Waweza Kuishi na Yesu, lakini huwezi kuishi bila Yesu.Yohan 3:16



MBINU ZA IBILISI KUONDOA MATENGENEZO KWA WAKRISTO
Shabaha Kubwa Ya ibilisi ni kuwaondoa watu katika Utii wa neno la Mungu
kwasababu kutii Biblia ni kiini cha matengenezo, na utakaso . Yohana 17:17. 


Katika biblia, Yuda 1:3 Biblia yasema tuipiganie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara Moja...


Miongoni mwa mambo makubwa aliyhoyafanya Ibilisi, ni kuondoa hali ya matengenezo kwa watu wa Mungu, zifuatazo ni agenda kuu kumi zilizoandaliwa na jamii za siri ili kuwafanya Wakristo wabweteke , na kuachana na juhudi ya kufanya matengenezo. 

Mambo aliyopangilia Ibilisi kupitia kikao cha siri, kama utakavyoyasoma utagundua kwamba ni udhihirisho katika yale yaendeleayo miongoni mwa Wakristo wengi.

Hizi ni agenda za kikao cha siri

  1. Kuzusha magombano baina ya waombezi ili kuwavunja wasiendelee kumtafuta Mungu wao.
  2. Sababisheni hadithi kwa wingi watakapoingia ndani ya makanisa yao wakati wa kuja kumuomba Mungu wao.
  3. Msiwaruhusu kuomba wakati wa kulala kwao (Janatus) maana hamuwezi kuwaona wakifunikwa na nguvu za Mungu wao.
  4. Msiwape nguvu au nafasi ya kusoma Biblia, baadala yake wapeni wakati mwingi wa kusoma magezeti na kuangalia televishini zao.
  5. Sababisheni ufukara, mateso na pesa zao kupotea bila wao kujua ili wasimtolee Mungu wao, na walio na pesa roho ya ubahili ya kutokutoa.
  6. Inueni nguvu za kuzimu makanisani kwao baina ya viongozi na washirika wao na vijana kwa wasichana ili kupata nafasi ya kuzima nguvu zao.
  7. Ibada zao ziwe baridi kabisa ili Roho wa Mungu wao asipate nafasi ya kuongea na kusikia kutoka kwake.
  8. Tumieni ajali maana damu yao tutaitumia katika vikao vyetu.
  9. Akina mama wajawazito wazalishwe kwa operesheni ili kupata damu.
  10. Tumieni Ukimwi wa kutengeneza kama pigo kwao ili kuwamaliza na kuwaletea aibu katika vifo vyao.
  11. Vurugeni umoja wa nyumba zao kati ya mke na mume, wazazi na waatoto wao ili maombi yasipatikane.
Hayo ni Baadhi ya Mambo yhaliyoorodhesha katika barua ya kikao hicho.

Ukristo ni gharama, kujikana nafsi. Je katika hayo ni lipi ambalo walitenda na kumpatia mwanya Ibilisi katika maisha yako? 

Habari njema ni kwamba , ukimtegemea Yesu kwa moyo wote bila kujichanganya na mabo ya dunia ,kwake ushindio ni wa Lazima. 

Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 

Biblia izungumziapo Mbinu za ibilisi dhidi ya wale wamtegemeao Yesu huishia na kauli ya ushindi , hii ni kutokana na Ukweli kwamba KUPITIA KIFO CHA YESU PALE MSALABANI IBILISI ALINYIMWA UWEZO DHIDI YA WOTE WAMTEGEMEAO YESU

Ufunuo 12:11. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakuyapenda maisha yao hata kufa.

No comments:

Post a Comment