupatia dhana finyu, yaani kila tusikiapo neno uchawi tuwaze tu watu wanaowanga usiku, waganga wa kienyeji wapigao ramli.

   “Laiti kama tungejua shetani hutuloga na kutupotosha kwas uchawi wake (famacia) kupitia kiwanda cha maburudisho (entertainment), tungegesali kuliko kawaida.”

Katika Biblia wapo watu waliojioepusha na uchawi huu na hatimaye walichukuliwa kwenda Mbinguni kama henoko.

 Henoko (Mwanzo 5:21-23), alitembea na Mungu kwa muda wa miaka mia tatu. Yaani alimtafakari Mungu na mabo ya kimbingu, hakutumia mda wake kwa kuijazaakili na mabo ya dunia, hatimaye Mungu akaamua kumchukua mbinguni.

Wale wajiitao mastaa katika entertainment indusry ni wakala wa Malaika wa Shetani waliotupwa toka mbinguni.

Ufunuo 12: 9, 4. 9 Yule joka akatupwa, yule mkkubwa , nyoka wa zamani, aitwae Ibilisi na Shetani, audanganyae ulimwengu wote , akatupwa hata nchi na malaika zake pamoja nae. 4 Na mkia wake ukakokota theluthi ya nyota za Mbinguni, na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
Baada ya Shetani kuleta uasi wa kutaka kufanana na MunguMalaika mkuu Lusifa (kwa sasa ni shetani) alitupwana theluthi ya malaika waliofuata uongo wake.

Ni nini kilichomfanya Shetani na theluthi ya nyota (malaika) watupwe.
Ukisoma Isaya 14 utagundua yafuatayo.

  • (1)Alitaka kuwa kama Mungu.
  • (2)Aliwashawishi malaika wamuunge mkono akimshutumu Mungu kama dikteta.
  • (3)Alitaka kuwa zaidi ya Mungu, yaani alitaka kuwa maarufu (famous) kuliko Mungu.

KKwa kadri Muda ulivyozidi kwenda uongo wa shetani ulijulikana akatupwa kutoka mbinguni na kuhamishia mashambulizi yake duniani.

Alipofika duniani alimdanganya Hawa kwa kutumia medium (mfumo) wa nyoka, leo hii hutumia media (mass media) yaani vyombo vya habari kwa ujumla.
 
Wafuasi wa shetani ambao kwa sehemu kubwa hutumia media (mass media) vyombo vya habari nao hufanya kazi wakiongozwa na madhumuni hayo hayo ya kutaka kuwa maarufu, na kuwaburudisha (entertain) watu.

Wanafanya kazi ya kuwahimiza watu nao waitwe nyota (mastaa), na hivyo si kazi kuona matokeo ya kazi zao. Ukiona mtu anafanya kazi akidhamiria kuwa staa, kuwa maarufu ni msukumo uleule wa shetani.


Watu wejiitao au kuitwa masupastaa huomgozwa na Ibilisi


  Ndiyo maana tuna mastaa wa aina nyingi;
(1)Mastaa wa filamu.
(2)Mastaa wa mpira.
(3)Mastaa wa ngumi.
(4)Mastaa wamuziki.
(5)Mastaa wa michezo mbali mbali.

Siku kwa siku tunaabudu mastaa bila kujua na wakati mwingine tunajua, na kiukweli kupitia maburudisho shetani huwatumia kutu entertain ( kuingia, kutumiliki ,na
kutuweka katika hali ya kutumiliki.)

   baada ya siku chache tunajikuta.
(1)Tunaongea kama mastaa.
(2)Tunatembea kama mastaa.
(3)Tunavaa kama mastaa. Mabinti huvaa vimini kwasababu ya msukumo wa mastaa, vijana huvaa milege kwasababu ya msukumo wa mastaa. Huu ndiyo uchawi wa Babeli ufanyavyo kazi.                                                                          



“Mahali walipoweka ngome malaika wa shetani (NYOTA.Ufunuo 12:4  Na mkia wake ukakokota theluthi ya nyota za Mbinguni...”)
  
Bila shaka theluthi hii ya malaika hupatikana mahali ambapo ngome ya mastaa (nyota) wa maburudisho duniani hupatikana. Na sehemu hii Hujulikana kama Hollywood hasa katika jiji la Losangeles lililoko  California. Hapa ndipo wapatikanapo mastaa wa movies na maburudisho ya aina zote duniani , tena hutumia media kuwafikia mashabiki wao.

"Mfumo wa waigizaji nyota, ulikendelea kukua kama sehemu ya sinema za Hollywood"(Stokes, 2003, uk 85)

Majina tu ya sehemu hizo yanadhihirisha kuwa hizo ni ngome za shetai. HOLLYWOOD, LOSANGELES. Je umewahi kutafakari maana ya majina haya.
  
HOLYWOOD, jina hili limetokana na jina HOLLY TREE mojawapo ya miti ya nguvu za giza na ulikuwa na matunda ya kuvutia ambayo ni sumu , ulikuwa ikitumika kuwafanya watu wafikie kifo bilo tabu.
  
Je haiwezekani pia kupitia hiollywood shetani huwaloga watu kwa uchawi wa wanamaburudisho kuwafanya watu wafe kiroho kwa kile wanachoshabikia au kutazama kama kitu cha kuvutia na kupendeza ?

  
LOSANGELES, jina la jiji hili waishio mastaa wakubwa wenye msukumo sana dunia nzima limetokana nna neno la kiingereza (LOST ANGELS) LIMAANISHALO MALAIKA WALIOPOTEA.

Hapa tunapata jambo moja la uhakika, malaika (nyota) waliodanganywa na shetani na hatimae kutupwa kutoka mbinguni pamoja na shetani hata kama si wote basi kwa sehemu kubwa sana waliangukia katika jiji hili lililoitwa kwa jina lao.(Loss angeles-lost angels au malaika waliopotea).

Historia fupi ya uchawi Hollywood.

Miaka ya 1920: Akijulikana kama mpendaji mahiri “the great lover”, muigizaji Robert na mkewe Valentino wote walikuwa wakijihusisha na mambo ya uchawi
Kila usiku Natasha  alikuwa akiwasiliana na kuvuviwa na mizimu ili aweze kuandika muongozi (script) ya kuongoza filamu , baada ya kupagawa na kumaliza uandishi wa script siku iliyofuata aliikabidhi kwa director 9muongozaji wa filamu) tayari kwa kuigizwa.
Pia miaka ya 1930: Muigizaji  Mae West, alimwita mwanamke mmoja mwanamapinduzi wa ngono, Malkia wa Mapenzi ambae aliwahi kusema:
“Nikiwa mahiri, ni mahiri sana. Nisipokuwa mahiri, ni bora zaidi.”
Kazi ya West ilichangia sana kuua maadili ya Biblia Marekani ya Kaskazini. Mahusiano yake na mizimu yalimfanya aweeze kuhusika vyema katika maudhui ya filamu. Alijitoa kuwa  chombo (medium) cha mizimu, na usiku aliutumia kusoma na kuandika mambo ya umizimu.
Mojawapo ya maandiko yake yanaonyesha “alipokasirika baada ya watu kukosa  wazo la kuandika kwaajili ya kuigiza (script idea) , alizunguka katika chumba chake, na kusema , nguvu , nguvu , nguvu, na ije juu yangu inisaidie kuandika script. Aliweza kuanza kusikia sauti na kuona picha, kwa kadri mtiririko ulivyofunuliwa kwake  muda huo huo aliwaita wapiga picha washughulike pamoja nae, akiwa amelala katika hali isiyo ya kawaida, na kuongea kwa kadri roho wachafu walivyomuongoza.


Miaka ya 1950: Lucille Ball alikuwa  mchezaji Nyota maarufu wa filamu miaka ya 1940 lakini aliamua kurudi katika uigizaji mwaka 1951 baada ya mzimu wa muigizaji Carole Lombar kuongea nae.Lombard ambaye alikuwa ni mwana komedy maarufu allifariki kwa ajali ya ndege mwaka  1942.
It was the spirit of actress Carole Lombard who guided Lucille Ball into taking a chance and accepting the offer to star in I Love Lucy. The glamorous comedian, who had died in an airplane crash in 1942, appeared to Lucy in 1951. Because Lucille Ball accepted the spirit’s urging to “take a chance, honey,” she made television history.v

1960s: Peter Sellers, afahamikae sana kwa  filamu za ( Pink Panther film series,) anasema yafuatayo kuhusu uigizaji:
Ni kama kuwa chombo (medium ) na kujitoa na kusema, nataka mhusika (character) kuingia katika mwili wangu na kuniongoza ili niweze kufanya lile nitakalo kulifanya.
Mastaa wachawi wa hivi karibuni
Uchawi haukuiunda Hollywood yta zamani bali hata ile ya sasa, kama Robin Williams anavyoliambia gazeti la US Weekly:

“Ndiyo!Ni kama kumiliki,— ghafla unajikuta ndani yake,... unapata tu nguvu hii ambayo inaanza kutenda kazi…ni umilikwaji…ambapo  unajikuta kiuhalisia unakuwa nguvu hii mpya”
Dairekta wa The Devil's Advocate ,Taylor Hackford anazungumza yfuatayo kuhusu muigizaji Keanu Reeves:
Keanu ni mtu wa ajabu mwenye mizimu ndani yake, nilikuwa najaribu kulichukua na kulitumia hilo…”
Dairekta Leonardo Dicaprio's wa Agnieszka Holland katika  Total Eclipse anasema:
Leo ni kama chombo. Hufungua mwili na akili yake  ili apokee ujumbe kutoka katika maisha ya mtu mwingine. .xii
Kama waigizaji hawa wanahusika na uchawi:
  •  Ni nini kitokacho katika Televisheni?
  • Ni ujumbe gain wajaribuo kutwambia?
UHARIBIFU ULIOFANYWA KATIKA TENDO LA NDOA
Mojawapo ya mambo yanayoharibiwa na shetani ni tendo la ndoa, Mungu kaagiza lifanyike ndani ya ndoa, kati ya mwanaume na mwanamke tena amekataza kulawiti au kufanya tendo hilo kinyume na maumbile.
Filamu za sasa zinavuruga mpango huo.
  •  Ndoa ya mwanamke na mwanamke (Lesbianism)
  • Ndoa ya mwanaume na mwanaume (guyism)
  • Wanawake wavaao viungo vya kiume (vya bandia)

Filamu hizi huharibu mahusiano ya ndoa, wapo wanandoa wanaoweka TV chumbani uli wae wanachukua utaalamu kwenye kanda za ngono, matokeo yake wanajikuta wakitoka nje ya ndoa.
  •  Jamaa wa kwenye mkanda wanapiga kazi nusu saa hadi saa zima. (Mwanandoa anashangaa mumewe/ mkewe dak 5-15 eme exost)
  • Filamu zinaonyesha watu katika muwasho na msisimko usio wa kawaida amabao wanaoigiza hawawezi kuufikia, matokeo yake wanandoa wanaanza kutafuta mshindo wa kwenye filamu kwa kusaka wazoefu nje ya ndoa.
  • Waigizaji wengi wa filamu za ngono si binadamu halisi ni mizimu, hawapo katika ulimwengu wa wanadamu. Kazi hii hufanywa na geti la tatu la kuzimu (geti la malkia) kuzalisha mikanda ya ngono.
Vyombo vya habari leo ni kama usambazaji wa imani ya Injili ya Gnistizim. (Gnostisism)
Maana ya Gnostisism
Kupindisha ukweli wa kibiblia. Hii ni kanuni iliyokumbatiwa sana na waigizaji wa filamu duniani.
Mahudhui ya Gnostic katika filamu
Filamu nyingi zimejengwa katika mahudhui yanayopotosha kabisa ukweli na maadili ya kibiblia, kwa kuangalia tunajiharibu kwa kuruhusu mambo hayo yaingie akilini mwetu.
 
Mwezi Agosti 2005, American Psychological Association , iliibuka na hitimisho juu ya mjadala wa migogoro katika video gem na vyombo vingine kama hicho , wakasema “katika maonyesho 73% ya vurugu na migogoro wakosaji huachwa bila adhabu,kwahiyo wanafundisha kwamba ugomvi ni njia pekee ya kumaliza mifarakano.


Muziki na Televisheni vina msukumo wenye nguvu ya kupumbaza akili.Tunapotaama maonyesho ya mapigano au kusikilia muziki wa hasira tunajiruhusu kuweza kutengenezwa na kanuni hizo katika bongo zetu.Japokuwa hatupigani au kufanya uhalifu, kwa kucheza videogames zinasukuma wachezaji kuhusika katika uhalifu na mauaji kupitia wahusika wanaocheza au kuchezeshwa humo.

Yesu katukomboa na kutuita katika maisha matakatifu,  (2 Timotheo 1:9...ambaye alituokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi ya neema yake yeye na neema yake. Neema hiyo tuilipewa katika Kristo Yesu tangu milele).

Hebu basi kwa kuutambua upendo wa Mungu na kazi aliyotufanyia Yesu tuzingatie kile alichosema Paulo.
Wafilipi 4:8,9 .Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo na sifa njema, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote ya kupendeza, yo yote yenye staha, ukiwako uzuri wo wote, pakiwepo cho chote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. 9Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi. .’’ (Kiswahili cha kisasa)

KANUNI ZITAWALAZO KATIKA KAZI YA SHETANI KUPITIA MABURUDISHO (UCHAWI)
­
AMUSE

Kama litumikavyo katika filam likimaanisha kuonyesha mambo ya  kushangaza . Neno hili linamaanisha kudangaanya kwa kupindisha ukweli, bahati mbaya wengi hupenda kutazamba mambo ya kushangaza bila kutambua kuwa shetani  anawadanganya maana ni kanuni ya kazi zake.
Ufunuo 12:9. Yule Joka aaakatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwae Ibilisi na shetani, audanganyae ulimwengu wote, akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.
Pia Mtume Paulo, amesema katika  1 Timotheo 4:1 Basi roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafindisho ya mashetani.

Filamu nyiongi hatawaliwa na shetani na roho wachafu wa shetani ndiyo maana zimejengwa katika kanuni ya uongo.

“Asilimia kubwa ya Filamu , vipindi na program zote zifuraishazo na kushangaza zimejengwa katika kanuni ya Uongo (yaana kanuni ya shetani)”

Maana ya CHANELLING

The ability to communicate with evil spirits through medium, (uwezo wa kuwasiliana na roho waovu/wachafu kupitia mfumo au chombo fulani).

Uwashapo TV ilkiyounganishwa na kebo, dishi (satelite), unakuta chaneli nyingi. Hapo shetani shetani ameweka mawasiliano yake kupitia chombo hicho ili unapoendelea kuchaneli japokuwa kuna baadhi ni za mabo ya Mungu. Tabia yake anaihamishia kwako kupitia chaneli mbaya uzitazamazo.
“By beholding we become changed ( Ellen G white), yaani anamaanisha kwa kutazama tunabadilishwa.”

“Kama tunavyobadilishwa kwa kumtazama Yesu, kwa kutazama chaneli za shetani tunafanana na shetani mwenyewe na ndo maana ana mawasiliano ya kula aina katika chaneli.”
lKuchochea ugomvi anachaneli ya ngumi.
lKukuchochea uzini ana chaneli za Ngono “X”
lKuchochea kanuni ya kujikweza ana chaneli za Muzinki wa kidunia n.k.

KUPROGRAM (PROGRAMING)
Ni kuendesha au kuunda kitu unavyo taka wewe, shetani pia hutuunda atakavyo kupitia program mbali mbali za TV, Redio, Intaneti n.k.

Remote control (Kuendesha kwa limonti)
  
Neno hili tunalitumia sana tubadilidhapo program za redio na TV bila kuigusa tukitumia kifaa cha rimonti. Remote inamaanisha mbali.
  
Shetani hutuendesha (control) bila sisi kujua maana hutumia mawakala ambao wako mbali (remote) hata yeye yuko mbali na hivyo si rahisi kujua kama huna Roho wa Mungu. Na hii ndiyo maana ya Remote Control kaatika uchawi wa shetani (Babeli).

   Matokeo yake tunaanza kufanya mambo ambayo hakuna aliyetwambia tufanye ila kwasababu tumevutiwa na program za shetani, na anatuendesha  tunajikuta tunafanya tu. Kuvuta sigara, kuivaa nguo fupi (Vimini).

 HYPNOTISM.
Kamusi ya Kiingereza Kiswahili -hypnosis n kiinimacho; hiponozi: hali ya kuwa kama katika usingizi mzito ambapo mtu anaweza kukuamrisha na wewe ukatenda bila kujijua. hypnotic adj. hypnotism n. hypnotize vt laza/pumbaza akili. hypnotist n mtu apumbazaye akili.
 
Inamaana akili ya  mtu mmoja kuendesha akili ya mtu mwingine hatimmaye anayeendeshwa (kupumbazwa) anajikuta anaenenda katika tabia na mtindo ambao si wake.


  
Mfano- Vijana wengi tokea utotoni huwa wanatenbea vizuri na kuongea vizuri lakini waanzapo kuangalia filamu za muziki na hata zile za kizungu wanaanza kuongea kizungu (what's up man,) na hata mwendo hubadilika na kuwa wa mdundo wengine kama wamevaa viatu vyenye spiringi.

Akili zao zinaanza kuendeshwa na mastaa (malaika wa shetani) kwa hiyo kila kitu wanachofanya wanataka wawe mastaa.




Muvi nyingi za kidunia zimejengwa katika mafundisho ya kishetani


Muvi (Movie,Emotion)
 
Emotion ni neno ka kiingereza litumikalo kuelezea , mhemko au hisia au mwenendo wa mwanadamu. Movie inamaanasha kuhamisha na limetokana na neno move ambalo halina tofauti na e-motion.Hata neno Cinema limetokana na neno la Kigiriki Kinema limaanishalo kuhamisha (to move)

 “Shetani hutumia movie kutuhamiosha na kunadilisha miendendo(e-motion) kwa kutugeuza tabia”.

Wakolosai 1:23. Mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa  na kuliacha tumaini la injili mliyosikia habari zake...
  
Dhumuni la Mungu ni kwamba tusiondolewe klatika injili, dhumuni la shetani ni kutuondoa (move) katika injili.

Kuhamishwa- “kutolewa katika sehemu yako kwa falsafa za kiusanii za walimu wa uongo au misukumo ya dhambi” “to be shifted from your position by the philosophical arts of false teachers or the seductive allurements of sin.”, kitenzi kinaonyesha kwamba “ usowe katika hali endelevu ya kuhamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine           1  Wakorintho. 15:58 imeandikwa “Basi ndugu znagu mwimarike , msiktikisike…

 Msipogeuzwa
  
Neno la Paulo msipogeuzwa limetokana na neno la kigiriki (metakineo-move away) limaanishalo kuhamisha, hata neno Sinema limetokana na neno Kinema-Kinein limaanishalo kuhamisha.
 
Unapoangalia movie unahamishwa kutoka sehemu mojaa hadi nyingine, staa akiumizwa unaumia, akifurahi unafurahi, akitaka kuua unafurahia. Kwa njia hiyo shetani anmatubadilisha tofauti na Mungu alivyokusudia kuwa tusibadilishwe kutoka katika tumaini letu la Kikristo.


Video Game zimejengwa katika kanuni ya ukatili ili kutuweka
katika hatia ya dhambi ya mauaji na chuki. 

VIDEO GAME
Video game nyingi zimejengwa kaatika kanuni ya  hasisra na ukatili, yaani mauaji na ushindani. Kanuni hizi huunda tabiaya shetani.

Ukiua katika video game Mungu unahesabiwa na hatia ya mauaji. Dhambi haaihesabiwi hadi ufanyapo tendo bali huanzia katika fikra. Yesu alisema yeyote amtazamae Mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini nae.

Vivyo hivyo ukiangalia mauaji na mambo mengine machafu katika video, unahesabiwa hatia, na mungu amekataza katika maandiko..
Biblia inaonyesha wazi kwamba watakaoweza kuishi na Mungu (Moto ulao)ni wale wasiotazama mauaji na maovu yaliyotawala katika muvi za kidunia.

Isaya 33:14,15. Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu, kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu:Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao? Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?’’  Yeye aendaye kwa uadilifu na kusema lile lililo sawa, yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma  na kuizuia mikono yake isipokee rushwa, yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu.  

“Shetani hucheza na fikra zetu ili ahakikishe kwamba kwa namna yoyote ziko katika hatia. Hata kipindi cha Nuhu fikra za wanadamu zilikuwa zimejaa dhambi ndo maana Mungu akaleta gharika.”
Shetani hutambua kwamba kwa kufikiri tunatenda dhambi, tunachofikiri husababishwa na tunachiotazama au kusikia . Kwa msingi huo huzalisha filamu za maovu, miziki ya uovu ili achafue fikra au mawazo yetu, tunadhani mawazo yetu ni siri, lakini kwa Mungu sio siri na yatatuhukumu tusipobadilika
Mhubiri 12:14.Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri,ikiwa jema au baya.
Gharika ilishushwa kipindi cha nuhu kwa sababu watu waliwaza mauvu..Mwanzo 6:5 . BWANA akaona jinsi ambavyo uovu wa mwanadamu umekuwa mkubwa duniani na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu.



 
   TABIA NA MUZIKI
   TABIA HUUNDWA NA MAMBO MAWILI

lMawazo (feelings)
lMwenendo (Emotions)

MUZIKI HUUNDWA NA MABO MAWILI

lManeno- ambayo huelezea mawazo (feelings)
lMuziki-ambao huelezea mwenendo (emotions)

   “Muziki ni silaha kubwa atumiayo shetani kubadili tabia zetu, yaani kupitia muziki wa kidunia (blues, rnb, hip hop, bongo fleva, taarabu n.k) shetani hubadili mawazo yetu na mwenendo.”

"muziki hufanya kazi ya kurudia ujenzi (reconstruct) hali ya jamii."(Stokes, 2003, uk 85), 
 
Muziki wa kidunia umeingizwa mpaka kanissani, siku hizi tuna muziki wa injili au disko la Yesu , ikumbukwe kuwa shetani ana kanuni mooja kubwa sana ya kuwateka wakristo. Kila akitaka kuingiza kitu chake katika ukristi huongezea neno kristo mbele. Ndio maana zamani tulikuwa na disko sikuhizi tuna Disko la Yesu. Vitu vingi huvibadilisha kwa njia hii.
 

 DHUMUNI LA MUZIKI NI KUTUKUMBUSHA UTAKATIFU SI MABURUDISHO.

Russano (2000) alisema, Muziki unamiliki kiwango cha maadili na unaweza kumuathiri msikilizajitabia na mwenendo... miziki unawakilisha shauku ya moyo kama vile hamasa, hasira, kiasi, na kinyume na hayo.

Aliendelea kusema kuwa “muziki unaowakilisha shauku fulani pia unaamsha shauku hiyo kwa msikilizaji.aina mbaya ya muziki inakufanya uwe mtu mbaya na aina nzuri inakufanya uwe mtu mzuri.

katika Karne ya 15 makanisa na wanafalsafa walikataa wazo kwamba muziki lazima ufurahiwe kwa jinsi unavyochezwa na sauti...bila kupinga uzuri wa sauti walisema...
      
      
(1)Vitu vizuri vipo kutukumbusha juu ya utukufu na uzuri wa Mungu.
(2)Siyo kufurahisha furaha binafsi.

Bila shaka walichokisema kiko sambamba na madhumuni ya muziki katika biblia tofauti na vile ilivyo sasa katika sehemu nyingi.

Nyimbo nyingi tunazosikiliza makanisani hutufurahisha nafsi zetu na hazitukumbushi utukufu wa Mungu hivyo tumetanga mbali na kusudi la Mungu katika Muziki na kuingiza uchawi wa babeli (Machafuko kanisani).


 Muziki wa unaoingizwa katika makanisa mengi ya kikristo sasa umejengwa katika kanuni za kishetani.
(1)Mkazo mkubwa uko kwenye kucheza (kudansi) na sio kumsifu Mungu katika heshima na kicho. Husababisha kujitukuza nafsi,
(2)Midundo huchochea msisimko nambao hufukuza uwepo wa malaika wa Mungu.
(3)Makelele na fujo huondoa kabisa uwepo wa Mungu.
 
Shetani amefanya yote hayo kwasababu muziki ndiyo njia pekee ambayo binadamu anaweza kuitumia kuweka kumbu kumbu ya maneno na mawazo yoyote yale kwa kuyakariri.

Yawekana katika yote  haya umetambua kwamba wewe ni miongoni mwa waliokamatwa na uchawi wa babeli, usalama pekee ni kuachana na yote uonayo kwamba yatakupoteza na kumtazama Yesu tu.   Wakolosai 1:23. Mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa  na kuliacha tumaini la injili mliyosikia habari zake...

Kusudi la Yesu ni kumtazama Yeye pekee ili atubadilishe, kusudi la shetani ni kutugeuza pale tu tunapoacha kumtazama Yesu na kutazama mambo ya dunia hii.

“Yeye ambaye macho yake humtazama Yesu tu ataacha yote, ataifia nafsi. Ataamini neno la Mungu kama lilivyo”

“Katika msalaba mvutano huishia pale na kutoka pale msukumo wote husambaa, nio kituo kikuu cha mvuto na kutoka hapo msukumo wote husambaa.



   Rejea
èBarnaba R. Hanning.(2000). Concise History of Western music.2nd Ed
èEllen g white, Counsels on Music.
èwww.amazingdiscoveries.org
èDVD - Escape From the Black Hole (Agujero Negro). 
èSDA Bible commentary .Vol 6,pg1113.
èJane Stockes.(2003) How to do Media.Inc Britain london.
èBob Pritchett & Kiernon Reiniger. (1991) SDA Bible Dictionary. Logos Research    Systems Inc.USA